The Official Azam FC Thread

Kwani mkuu hujui migongo wazi ndio wateja wazuri wa vijigazeti vya udaku.Jana kalaliwa magazeti ya 500 leo hayana bei.
 
January 10, 2017
Dar es-Salaam, Tanzania

BREAKING NEWS : Kocha wa zamani wa Aduana Stars, Cioaba Aristica ametua Azam FC

Kocha wa zamani wa Aduana Stars ya nchini Ghana, Cioaba Aristica amesaini mkataba na klabu ya Azam FC ya jijini Dar-es Salaam kuchukua nafasi ya Kocha Zeben Hernandez raia wa Hispania.

images


Kocha huyo mpya wa AZAM FC, Cioaba Aristica raia wa Romania aliiongoza klabu ya Aduana Stars Aduana Football Club - ADUANA STARS COACH CIOABA ARISTICA SATISFIED WITH SLIM WIN OVER WAFA ya Ghana kumaliza ligi ikiwa imeshika nafasi ya pili katika msimamo wa ligi ya nchini Ghana. Kocha Cioaba Aristica aliondoka klabu ya Aduana Stars baada ya ligi ya Ghana kumalizika. Baadhi ya wachezaji wa Aduana Stars waliojiunga Azam FC katika usajili wa dirisha dogo la ligi ya VPL ya Tanzania 2016/2017 kina Yakubu Mohammed na Yahaya Mohammed walikuwa chini ya kocha Cioaba Aristica huko nchini Ghana.

Akizungumza na mtandao rasmi wa klabu www.azamfc.co.tz Ofisa Mtendaji Mkuu wa timu ya Azam FC, Saad Kawemba amesema wameingia naye Kocha Cioaba Aristica mkataba wa muda wa miezi sita wenye kipengele cha kuongezwa. Kwa sasa uongozi wa Azam FC unasubiri vibali vya kumruhusu kocha huyo mpya kufanya kazi nchini kabla ya kuanza rasmi nafasi hiyo ya ukocha.

Alisema Cioaba ana uzoefu mkubwa wa soka la Afrika na ataiongoza Azam FC kwa kipindi hiki hadi mwishoni mwa mwa msimu, ambapo baada ya kuisha watakaa tena mezani kufanya tathimini ya mafanikio yake na wapi wanaweza kuendelea kutokana na kazi iliyofanyika. Cioaba pia amewahi kuwa kocha msaidizi wa klabu kubwa barani Afrika ya Raja Casablanca ya Morocco Raja Casablanca - International Football Clubs Website katika msimu wa 2011/12.

Source: Mromania Kocha Mpya Azam FC | The Official Website of Azam Football Club + Breaking News: Former Aduana coach Cioaba Aristica joins Azam FC - Football Ghana
 
January 11, 2017
Zanzibar, Tanzania

‘Tunajua namna ya kupata matokeo dhidi ya Simba’ ktk Mapinduzi Cup 2017

By Abducado Emmanuel

KUELEKEA fainali ya michuano ya Kombe la Mapinduzi 2017 keshokutwa Ijumaa, Kocha Msaidizi wa Klabu Bingwa ya Afrika Mashariki na Kati Azam FC, Idd Nassor Cheche, ameweka wazi kuwa wanajua namna ya kuikabili Simba na kupata matokeo mazuri kwenye mchezo huo.

Iddi Cheche ametoa kauli hiyo kwenye mazoezi ya kwanza ya Azam FC jioni ya leo ya kujiandaa na mchezo huo, ambapo imeingia fainali baada ya kuichapa Taifa Jang’ombe bao 1-0, lililofungwa kwa shuti kali na kiungo Frank Domayo.

“Mchezo utakuwa mgumu, sisi tumewaona tokea mwanzo kwenye michuano hii na tunawajua tokea huko nyuma na mwalimu waliokuwa naye na sisi tulikuwa naye tunamjua na tunajua ni vitu gani tutafanya, hatuwezi kusema hivi sasa utakuja kuviona uwanjani wakati tunacheza kama tulivyowaahidia kwenye mechi na Yanga,” alisema Cheche wakati akizungumza na mtandao rasmi wa klabu www.azamfc.co.tz

Alisema katika mazoezi ya kwanza wachezaji wa kikosi hicho wameyaanza vema wakiwa na furaha na mwanzo mpya huku akidai kuwa licha ya ushindani utakaoonyeshwa kwenye mchezo huo wamejipanga kukabiliana na hali hiyo.

Cheche ambaye atakiongoza kikosi hicho kama kocha mkuu hadi kumalizika kwa michuano hiyo kabla ya kumpisha Kocha Mkuu mpya wa Azam FC aliyetambulishwa jana, Aristica Cioaba raia wa Romania, mpaka sasa amekiongoza kikosi hicho kuandika rekodi ya aina yake ya kutofungwa mchezo wowote wala kuruhusu bao.

Hadi inaingia fainali kwa kuitoa Taifa ya Jang’ombe, Azam FC kwenye hatua ya makundi iliichapa Zimamoto bao 1-0, ikatoa suluhu na Jamhuri kabla ya kuifumua Yanga mabao 4-0, ukiwa ni ushindi wa kihistoria tokea timu hizo zianze kukutana jikumbushe video:

Source: Azam Football Club

Azam FC kesho Alhamisi jioni itamalizia mazoezi yake ya mwisho kabla ya kuivaa Simba kwenye mchezo wa fainali unaosubiriwa kwa hamu na mamilioni ya Watanzania wapenzi wa soka.
Source: ‘Tunajua namna ya kupata matokeo dhidi ya Simba’ | The Official Website of Azam Football Club
 
MAPINDUZI CUP 2017 ZANZIBAR, TANZANIA

Mapinduzi Cup Final Build Up Azam FC Vs Simba SC.


Source: Soka360 TV
 
Tambo za mashabiki wa Simba SC ''kitakwimu na ukongwe dhidi ya timu "ndogo" ya Azam FC kuelekea mchezo wa fainali ya Mapinduzi Cup mjini Zanzibar baadaye jioni ya leo tarehe 13/01/2017

source: simu tv
 
Goli moja la ushindi la Azam FC kupitia kwa Himid Mao dakika ya 13 ya mchezo wa fainali ya Mapinduzi Cup 2017 dhidi ya Simba SC limetosha kuipa Azam FC ubingwa wa michuano ya Mapinduzi Cup mbele ya maelfu ya wakazi wa visiwa vya Unguja na wageni toka Tanganyika

Dakika ya 90" + 3" Full time results : Azam FC 1 - Simba SC 0
Azam FC have been crowned as the champion of Mapinduzi Cup 2017 at the Amaan Stadium in Zanzibar,Tanzania
 
Azam FC yatwaa Mapinduzi Cup 2017, yaweka rekodi mpya
By Abducado Emmanuel on January 14, 2017
IMG_5580.JPG

Picha: Wachezaji wa Azam FC wakishangilia Kombe lao la Mapinduzi Cup 2017 baada ya kukabidhiwa na Rais wa Zanzibar ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dr. Ali Mohamed Shein ktk uwanja wa Amaan, Zanzibar.

NI raha tu! Hivi ndivyo hali ilivyo kwa timu ya Azam baada ya usiku wa kuamkia leo kutwaa taji la michuano ya Kombe la Mapinduzi, ikiichapa Simba bao 1-0 katika mchezo uliofanyika Uwanja wa Amaan, Zanzibar.

Klabu hiyo Bingwa ya Afrika Mashariki na Kati, imetwaa taji hilo kwa kuandika rekodi mpya na ya aina yake baada ya kutofungwa mchezo wowote katika mechi tano ilizocheza za michuano hiyo, huku pia ikiwa haijaruhusu bao lolote.

Azam FC ikicheza kwa ari kubwa na morali ya hali ya juu kwenye mchezo huo, iliwachukua dakika 13 tu kuweza kuandika bao hilo la ushindi lililofungwa kiufundi kwa shuti kali la umbali wa mita 25 na Nahodha Msaidizi, Himid Mao ‘Ninja’.

Mao alipiga shuti hilo lililomshinda kipa wa Simba, Daniel Agyei, kufuatia pasi safi aliyopigiwa na kiungo Salum Abubakar ‘Sure Boy’.

Licha ya Simba kufanya mashambulizi kadhaa, ilijikuta ikutana na upinzani mkali wa kuweza kuipenya safu ngumu ya ulinzi ya Azam FC chini ya mabeki wa kati visiki, Aggrey Morris na Yakubu Mohammed.

Haikushangaza kusikia mwishoni mwa mchezo huo, Morris akitangazwa kuwa mchezaji bora wa mechi hiyo na kupewa zawadi ya katoni nne ya kinywaji safi cha Azam Malti, kiatu cha kuchezea mpira na kikombe maalum.

Azam FC kutwaa ubingwa huo, kumeifanya kujibebea kombe walilokabidhiwa na mgeni wa heshima wa mchezo huo Rais wa Zanzibar, Dk. Ali Mohammed Shein, pia walijizolea medali na kitita cha Sh. Milioni 10 na Rais wa Zanzibar, Dk. Ali Mohammed Shein, huku Simba wakipewa medali za mshindi wa pili na Sh. Milioni 5.

Kamati ya mashindano hayo pia ilimtangaza kipa wa Azam FC, Aishi Manula, kuwa Kipa Bora wa michuano hiyo, Beki Bora amekuwa ni Mzimbabwe Method Mwanjali wa Simba na Mfungaji Bora ni Simon Msuva wa Yanga.

Taji la tatu

Ubingwa huo umeifanya Azam FC kuifikia rekodi ya Simba ya kulitwaa taji hilo mara tatu, lakini mabingwa hao safari hii wakibebwa na rekodi ya kulitwaa bila kufungwa mchezo wowote wala kuruhusu wavu wake kuguswa.

Mara mbili za nyuma, iliweza kuweka rekodi ya kuwa timu pekee kulitwaa taji hilo mara mbili mfululizo, ikilibeba mwaka 2012 na 2013.

Rekodi zakolea Azam FC

Ubingwa huo unaifanya Azam FC kufikisha taji la pili msimu huu na hii ni baada ya Agosti mwaka jana kutangulia kwa kutwaa Ngao ya Jamii kwa kuifunga Yanga kwa mikwaju ya penalti 4-1 kufuatia sare ya mabao 2-2 ndani ya dakika 90.

Hiyo ni rekodi ya pili mfululizo kwa Azam FC kutwaa taji bila kuruhusu wavu wake kuguswa, itakumbukwa walifanya tena hivyo mwaka juzi walipotwaa taji la kwanza la michuano ya Kombe la Kagame (CECAFA Kagame Cup), ambapo kwenye fainali waliichapa Gor Mahia mabao 2-0.

Msimu wa 2013/2014, Azam FC ilifanya maajabu mengine ya kutwaa taji la kwanza la Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL) bila kufungwa mchezo wowote.

Kikosi cha Azam FC kilikuwa:

Aishi Manula, Shomary Kapombe, Gadiel Michael, Aggrey Morris, Yakubu Mohammed, Stephan Kingue, Salum Abubakar, Himid Mao/Enock Atta Agyei dk 82, John Bocco, Yahya Mohammed/Mudathir Yahya dk 69, Joseph Mahundi/Frank Domayo dk 57
Source: The Official Azam FC Thread
 
January 31, 2017
Dar-es-Salaam, Tanzania

Mamelodi Sundowns FC Vs Azam FC Friendly Match in Tanzania

Mamelodi Sundowns FC a South African football team and winner of 2016 CAF African Champions League, is a club based in Pretoria, South Africa. The Mamelodi Sundowns is to play a friendly match against Azam FC on Wednesday Feb 1, 2017 at the National Stadium in Dar-es-Salaam, Tanzania at 19:00 hrs (EAT). Mamelodi Sundowns are South Africa second club from the country to ever win the African Champions League, Orlando Pirates won in 1995. The South African team is in Tanzania training ready to face TP Mazembe of DRC Congo who are the CAF African Confederation Cup champions in the CAF Super Cup match in February 18, 2017.

Azam FC will miss key players, John Bocco and Stephan Kingue who both are nursing injuries sustained when Azam FC played against Simba in the Tanzania Vodacom sponsored Premier League game last week.


Source: Millard YouTube

Additional Info:
Mamelodi Sundowns FC is scheduled to fly back to South Africa on Friday, February 3, where they will return to normal training as they prepare to gear up for their first league encounter of the year.

The Absa Premiership will return to action next month, and Sundowns will get their second-half of the 2016/17 campaign underway when they face Bloemfontein Celtic away on February, 8.

Head coach Pitso Mosimane’s side are faced with a tight schedule for the month of February, due to the team having to play catch up on their previously postponed league encounters. Source: South African soccer news — Mamelodi Sundowns To Play Friendly Encounters In Tanzania
 
January 31, 2017
Dar-es-Salaam, Tanzania

Azam FC kukipiga na Mamelodi Sundowns kesho
By Abducado Emmanuel on January 31, 2017

Source: Millard Ayo
KLABU Bingwa ya Afrika Mashariki na Kati, Azam FC, inatarajia kukipiga na Mabingwa wa Afrika, Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini, kwenye mchezo wa kirafiki utakaofanyika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kesho Jumatano saa 1.00 usiku.

Hii ni mara ya pili kwa timu hizo kukutana kwenye mechi ya kirafiki, Agosti 7 mwaka 2013 zilikutana kwa mara ya kwanza jijini Johannesburg, Azam FC ilipoenda kuweka kambi ya maandalizi ya msimu mpya na kuichapa timu hiyo bao 1-0 lililofungwa na mshambuliaji wa zamani, Gaudence Mwaikimba.

Kwa mujibu wa muandaaji wa ziara hiyo ya Mamelodi nchini, Rahim Kangezi Zamunda, amesema kuwa mchezo huo ni maalumu kwa ajili kampeni ya kupinga vita ujangili, iitwayo Linda Tembo Wetu.

Mamelodi iliyokuja kuweka kambi hapa nchini, pia itautumia mchezo huo kama sehemu ya kupasha misuli kujiandaa na mchezo wa Super Cup dhidi ya mabingwa wa Kombe la Shirikisho Afrika TP Mazembe, utakaopigwa Februari 18 mwaka huu.

Mara baada ya mchezo huo, Mamelodi itakipiga tena na African Lyon Alhamisi ijayo katika mchezo wa mwisho wa kirafiki nchini.

Azam FC ambayo itashiriki michuano ya Kombe la Shirikisho ikianzia raundi ya kwanza, hiko ni kipimo tosha kwa upande wao katika kuwapima wachezaji wake namna watakavyoanza changamoto za kusaka hatua ya makundi ya michuano hiyo.

Mabingwa hao wa Ngao ya Jamii na Kombe la Mapinduzi msimu huu, wanatarajia kuanza changamoto ya michuano hiyo mwezi Machi mwaka huu, ikikutana na mshindi wa jumla wa mechi ya raundi ya awali baina ya Orapa United ya Botswana au Mbabane Swallows ya Swaziland.
Source: Azam FC kukipiga na Mamelodi Sundowns kesho | The Official Website of Azam Football Club
 
February 5, 2017
Dar-es-Salaam, Tanzania
Azam FC inaivaa Ndanda leo Jumapili
KLABU Bingwa ya Afrika Mashariki na Kati, Azam FC, inatarajia kushuka dimbani kuvaana na Ndanda ya Mtwara katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL) utakaofanyika Uwanja wa Azam Complex leo Jumapili saa 1.00 usiku.

Kuelekea mchezo huo, wachezaji wa Azam FC wamejipanga vilivyo kufanya kweli kwa kuibuka na ushindi kufuatia mafunzo makali wanayopewa na benchi la ufundi la timu hiyo chini ya Kocha Mkuu Aristica Cioaba, Msaidizi wake Idd Cheche na Kocha wa Makipa, Idd Abubakar.

Azam FC ipo katika nafasi ya nne kwenye msimamo ikiwa na pointi 34, ikiwa nyuma ya pointi 15 na kinara Yanga aliyejikusanyia 49, Ndanda yenyewe ipo kwenye hatari ya kushuka daraja baada ya kujizolea pointi 19 ikiwa nafasi ya 15.
Source: Abducado Emmanuel : Azam FC inaivaa Ndanda ikiwa na bonge la rekodi | The Official Website of Azam Football Club
 
February 5, 2017
Dar-es-Salaam, Tanzania

Results Tanzania Vodacom Premier League 2016/2017
Full time: Azam FC 1 - Ndanda FC 0. Goal scorer for Azam FC in 85" min Yahaya Mohammed connecting a nice pinpoint cross from his mate Himid Mao.

Source: Brother Mako
Azam FC team starting eleven : Aishi Manula, Erasto Nyoni, Gadiel Michael, Yakubu Mohammed, Aggrey Morris, Himid Mao (C), Abdallah Masoud/ Sub:Afful 56'', Frank Domayo, Yahaya Mohammed, Shaaban Idd/Sub: Mudathir 80'', Joseph Mahundi/ Sub : Singano 68''
 
March 3, 2017
Dar-es-Salaam, Tanzania

by Abducado Emmanuel

Aishi%20Manulaaa%20Edittt.jpg

Photo: Aishi Manula, Azam FC number one goalkeeper.

WAKATI kikosi cha Klabu Bingwa ya Afrika Mashariki na Kati, Azam FC, kikitarajia kushuka dimbani kesho Jumamosi saa 1.00 usiku kuvaana na Stand United, kipa wa timu hiyo Aishi Manula, ameweka bonge la rekodi miongoni mwa makipa wote wanaoshiriki kwenye Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL). Source: Aishi Manula anashikilia bonge la rekodi Ligi Kuu | The Official Website of Azam Football Club
 
Back
Top Bottom