Tetesi: Mjengo uko sokoni

Tegelezeni

JF-Expert Member
Dec 31, 2009
268
124
Habari ambazo hazijathibitishwa, zinabainisha kwamba Mjengo huu uko sokoni na mnunuzi ameshapatikana. majadiliano ya hatua za mwisho yameshafikiwa na si muda mrefu mjengo utabadilishwa tena jina kwa mara ya nne.....Ilianza kama Sheraton, wakaja Legacy Hotel ya South Africa, kisha Movenpick, baadae sijui wanunuzi watakuja na jina gani.....................
 
Attachments

  • Jengo.JPG
    Jengo.JPG
    34.2 KB · Views: 95
naomba kuuliza na nielimishwe ipasavyo, kwanza kabisa sheraton, movenpick, kempinsik, na zingine nyingi kama vile accor ni chain ambazo zinamiliki hotel mbalimbali, kwa mfano, mbongoi akataka kujenga hotel yake na akaamua iitwe mbongo luxury hotel, ni lazima atalazimika kutafuta management inayofaa kuendesha hotel yake,( FRANCHISE) kwa hiyo basi anaweza kuchagua mojawapo au nyingine nyingi ambazosijataja hapo juu, mfano kilimanjaro hotel imemaliza mkataba wake na Kempinski , JE NAPENDA KUULIZA HUWA WANAUZA HILO JENGO AU WANABADILISHA MANAGEMENT YA HOTEL?
 
Ukweli ni kwamba bado kuna wingu zito la uelewa kwa baadhi ya WaTZ kuhusiana na swala zima la FRANCHISE, kwa sababu wengi huchanganya kati ya Franchise na uuzwaji wa property. kwa mfano ilijengwa Hotel na wafanyabiashara wa Kitanzania wakishirikianan na Wa-Russia ambapo waliunda kampuni wakaiita TANRUSS ikiwa ndio mmiliki wa jengo lakini Hotel ikaitwa Sheraton, kwa sababu ilikuwa ikiendeshwa na menejimenti ya chain ya Sheraton........... Baada ya TUNRUSS kutoridhishwa na namna menejimenti ya Sheraton ilivyokuwa ikiendesha Hotel hiyo wakaitimua Kimafia na kuisimika menejimenti ya Legacy Hotel ya kule South Africa, lakini wakaamua kuweka Property name ili wasije wakapoteza Identity kama wakibadilisha menejimenti kwa mara nyingine. Kwa hiyo ikaitwa Royal Palm Hotel. na kunzia hapo Hotel ikajulikana kwa jina la Legacy Royal Palm Hotel. baada ya miaka kadhaa TUNRUSS wakaamua kuuza mjengo kwa Mwana wa Mfalme wa Saudia Walid BinTalal kwa silimia 99 huku TANRUSS wakibakiwa na asilimia 1 ambapo umiliki ukahamia kwenye kampuni ya mwana huyo wa Mfalme iitwayo Kingdom Hotel Investment. Hotel ilikabidhiwa kwa menejimenti ya Movenpick ambapo mwana wa mfalme ana hisa zaizokadiriwa kufikia asilimia 36 katika Chain ya Movenpick. Na sasa Mwana wa Mfalme ameuweka mjengo huo sokoni kwa mara nyingine.................

Labda sasa wana sheria watusaidie kutueleimisha kama Wafanyakazi waliofanya kazi tangu Sheraton Mpaka sasa wanayo mafao yoyote au wataendelea na kazi wakiwa na mwajiri mpya bila kulipwa mafao yao?

ANGALIZO: Ikumbukwe kwamba Hotel ina miaka 16 sasa tangu ifunguliwe hapo mnamo mwaka 1995
 
Back
Top Bottom