The rise and fall of Colonel Muamar Gadaffi

Itashangaza watu wakianza kuhusisha kifo cha Gaddafi na mambo ya kidini, mfumo wa utawala na siasa ndivyo hasa vilivyohusika na sidhani kama kuna dini itafurahia mauaji labda tu itaongelea sababu zilizopelekea hayo mauaji.
 
article-2051361-0E76175A00000578-996_634x837.jpg


Hapo amezingirwa na wapiganaji wa vikundi mbali mbali vya waasi wa nchi hiyo pamoja na vijana wadogo wa kijijini kwao.

Ajabu kubwa ni kwamba hawa vijana
wanaonekana kuwa ni wenye furaha kubwa kwenye nyuso zao huku wakiendelea kujichukulia kumbukumbu za mwisho wa kiongozi huyo kwa kutumia simu za kiganjani
Mkuu nimefatilia sana vyombo vya habari vya nje,vimekuwa vikisema walibya wanafurahia kuuwawa kwa Gaddafi,cha kushangaza naona ni vikundi vya watu wachache wachache......siyo kwamba namtetea Gaddafi lakini nchi hz za kiafrika ili ziweze kupata maendeleo lazma kiongoz atumie njia zote ikiwemo na dictatorship...alichotakiwa kujifunza Gaddafi ni kuwa si mtu mmoja anayeweza kuongoza nchi milele....all in all nahic Libya haitakuwa na amani ya kudumu kama ilivyo kwa Iraq,Afhganstan
 
mkuu nimefatilia sana vyombo vya habari vya nje,vimekuwa vikisema walibya wanafurahia kuuwawa kwa gaddafi,cha kushangaza naona ni vikundi vya watu wachache wachache......siyo kwamba namtetea gaddafi lakini nchi hz za kiafrika ili ziweze kupata maendeleo lazma kiongoz atumie njia zote ikiwemo na dictatorship...alichotakiwa kujifunza gaddafi ni kuwa si mtu mmoja anayeweza kuongoza nchi milele....all in all nahic libya haitakuwa na amani ya kudumu kama ilivyo kwa iraq,afhganstan

kaacha misikiti yake ambayo watz wanmkumbuka. Sielewi na sijaelewa, kiongozi mmoja anadiriki kusema eti watz watamkumbuka sana kwa mema. Hivi watz wote wanasali kwenye huo msikiti wa gadhafi ulioko dodoma? Viongozi oneni aibu na mwogopeni mungu kuona kila mtanzania kuwa ananufaika na msikiti huo.

Acha aende wamebaki viongozi wengine wanaotumia nafasi zao kwa manufaa yao binafsi au dini zao kama iliyo sasa hapa tz
 
Unajua usichokijua kitakusumbua! Hivi kwa mawazo yako unafikiria kuwa waasi pamoja na watu walioandamana libya ni kwa maslahi ya watu wa libya? Chunguza kwa sasa Obama anaidai mapesa mangapi hiyo libya unayojivunia kwa mapinduzi ya kishetani, vituo vya mafuta nani ameviteka mpaka fidia ya mapesa yanayodaiwa mpaka yarudi yote.

acha ukenge ww , kila siku mnawasingizia wazungu wazungu et marekan mara ulaya mara westen country
mpaka lini ss waafrika tutakuwa tumejitambua kuwa ss n mabwege
kwan huyo mzungu akikutumia anakulazimisha huwez kataa
m nasema ukenge n wetu wenyewe kutokua na umoja na kuendekeza ubinafsi
NA WAZUNGU KWA KULIJUA HILO BASI WANATUTUMIA KAMA MABOYA VILE
LAST BUT NOT LEAST ******* N SS WAAFRIKA KUKUBALI KUTUMIWA KUTOKANA NA USENGE WE2!
 
Aliiishi kama Mwanadamu lakini AKUMUHESHIMU MUNGU NDIO MAANA KAFA KIFO CHA AIBU MIKONONI MWA RAIA ZAKE MWENYEWE.Mungu daima yupo katika sura zetu wenyewe.UTU UTU UTU UTU UTU UTU HASA WA MWANADAMU [DIGNITY] ,vaaa mavazi ya UTU utaishi siku nyingi duniani na kuwa UKIWA KIONGOZI UKAVAA KIATU CHA UTU unabaki kuwa ALAMA AU KIOO CHA WALIOBAKI KWENENDA NA MATENDO YAKO.

Mungu awezi kushuka kuja kuonyesha njia ila kwa kupitia wanadamu Mungu anakuwa nasi kutonyesha UPENDO WAKE KWETU,HAKIKA INAPENDEZA SANA KIONGOZI WA TAIFA ANAPOMJUA MUNGU KWA MATENDO YA UTU NA SIO MBWEMBWE ZA KIBINADAMU,MATENDO YA KUWAJALI WATU WOTE BILA KUCHAGUA,KUWALINDA NA KUWATETEA WASIO NA SAUTI,WASIO NA MSEMAJI,WENYE UITAJI.

Hakika kinachouma ni kuwa raia wenzie wenye kuswali nae ibada ya aina moja ndio waliomtendea hayo ambayo kwa imani yao wao ni ishara kuwa MUNGU waliemuomba awaonyeshe adui yao leo hii kawaonyesha.Ndio maana waliomkamata baada ya kumuona na kumkamata SAUTI KUBWA ZILISIKIKA ZIKISEMA ALLAHU AKBAR -[GOD IS GREAT] KIBONGO -MUNGU MKUBWA.

Nyerere atabaki kuwa Mtu wa ajabu dunia aijapata kuona kwa kuwa yale yale aliyoyasimamia miaka nenda ludi ya kuunda TaIFA lenye kujali utu wa Mtu ndio yanayosumbua dunia kuwa watu wanataka UTU wao USAMINIWE NA WAHESHIMIKE.

Jamani sioalikuwa muumini Allah Subhana u Wataalah na anajenga miskiti? Mbona skuelewi hapa?


Aha kumbe unamaanisha hakumjua Mungu wa kweli aliyejifunua kupitia Yesu Kristo, sasa nimekupata ndugu yangu maana huyo ndiye njia kweli na uzima mtu haingii mbinguni isipokuwa kupitia katika Yeye huyo tu, soma Injili ya Yohana 14:6. Tena huyu jamaa si ndiye alisema Biblia sio kitabu cha Mungu eheee halafu tena kajiita Mfalme wa Wafalme huyu alimkufu Mungu Mkuu na muumba mbingu na dunia ndiyo maana kafanywa hivi. Kwa hiyo kwa ufupi tu kifo chake kina mkono wa Mungu aliye hai, soma Daniel 1:40-43; Ufunuo 19:15-16.
 
Dakika chache kabla ya mauti kumkuta, taarifa zinabaini kukutwa kwake na silaha ya mwisho mkononi; bastola iliotengenezwa kwa dhahabu tupu.

Hii ilikua ni eneo fulani kwenye li-kalivati iliochimbwa chini ya barabara. Ilikua ni baada ya kupata majeraha mabaya sana kutoka kwa shambulio la anga kutoka kwa NATO kwenye kiji-gorofa alikojificha na kundi la mwisho wa jeshi wenye kumuamini hadi kufa.

Katika kukimbia kwao kujiokolea maisha kwingineko ndipo wakaamua kuingia chini ya kalivati ambapo kulikua na miili miwili kwenye lango lake kabla ya mtu yeyote kuweza kutia jicho kwa Gaddafi ambaye bado alikua hai.

Maiti hizo moja ilikua ni ya 'Mwamnyange' wake na nyingine ikiwa ni wa mkurugenzi wa usalama wa taifa la Libya.
 
article-2051361-0E76175A00000578-996_634x837.jpg


Hapo amezingirwa na wapiganaji wa vikundi mbali mbali vya waasi wa nchi hiyo pamoja na vijana wadogo wa kijijini kwao.

Ajabu kubwa ni kwamba hawa vijana
wanaonekana kuwa ni wenye furaha kubwa kwenye nyuso zao huku wakiendelea kujichukulia kumbukumbu za mwisho wa kiongozi huyo kwa kutumia simu za kiganjani
[/QUOTE



picha hii inaonyesha jinsi ambavyo waafrika na hasa waarabu katika tukio hli la kumdhalilisha Gadaff tusivyo na akili. picha inaonyesha waarabu hawa wakikiuka kanuni na alama muhimu za uislamu za kutoonyesha maiti na kuungana na watu wa magharibi kufanya unyama huu.... haikubariki na ni mbaya kwa kumbukumbu ya kizazi kijacho.
 
Gagaff hakusitahili mwisho huu hata kama ana madhambi ingependeza wote tungejiridhisha makosa ya kustahili mwisho huu.... waarabu walibya walioungana na nchi za magharibi kummaliza Gagaff kwa mwisho huu hawatakaa salama ndani ya Libya na dhambi hii naomba iwamalize wale wote wanaofikiri anayetumia upanga ni lazima alipwe kwa upanga. Kama Gadaff alifanya kosa basi na hawa wamefanya kosa ambalo halitawafanya wakae salama baada ya kifo cha Gadaff. Wangejijengea heshima iliyotukuka kama wangemkamata Gadaff na kumfungulia mashitaka na kisha sheria ingechukua mkondo wake
 
Jamani sioalikuwa muumini Allah Subhana u Wataalah na anajenga miskiti? Mbona skuelewi hapa?


Aha kumbe unamaanisha hakumjua Mungu wa kweli aliyejifunua kupitia Yesu Kristo, sasa nimekupata ndugu yangu maana huyo ndiye njia kweli na uzima mtu haingii mbinguni isipokuwa kupitia katika Yeye huyo tu, soma Injili ya Yohana 14:6. Tena huyu jamaa si ndiye alisema Biblia sio kitabu cha Mungu eheee halafu tena kajiita Mfalme wa Wafalme huyu alimkufu Mungu Mkuu na muumba mbingu na dunia ndiyo maana kafanywa hivi. Kwa hiyo kwa ufupi tu kifo chake kina mkono wa Mungu aliye hai, soma Daniel 1:40-43; Ufunuo 19:15-16.

Kweli nakubaliana na wewe, kosa la Gaddafi ni kumkufuru Mungu, ni kosa kubwa kujiita MFALME WA WAFALME. MAANA MUNGU AMEAPA HATASHEA UTUKUFU WAKE NA MWANADAMU. NA YEYE NI MUNGU MWENYE WIVU. MUNGU ANAPOMUINUA MWANADAMU NI ILI YEYE MWENYEWE AINULIWE NA SI MWANADAMU AJIINUE.
 
Watu walisema Obama wanahisi atauwa,au walisema Iraq au Afghanistan zisingetulia leo kimya kimya tunaanza kusau mabomu ya milipuko ya Nchi hizo na tunaaanza kuona picha za matukio mengine kabisa.Libya na mataifa mengine yatajengwa na kupewa ushirikinao na marafiki wao wa kweli,ubaya imekula kwetu kwa kuwa viongozi wetu wamekosa maono [Vision] wengelijua wakasimama katika misingi ya kusimamia sauti kama

"TUNAUNGA MKONO MHESHIMIWA RAIS WA LIBYA KUWASIKILIZA RAIA WAKE NA KUCHUKUA MAAMUZI KWA MUJIBU WA MATAKWA YA RAIA ZAKE "


Sentensi kama hii,leo hii tusingejichongeaa kwenye mapinduzi haya kwa kuwa Nchi ni Mali ya Raia na si kuwa ni Mali Ya Gadhafi na Serikali na Wapambe wake wa Karibu.

Leo hii tumetengeneza ukuta wa kidplomasia wa umma na Taifa hilo la Libya,nashukuru Mungu Kikwete aliliona hilo akalekebisha kwa kutumia uzoefu wake pale alipokuwa United Nations.Ila kwa hapa Nchini Waziri wa Mambo ya Nchi Za Nje amekuwa akiliweka katika Sura mbaya na isiyopendeza kwa kuwajengea wanachi muono mbaya wa sura halisi ya mapinduzi ya Umma ya Libya.Mimi binafsi imekuwa inanichefua vibaya pindi anapoongelea siasa za dunai mpya zinazoendela hasa habari za mapinduzi ya Nchi za Kiarabu.

Sasa ni zamu ya Syria na Yemen sijui ataweka nyongo gani ndani ya Wananchi kuendelea kuichukia Marekani kwa visingizo vya kijinga pasipo kuangalia ukweli halisi.

Nakumbuka miaka ya Nyuma watanzania walilishwa chuki mbaya sana swala la YUGOSLAVIA NA KOSOVO kiasi kuwa kuna mataifa yalibambikiziwa misimamo ya kiovu leo hii kosovo na Yugoslavia ni mataifa yanasonga mbele kustawisha Taifa.

Viongozi wetu wajitume kusoma alama za nyakati [Vision] wasimamie upande wa wenge hiyo ndo asili yetu toka enzi ya Mwalimu aijalishi alikuwa anatupatia nini?Isingekuwa busara za kikwete kuonyesha kuwa yuko pamoja nao kabla ya kifo cha huyu jamaa na hakika mafuta ya Libya tungeyaskia kwenye bomba.

libya1.jpg
Rais Wa Tanzania Jakaya Kikwete na Kiongozi wa Mapinduzi Ya Libya Mustafa Abdel -Jalil walipokutan Nwe York United Nations
10-22-2011 10-27-42 AM.jpg
Rais Jakaya Kikwete na Kiongozi huyo wa Libya Wakifanya Mazungumzo Muhimu ya faragha tena yanaonekana Matamu kwelikweli [Yani kwa tafsili Nyingine ni Mtanzania anaongea na Mlibya kama Marafiki wanaotegemeana kwa ushirikiano]
10-22-2011 10-28-12 AM.jpg
Rais Jakaya Kikwete na Kiongozi huyo wakitakina mikonno ya heri kuwa tuko pamoja [Tafsiri sahihi ni kuwa Mtanzania anamtakia heri Mlibya ambae ni rafiki yake kwa mafaniko yake].Hapa ndipo uwa naona kweli jamaa huyu anastahiki Kofia take ya Udaktari wa Heshima ya Juzi ya SHERIA ya Chuo kikuuu
10-22-2011 10-45-05 AM.jpg
Rais Jakaya Kikwete akimtambulisha Barozi wa Kudumu wa Tanzania kwenye Umoja wa Mataifa Bwana Ombeni Sefue.

View attachment 39644
Haaaaaaaaaaaaaaaa!!!!!!!!!!!!! Enzi hizo imebaki kuwa story aksnnte Kikwete kwa kucheza pele kuwa ulifanya kuwakubali Wapinzani wa Gadhafi kabla HAJAFA vinginevyo tungeweka wapi sura kujitokeza kuonyesha tuko pamoja nao baada ya kuona huyu asieleweka na mkosa utu kashindwa.Lakini leo tuko kifua mbele kwa kuwa uliwatakia heri toka mwanzo RAFIKI WAKATI WA DHIKI NDIO RAFIKI WA KWELI,LEO WAKIKUPA MAFUTA KWA AJILI YA RAIA WAKO NI HAKI YAKO.

Ila bado nalia na wewe na UFISADI WA BONGO, japo ukuuanzisha lakini watanzania wanataka kuona unaumaliza !!!!!!!!!!!!!!!!
 
RIP Gadhafi. Maisha yetu hapa duniani ni mafupi. Ni muhimu kila mmoja wetu kuwa mtumishi wa WATU kuliko kuwa MFALME WA WAFALME. Viongozi wetu wa kiafrika hawazingatii haya. Daima maneno ni mengi kuliko vitendo, kupendelea ndugu na rafiki zao, kukandamisha wapinzani wao wa kisiasa kwa kutumia vyombo vya usalama, kupindisha sheria na katiba kwa manufaa yao. Mara unasikia fulani ni Rais wa Maisha au katiba ibadilishwe ili apate muda wa kutekeleza manifesto ya chama chake na UONGO mwingine mwingi.
 
Gadaff hakuwa wa waislamu tu kama baadhi ya watu wanavyotaka tuelewe hivyo, Gagaff amesaidia jamii nyingi na nchi mbalimbali ikiwemo Tanzania na fedha yake walikula watu wa jamii yote bila kuja dini, kabila na hata rangi kama alikuwa ni mhalifu kwa upande mwingine bado sheria za haki za binadamu zinazuia kutoa adhabu bila kufuata misingi ya sheria. wengi tulikuwa na matumaini kwamba Gadaff angekamatwa akiwa hai na hasa kwa umri wake mkubwa ambao ulikuwa unaelekea mwisho wa maisha yake duniani
 
Hatujapiga hatua yoyote ndani ya miaka hamsini ya uhuru juu ya vyombo vya habari, tuige mfano wa nchi jirani zetu kama Kenya na Uganda!
 
Picha ya kwanza ndani ya freezer la mboga'
Picha ya pili watu wakiwa kwenye foleni





edaf4082ab743717fc0e6a706700ea7a.jpg
4ebc1141abe53917fc0e6a70670016ff.jpg
 
Sasa Great thinker Kila nchi ikipeleka au kila chombo cha habari kikipeleka mwandishi yaani mshika mike picha mnatoi na mpicha mtembeo na mshika mnara wa ku broadcust hayo matangazo si kitakuwa kiloja. Great thinker bbc na voa na aljzeera vinatosha bana.

Ni maswali mengi sana watz huwa wakijiuliza pindi vitu vya msingi huwa vikitokea duniani ila cha ajabu zaidi vyombo vyetu vya habari vinakuwa vinatanguliza sana burudani kuliko habari za msingi,,
Hivi juzi yametokea mapigano na hatimaye aliyekuwa rais wa Libya kupigwa risasi na kuuawa, na baada ya kufa vyombo vya habari vya nchi za magharibi na Ulaya kama VOA, BBC,CNN,SKY NEWS na ALJAZEERA vimekuwa mstari wa mbele kuwapa habari wananchi wao na ulimwengu kiujumla kuhusu kifo cha Gadafi ila cha kushangaza ni kuwa kila nilipokuwa nafungua vyombo vyetu vya habari vilikuwa vianapiga mziki, vikionyesha maigizo ya kitz, kinigeria, kihindi, kiphilipino badala ya kuwapa watz habari juu ya habari tete iliyotokea duniani,,
Tunafahamu kuwa hivyo vyombo vya habari vya Ulaya na Magharibi ni vya kimataifa na kila mtu ana uwezo wa kuona ,,lakini siyo kila mtz ana uwezo wa kuelewa kiingereza na kama ingekuwa ndoo hivyo kuvitegemea vyombo vya magharibi kutupa habari pekee basi kusingekuwa na umhimu wa kuwa na vyombo vya habari hapa TZ,,

Na sijaelewa hivi vyombo vyetu vya habari vinafanya kazi kwa matakwa yapi na kwa faida ya nani maana hata habari wanayoitoa wanakuwa wamecopy na kupaste kwa maana hakuna hata chombo kimoja cha habari cha TZ ambacho kinapeleka mwandishi wa habari huko nje kwa ajili ya kukusanya habari zaidi ya kuangalia nao CNN, BBC, VOA na ALJAZEERA na kututangazia bila kujua kuwa wana umhimu wa kwenda huko na kukusanya habari,,,
Je tutafika kama tv zetu na radio zimeweka mbele zaidi burudani za miziki na maigizo kuliko vitu vya msingi?????
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom