TGIF: Mrema alipokutana na JK wiki hii (Picha)

Status
Not open for further replies.
Unajua nadhani imewachukua watu muda mrefu sana kuamini kuwa Mrema ni mpinzani. Wengi walidhani ni "kibaraka".. lakini vibaraka wote wamesharudi CCM.
 
Mrema ni kati ya watu ninaowaheshimu sana, Ni shujaa alieenda vitani akapigana mwenyewe mstari wa mbele, hakukaa kimya, sera zake za siku saba hazikuwa na utata wala kutokueleweka, aliwaweza majambazi, waliweka silaha chini.
Aliwaweza viongozi wa juu mafisadi, aliwaweza wauza unga, aliwaweza wafanyakazi wa serikali irresponsible.
Jamani nani anakumbuka the good old days, alipokuwa gumzo? yani hata wafanyabiashara walimuunga mkono sana wakijua biashara zao zitastawi baadae katika Tanzania bora.
Mara!!!
Ghafla wakampfanya tumuone kama katuni, akisema kitu watu wanacheka wanapuuza, ilikuwa strategic plan kwani mabomu yake yalikuwa makali na yanalenga.
Katika mambo amabyo Mwinyi atakumbukwa nayo ni kumuweka Mrema an kumtoa.(it was such an impact)
Nani mwingine anayeweza kuwa firm miaka yote hii katika vita, mstari wa mbele kama Mrema? Hakuna, wote wamejificha, au wanakuja kwa msimu.
huyu ndie shujaa wa kweli wa mustakabali wa uchumi wa watanzania
 
Nilikuwepo binafsi kwenye ile mitafaruku ya mabomu!Mzee wa kiraracha na sukari yake hakukata tamaa!Alikuwa achukue nchi na mwl alikuwa anampenda ila wasiwasi wake ndio uliomfanya asikubali aende ikulu!
Lakini kunzia kashfa ya minofu ya samaki na kina chavda!Pamoja na yeye kutimuliwa bungeni kwa kigezo cha ukiukwaji wa "collective responsibility"..Mrema alikuwa upande wa wananchi! Akautema uwaziri na unaibu waziri mkuu na kukaa benchi la nyuma kama mbunge wa kawaida tu na kuanza kuwalima maswali mafisadi aliokuwa akifanya nao kazi na wengine waliokuwa chini yake!
Huyu jamaa kweli ni mzalendo! Alikuwa upande wa wananchi toka wakati akiwa CCM na alikuwa maarufu kwa kusimamisha shilingi!Alikuwa mpiganiaji haki za wananchi pamoja na mazao yao kama vile kahawa na korosho,pamoja na sekta za madini!Na CCM ndio walimuona kuwa ni kizuizi kwenye ufisadi!Na yeye kwa kuona kuwa CCM wanamzuia yeye kuwatumikia wananchi ipasavyo aliamua kujiunga na upinzani!Akayatema maslahi na kuhimili ujasusi wa Mkapa na Mahita ambao walimtreat kama jambazi!Na kumbe majambazi ni wao!
Hii picha hapo juu kwa vile ninavyomfahamu mzee wa kiraracha..utaona kuwa ana uchungu mwingi sana kwa sababu huyu jamaa anajua mengi sana!Anapo mwangalia Kikwete hapo ni kama vile anamwambia.."You think i don't know you huh?"
 
Mzee Mwanakijiji umenichekesha sana,yaani Mrema anatia Huruma,sijui anaomba na yeye apewe hata ubunge wa kuteuliwa..angalia mikono hiyo...lugha hapo inampiga chenga

Mrema hawezi kupigwa chenga na lugha, ana degree (sijui ya nini vile!!!) aliipata online. Au walikuwa wanamfundisha kwa kiswanglish?
 
Mrema hawezi kupigwa chenga na lugha, ana degree (sijui ya nini vile!!!) aliipata online. Au walikuwa wanamfundisha kwa kiswanglish?
Ndio wasiwasi na lugha kama hizi zilizopelekea wananchi kusahahu hoja muhimu wakati huo na kumjengea Mrema chuki mbali mbali zisizokuwa na msingi na shutma mbali mbali na kejeli kama vile hawakuziona hizo issue wakati huo akiwa na madaraka makubwa serikalini!Sasa kama usipokuwa CCM uko hatarini kuwa under intense scrutiny..scrutiny ambayo hauipati kama uko CCM kwani kuna ushaidi mwingi tu wa vyeti vya kuchonga huko mawizarani na masirkalini!MH BORA YA ONLINE KULIKO FEKI!
 
MREMA NI SHUJAA WA KWELI.

Mrema ni kati ya watu ninaowaheshimu sana, Ni shujaa alieenda vitani akapigana mwenyewe mstari wa mbele, hakukaa kimya, sera zake za siku saba hazikuwa na utata wala kutokueleweka, aliwaweza majambazi, waliweka silaha chini.
Aliwaweza viongozi wa juu mafisadi, aliwaweza wauza unga, aliwaweza wafanyakazi wa serikali irresponsible.
Jamani nani anakumbuka the good old days, alipokuwa gumzo? yani hata wafanyabiashara walimuunga mkono sana wakijua biashara zao zitastawi baadae katika Tanzania bora.
Mara!!!
Ghafla wakampfanya tumuone kama katuni, akisema kitu watu wanacheka wanapuuza, ilikuwa strategic plan kwani mabomu yake yalikuwa makali na yanalenga.
Katika mambo amabyo Mwinyi atakumbukwa nayo ni kumuweka Mrema an kumtoa.(it was such an impact)
Nani mwingine anayeweza kuwa firm miaka yote hii katika vita, mstari wa mbele kama Mrema? Hakuna, wote wamejificha, au wanakuja kwa msimu.
huyu ndie shujaa wa kweli wa mustakabali wa uchumi wa watanzania

Nakubaliana na wewe asilimia zote mzee ila napata uchungu kujua kuwa watu wa aina yake ni kama wameisha Tanzania. Kitu kingine, napata uchungu kuona kuwa anazeeka bila kufanikisha malengo, hivi huyu mzee ana watoto kweli? Wako wapi, manake sijawahi kuwasikia?
Hivi kuna walau shule moja au mtaa unaoitwa kwa jina lake hapo bongo? Tunahitaji kitu cha kutukumbusha kuhusu shujaa huyu wa nchini mwetu.
Watu wangapi ndani ya sisiemu wameshindwa kuutema ubunge kwa kuhofia kupoteza posho na mashangingi? Naona viongozi wote (wanawake kwa wanaume)wa serikali ya tatu, Mkapa angeweza kuwaoa angetaka!!! Ona mambo aliyofanya na hakukuwa na wa kumpinga!! Nina wasiwasi alikuwa hata anawachapa viboko Ikulu ila paparazi hawakuona tu! Mniwie radhi watu wote ambao ni maswahiba wa viongozi wa serikali ya awamu ya tatu.
Issue zingine tunamlaumu JK bure, matatizo mengi tu yametokana na Ben na serikali yake na yako nje ya uwezo wa JK wa kuyashughulikia kwa sababu ya mizizi iliyowekwa na Ben. Ni kama paradox ya Magufuli na kutaka kuinyoosha wizara ya ardhi!!!!!!
Tafadhali msinichukie!!
 
Jambo linalosikitisha katika yote ni kuwa watu wengi wanachukia mafisadi na kuwalaani. Wakati huohuo wao ndio mstari wa mbele kumdhihaki na kumcheka mtu kama mrema kwa sababu hajajilimbikizia mali na pia hana suti ya kufuliwa ulaya kama wengine. Nadhani katika mioyo ya watanzania wengi wangetaka kuwa mafisadi wakipata nafasi. Tunadhamini watu kwa mali zao na mavazi yao na muonekano wa nje, hatudhamini utu na mchango wao kwa jamii. Inanisikitisha sana.
 
Hapa tz ukiwa mwadilifu na mpiga filimbi, unatengenezewa mazingira ya kuonekana adui wa taifa. Wale walafi ndio wanaonekana ni watu wa watu.
ALM alionekana kioja mbele ya watz, ila he is so daring..(forget about the college degrees).
Ni wakati wa kuwakumbuka mashujaa wetu, wakiwa hai ni bora zaidi.
 
Yote tisa, heri mrema n amaisha haya kuliko mafisadi na AIBU yote hiyo...!

Naomba kuwakilisha!
 
Nimepingana na wengi juu ya Augustine Lyatonga Mrema, mimi namkubali kuwa ni mchapa kazi,hodari,jasiri,mkweli,mwenye jazba,mzalendo,mtu wa watu na mcha mungu. Huyu ni sawa na awamu ya kwanza ya Julius K.Nyerere alipotokea Sokoine wengi tulimkubali lakini wachache wanaojifanya leo kuwanyoshea wenzao vidole walinuna sana na hata kifo chake walikifurahia moyoni,alipokuja Mwinyi akamzaa Lyatonga kwa ushauri wa Malecela,huyu ni mtu ambaye alishabikiwa sana na wa Dkt.Malecela taratibu ikawa ni Malecela ,Mrema na kidogo ktk maafa na Bungeni kijana Lowasa akaanza kung'ara, walianza kung'aka pale Dkt.Cigweyimis alitamka hadharani kama mawaziri (Especially Msuya)mnaona huyu Lyatonga anawaingilia basi subirini tumuongezee nguvu na uhalali na akatamka hii si nguvu ya soda bali ni gongo , mara Alhaj Mwinyi akampa nafasi ya Naibu waziri mkuu na Mambo ya Ndani huku akimsogeza Jaji Edward Mwesiumo kama naibu wake mambo ya ndani ...hapo sasa wakuu ndiyo shughuli ilipoiva mpaka deal ya airport na kadhalika; he was the man Tz wanted in place of the Late Edward Moringe Sokoine. Tunakuomba Mh.JK MKUMBUKE HUYU Ndg kwa heshima na mchango aliompatia Mzee Mwinyi hata kama mwishoni alishindwa kumstah mzee Ruksa,fanya kama mwenzio alivyofanya kwa Chief Fundikira,historia itakulinda kwa hilo.
 
1985-Salimu alipozwa kwa kofia hiyo ya unaibu waziri mkuu na waziri nchi -ikulu Jwtz &JKT baada ya palea aliponyimwa urais kwa mara ya kwanza licha ya Julius kumtaka. ndie deputy PM wa kwanza
 
Mrema ni kati ya watu ninaowaheshimu sana, Ni shujaa alieenda vitani akapigana mwenyewe mstari wa mbele, hakukaa kimya, sera zake za siku saba hazikuwa na utata wala kutokueleweka, aliwaweza majambazi, waliweka silaha chini.
Aliwaweza viongozi wa juu mafisadi, aliwaweza wauza unga, aliwaweza wafanyakazi wa serikali irresponsible.
Jamani nani anakumbuka the good old days, alipokuwa gumzo? yani hata wafanyabiashara walimuunga mkono sana wakijua biashara zao zitastawi baadae katika Tanzania bora.
Mara!!!
Ghafla wakampfanya tumuone kama katuni, akisema kitu watu wanacheka wanapuuza, ilikuwa strategic plan kwani mabomu yake yalikuwa makali na yanalenga.
Katika mambo amabyo Mwinyi atakumbukwa nayo ni kumuweka Mrema an kumtoa.(it was such an impact)
Nani mwingine anayeweza kuwa firm miaka yote hii katika vita, mstari wa mbele kama Mrema? Hakuna, wote wamejificha, au wanakuja kwa msimu.
huyu ndie shujaa wa kweli wa mustakabali wa uchumi wa watanzania

Kiongozi wa chama cha kujali masilahi ya wafanyakazi tanzania na mkombozi wa wanawake Augustino Mrema atalipwa na MUNGU kwa yote mazuri aliyoifanyia Tanzania na watu wake.
 
Nilikuwepo binafsi kwenye ile mitafaruku ya mabomu!Mzee wa kiraracha na sukari yake hakukata tamaa!Alikuwa achukue nchi na mwl alikuwa anampenda ila wasiwasi wake ndio uliomfanya asikubali aende ikulu!
Lakini kunzia kashfa ya minofu ya samaki na kina chavda!Pamoja na yeye kutimuliwa bungeni kwa kigezo cha ukiukwaji wa "collective responsibility"..Mrema alikuwa upande wa wananchi! Akautema uwaziri na unaibu waziri mkuu na kukaa benchi la nyuma kama mbunge wa kawaida tu na kuanza kuwalima maswali mafisadi aliokuwa akifanya nao kazi na wengine waliokuwa chini yake!
Huyu jamaa kweli ni mzalendo! Alikuwa upande wa wananchi toka wakati akiwa CCM na alikuwa maarufu kwa kusimamisha shilingi!Alikuwa mpiganiaji haki za wananchi pamoja na mazao yao kama vile kahawa na korosho,pamoja na sekta za madini!Na CCM ndio walimuona kuwa ni kizuizi kwenye ufisadi!Na yeye kwa kuona kuwa CCM wanamzuia yeye kuwatumikia wananchi ipasavyo aliamua kujiunga na upinzani!Akayatema maslahi na kuhimili ujasusi wa Mkapa na Mahita ambao walimtreat kama jambazi!Na kumbe majambazi ni wao!
Hii picha hapo juu kwa vile ninavyomfahamu mzee wa kiraracha..utaona kuwa ana uchungu mwingi sana kwa sababu huyu jamaa anajua mengi sana!Anapo mwangalia Kikwete hapo ni kama vile anamwambia.."You think i don't know you huh?"

Jmushi,

Hata mimi bado nina makovu ya mabomu ya FFU ambayo walikuwa wanampiga Mrema bila kujali kuwa wanatupiga hata sisi watoto wadogo tuliokwenda kumsikiliza.

Mkapa ndiye amehusika moja kwa moja na kampeni ya kumdhoofisha Mrema na upinzani Tanzania kwa ujumla.
 
Mwafrika wa kike Mkapa ana roho mbaya jamani!Yeye na Mahita ni kama mashetani!yani nilikuwa najiuliza hivi kweli hawa ni watanzania wenzetu kweli ama ni nini hasa kinachotufanya tuwe tofauti hivyo?Do we have to be ruthless in order to be leaders?
Mkapa keshatunyanyasa sana ndani ya nchi yetu..hiyo haikutosha..sasa akaamua hata kutununua na kutumiliki sisi watanzania kwa kushirikiana na mabepari!
Kutuibia na kuwaacha wananchi wakiteseka kwa magonjwa na njaa!Ni wazi kuwa hana ubinadamu kabisa na ndio maana akawa anatoa amri za kidikteta licha ya kwamba hakuna sheria iliyokuwa ikivunjwa!HALAFU KUNA WATU WANATHUBUTU KUSEMA KATIBA ISIBADILISHWE!
 
Long life Mrema, watanzania tutakumbuka daima utumishi wako Serikalini na Uzalendo mkubwa uliouonyesha kwa nchi yetu, Mungu akubariki. Endelea kupigana, kuwaandaa vijana achana na wanao kukebehi.

Wana JF sioni kama ni busara kumdhihaki Mrema eti suti.., anamabaka.., amekosa ruzuku.., utadhani anatumia AVR nk tulitaka awe fisadi? tuwatie moyo viongozi waadilifu na wazelendo.
 
Haya wakuu tumewasikia, lakini zile dhahabu alizokamata airport zilienda wapi? Na wale mafisadi aliokuwa akikutana nao sana kwa siri kule Narobi akiwa waziri walikuwa na mission gani kwa taifa letu? Nyumba nzuri kuliko hata ya Mengi huko Kibororoni ameipataje?

Ni kweli kwamba kwa standard zetu za bongo za kuuma na kupuliza, Mrema stands very tall among others, lakini angalau alipiga kelele kidogo, na pia atakuwa na bahati sana ki-afya maana yule dada aliyekuwa mbunge wa chama chake, ambaye baadaye alirukia mtandao sio siri kuwa anaumwa,

Otherwise, kwa standard zetu za kibongo, kiuongozi Mrema stand tall.

Ahsante Wakuu!
 
Jmushi,

Hata mimi bado nina makovu ya mabomu ya FFU ambayo walikuwa wanampiga Mrema bila kujali kuwa wanatupiga hata sisi watoto wadogo tuliokwenda kumsikiliza.

Mkapa ndiye amehusika moja kwa moja na kampeni ya kumdhoofisha Mrema na upinzani Tanzania kwa ujumla.
Pole sana Mwafrika wa kike!Ndio historia ya ukombozi wa nchi yetu kutoka kwenye mikono ya mafisadi!
Mabomu tuliyapata kweli kweli na kumsukuma sana tu mzee wa Kiraracha!
Tunamwombea Amani mzee wetu na tunamuomba asikate tamaa kwenye mapambano aliyosaidia kuyaimarisha akiwa upinzani na hata uzalendo aliouonyesha pale alipokuwa na madaraka ndani ya chama tawala!Nafasi ya kuwa fisadi alikuwa nayo kama Mramba na wengineo!But he chose the right path and he's on the right side of the History!HE CHOSE THE SIDE OF THE PEOPLE!
 
Mrema hawezi kupigwa chenga na lugha, ana degree (sijui ya nini vile!!!) aliipata online. Au walikuwa wanamfundisha kwa kiswanglish?

hiyo ya mrema kutojua kingereza ilikuwa propaganda..mrema mwaka 1995 alikuwa akihojiwa na bbc na VOA english service na alikuwa akiongea vema tu...

zaidi ya hiyo degree ya online ambayo hatuihesabu...mrema anayo shahada ya propaganda na ushushu ambayo hakuitaja..na aalikuwa senior trainer pale malindi ....na later mkurugenzi wa usalama ccm.....so yote hiyo kuhusu lugha ilikuwa sehemu ya propaganda
 
..... Nyumba nzuri kuliko hata ya Mengi huko Kibororoni ameipataje?....

Heshma Mkuu FMES,
Hapa umenichanganya kidogo, Mrema ana nyumba Kiboriloni? Na Mengi pia ana nyumba Kiboriloni? Then ya Mrema ni nzuri kuliko ya Mengi?
Halafu suala l a dhahabu si ziliwahusu watu wa karibu na mkuu wake enzi hizo?
Mkuu nisaidie nisichanganyikiwe zaidi.
 
Kwa kuwa mzee wa Kiraracha amelitumikia taifa kwa unyenyekevu wa hali ya juu!

Na kwa kuwa Mzee wa Kiraracha ameshapata mtambo mpya wa kurusha mabomu tena kwa masafa marefu zaidi kuliko yale ya kwake. Na yenye impact kubwa kwa taifa.

Na kwa kuwa mzee wa Kiraracha anaelekea kuwa Kisukari kina msumbua.

Naomba kutoa hoja kwamba JF tumwombe mzee wa kiraracha sasa apumzike kidogo kwenye siasa kwa heshima zote kabisa tena akiwa kama shujaa wetu kwa kuwa tunampenda na tunamtakia maisha mema na ya munga mrefu.

Mungu ibariki Tanzania
Mungu mubariki mzee wa Kiraracha
 
Status
Not open for further replies.

Similar Discussions

Back
Top Bottom