be blessed.Russia alipoivamia na kuitwanga na kuua watu kule Geogia (Abakazia/S. Osertia) sikuona manung'uniko hapa jamvini.
Russia alivyoua maelfu ya wananchi wa Chechnia sikuona kelele hapa jamvini
JK alivyovamia Comoro hakuna mtu alisema neno JF
Wasomali wakiteka meli kila kukicha sijaona kelele hapa JF ndio kwanza watu wanashangilia
Saudia kupeleka majeshi Bahrain, sijaona kelele hapa JF
Gadhafi kumsaidia Idd Amin, sijasikia ikikumbushwa hapa JF
Gadhafi kusponsor mauaji ya Pan Am flight hakuna mtu ameongelea jamvini
Ethiopia kuivamia Somalia watu mmekuwa mabubu hapa JF
Qatar, UAE, Norway and others kupeleka fighter jets Libya, sijasikia manung'uniko hapa jamvini.
El Bashiri akituma Janjaweed kuwabaka na kuwalawiti wanawake Darfur mchana kweupee na kuwaua waume zao, JF kila mtu kimya!
Halafu kwenye maombi ya viza balozini sijaona wabongo wengi wakienda nchi za kiarabu kupanga foleni za viza...bali ni UK na American embassy.
Tuache double standards wana JF