The Official Azam FC Thread

July 30, 2016
Dar-es-Salaam, Tanzania

By Abducado Emmanuel

Nyota Medeama asaini miaka miwili Azam FC
KLABU Bingwa ya Afrika Mashariki na Kati Azam FC, imefanikiwa kunasa saini ya winga nyota wa timu ya Medeama ya Ghana, Enock Atta Agyei, ambaye tayari amesaini mkataba wa miaka miwili kujiunga na timu hiyo.
IMG-20160729-WA0009.jpg

Picha: Mchezaji ya Medeama, Enock Atta Agyei akiwa ofisini tayari kukamilisha kutia saini mkataba wa kuhamia Azam FC.

Kinda huyo anatua baada ya kulivutia Benchi la Ufundi la Azam FC chini ya Kocha Mkuu, Zeben Hernandez, ambaye amependekeza asajiliwe baada ya kumuona kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam wakati Medeama ikiilazimisha sare ya bao 1-1 Yanga katika mchezo wa Kundi A wa Kombe la Shirikisho Afrika.

Uongozi wa mabingwa hao umefanya jitihada za hali ya juu hadi kunasa saini yake, ambapo umelazimika kumpandia ndege mshambuliaji huyo hadi mjini Takoradi, Ghana, usajili huo ukiratibiwa na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Azam FC, Saad Kawemba, aliyeenda huko na kukamilisha vema kazi hiyo maalumu kwa kuzungumza na pande zote mbili mchezaji na uongozi wa Medeama akiwemo Mmiliki wa timu, Moses Armah.

Akiwa nchini Ghana, Kawemba alipata fursa ya kukutana na Kocha Mkuu wa timu ya Taifa ya Ghana ‘Black Stars’, Avram Grant raia wa Israel, wakati wa mchezo wa marudiano kati ya Medeama na Yanga ulioisha kwa wenyeji kushinda mabao 3-1.

Katika mazungumzo yake na Kawemba, Grant aliyewahi kuifundisha Chelsea na kuifikisha kwenye fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya mwaka 2008, aliipongeza Azam FC kwa kutambua kipaji cha Enock na kumsajili.

“Nawapongeza sana Azam FC kwa kutambua kipaji cha Enock akiwa amefikisha umri wa miaka 18, nawaahidi nitakuwa namfuatilia kwa karibu kwa kipindi chote cha mkataba wake atakachokuwa Azam FC,” alisema Grant katika moja ya mazungumzo yake na Kawemba.

Enock, 18, mwenye kipaji cha hali ya juu, mara baada ya kukamilisha taratibu zote za kujiunga na Azam FC, anatarajia kutua nchini kesho Jumamosi saa 2.15 asubuhi na ndege ya Shirika la Ndege la Kenya (KQ).

Winga huyo mwenye kipaji cha hali ya juu anayetabiriwa kutikisa zaidi miaka michache ijayo, ameanza kung’ara wakati akiwa hana uzoefu mkubwa sana na Ligi Kuu ya Ghana kwani amejiunga na Medeama Desemba mwaka jana baada ya kufanya vizuri akiwa na Windy Professionals ya Ligi Daraja la Kwanza nchini humo.

Azam FC inayodhaminiwa na Benki ya NMB na kinywaji safi cha Azam Cola, hivi sasa ipo kwenye kambi Visiwani Zanzibar ikifanya maandalizi kabambe ya kujiandaa na msimu ujao, kikosi kikiwa chini ya makocha wapya kutoka nchini Hispania.
IMG_7465.JPG

Picha: Timu ya Azam FC ikifanya mazoezi kwa kuendesha baiskeli Zanzibar.

KOCHA Mkuu wa Klabu Bingwa ya Afrika Mashariki na Kati Azam FC, Zeben Hernandez, ameendelea kukiandaa kikosi chake kisayansi zaidi, ambapo leo amewashangaza baadhi ya wakazi wa Visiwani Zanzibar baada ya kuwafanyisha zoezi la kuendesha baiskeli barabarani wachezaji wake.
Source: Nyota Medeama asaini miaka miwili Azam FC | The Official Website of Azam Football Club
 
Aug 17, 2018
By Abducado Emmanuel

Azam FC mabingwa wapya Ngao ya Jamii 2016/2017

KLABU Bingwa ya Afrika Mashariki na Kati Azam FC, imefanikiwa kuufungua msimu mpya wa 2016/17 kwa kutwaa ubingwa wa Ngao ya Jamii 2016 baada ya kuichapa Yanga kwa mikwaju ya penalti 4-1 kufuatia sare ya 2-2 ndani ya dakika 90 katika mchezo uliofanyika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam jioni ya leo.

Source: MCL Digital

Hilo ni taji la kwanza la Ngao ya Jamii kwa Azam FC baada ya kulikosa kwa miaka mitatu mfululizo ikipoteza dhidi ya Yanga, pia ni ubingwa wa kwanza kwa makocha wapya kutoka Hispania wa Azam FC wanaoongozwa na Kocha Mkuu, Zeben Hernandez.

Kipindi cha kwanza hakikuwa kizuri kwa Azam FC kutokana na kupwaya kwa eneo la ulinzi, hali iliyopelekea Yanga kupata mabao mawili ya haraka yaliyofungwa na Donald Ngoma.

Ngoma alianza kufunga bao la kwanza dakika ya 20 kwa mkwaju wa penalti kufuatia kuangushwa ndani ya eneo la hatari na beki David Mwantika kabla ya kufunga jingine dakika ya 26.

Azam FC ilijitahidi kurejea mchezoni kuelekea mwishoni mwa kipindi cha kwanza, lakini kulikosekana umakini kwenye eneo la ushambuliaji kila walipolikaribia lango la Yanga,

Mabadiliko yaliyofanywa kipindi cha pili na kocha wa Azam FC, Zeben Hernandez, akiwaingiza kiungo Mudathir Yahya na mshambuliaji Francisco Zekumbawire na kutoka Ramadhan Singano ‘Messi’, Shaaban Idd, yaliongeza uhai kwenye eneo la kiungo la mabingwa hao.

Huku pia akiongeza mashambulizi zaidi kwa kumrejesha katikati kiungo Salum Abubakar aliyekuwa akicheza kama namba saba kipindi cha kwanza pamoja huku akimpeleka pembeni beki Shomari Kapombe aliyeanza mchezo huo kama beki wa kati.

Zekumbawira, aliyesajiliwa kwenye usajili huu wa dirisha kubwa, alishirikiana vema na Bocco kuwasumbua mno mabeki wa Yanga kwa kupeleka mashambulizi mfululizo, wakibadilishana kushambulia pembeni ya uwanja na katikati.

Juhudi za Azam FC za kulishambulia lango la Yanga zilizaa matunda dakika ya 74 baada ya Kapombe kufunga bao la kwanza kwa shuti la kulala kufuatia kusetiwa mpira na kiungo Jean Mugiraneza ‘Migi’.

Bao hilo lilizidi kuongeza ari zaidi kwa upande wa Yanga na hatimaye ikafanikiwa kupata penalti dakika ya 90 kufuatia beki wa Yanga kuunawa mpira uliokuwa umepigwa na Mudathir na penalti hiyo ilifungwa kiufundi na nahodha John Bocco ‘Adebayor’.

Kufuatia dakika 90 kumalizika kwa sare hiyo, mwamuzi wa mchezo huo Ngole Mwangole kutoka Mbeya, ilibidi aaamue mshindi wa mchezo huo apatikane kwa changamoto ya mikwaju ya penalti kama sheria zinavyotaka.

IMG_7132.JPG

Shujaa wa Azam FC kwenye hatua hiyo, alikuwa ni Kipa Bora wa msimu uliopita wa mashindano ya Ligi Kuu na Kombe la FA, Aishi Manula, aliyepangua penalti ya beki Ramadhan Kessy huku nyingine ya Yanga ikikoswa na Haruna Niyonzima aliyegongesha mwamba wa juu na mpira kutoka nje.

Penalti ya kiufundi za Azam FC zilifungwa na Bocco, Nahodha Msaidizi Himid Mao, Kapombe na Michael Bolou, aliyetupia ya mwisho na kuipa ushindi Azam FC.

Baada ya mchezo huo, Azam FC kesho inatarajia kuanza tena mazoezi ya kujiandaa na mchezo wa kwanza wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL) dhidi ya African Lyon utakaofanyika Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam Jumamosi ijayo.
Maoni ya wachezaji baada ya Azam kuifunga Yanga

Source: MCL DIGITAL
Vikosi vilivyocheza:

Azam FC: Aishi Manula, Isamil Gambo, Bruce Kangwa, David Mwantika, Himid Mao, Jean Mugiraneza, Shomary Kapombe, Salum Abubakar/Michael Bolou dk 90, John Bocco, Shaaban Idd/Mudathir Yahya dk 46 na Ramadhani Singano ‘Messi’/Francisco Zekumbawira dk 46.

Yanga: Deogratius Munishi ‘Dida’, Hassan Kessy, Mwinyi Haji, Mbuyu Twite, Vincent Bossou, Said Juma, Haruna Niyonzima, Juma Mahadhi/Malimi Busungu dk 81, Thabani Kamusoko, Amissi Tambwe/Simon Msuva dk dk 67, Donald Ngoma.
Source: Azam FC mabingwa wapya Ngao ya Jamii | The Official Website of Azam Football Club
 
Naikubal sna hii team, naona mafanikio makubwa yanakuja hko mbeleni
 
Aug 18, 2016
Dar-es-Salaam, Tanzania

By Abducado Emmanuel

Safari ya Azam FC ktk Vodacom Premier League (VPL) yaanza

Wakati Azam FC inayodhaminiwa na Benki ya NMB na kinywaji safi cha Azam Cola ikianza kwa vema msimu huu kwa kutwaa taji la Ngao ya Jamii 2016/2017 kama ilivyofanya msimu uliopita kwa kubeba Kombe la Kagame, inatarajia kuanza safari yake ya kufukuzia ubingwa wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzani Bara (VPL) keshokutwa Jumamosi kwa kumenyana na African Lyon.
IMG_6931.JPG

Mchezo huo unaotarajia kuwa mkali na wa aina yake utafanyika kwenye Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam, ambapo awali ulitakiwa upigwe saa 10.00 jioni, lakini Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) limebadili muda na kuupeleka hadi saa 1.00 usiku.

TFF imebadilisha muda huo, ili kuiwezesha timu ya Taifa ya vijana ya Afrika Kusini (U-17) ‘Amajimbos’ kuweza kuutumia uwanja huo saa 9. 00 Alasiri siku hiyo kufanya mazoezi yake kama sheria za Shirkisho la Soka Afrika (CAF) zinavyotaka kabla ya kurudiana na vijana wa Tanzania ‘Serengeti Boys Jumapili ijayo.
Source: Taji la Ngao ya Jamii lampa mwanga Zeben | The Official Website of Azam Football Club
 
Aug 20, 2016
Dar-es-Salaam, Tanzania

By Abducado Emmanuel

MATCH OF THE DAY: Azam FC vs African Lyon
Azam FC inaingia kwenye ligi ikiwa imesajili wachezaji wapya wa kimataifa, ambao ni mabeki Daniel Amoah (Ghana), kiraka Bruce Kangwa (Zimbabwe) na winga Enock Atta Agyei (Ghana) atayeanza kuichezea timu hiyo Januari mwakani pamoja na washambuliaji Francisco Zekumbawire (Zimbabwe), Gonazo Bi Thomas (Ivory Coast).

KLABU Bingwa ya Afrika Mashariki na Kati Azam FC, leo Jumamosi inatarajia kuanza rasmi patashika ya kuwania taji la Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL) msimu 2016/17 kwa kuwakaribisha mahasimu wao African Lyon ndani ya Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam.

Mchezo huo utaanza saa 1.00 usiku.

Match of the Day Final Results / Matokeo
Azam FC 1 - African Lyon 1
Goal scorer for African Lyon on 46 minute is Hood Abdul Mayanja whose corner kick went straight in and Azam Fc had to wait until added time on 93 minutes when captain John Bocco scored after receiving a much waited pass from team mate Salum Abubakar "Sureboy".

Rekodi zao (Head To Head)

Hadi zinaingia kwenye mchezo huo msimu huu, Azam FC ikitoka kushika nafasi ya pili msimu uliopita na African Lyon ikirejea tena Ligi Kuu ikitokea Ligi Daraja la Kwanza (FDL), timu hizo zimekutana mara nne katika michuano hiyo.

Azam FC inayodhaminiwa na Benki ya NMB na kinywaji safi cha Azam Cola, ndio wanaaongoza kushinda mechi nyingi, ikiifunga mara tatu African Lyon huku yenyewe ikishinda mara moja tu (1-0), katika mchezo wa kwanza kabisa waliokutana Agosti 23, 2011.

Mechi tatu zote zilizofuatia hadi Lyon inashuka daraja msimu wa 2012/13, Azam FC iliibuka kidedea kwa kuifunga mabao 2-1 (Januari 25, 2012), 1-0 (Oktoba 6, 2012) na 3-1 (Aprili 11, 2013).

Katika mechi zote nne, Azam FC ndio iliyofunga mabao mengi zaidi ikitupia sita katika lango la wapinzani wao hao, huku Lyon yenyewe ikitingisha nyavu za matajiri hao mara tatu tu.

Azam FC kufukuzia rekodi

Mbali na kunuia kutwaa taji la pili la ligi msimu huu, Azam FC itaingia kwenye patashika hiyo ikiwa na rekodi nzuri ya kushika nafasi mbili za juu kwa misimu mitano mfululizo na msimu mmoja (2013/14) ikiibuka mabingwa kwa mara ya kwanza bila kufungwa mchezo wowote.

Hivyo msimu huu utakuwa wa sita mfululizo ikifanikiwa kushika nafasi hizo mbili na itakuwa ni mara pili kama ikitwaa ubingwa huo, ambapo kwa mujibu wa kikosi cha timu hiyo, safari hii kimeimarika sana hali ambayo inatoa mwanga wa kufanya vizuri zaidi katika michuano yote inayoshiriki.

Na moja ya malengo makubwa ya makocha wapya wa Azam FC ni kuifanya Azam FC kuwa timu bora Afrika Mashariki na Kati na Afrika kwa ujumla hadi kufikia mwakani kuanzia kucheza soka zuri uwanjani na kupata matokeo bora kwenye mechi inazocheza
Source: MATCH DAY: Azam FC vs African Lyon | The Official Website of Azam Football Club
 
Tanzania Vodacom Premier League (VPL) 2016/2017 : Highlights
RESULTS : AZAM FC 1 - 1 AFRICAN LYON : AUGUST 20/2016 ALL GOALS
Commentators: Azam FC vs African Lyon are Baraka Mpenja and Pascal Kabombe
Simba SC 3-1 Ndanda FC . Commentators Florian Kaijage na Ahmed Hassan.

Source: MpenjaSports TV

Zeben aomba muda zaidi, kurekebisha makosa vs Majimaji
By Abducado Emmanuel on August 22, 2016
IMG_5658.JPG

KOCHA Mkuu wa Klabu ya Azam FC, Zeben Hernandez, amesema kuwa anahitaji muda zaidi ili kukisuka kikosi chake na kucheza kupitia mifumo wanayoendelea kuwafundisha wachezaji wa timu hiyo.

Zeben pia ametanabaisha kuwa atayafanyia kazi makosa yote yaliyojitokeza kwenye mchezo wa kwanza wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL) dhidi ya African Lyon ulioisha kwa sare ya 1-1, ili waweze kufanya vizuri mchezo ujao dhidi ya Majimaji.
“Kwa sasa tunafanya tathimini ya mchezo uliopita, kutoa makosa na kurekebishana pale tulipokosea” alisema.

Mechi vs Lyon
Akizungumzia mchezo wa kwanza dhidi ya African Lyon, Zeben alisema timu yake haikucheza vibaya sana kulingana na mechi zilizopita huku akidai kuwa tatizo kubwa linalokikabili kikosi chake ni ufungaji wa mabao.

Mbali na hilo amesema kuwa wiki hii, atalifanyia kazi suala la wachezaji wake kushindwa kumaliza mechi kipindi cha kwanza, akidai kuwa kwa mechi kadhaa zilizopita kikosi chake kimekuwa kikitafuta ushindi kipindi cha pili kuliko mwanzoni mwa mechi.

“Sikuwa na timu mwanzo, nimeingia kikosini hivi sasa na nimeanza kubadilisha mfumo na mbinu kwa timu kucheza namna tunavyotaka sisi kulingana na mifumo, hilo ni tatizo ambalo lipo ni kubwa kwa sasa na tunaendelea kujitahidi kulifanyia kazi na hata wiki hii tutaendelea nalo ili kwa mechi zijazo liweze kuondoka,” alisema.

Azam FC inakamiwa

Zeben aliendelea kusema kuwa jambo linaloonekana hivi sasa ni timu zote zinazokuja Azam Complex kucheza na timu yake, hufanya jitihada kubwa kuliko uwezo wao ili kuonyesha nao wanaweza kucheza mpira.

“Hili si tatizo kubwa sana inabidi tuendelee kulizoea na nitaendelea kuiboresha timu, ili kwa yoyote atakayekuja Chamazi au nje ya Chamazi tuweze kumfunga,” alisema.

Ligi itakuwa ngumu

Kocha huyo wa zamani wa Stanta Ursula ya Hispania, alisema ameshuhudia mechi za kwanza za ligi msimu huu na kudai kuwa haitakuwa ligi rahisi sana na ngumu kwake yeye kutokana na kikosi alichonacho.

Kikosi cha Azam FC kinachodhaminiwa na Benki ya NMB na kinywaji safi cha Azam Cola, kitaanza rasmi mazoezi ya kujiandaa na mchezo ujao dhidi ya Majimaji kesho Jumanne asubuhi, mechi itakayopigwa Uwanja wa Azam Complex, Jumamosi ijayo saa 10.00 jioni.
Source: Zeben aomba muda zaidi, kurekebisha makosa vs Majimaji | The Official Website of Azam Football Club
 
November 9, 2016
Mwadui Shinyanga , Tanzania

By Abducado Emmanuel

VODACOM VPL 2016/2017 Results : Mwadui 1 : Azam FC 4

KLABU Bingwa ya Afrika Mashriki na Kati, Azam FC, jioni ya leo imemuenzi vema aliyekuwa Mwenyekiti wake, Mzee Said Mohamed Abeid, aliyefariki dunia juzi jioni, kwa kuipa dozi kali ya mabao 4-1 Mwadui FC katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL) uliofanyika Uwanja wa Mwadui, Shinyanga.

Mwadui walitangulia kupachika bao la uongozi dakika ya 30 lililofungwa na Hassan Kabunda.

Kabla ya kuingia bao hilo, mshambuliaji wa Mwadui Jerry Tegete dakika ya 19 alizua kizaazaa baada ya kufunga bao kwa mkono, ambalo lilikubaliwa na mwamuzi Enock Onoka, lakini baadaye alilikataa baada ya kushauriana na wasaidizi wake kufuatia wachezaji wa mabingwa hao kulilalamikia, jambo ambalo lilimfanya kuwalima kadi za njano Tegete na Abdallah Mfuko na kuamuru faulo ipigwe kuelekea lango la Mwadui.

Azam FC ililazimika kufanya mabadiliko ya kwanza mchezoni dakika ya 36 baada ya kiungo Mudathir Yahya kuumia na nafasi yake ilichukuliwa na winga machachari Ramadhan Singano ‘Messi’ na hadi mpira huo unaenda mapumziko Mwadui ilitoka kifua mbele kwa bao hilo.

Kipindi cha pili Azam FC ilirejea mchezoni na kuanza kuonyesha kandanda safi baada ya mabadiliko ya kuingia washambuliaji wawili Francisco Zekumbawira na Shaaban Idd, ambao waliongeza kasi kwenye eneo la ushambuliani la mabingwa hao.

Shambulizi kali ililofanya Azam FC dakika ya 54 lilizaa bao la kusawazisha kwa timu hiyo, lililofungwa na nahodha John Bocco ‘Adebayor’, aliyepiga shuti kali lililomshinda kipa wa Mwadui. Bao hilo linamfanya Bocco kutimiza mabao sita msimu huu.

Mwadui iliyoshindwa kabisa kuwadhibiti washambuliaji wa Azam FC hasa Shaaban Iddi na Francisco Zekumbawira, ilijikuta ikipigwa bao la pili na Shaaban dakika ya 71 kabla ya Zekumbawira kupigilia msumari wa tatu dakika ya 74 akimalizia kazi nzuri iliyofanywa na kinda huyo.

Shaaban aliendeleza moto wake kwa kuipatia bao la nne Azam FC dakika ya 77 baada ya kuwatoka walinzi kadhaa wa Mwadui na kupiga shuti lililomshinda kipa na hivyo kuhitimisha ushindi huo mnono kabisa kwa timu hiyo msimu huu.

Ushindi huo unaifanya Azam FC kumaliza mzunguko wa kwanza wa ligi ikiwa wenye nafasi ya tatu katika msimamo wa ligi ikijikusanyia pointi 25 .

Katika mchezo huo, Kocha Mkuu wa Azam FC, Zeben Hernandez, alianza kutumikia adhabu yake ya kutokaa benchi baada ya kutolewa nje na mwamuzi katika mechi iliyopita dhidi ya Mbao, hivyo benchi la mabingwa hao leo lilitawaliwa na Kocha Msaidizi, Yeray Romero.

Kikosi cha Azam FC leo.

Aishi Manula, Erasto Nyoni, Gadiel Michael/Shaaban dk 46, Daniel Amoah, Aggrey Morris, Himid Mao, Mudathir Yahya/Singano dk 36, Salum Abubakar, Frank Domayo/Zekumbawira dk 54, John Bocco (C), Bruce Kangwa
Source: Azam FC yamuenzi Mzee Said kwa kuipa dozi nene Mwadui | The Official Website of Azam Football Club
 
Nafasi ya tatu, sio mbya. gradually tunasonga ngoj msimu upinduke... mambo yataenda sawa tu
 
November 11, 2016
Dar-es-Salaam, Tanzania

Enock Atta Agyei asaini miaka mitatu Azam FC

By Abducado Emmanuel,

UONGOZI wa Klabu Bingwa ya Afrika Mashariki na Kati Azam FC, unayofuraha kuwaataarifu wapenzi wa soka kuwa jioni ya leo umefanikiwa kuingia mkataba wa miaka mitatu na kiungo mshambuliaji kutoka Ghana, Enock Atta Agyei.

Agosti mwaka huu, Azam FC tuliingia makubaliano maalumu na Medeama ya Ghana juu ya kumsajili kinda huyo anayetimiza umri wa miaka 18 mwakani baada ya benchi la ufundi kuridhishwa na uwezo wake na sasa amejiunga rasmi kwenye viunga vya Azam Complex.

Agyei anasaini mkataba tayari kabisa kuanza kuitumikia Azam FC katika mzunguko wa pili wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL) mwakani pamoja na michuano mingine ikiwemo Kombe la Shirikisho Afrika.

Tunaamini ya kuwa ujio wa nyota huyo wa timu ya Taifa ya Vijana ya Ghana chini ya miaka 17, utazidi kuipa nguvu timu yetu kuelekea kwenye michuano inayotukabili mbeleni, hivyo tunapenda kumtakia mafanikio mema kwa kipindi chote atakachokuwa akiipigania jezi ya Azam FC.

Azam FC tunapenda kuwafahamisha mashabiki wetu kuwa tutaendelea kukifanyia marekebisho kikosi chetu kuelekea usajili wa dirisha dogo, lengo ni kukipa nguvu kikosi hicho ili kifanye vizuri zaidi katika michuano ya hapa nchini pamoja na ile ya Kimataifa.
IMG_5592.JPG

Picha: Enock Atta Agyei akitia saini mkataba wa miaka mitatu na Azam FC.

Wakati huo huo, leo tumewapokea wachezaji saba waliokuja kwenye majaribio ya kujiunga na Azam FC, ambao ni mabeki wa kati Mbimbe Aaron Nkot (Cameroon), Kone Nabil Ibrahim (Ivory Coast), kiungo mkabaji Kingue Mpondo Stephane (Cameroon),

Wengine ni washambuliaji Yaya Awaba Joel (Cameroon), Samuel Afful, Benard Ofori (wote Ghana) na Konan Oussou kutoka Ivory Coast.

Imetolewa na Uongozi wa Azam FC Agyei asaini miaka mitatu Azam FC | The Official Website of Azam Football Club
 
November 15, 2016
Dar-es-Salaam, Tanzania

By Abducado Emmanuel

Nyota wa majaribio wamvutia Coach Zeben Hernandez

KOCHA Mkuu wa Azam FC, Zeben Hernandez, ameweka wazi kuwa amefurahishwa na viwango vya baadhi ya nyota waliokuja kufanya majaribio ya kujiunga na timu hiyo kwenye usajili wa dirisha dogo uliofunguliwa leo.

Azam FC jana usiku ilimaliza programu ya kukifanyia tathimini kikosi chake kwa kuichapa Ruvu Shooting mabao 3-1 kwenye mchezo wa kujipima ubavu, ambao pia iliutumia kuwapima wachezaji tisa waliokuja kwa majaribio, mabeki wa kati Nkot Mandeng Eric (Coton Sport De Garoua, Cameroon), Kone Nabil Ibrahim (Asec Mimosa, Ivory Coast).

Kiungo mkabaji Kingue Mpondo Stephane (Coton Sport Garoua, Cameroon), Abdallah Khamis pamoja na washambuliaji Yaya Anaba Joel (Coton Sport Garoua, Cameroon), Samuel Afful (Sekondi Hasaacas, Ghana), Bernard Ofori (Medeama, Ghana), Konan Oussou (Tala’ea El-Gaish SC, Misri) na Jean Karekezi.

Mabao mawili kati ya matatu ya Azam FC usiku wa jana yalifungwa na nyota waliokuwa majaribio, ambao ni Bernard Ofori aliyefunga la kwanza kwa kichwa akimalizia krosi safi ya Gadiel Michael na Samuel Afful akitumia juhudi binafsi kwa kumzidi maarifa beki pembeni ya uwanja na kupiga shuti kali lililojaa wavuni.

Hernandez ameuambia mtandao rasmi wa klabu www.azamfc.co.tz kuwa muda kuanzia sasa anatarajia kupeleka mapendekezo yake kwa uongozi wa timu hiyo juu ni nyota gani kati ya hao wasajiliwe, huku akidai kwa viwango alivyoviona anaamini ya kuwa wachezaji watakaosajiliwa wataweza kuisaidia sana timu ya Azam FC.

Kocha huyo wa zamani wa Club Deportivo Santa Ursula Zeben Hernández abandona el Santa Úrsula y se va a Tanzania ya Hispania, alisema anaamini ya kuwa kikosi chake kikiingia raundi ya pili kitaweza kupambana ipasavyo basi matokeo yatakuwa mazuri na hatimaye kuweza kufikia nafasi nzuri zaidi kwenye msimamo kuliko nafasi ya tatu.

Mara baada ya mchezo wa jana dhidi ya Ruvu Shooting, benchi la ufundi la Azam FC limewapa mapumziko ya wiki mbili wachezaji wa kikosi hicho kabla ya kuanza tena mazoezi Desemba 3 mwaka huu kwa ajili ya kuanza maandalizi ya mzunguko wa pili wa ligi, Kombe la Shirikisho (Azam Sports Federation Cup) na michuano ya Kimataifa. Source: Nyota wa majaribio wamvutia Hernandez | The Official Website of Azam Football Club
 
November 16, 2016
Dar-es-Salaam, Tanzania

By Abducado Emmanuel

Azam FC yawasajili rasmi Samuel Afful na Yahaya Mohammed

UONGOZI wa Klabu Azam FC, unayofuraha kuwaataarifu wapenzi wa soka kuwa jioni ya leo umefanikiwa kuingia mikataba na washambuliaji nyota kutoka Ghana, Samuel Afful na Yahaya Mohammed.

Zoezi la kuingiana mikataba limehudhuria na baadhi ya viongozi wakuu wa timu wakiwemo Ofisa Mtendaji Mkuu, Saad Kawemba, Meneja Mkuu, Abdul Mohamed, Kocha Mkuu Zeben Hernandez pamoja na wakala anayewasimamia wachezaji hao, Kingsley Atakorah, ambaye pia ni Ofisa Mtendaji Mkuu wa Adom Wonders Academy ya nchini Ghana.

Wakati Samuel Afful, 20, akisaini mkataba wa miaka mitatu, Yahaya Mohammed aliyetua nchini leo mchana akitokea Ghana naye amesaini kandarasi ya miaka miwili tayari kabisa kuanza kuitumikia timu hiyo yenye maskani yake Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam.

Afful ambaye mpaka sasa yumo katika vikosi vya timu za vijana za Ghana chini ya umri wa miaka 20 na 23, anajiunga Azam FC akitokea timu ya Sekondi Hasaacan ya Ghana, ambayo aliifungia mabao tisa timu hiyo msimu uliopita.
Video :Two goals by Samuel Afful gives Hasaacas win over WA All Stars

Source: FootPro Players

Moja ya rekodi yake ni kuifungia bao muhimu timu ya Taifa ya Ghana chini ya umri wa miaka 20 (U-20) mwaka jana dhidi ya Zambia kwenye ushindi wa mabao 2-1, lililoipa nafasi ya kushiriki fainali za Kombe la Dunia nchini New Zealand, baada ya kutinga nusu fainali ya Mataifa ya Afrika kwa Vijana (U-20) zilizofanyika Senegal mwaka jana.

Yahaya Mohammed, 28, ambaye ni mshambuliaji mzoefu anayetokea Aduana Stars MATCH REPORT: Aduana Stars 1-0 Berekum Chelsea - Yahaya Mohammed sends Aduana to second place - Football Ghana , alikuwa ni mfungaji bora namba mbili wa Ligi Kuu ya Ghana msimu uliopita akifunga mabao 15, pungufu ya mabao mawili na kinara Latif Blessing (Liberty Professional) aliyetupia 17.
Yahaya Mohammed.mpg Video:

Source: wizzy ekuus

Azam FC tunaamini ya kuwa ujio wa nyota hao, utazidi kuipa nguvu timu yetu kuelekea kwenye michuano inayotukabili mbeleni, mzunguko wa pili wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL), Kombe la Kagame (CECAFA Kagame Cup) tukiwa kama mabingwa watetezi, Kombe la Shirikisho (Azam Sports Federation Cup) na Kombe la Shirkisho Afrika (CC) mwakani.
Imetolewa na Uongozi wa Azam FC source:Azam FC yawasajili Afful, Mohammed | The Official Website of Azam Football Club
 
November 18, 2016
Dar-es-Salaam, Tanzania

‘Subirini moto, tutakuwa tishio eneo la ushambuliaji’ - Samuel Afful
By Abducado Emmanuel,
NYOTA mpya wa Azam FC, Samuel Afful, ameweka wazi kuwa kikosi hicho kitakuwa moto kuelekea michuano mbalimbali itakayoshiriki kuanzia mwezi ujao kutokana na ujio wake na aina ya wachezaji aliowaona ndani ya timu hiyo.

Mshambuliaji huyo kutoka Ghana amesaini mkataba wa miaka mitatu juzi akitokea timu ya Sekondi Hasaacas ya huko, anaungana na nyota wengine Waghana waliosajiliwa na Azam FC msimu huu, beki wa kati Daniel Amoah, winga Daniel Atta Agyei na mshambuliaji Yahaya Mohammed.

Afful, 20, alifunga bonge la bao kwa shuti kali kwenye mechi yake ya mwisho ya majaribio dhidi ya Ruvu Shooting Jumatatu iliyopita katika ushindi wa 3-1 wa Azam FC.

Akizungumza na mtandao rasmi wa klabu www.azamfc.co.tz Afful alisema kwa aina ya wachezaji ambao Azam FC imewasajili kutoka Ghana akiwemo yeye basi itarajia kuwa na safu tishio ya ushambuliaji kwenye mechi zinazokuja.

“Nimefurahi sana kujiunga na Azam FC kama mchezaji mwingine anavyofurahia kusaini mkataba na timu mpya, namshukuru Mungu kwani yeye ndiye amefanikisha hili, nimejiandaa vilivyo kuisaidia timu hii na naamini kwa namna nilivyowaona wachezaji kwenye mechi mbili nilizocheza na usajili uliofanywa Azam FC itakuwa moto sana kwa mechi zinazokuja na eneo la ushambuliaji litakuwa tishio,” alisema.

Afful aliongeza kuwa: “Ni wapya kwenye timu lakini tutakapokuwa tukicheza wote tutakuwa tukizungumza lugha moja ya kusaidia timu kwenda mbele, naamini kwa aina ya wachezaji niliowaona na sisi tulioongezeka, Azam FC itakuwa na kikosi bora kabisa cha muhimu ni mashabiki kujitokeza kwa wingi kutusapoti, nilifurahishwa na ujio wao kwenye mechi ile iliyopita (Ruvu Shooting), hali hiyo inatupa nguvu sisi wachezaji.”

Afful pia amewahi kuwemo kwenye kikosi cha timu ya Taifa ya Ghana cha wachezaji wa ndani, kilichoshiriki fainali za Mataifa ya Afrika kwa Wachezaji wa Ndani (CHAN) zilizofanyika South Africa mwaka juzi (2014) The 3rd Orange-African Nations Championship, CHAN 2014 | South African Government na timu hiyo kushika nafasi ya pili akiwa sambamba na nyota mwingine aliyesajiliwa na Azam FC, Yahaya Mohamed Ghana announce final CHAN squad - 2014 Chan - Ghana .

Kikosi cha Azam FC kwa sasa kipo kwenye mapumziko ya wiki mbili hadi Desemba 3 mwaka huu, kitakapoanza mazoezi ya kwanza kujiandaa na mzunguko wa pili wa ligi pamoja na michuano mingine mbalimbali.
Source: ‘Subirini moto, tutakuwa tishio eneo la ushambuliaji’ | The Official Website of Azam Football Club
 
November 2016
Dar-es-Salaam, Tanzania

John Bocco All Goals in Tanzania Vodacom Premier League First Round 2016/2017 - Azam FC

Source: Azam Football Club
 
November 2016
Dar-es-Salaam, Tanzania

John Bocco All Goals in Tanzania Vodacom Premier League First Round 2016/2017 - Azam FC

Source: Azam Football Club

Huyu jamaa angekuwa anachezea timu mojawapo ya Kariakoo, tungeisoma namba.
 
January 7, 2017
Zanzibar, Tanzania

Mapinduzi Cup 2017: Results : Match of the Day : Azam FC 4 - Young Africans 0

Azam 4G, yaigonga Yanga 4-0
By Abducado Emmanuel
IMG_0362_0.JPG

HUKU ikicheza soka la hali ya juu, Klabu Bingwa ya Afrika Mashariki na Kati Azam FC usiku huu imeiendesha mchakamchaka Yanga kwa kuigonga kipigo kizito cha mabao 4-0 kwenye mchezo wa michuano ya Kombe la Mapinduzi.

Aina ya ushindi iliyoupata Azam FC na kasi iliyoonyesha mchezoni, ilitosha kabisa kwa mashabiki kuifananisha timu hiyo na ile kasi ya juu ya mtandao wa ‘intaneti’ ya 4G.

Iliichukua Azam FC dakika ya pili kuandika bao la kwanza lilifungwa na nahodha John Bocco ‘Adebayor’ kwa shuti akimalizia mpira uliotemwa na kipa wa Yanga, Deogratius Munishi ‘Dida’, kufuatia kupangua shuti lililopigwa na Joseph Mahundi.

Azam FC iliendeleza kasi ya mshambulizi, ambapo dakika ya 23 ilifanya shambulizi jingine kali langoni mwa Yanga, lakini shuti lililopigwa na kiungo mkabaji Stephan Kingue, lilitoka sentimita chache ya lango.

Dakika ya 41 Bocco alikaribia kuipatia bao la pili Azam FC baada ya kuwatoka mabeki kadhaa wa Yanga na kupiga shuti kali lililopanguliwa na kipa na kukosa mmaliziaji kabla ya kuwaahi tena na kuudaka.

Mchezaji bora wa mchezo huo, Salum Abubakar ‘Sure Boy’, dakika ya 43 aliwatoka mabeki watatu wa Yanga na kuingia kwenye eneo la 18 lakini shuti alilopiga lilimbabatiza beki kabla ya mpira kuokolewa.

Hadi dakika 45 za kipindi cha kwanza zinamalizika, Azam FC iliondoka kifua mbele kwa bao hilo ambapo ilirejea tena makali kipindi cha pili na kufanya mashambulizi kadhaa mwanzoni mwa kipindi hicho.

Shambulizi kali lililofanywa kuelekea langoni mwa Yanga dakika ya 54 lilizaa matunda baada ya Yahaya Mohammed kuipatia bao la pili Azam FC kwa kichwa akimalizia krosi safi iliyochongwa na Sure Boy.

Winga Mahundi ambaye naye aliendeleza kiwango chake bora dakika ya 80 alifunga bao zuri la umbali wa takribani mita 25 na kuipa uongozi wa mabao 3-0 Azam FC.

Mabadiliko yaliyofanywa na Azam FC dakika ya 79 ya kuingia winga Enock Atta Agyei na kutoka kiungo Frank Domayo, yalizidi kuitakatisha timu hiyo baada ya Enock kuifungia bao la nne dakika ya 84 akimalizia pasi safi ya Samuel Afful ambaye naye aliingia dakika ya 65 kuchukua mikoba ya Yahaya aliyeumia.

Kuelekea dakika za mwisho, Azam FC ingeweza kupata bao la tano na sita kama Sure Boy na Afful wangeweza kuzitumia vema nafasi walizopata.

Kama kawaida mchezaji bora wa mchezo huo, Sure Boy, alikabishiwa katoni nne za kinywaji safi kisicho na kilevi cha Azam Malti huku timu zote mbili nazo zikipewa idadi hiyo ya katoni kila mmoja.

Ushindi huo mnono unaifanya Azam FC kumaliza hatua ya makundi ya michuano hiyo ikiwa kileleni mwa Kundi B baada ya kufikisha pointi saba, Yanga ikifuatia wakiwa nazo sita, Zimamoto (3) na Jamhuri (1).

Azam FC, Bocco rekodi

Ushindi huo umeiongezea rekodi Azam FC katika mechi za mashindano mbalimbali walizokutana na Yanga, ambapo hivi sasa rekodi inasomeka kuwa katika mechi 28 walizokutana kila timu imeshinda mara 10, sare nane, huku matajiri hao wakiwa wamefunga mabao mengi zaidi, 38 na Yanga 37.

Bao alilofunga Bocco linamfanya kutimiza mabao 13 aliyoifunga Yanga kihistoria akiwa ni mchezaji pekee aliyeifunga mabao mengine timu hiyo pamoja na Simba, ambayo nayo ameitupia wavuni mara 18.

Mwaka 2012 Azam FC ilipotwaa kombe hilo kwa mara ya kwanza, iliifunga Yanga mabao 3-0 na kuiondosha mashindanoni timu hiyo, safari hii ushindi unaifanya iandike rekodi ya kuipa kipigo kizito Yanga kihistoria.

Kikosi cha Azam FC kilikuwa hivi:

Aishi Manula, Shomari Kapombe, Gadiel Michael, Yakubu Mohammed/Abdallah Kheri dk 90, Aggrey Morris, Stephan Kingue, Salum Abubakar, Frank Domayo/Enock Atta dk 79, John Bocco (C)/Mudathir Yahya dk 86, Yahaya Mohammed/Samuel Afful dk 65, Joseph Mahundi
Source: Azam 4G, yaigonga Yanga 4-0 | The Official Website of Azam Football Club
 
January 7, 2017
Zanzibar, Tanzania

Mapinduzi Cup 2017 : Match of the Day : Young Africans Vs Azam FC .
Final Results Young Africans 0 - Azam FC 4

Young Africans SC ilivyocharazwa Mabao 4 kwa 0 na Azam FC

Source: BongoStars
 
Ahsante Azam. Leo jiji kimya. Migongo wazi wametulizwa. Magazeti leo hayana bei. Wauza maandazi na samaki watafaidi sana.
 
Ahsante Azam. Leo jiji kimya. Migongo wazi wametulizwa. Magazeti leo hayana bei. Wauza maandazi na samaki watafaidi sana.
Hapo kwenye Magazeti, yameniuzi sana leo. Habari ya VYURA KUFA haijapewa kipaumbele kabisa.

Eti kuna gazeti limeandika: YANGA KAMA MLIVOSKIA ZANZIBAR (sina uhakika kama ni DIMBA)
 
10 Reactions
Reply
Back
Top Bottom