Utajiri wa Magofu ya Rapta

Mugabonihela

JF-Expert Member
Dec 12, 2022
299
1,731
THE WEALTH OF RAPTA RUINS
(Get Rich or Die Tryin)

Msimuliaji: LUDOVIC MASSAWE

PROLOGUE/DIBAJI

Mji wa rapta ni mji uliozama baharini kisiwani mafia kwa zaidi ya miaka 2000. Unaweza kua mji mgeni Kwa baadhi ya watu, lakini wengi mnaweza kua mmepata kuusikia uwepo wa mji huu wa kale pembezoni mwa pwani ya Africa mashariki. Wapo wanaodai mji huu unapatikana maeneo ya rufiji kwa sasa na wapo wanaodai mji huu unapatikana pembezoni mwa kisiwa cha mafia. Je, ni nani yupo sahihi?

Mji huu ulipata kuwepo mwanzoni mwa karne ya 1 na imepita zaidi ya miaka 1600 mpaka 2000 tangu kuwepo kwa mji huu. Unaaminika kuwa mji wa kwanza tajiri barani Africa na pia ni miongoni mwa miji kumi na tano inayopatikana chini ya maji. ukiacha miji kama vile Thonis-Heracleion na Alexandria iliyopo Egypt, Yonaguni Jima (Japan), Port Royal (Jamaica) Dwarka (India), Pavlopetri iliyopo south-western Greece, Villa Epecuen (Argentina) nk.

Tofauti na ilivyo kwa watanzania na wakazi wa Africa mashariki wakiwemo wana archeologia. Wengi wamechelewa kuzipata habari za mji huu, mimi nilizipata habari hizi nje kabisa ya ukanda huu. Nilizipata habari hizi nikiwa jiji la Tehran uko inchini Iran (uajemi ya kale) ndani ya maktaba ya taifa (National Library of the Islamic Republic of Iran) iliyoanzishwa mwaka 1937 ikiwa na zaidi ya items milion 15 ndani yake.

Wakati nafika Iran nilikua nikitokea nchini Colombia na Peru kwenye mashamba ya koka (coca plantations). kwa wasiojua koka leaf ndio mmea unaotumika kutengeneza madawa ya kulevya aina ya Cocaine kupitia mchakato mrefu. Na ugumu wa ku control uzalishaji wa cocaine unasababishwa au unatokana na kushindwa kuthibiti chemicals zinazotumitumika kwenye mchakato huo kwani ni chemicals za kawaida zinazotumiwa kila siku kwenye matumizi ya binadamu.

Mfano; ku process coca leaf kuwa coca paste mpaka kupata cocaine base na HCI zinatumika chemicals kama, Sulfuric Acid, Sodium Bicarbonate, Sodium Hydroxide, benzene, Potassium Permanganate, Dichromate, Ammonia Hydroxide, Sodium Hydroxide, Methyl Ethyl Ketone na kerosene. Tutajuzana mengi kuhusu cocaine hapo mbele tukiendelea na simulizi.

Sasa basi Niliwezaje kufika Colombia, Peru kisha Iran na miji mingine mikubwa duniani? Niliwezaje kuzisikia habari za mji wa rapta? nani alinipa habari hizi? na mji huu wa rapta una utajiri kiasi gan ndani yake? Nilifikaje rapta na kwa msaada wa technologia gan nilifanikisha zoezi langu? Kipi kilisababisha mji huu kuzama baharini?

Swali lingine la msingi, wageni wa kwanza wa pwani ya Africa mashariki walikua ni warumi na wachina kabla ya waarabu na waajemi, sasa imekuaje details za rapta zilizoandaliwa na warumi zikafika Iran (Persian gulf) zilifikaje huko?

Najua baada ya kutaja wachina wengi mtajiuliza maswali lakini msijali tutaona ushahidi wa uwepo wa wachina ndani ya mji wa rapta. 90% ya wachunguzi wa mji huu wanatumia taarifa za warumi zilizoandaliwa na Claudius Ptolemaeus (Claudio Ptolemy). Je wana fahamu kua details hizo kabla ya kuwafikia zilishatumiwa na waajemi wa kale Na kuna uwezekano taarifa hizo zilichakachuliwa!?

Je! Mzungu bwana Alan Sutton (mzamiaji) aliyegundua kuta za rapta akiwa kwenye helicopter hivi karibuni, ilikua ni bahati mbaya tu au na yeye ni moja ya wale treasure hunters ila hajaliweka hili wazi?
Ungana nami kwenye simulizi hii ya kuvutia ili kupata majibu ya maswali yote na kwa hakika utajifunza mambo mengi ndani yake.

SEHEMU YA 01

Mgomo sengerema secondary

Wakati unajiuliza Niliwezaje kufika Colombia, Peru na kisha Iran unatakiwa kujua safari yangu ya jasho na damu pamoja na misukosuko mingi ilianzia shule ya sekondari ya sengerema nikiwa kidato cha sita. Kwa waliopata kupita shule hii wanaweza kua mashihidi kwa namna shule hii ilivyokua ya kikomando yaan wenyewe tulikua tunaita late-summer boot camp.

Kwa haraka haraka tu ni shule aliyowahi kufundisha hayati magufuli kabla hajawa waziri na kisha raisi. Nadhani umeanza kupata picha ilikua shule ya aina gani, Ni shule ambayo kila mtu alikua jeuri kuanzia headmaster mpaka mpishi wa jikoni. Wakati nikiwa hapo tuliwahi kushuhudia kesi nyingi ngumu na za ajabu kama wanafunzi kukutwa na kombati za jeshi full set. Kuna mengi kuhusu sengerema ambayo hatuyajui nitawaeleza machache tu na ni kwa namna gani safari yangu ilianzia hapo.

Nilifika hapo kwa mbinde huku o'level nikitokea Ngerengere kizuka sekondari baada ya kufukuzwa MAKOKO SEMINARY, kiukweli nilikua mtoto mtukutu na jeuri ilifika hatua mzee wangu mzee MASSAWE alisema hizi tabia nimeridhi kutoka kwa babu yangu. Ambae alikimbia nchi baada ya kuhusika kwenye matukio mawili, lile la utekaji wa ndege ya ATC mwaka 1982 February kwa makusudi ya kushinikiza mwalimu ajiuzulu na lile jaribio la kuangusha serikali ya mwalimu Nyerere la mwaka 1980's. Babu Yangu alikua ni miongoni mwa wale maafisa wakuu waliosuka ule mpango, Tuachane na babu na tuludi zetu sengerema.

Tukio la mgomo ndio lililoanzisha safari yangu Na lilipangwa usiku baada ya mlo wa jioni, vidume baada ya kushiba dona maharage pamoja na nchima boyo akili zikatutuma tufanye mgomo usiku wa siku hiyo. Sababu za mgomo zilikuwepo japokua hazikua na mashiko sana naweza sema ni ujana tu ndio ulikua unatusumbua ukiongeza na zile bangi zakuvutia maporini (chaka).

Kama kawaida mzee baba siku hiyo ya mgomo niliwekwa kitengo cha TANESCO, yani niliambiwa ikifika saa 2 kamili usiku ni hakikishe shule nzima umeme umezima. Hii ilitokana na ujuzi wangu wa mambo ya electronics na wiring za ujanja ujanja za mabwenini especially bweni la kimweri na sokoine.

Basi ilipotimu saa 2 kamili nilihakikisha Giza limetanda shule nzima kasoro nyumba za walimu tu, na kazi yangu iliishia hapo na Majukumu mengine yaliyobaki yalikua kwa wenzangu wahamisishaji kuhakikisha kila mmoja anashiriki. Lakini pia kuna jamaa mmoja wa mwananyamala yeye alikua na dumu la petrol lita 5 sijui alilitolea wapi usiku ule huyu bwana kazi yake ilikua kuhakikisha moto unawaka maeneo yote yaliyopangwa kuchomwa.

Mpaka kufika saa nne usiku stationary ya mwalimu wetu siwezi kumtaja jina ilikua haitamaniki na baadhi ya walimu walikimbiza familia zao mjini. 90% ya wanafunzi tulikua michepuo ya sayansi yani PCM, PCB na combination nyingine hivyo tulikubaliana kutokugusa maabara wala library wala darasa, wachache sana walikua arts na cha ajabu kwenye hii shule watu wa arts walikua wamestaarabika ukilinganisha na sayansi.

Shule imejengwa mlimani kabisa kiasi kwamba ilipofika saa 4 na nusu usiku defender ilionekana ikipandisha na wote tukapotelea maporini. Jambo la kufurahisha ni kwamba askari hawakufanikiwa kukamata ata mwanafunzi mmoja kati ya wanafunzi 800. Wengi waliishia kulala kwenye miembe na majaruba ya mpunga kwa usiku huo kwani shule ilizungukwa na makachero wakutosha. Lakini massawe nikasema siwezi lala juu ya mti Kama tumbili, usiku ule ule nikaanza safari ya kuelekea mjini mitaa ya soko mjinga.

Pale mjini kuna binti alikua anasoma shule ya jilani inaitwa NTUNDURU alikua amepanga ghetto. Can you imagine! Shule ya boarding na bado amepanga mtaani! asee. Merry alikua ni hatari sana mnyaturu yule wa singida.

Mishale ya saa tano usiku nilikua mlangoni kwa merry nabisha hodi, baada ya dikaka 3 alifungua mlango nikaingia. Walikua wawili yeye na mwenzie anaitwa jane. Ndani kulikua na chupa za safari na mzinga mkubwa wa konyagi, nilipoingia nilihisi uwepo wa mwanaume mule ndani na baadae niliona funguo za sun LG na vipisi vya sigara. Ila sikujali sana nilijitupa kitandani nikapitiwa na usingizi mzito uliotokana na uchovu wa mgomo na mbio za kuwakimbia field Force.

Nilikuja kustuka saa kumi alfajiri na mlio wa pikipiki uliokua unamrudisha merry ambae alikuja yupo hoi na kwa haraka niligundua jane amebaki na yule kidume wa jana.

Merry akilewa bia hua zinashuka chini, waliosoma cuba wamenielewa hapa. Hivyo baada ya kuingia ndani hakutaka story zaidi ya kutupa nguo kwenye kila kona ya chumba hicho kama mwehu. Na mimi kutokana na nilikua namjua vizuri haikusumbua kujua anataka nini zaidi ya kuanza mtanange wa kukata na shoka uliochukua zaidi dakika 90 kama finally ya Argentina vs France kule Qatar.

Tulikuja kuamshwa na mwanga mkali wa jua la saa 4 asubuh uliokua unapita dirishani Huku merry akiwaza supu. Ilituchukua muda mfupi kujiandaa kwenda maeneo ya stendi kupata supu, nilishangaa baada ya kufika stendi nilikutana na wanafunzi wenzangu wakiwa na mabegi wengine ma tranka. Nilipowauliza walijibu shule imefungwa kwa muda wa week 3 na tutapewa utaratibu wa jinsi ya kurud tukiwa nyumbani. Hapo nilianza kuwaza namna ya kurud nyumbani huku mizigo yangu yote imebaki shule na hakuna mwanafunzi anaeruhusiwa kwenda tena shule kwa muda huo.

Basi bwana tulipata supu na mrembo merry kisha tukarud zetu ghetto kupumzika, nakumbuka ilikua siku ya alhamisi hivyo merry hakuenda shule kutokana na hangover na tulishinda ndani siku nzima mpaka kesho yake asubuhi.

Siku ya pili akili ilivurugika zaidi baada ya kupata habari kwenye vituo vya habari viwili tofauti kuhusu mgomo wa sengerema, kituo cha kwanza ni redio sengerema ilitangaza wanafunzi kumi na tisa (19) wamefukuzwa na wengine kusimamishwa masomo kwa muda usiojulikana. Hivyo hivyo kwa redio free Africa na gazeti la mwananchi, gazeti hili lilitoa majina ya waliofukuzwa na mimi nilikua jina la kwanza kwenye ile list.

Niliwaza namwambia nini mzee massawe ambae alichoshwa na tabia zangu.

Akili ikanituma kuangalia upande wa pili wa maisha na sio kukomaa na shule, niliamini siku Moja nikiludi home na pesa nyingi mzee massawe atanikubali sana jembe lake.

Baada ya kupata wazo la kutoendelea na shule nikaanza kuwaza natakiwa nianzie wapi kutafuta pesa. Apo apo akili ikaniambia dar ndio sehemu pekee naweza tengeneza pesa nyingi, lakin kwa bahati mbaya sikua mzoefu wa mji huo na wala sikutakiwa kufikia kwa ndugu yoyote na bado sina nauli ya kufika huko. Niliamini nikifika Mwanza kwenda dar itakua rahisi hivyo nikaanza mchakato wa kufika mwanza (nyegezi).

Nilimshirikisha merry kwa makusudi ili anisaidie nauli ya kufika nyegezi kwani kutoka sengerema hadi nyegezi ni kiasi cha shilingi 4000 tu. Na kwa maelezo ya merry aliniomba tufike stendi kuna mtu atampatia tukifika hapo.tukiwa stendi Merry alimfuata jamaa mmoja bonge hivi anadeal na tickets pale stendi, Kwa haraka niligundua huyo ndio sponsor waliekua nae jana. Sikujua waliongea nini na merry ila merry aliniambia tusubiri kuna coaster inatokea katolo ndio tutaenda nayo mwanza.

Haikuchukua muda mrefu ile coaster ilifika na walipanda abiria kadhaa kisha bonge akamwambia konda hawa ndio wadogo zangu wanaoenda nyegezi. na sisi tulipanda tukaanza safari, nilishangazwa na uwepo wa Merry kwenye safari sikujua na yeye anaelekea wapi kwani hakua na sababu ya kutoka sengerema siku hiyo kwani masomo kwa upande wake yalikua yanaendelea. Merry alikua mwanafunzi wa kidato cha nne NTUNDURU sekondari na ile siku tumeshinda ote ndani nilitumia fursa kumfundisha almost topics tatu za msingi.

Sasa tukiwa ndani ya coaster kuelekea nyegezi nilimuuliza kwanini na yeye ameamua kusafiri, majibu yake yalikua ni kwamba ana muda mrefu hajafika mjini mwanza hivyo alitaka kwenda kuosha macho kwa muda kisha baadae ataludi sengerema.

Nilipata nafasi ya kupiga stories na konda ndipo niligundua wametokea geita walipeleka msiba na hapo wanarudi dar es salaam. Niliamini safari yangu kufika Dar es Salaam imerahisishwa nachotakiwa ni kuwaza namna gani naweza kushawishi jamaa ili aniruhusu nisafiri nae.

Majadiliano na konda yalikua hivi.

Konda:"dogo! we ni mwanafunzi Nini? Jana tukiwa na msiba tulibeba madogo kama watatu hivi wakiwa na suruali nyeusi na tishet za bluu kama ulivyovaa wewe"

Merry alijibu fasta kama ameulizwa yeye.

Merry: ndio sisi ni wanafunzi, ila tumerudishwa nyumbani ghafla sababu ya mgomo wa juzi usiku.
(konda hakujua kama sengerema ni shule ya wavulana pekee)

Konda: kama wanafunzi wenyewe ndio nyinyi hiyo shule kazi ipo. Kwaiyo nyumbani ni wapi??
Nilitumia swali hilo kama fursa ya kufanikisha misheni yangu.

Mimi: home dar na hatujatumiwa nauli sijui tunafikaje?

Konda: we mtoto wa kiume jitahidi upambane.

Jibu lile lilinikatisha tamaa ya kuendelea na maongezi yale. Haikuchukua muda tulikua tumefika kivukoni busisi. Abiria wote tulishuka na kupanda kivuko, lakini nilifurahi baada ya kumuona konda anajisogeza kwa merry na kujiongeresha. nilijua kwa ujanja wa merry anaweza kufanikisha safari yangu kirahisi sana.

Baada ya kufika upande wa pili tulirudi ndani ya coaster na kuendelea na safari na wakati huu merry aliniambia ameshampanga konda hivyo tutafika wote dar es salaam.

Merry alikua binti mjanja sana na anamacho Fulani akikuangalia tu unajua atakua fundi, hahahahahaha kwa wale tuliopita sengerema miaka ile najua mtakua mnamkumbuka kwani alikua maarufu sana. Especially tukienda shuleni kwao kwa ajili ya michezo wengi walimtolea macho, nitakuja kueleza nilimpataje hapo baadae.

Baada ya kufika nyegezi tukijiandaa na safari ya kuanza kuitafuta dar es salaam nilishangaa konda aliniita na kunipa buku tano nikatafute msosi. Na kisha konda na merry walipotelea kusiko Julikana, Nilijua merry ameshafanya yake tayar niliishia kuitunza ile buku tano nikiamini itanisaidia mbele ya safari kwani sikua na chochote mfukoni.

Baada ya nusu saa merry na konda walirudi huku nikimuona merry na vifurushi vya kutosha bila shaka ilikua ni misosi na kimoyomoyo nikasema merry hajawahi kuniangusha ata siku moja. Tulikaa kwenye siti na kuendelea na safari Huku tukipiga msosi mzito nakumbuka ilikua ni Sato na chipsi kavu za kutosha.

Mimi: merry ulisema unaishia nyegezi vipi mbona unaendelea na safari?

Merry: sijawahi kufika Dar es Salaam, nadhani hii ni fursa ambayo sitakiwi kuichezea. Najua nipo na wewe hakuna kitachoharibika nitakaa week moja kisha nitarudi shule.

Daaaaah!!!!! Nilihisi mwili unakufa ganzi nilitaman kumwambia Mimi mwenyewe sina pa kufikia ila nikapiga moyo konde. tukaendelea na safari yetu huku stories zikiwa nyingi. Merry pekee ndio alikua na simu Mimi kilichokua mfukoni ni ile buku tano, kibiriti cha gesi na scientific calculator tu.

Baada ya safari ya muda mrefu wote tulipitiwa na usingizi, safari ile ni ya kutwa nzima kwani nakumbuka tuliingia morogoro usiku wa saa tano tena hiyo ilikua ni baada ya abiria kulalamikia speed ya gari ilikua kali mno. Tulipotoka moro baada ya kufika maeneo ya chalinze nilipitiwa tena na usingizi mzito. Nilikuja kushtuliwa na konda akidai alitusahau tumeshaingia mjini mda mrefu.

Konda: nyie mnashukia wapi tumeingia Dar es Salaam tayari. Lile swali lilikua gumu kwangu kwani sikua ata najua tunapoelekea baada ya kufika dar. Kwa Dar es Salaam nachojua ni ubungo tu hivyo nilimjibu tunashuka ubungo.

Konda: ubungo tumepita tayari sisi tunaelekea mbagara, shukeni hapa mrudi vertinary mkapande gari za ubungo.

Kiukweli sikumuelewa konda ata kidogo kila alichonambia kilikua kipya ila sikutaka kuonyesha kutokujua mbele ya Merry hivyo tulishuka. Tulishushwa eneo moja lina mataa na ilikua saa saba na nusu usiku, nikiwa sijui cha kufanya Merry alianza kulalamika maumivu makali ya tumbo. Nilijua tu itakua njaa kwani ni muda mrefu hatujapata chakula, baada ya kupepesa macho huku na kule niliona sehemu kwa mbaali kuna watu na mataa mengi yanawakawaka nikajua fika hapo patakua na bar hivyo hatuwez kosa msosi.

"Massawe hapa na kwenu kuna umbali gani?" Lilikua ni swali la Merry na mimi sikuona haja ya kuendelea kumficha ukweli, nilimueleza kila kitu kama nimeenda huko kutafuta maisha na nimeachana rasmi na masomo baada ya kufukuzwa shule na nilimueleza siwezi kurudi moshi kwa mzee massawe hatonielewa kabisa.

Kwa maumivu ya tumbo aliyokua anapitia Merry hakutaka kuendelea na mjadala nilimuona akiongoza kwenye lile eneo tuliloliona likiwa na watu wengi usiku ule. Baada ya kufika eneo Hilo niliona maandishi makubwa yakiwakawaka yameandikwa SUGAR REY. Ni dhahiri ilikua ni bar, nilishangazwa na mavazi ya wadada wa eneo hilo na sio mimi tu ata merry pia.

"Hhhmmm kweli hii ndio dar es salaam ninayoisikia kila siku" yalikua ni maneno ya Merry. Tukiwa bado tumeduwaa alikuja bodaboda

Bodaboda: vipi mnaenda?

Mimi: hapana tumefika bro.

Bodaboda: punguzeni kushangaa basi.

Tulisogea mpaka eneo lile nikiamini hatuwezi kukosa chakula ukizingatia nilikua bado na lile buku tano la konda.

Tulipofika tu merry alimfuata Binti mmoja aliekua amekaa pembeni akiwa kwenye pozi Kama anamsubiri mtu na waliongea baadae wakafatana sikujua wameenda wapi. Nilijisogeza kwa jamaa wa bodaboda wakiwa na makoti makubwa nikajiunga kupiga nao story huku nikimsubiri Merry.

Mimi: bro samahan hawa wadada mbona wapo wengi na wana mishe gani apa mbona wamevaa kiasala asala?

Bodaboda: hao wanajiuza mjomba. We mgeni nini?

Mimi: ndio mi mgeni.

Bodaboda aliniangalia tu na hakuendelea kuongea chochote Zaidi ya kuwafata abiria wawili waliokua mbele yake. Baada ya muda kidogo hivi nilimuona merry akiludi eneo nililokuwepo.

Mimi: merry punguza kujifanya unamjua kila mtu apa sio singida hii dar rafiki angu.

Merry: lile tumbo lilikua ni la siku zangu na sio njaa kama ulivyohisi hivyo nilienda kwa yule mdada kuona kama ata nipa msaada wowote si unajua sijatembea na chochote. Lakini pia nimemueleza changamoto niliyonayo kwamba hatuna pa kulala na ndio tumefika mjini.

Mimi: akasemaje?

Merry: kasema atanisaidia kwa leo sehemu ya kulala ila kuanzia kesho nitajua pa kwenda, lakini pia amenieleza kama sina ndugu kabisa atanionyesha kazi ya kufanya na tutakua tunachangia wote kulipa pango la nyumba hivyo mi nimeona niende nae tu.

Kiukweli sikutamani merry aondoke na yule dada lakini sikua na jinsi kwani hata hivyo sikua na sehemu yoyote ya kumpeleka. Merry alinikabidhi simu yake ili iwe rahisi kunipata siku inayofuata kwani alikua anajua sikua na simu. Tuliagana na merry na mimi nikabaki eneo hilo nikiwaza naelekea wapi kwa usiku huo wala sikutaka kujutia maamuzi yangu ata kidogo niliamini nipo sahihi kabisa.

Tunaendelea baadae usikae mbali.

GridArt_20230408_143834079.jpg
 
Attachments

  • GridArt_20230408_143834079.jpg
    GridArt_20230408_143834079.jpg
    65.9 KB · Views: 70
THE WEALTH OF RAPTA RUINS
(Get Rich or Die Tryin)

Msimuliaji: LUDOVIC MASSAWE

NB: SIMULIZI HII IMEAMBATANISHWA NA BAADHI YA PICHA ZINAZOTUMIKA KUELEZEA MATUKIO, HURUSIWI KUTUMIA PICHA HIZO MAHALI POPOTE.

PROLOGUE/DIBAJI

Mji wa rapta ni mji uliozama baharini kisiwani mafia kwa zaidi ya miaka 2000. Unaweza kua mji mgeni Kwa baadhi ya watu, lakini wengi mnaweza kua mmepata kuusikia uwepo wa mji huu wa kale pembezoni mwa pwani ya Africa mashariki. Wapo wanaodai mji huu unapatikana maeneo ya rufiji kwa sasa na wapo wanaodai mji huu unapatikana pembezoni mwa kisiwa cha mafia. Je! ni nani yupo sahihi?

Mji huu ulipata kuwepo mwanzoni mwa karne ya 1 na imepita zaidi ya miaka 1600 mpaka 2000 tangu kuwepo kwa mji huu. Unaaminika kuwa mji wa kwanza tajiri barani Africa na pia ni miongoni mwa miji kumi na tano inayopatikana chini ya maji. ukiacha miji kama vile Thonis-Heracleion na Alexandria iliyopo Egypt, Yonaguni Jima (Japan), Port Royal (Jamaica) Dwarka (India), Pavlopetri iliyopo south-western Greece, Villa Epecuen (Argentina) nk.

Tofauti na ilivyo kwa watanzania na wakazi wa Africa mashariki wakiwemo wana archeologia. Wengi wamechelewa kuzipata habari za mji huu, mimi nilizipata habari hizi nje kabisa ya ukanda huu. Nilizipata habari hizi nikiwa jiji la Tehran uko inchini Iran (uajemi ya kale) ndani ya maktaba ya taifa (National Library of the Islamic Republic of Iran) iliyoanzishwa mwaka 1937 ikiwa na zaidi ya items milion 15 ndani yake.

Wakati nafika Iran nilikua nikitokea nchini Colombia na Peru kwenye mashamba ya koka (coca plantations). kwa wasiojua koka leaf ndio mmea unaotumika kutengeneza madawa ya kulevya aina ya Cocaine kupitia mchakato mrefu. Na ugumu wa ku control uzalishaji wa cocaine unasababishwa au unatokana na kushindwa kuthibiti chemicals zinazotumitumika kwenye mchakato huo kwani ni chemicals za kawaida zinazotumiwa kila siku kwenye matumizi ya binadamu.

Mfano; ku process coca leaf kuwa coca paste mpaka kupata cocaine base na HCI zinatumika chemicals kama, Sulfuric Acid, Sodium Bicarbonate, Sodium Hydroxide, benzene, Potassium Permanganate, Dichromate, Ammonia Hydroxide, Sodium Hydroxide, Methyl Ethyl Ketone na kerosene. Tutajuzana mengi kuhusu cocaine hapo mbele tukiendelea na simulizi.

Sasa basi Niliwezaje kufika Colombia, Peru kisha Iran na miji mingine mikubwa duniani? Niliwezaje kuzisikia habari za mji wa rapta? nani alinipa habari hizi? na mji huu wa rapta una utajiri kiasi gan ndani yake? Nilifikaje rapta na kwa msaada wa technologia gan nilifanikisha zoezi langu? Kipi kilisababisha mji huu kuzama baharini?

Swali lingine la msingi, wageni wa kwanza wa pwani ya Africa mashariki walikua ni warumi na wachina kabla ya waarabu na waajemi, sasa imekuaje details za rapta zilizoandaliwa na warumi zikafika Iran (Persian gulf) zilifikaje huko?

Najua baada ya kutaja wachina wengi mtajiuliza maswali lakini msijali tutaona ushahidi wa uwepo wa wachina ndani ya mji wa rapta. 90% ya wachunguzi wa mji huu wanatumia taarifa za warumi zilizoandaliwa na Claudius Ptolemaeus (Claudio Ptolemy). Je wana fahamu kua details hizo kabla ya kuwafikia zilishatumiwa na waajemi wa kale Na kuna uwezekano taarifa hizo zilichakachuliwa!?

Je! Mzungu bwana Alan Sutton (mzamiaji) aliyegundua kuta za rapta akiwa kwenye helicopter hivi karibuni, ilikua ni bahati mbaya tu au na yeye ni moja ya wale treasure hunters ila hajaliweka hili wazi?
Ungana nami kwenye simulizi hii ya kuvutia ili kupata majibu ya maswali yote na kwa hakika utajifunza mambo mengi ndani yake.

SEHEMU YA 01

Mgomo sengerema secondary

Wakati unajiuliza Niliwezaje kufika Colombia, Peru na kisha Iran unatakiwa kujua safari yangu ya jasho na damu pamoja na misukosuko mingi ilianzia shule ya sekondari ya sengerema nikiwa kidato cha sita. Kwa waliopata kupita shule hii wanaweza kua mashihidi kwa namna shule hii ilivyokua ya kikomando yaan wenyewe tulikua tunaita late-summer boot camp.

Kwa haraka haraka tu ni shule aliyowahi kufundisha hayati magufuli kabla hajawa waziri na kisha raisi. Nadhani umeanza kupata picha ilikua shule ya aina gani, Ni shule ambayo kila mtu alikua jeuri kuanzia headmaster mpaka mpishi wa jikoni. Wakati nikiwa hapo tuliwahi kushuhudia kesi nyingi ngumu na za ajabu kama wanafunzi kukutwa na kombati za jeshi full set. Kuna mengi kuhusu sengerema ambayo hatuyajui nitawaeleza machache tu na ni kwa namna gani safari yangu ilianzia hapo.

Nilifika hapo kwa mbinde huku o'level nikitokea Ngerengere kizuka sekondari baada ya kufukuzwa MAKOKO SEMINARY, kiukweli nilikua mtoto mtukutu na jeuri ilifika hatua mzee wangu mzee MASSAWE alisema hizi tabia nimeridhi kutoka kwa babu yangu. Ambae alikimbia nchi baada ya kuhusika kwenye matukio mawili, lile la utekaji wa ndege ya ATC mwaka 1982 February kwa makusudi ya kushinikiza mwalimu ajiuzulu na lile jaribio la kuangusha serikali ya mwalimu Nyerere la mwaka 1980's. Babu Yangu alikua ni miongoni mwa wale maafisa wakuu waliosuka ule mpango, Tuachane na babu na tuludi zetu sengerema.

Tukio la mgomo ndio lililoanzisha safari yangu Na lilipangwa usiku baada ya mlo wa jioni, vidume baada ya kushiba dona maharage pamoja na nchima boyo akili zikatutuma tufanye mgomo usiku wa siku hiyo. Sababu za mgomo zilikuwepo japokua hazikua na mashiko sana naweza sema ni ujana tu ndio ulikua unatusumbua ukiongeza na zile bangi zakuvutia maporini (chaka).
Kama kawaida mzee baba siku hiyo ya mgomo niliwekwa kitengo cha TANESCO, yani niliambiwa ikifika saa 2 kamili usiku ni hakikishe shule nzima umeme umezima. Hii ilitokana na ujuzi wangu wa mambo ya electronics na wiring za ujanja ujanja za mabwenini especially bweni la kimweri na sokoine.

Basi ilipotimu saa 2 kamili nilihakikisha Giza limetanda shule nzima kasoro nyumba za walimu tu, na kazi yangu iliishia hapo na Majukumu mengine yaliyobaki yalikua kwa wenzangu wahamisishaji kuhakikisha kila mmoja anashiriki. Lakini pia kuna jamaa mmoja wa mwananyamala yeye alikua na dumu la petrol lita 5 sijui alilitolea wapi usiku ule huyu bwana kazi yake ilikua kuhakikisha moto unawaka maeneo yote yaliyopangwa kuchomwa.

Mpaka kufika saa nne usiku stationary ya mwalimu wetu siwezi kumtaja jina ilikua haitamaniki na baadhi ya walimu walikimbiza familia zao mjini. 90% ya wanafunzi tulikua michepuo ya sayansi yani PCM, PCB na combination nyingine hivyo tulikubaliana kutokugusa maabara wala library wala darasa, wachache sana walikua arts na cha ajabu kwenye hii shule watu wa arts walikua wamestaarabika ukilinganisha na sayansi.

Shule imejengwa mlimani kabisa kiasi kwamba ilipofika saa 4 na nusu usiku defender ilionekana ikipandisha na wote tukapotelea maporini. Jambo la kufurahisha ni kwamba askari hawakufanikiwa kukamata ata mwanafunzi mmoja kati ya wanafunzi 800. Wengi waliishia kulala kwenye miembe na majaruba ya mpunga kwa usiku huo kwani shule ilizungukwa na makachero wakutosha. Lakini massawe nikasema siwezi lala juu ya mti Kama tumbili, usiku ule ule nikaanza safari ya kuelekea mjini mitaa ya soko mjinga.

Pale mjini kuna binti alikua anasoma shule ya jilani inaitwa NTUNDURU alikua amepanga ghetto. Can you imagine!!! Shule ya boarding na bado amepanga mtaani! asee!!... Merry alikua ni hatari sana mnyaturu yule wa singida.

Mishale ya saa tano usiku nilikua mlangoni kwa merry nabisha hodi, baada ya dikaka 3 alifungua mlango nikaingia. Walikua wawili yeye na mwenzie anaitwa jane. Ndani kulikua na chupa za safari na mzinga mkubwa wa konyagi, nilipoingia nilihisi uwepo wa mwanaume mule ndani na baadae niliona funguo za sun LG na vipisi vya sigara. Ila sikujali sana nilijitupa kitandani nikapitiwa na usingizi mzito uliotokana na uchovu wa mgomo na mbio za kuwakimbia field Force.

Nilikuja kustuka saa kumi alfajiri na mlio wa pikipiki uliokua unamrudisha merry ambae alikuja yupo hoi na kwa haraka niligundua jane amebaki na yule kidume wa jana.

Merry akilewa bia hua zinashuka chini, waliosoma cuba wamenielewa hapa. Hivyo baada ya kuingia ndani hakutaka story zaidi ya kutupa nguo kwenye kila kona ya chumba hicho kama mwehu. Na mimi kutokana na nilikua namjua vizuri haikusumbua kujua anataka nini zaidi ya kuanza mtanange wa kukata na shoka uliochukua zaidi dakika 90 kama finally ya Argentina vs France kule Qatar.

Tulikuja kuamshwa na mwanga mkali wa jua la saa 4 asubuh uliokua unapita dirishani Huku merry akiwaza supu. Ilituchukua muda mfupi kujiandaa kwenda maeneo ya stendi kupata supu, nilishangaa baada ya kufika stendi nilikutana na wanafunzi wenzangu wakiwa na mabegi wengine ma tranka. Nilipowauliza walijibu shule imefungwa kwa muda wa week 3 na tutapewa utaratibu wa jinsi ya kurud tukiwa nyumbani. Hapo nilianza kuwaza namna ya kurud nyumbani huku mizigo yangu yote imebaki shule na hakuna mwanafunzi anaeruhusiwa kwenda tena shule kwa muda huo.

Basi bwana tulipata supu na mrembo merry kisha tukarud zetu ghetto kupumzika, nakumbuka ilikua siku ya alhamisi hivyo merry hakuenda shule kutokana na hangover na tulishinda ndani siku nzima mpaka kesho yake asubuhi.

Siku ya pili akili ilivurugika zaidi baada ya kupata habari kwenye vituo vya habari viwili tofauti kuhusu mgomo wa sengerema, kituo cha kwanza ni redio sengerema ilitangaza wanafunzi kumi na tisa (19) wamefukuzwa na wengine kusimamishwa masomo kwa muda usiojulikana. Hivyo hivyo kwa redio free Africa na gazeti la mwananchi, gazeti hili lilitoa majina ya waliofukuzwa na mimi nilikua jina la kwanza kwenye ile list.

Niliwaza namwambia nini mzee massawe ambae alichoshwa na tabia zangu.

Akili ikanituma kuangalia upande wa pili wa maisha na sio kukomaa na shule, niliamini siku Moja nikiludi home na pesa nyingi mzee massawe atanikubali sana jembe lake.

Baada ya kupata wazo la kutoendelea na shule nikaanza kuwaza natakiwa nianzie wapi kutafuta pesa. Apo apo akili ikaniambia dar ndio sehemu pekee naweza tengeneza pesa nyingi, lakin kwa bahati mbaya sikua mzoefu wa mji huo na wala sikutakiwa kufikia kwa ndugu yoyote na bado sina nauli ya kufika huko. Niliamini nikifika Mwanza kwenda dar itakua rahisi hivyo nikaanza mchakato wa kufika mwanza (nyegezi).

Nilimshirikisha merry kwa makusudi ili anisaidie nauli ya kufika nyegezi kwani kutoka sengerema hadi nyegezi ni kiasi cha shilingi 4000 tu. Na kwa maelezo ya merry aliniomba tufike stendi kuna mtu atampatia tukifika hapo.tukiwa stendi Merry alimfuata jamaa mmoja bonge hivi anadeal na tickets pale stendi, Kwa haraka niligundua huyo ndio sponsor waliekua nae jana. Sikujua waliongea nini na merry ila merry aliniambia tusubiri kuna coaster inatokea katolo ndio tutaenda nayo mwanza.

Haikuchukua muda mrefu ile coaster ilifika na walipanda abiria kadhaa kisha bonge akamwambia konda hawa ndio wadogo zangu wanaoenda nyegezi. na sisi tulipanda tukaanza safari, nilishangazwa na uwepo wa Merry kwenye safari sikujua na yeye anaelekea wapi kwani hakua na sababu ya kutoka sengerema siku hiyo kwani masomo kwa upande wake yalikua yanaendelea. Merry alikua mwanafunzi wa kidato cha nne NTUNDURU sekondari na ile siku tumeshinda ote ndani nilitumia fursa kumfundisha almost topics tatu za msingi.

Sasa tukiwa ndani ya coaster kuelekea nyegezi nilimuuliza kwanini na yeye ameamua kusafiri, majibu yake yalikua ni kwamba ana muda mrefu hajafika mjini mwanza hivyo alitaka kwenda kuosha macho kwa muda kisha baadae ataludi sengerema.

Nilipata nafasi ya kupiga stories na konda ndipo niligundua wametokea geita walipeleka msiba na hapo wanarudi dar es salaam. Niliamini safari yangu kufika Dar es Salaam imerahisishwa nachotakiwa ni kuwaza namna gani naweza kushawishi jamaa ili aniruhusu nisafiri nae.

Majadiliano na konda yalikua hivi.

Konda:"dogo! we ni mwanafunzi Nini? Jana tukiwa na msiba tulibeba madogo kama watatu hivi wakiwa na suruali nyeusi na tishet za bluu kama ulivyovaa wewe"

Merry alijibu fasta kama ameulizwa yeye,

Merry: ndio sisi ni wanafunzi, ila tumerudishwa nyumbani ghafla sababu ya mgomo wa juzi usiku.
(konda hakujua kama sengerema ni shule ya wavulana pekee)

Konda: kama wanafunzi wenyewe ndio nyinyi hiyo shule kazi ipo. Kwaiyo nyumbani ni wapi??
Nilitumia swali hilo kama fursa ya kufanikisha misheni yangu.

Mimi: home dar na hatujatumiwa nauli sijui tunafikaje?

Konda: we mtoto wa kiume jitahidi upambane.

Jibu lile lilinikatisha tamaa ya kuendelea na maongezi yale.
Haikuchukua muda tulikua tumefika kivukoni busisi. Abiria wote tulishuka na kupanda kivuko, lakini nilifurahi baada ya kumuona konda anajisogeza kwa merry na kujiongeresha. nilijua kwa ujanja wa merry anaweza kufanikisha safari yangu kirahisi sana.

Baada ya kufika upande wa pili tulirudi ndani ya coaster na kuendelea na safari na wakati huu merry aliniambia ameshampanga konda hivyo tutafika wote dar es salaam.

Merry alikua binti mjanja sana na anamacho Fulani akikuangalia tu unajua atakua fundi, hahahahahaha kwa wale tuliopita sengerema miaka ile najua mtakua mnamkumbuka kwani alikua maarufu sana. Especially tukienda shuleni kwao kwa ajili ya michezo wengi walimtolea macho, nitakuja kueleza nilimpataje hapo baadae.

Baada ya kufika nyegezi tukijiandaa na safari ya kuanza kuitafuta dar es salaam nilishangaa konda aliniita na kunipa buku tano nikatafute msosi. Na kisha konda na merry walipotelea kusiko Julikana, Nilijua merry ameshafanya yake tayar niliishia kuitunza ile buku tano nikiamini itanisaidia mbele ya safari kwani sikua na chochote mfukoni.

Baada ya nusu saa merry na konda walirudi huku nikimuona merry na vifurushi vya kutosha bila shaka ilikua ni misosi na kimoyomoyo nikasema merry hajawahi kuniangusha ata siku moja. Tulikaa kwenye siti na kuendelea na safari Huku tukipiga msosi mzito nakumbuka ilikua ni Sato na chipsi kavu za kutosha.

Mimi: merry ulisema unaishia nyegezi vipi mbona unaendelea na safari???

Merry: sijawahi kufika Dar es Salaam, nadhani hii ni fursa ambayo sitakiwi kuichezea. Najua nipo na wewe hakuna kitachoharibika nitakaa week moja kisha nitarudi shule.

Daaaaah!!!!! Nilihisi mwili unakufa ganzi nilitaman kumwambia Mimi mwenyewe sina pa kufikia ila nikapiga moyo konde. tukaendelea na safari yetu huku stories zikiwa nyingi. Merry pekee ndio alikua na simu Mimi kilichokua mfukoni ni ile buku tano, kibiriti cha gesi na scientific calculator tu.

Baada ya safari ya muda mrefu wote tulipitiwa na usingizi, safari ile ni ya kutwa nzima kwani nakumbuka tuliingia morogoro usiku wa saa tano tena hiyo ilikua ni baada ya abiria kulalamikia speed ya gari ilikua kali mno. Tulipotoka moro baada ya kufika maeneo ya chalinze nilipitiwa tena na usingizi mzito. Nilikuja kushtuliwa na konda akidai alitusahau tumeshaingia mjini mda mrefu.

Konda: nyie mnashukia wapi tumeingia Dar es Salaam tayari.
Lile swali lilikua gumu kwangu kwani sikua ata najua tunapoelekea baada ya kufika dar. Kwa Dar es Salaam nachojua ni ubungo tu hivyo nilimjibu tunashuka ubungo.

Konda: ubungo tumepita tayari sisi tunaelekea mbagara, shukeni hapa mrudi vertinary mkapande gari za ubungo.

Kiukweli sikumuelewa konda ata kidogo kila alichonambia kilikua kipya ila sikutaka kuonyesha kutokujua mbele ya Merry hivyo tulishuka. Tulishushwa eneo moja lina mataa na ilikua saa saba na nusu usiku, nikiwa sijui cha kufanya Merry alianza kulalamika maumivu makali ya tumbo.
Nilijua tu itakua njaa kwani ni muda mrefu hatujapata chakula, baada ya kupepesa macho huku na kule niliona sehemu kwa mbaali kuna watu na mataa mengi yanawakawaka nikajua fika hapo patakua na bar hivyo hatuwez kosa msosi.

"Massawe hapa na kwenu kuna umbali gani?" Lilikua ni swali la Merry na mimi sikuona haja ya kuendelea kumficha ukweli, nilimueleza kila kitu kama nimeenda huko kutafuta maisha na nimeachana rasmi na masomo baada ya kufukuzwa shule na nilimueleza siwezi kurudi moshi kwa mzee massawe hatonielewa kabisa.

Kwa maumivu ya tumbo aliyokua anapitia Merry hakutaka kuendelea na mjadala nilimuona akiongoza kwenye lile eneo tuliloliona likiwa na watu wengi usiku ule.
Baada ya kufika eneo Hilo niliona maandishi makubwa yakiwakawaka yameandikwa SUGAR REY. Ni dhahiri ilikua ni bar, nilishangazwa na mavazi ya wadada wa eneo hilo na sio mimi tu ata merry pia.
"Hhhmmm kweli hii ndio dar es salaam ninayoisikia kila siku" yalikua ni maneno ya Merry. Tukiwa bado tumeduwaa alikuja bodaboda

Bodaboda: vipi mnaenda?

Mimi: hapana tumefika bro.

Bodaboda: punguzeni kushangaa basi.

Tulisogea mpaka eneo lile nikiamini hatuwezi kukosa chakula ukizingatia nilikua bado na lile buku tano la konda.

Tulipofika tu merry alimfuata Binti mmoja aliekua amekaa pembeni akiwa kwenye pozi Kama anamsubiri mtu na waliongea baadae wakafatana sikujua wameenda wapi. Nilijisogeza kwa jamaa wa bodaboda wakiwa na makoti makubwa nikajiunga kupiga nao story huku nikimsubiri Merry.

Mimi: bro samahan hawa wadada mbona wapo wengi na wana mishe gani apa mbona wamevaa kiasala asala?

Bodaboda: hao wanajiuza mjomba. We mgeni nini?

Mimi: ndio mi mgeni.

Bodaboda aliniangalia tu na hakuendelea kuongea chochote Zaidi ya kuwafata abiria wawili waliokua mbele yake.
Baada ya muda kidogo hivi nilimuona merry akiludi eneo nililokuwepo.

Mimi: merry punguza kujifanya unamjua kila mtu apa sio singida hii dar rafiki angu.

Merry: lile tumbo lilikua ni la siku zangu na sio njaa kama ulivyohisi hivyo nilienda kwa yule mdada kuona kama ata nipa msaada wowote si unajua sijatembea na chochote. Lakini pia nimemueleza changamoto niliyonayo kwamba hatuna pa kulala na ndio tumefika mjini.

Mimi: akasemaje?

Merry: kasema atanisaidia kwa leo sehemu ya kulala ila kuanzia kesho nitajua pa kwenda, lakini pia amenieleza kama sina ndugu kabisa atanionyesha kazi ya kufanya na tutakua tunachangia wote kulipa pango la nyumba hivyo mi nimeona niende nae tu.

Kiukweli sikutamani merry aondoke na yule dada lakini sikua na jinsi kwani hata hivyo sikua na sehemu yoyote ya kumpeleka. Merry alinikabidhi simu yake ili iwe rahisi kunipata siku inayofuata kwani alikua anajua sikua na simu. Tuliagana na merry na mimi nikabaki eneo hilo nikiwaza naelekea wapi kwa usiku huo wala sikutaka kujutia maamuzi yangu ata kidogo niliamini nipo sahihi kabisa.

Tunaendelea baadae usikae mbali.View attachment 2583318
Pole sana
 
MAISHA NDANI YA JIJI LA DAR ES SALAAM

Ilikua ni usiku wa manane merry aliniacha maeneo yale ambayo yalikua ni maeneo ya karibu na ile bar ya SUGAR REY. Nilijisogeza karibu na jamaa mmoja aliekua umbali wa kama mita 100 hivi kutoka ilipo ile bar yeye alikua anafanya biashara ndogo ndogo. Alikua anauza vinywaji especially pombe kali, sigara na vingine vidogo dogo.

Baada ya kukaa na yule jamaa niligundua anauza vitu vingi sana ukiacha vile nilivyoviona. Mfano wateja wengi walikua ni wateja wa condoms na bangi kwa usiku ule. Kwa kua na mimi nilikua mvutaji mzoefu nilinunua ( sigara kubwa) na kuinyonga kwa ustadi wa hali ya juu kitu ambacho kilimvutia sana muuzaji yule (pusher).

Kwa rafudhi yangu ilikua rahisi kugundua kama nilikua mgeni na natokea kaskazini upande wa Arusha. Jamaa aliniomba nisiivutie pale nitafute sehemu nyingine mbali na pale maana police wanapita mara nyingi maeneo hayo.

Wakati nanyanyuka kuelekea eneo la giza ilikuja gari aina ya alteza nyeusi na kupark pembeni ya ile meza ya jamaa anaeuza pombe kali. Waliongea Kama baada ya dakika moja gari iliondoka na yule muuzaji aliniita. Kisha akaniambia nisubiri kuna watu wanakuja kuna deal la masaa kadhaa naweza pata hela ya kula.

"Dogo unaonekana kuwa mzoefu kwenye matumizi ya weed, kuna jamaa watakuja mtaenda kufunga mzigo maeneo ya mbagala" yalikua maneno ya yule jamaa muuzaji. Na mimi sikua na kipingamizi sababu sikua na sehem ya kwenda kwa muda huo.
Walikuja jamaa wawili kwenye pikipiki aina ya sun LG na wakapewa maelezo ya kuondoka na mimi.
"Ras kasema mzigo umefika, mchukueni na huyo janja anaweza kazi. mudi amelewa sana ataharibu kazi" yalikua ni maelekezo waliyopatiwa wale jamaa waliokuja na pikipiki.

Na hapo tukaanza safari ya kuelekea mbagala ilikua mishale ya saa 9 kasoro usiku.
Ilituchukua muda wa dakika 20 kufika maeneo ya sabasaba kwa mpili kisha tulikunja kushoto kuitafuta njia ya kwenda kijichi. Umbali wa mita 150 tulikunja tena kulia na kusimama nje ya nyumba moja kuukuu sana.

Palionekana kua uswahilini sana maeneo yale, nilifanikiwa kuligundua hilo japo ilikua ni usiku sana.
Baada ya sekunde kadhaa niliiona tena ile alteza nyeusi na wakati huu alishuka mwanaume wa makamo mrefu mweusi na mwenye Rasta ndefu zilizoonekana kuwa matunzo ya hali ya juu. Rasta alikua na Heineken mkononi, na alielekea mlangoni na kufungua mlango bila kumsemesha yeyote kati yetu.

RASTA: oyaaa!! Huyu dogo mmemtoa wapi??
Jamaa walijibu kwa uoga sana "boni kasema tuje nae anaweza kazi"
RASTA: ingieni ndani anzeni kazi huyu dogo niacheni nae apa.

Rasta alinipa maelekezo ya kutoa kila nilichokua nacho mfukoni huku akiniangalia kwa makini sana. Sikua na vitu vingi zaidi ya simu niliyopewa na merry, kibiriti pamoja na scientific calculator.

RASTA: dogo unasoma? Nimeona scientific calculator umenikumbusha mbali sana.

MIMI: ndio bro!! Ila nimeacha.

RASTA: kwanini umeacha??

MIMI: ni story ndefu bro!! Tunaweza kuendelea na mambo mengine kwani siwezi rudi tena huko.

RASTA: ok! Hua sipendi kufanya kazi na watu nisiowajua, ila kwakua watu wa chuga hawaja wahi kuniangusha zama ndichi ila simu nitabaki nayo Mimi.

Ndani ya kile chumba kulikua na viroba kadhaa vya bangi na shughuli kubwa ilikua na kuiandaa na kufanya packing. Kwa haraka nilitambua kama mzigo huo ulikua unasafirishwa nje ya jiji. Ila sikutaka kuhoji sana zaidi ya kufanya kazi hiyo kama nilivyoelekezwa na wenyeji wangu.

Tulimaliza kazi ile saa tatu asubuhi huku nikiwa hoi kwa usingizi wa zaidi ya siku mbili. Nilipitiwa na usingizi kwenye kigodoro kidogo cha futi tatu kilichokua kimechoka mno. niliamshwa na mtu nisie mjua mida ya saa 9 mchana, jamaa yule alinipa maelekezo nimfuate anapoenda.

Tulitumia muda mchache kufika sehemu moja inaitwa kijichi, tuliingia ndani ya bar ambayo ilikua opposite na barabara. Tulikaa meza ambayo tayari ilikua na watu wawili ila niliweza kumtambua rasta peke ake.

RASTA: dogo inaonekana umechoka sana pole.

MIMI: Asante bro.

Alinipa simu yangu na shilingi elfu kumi kama malipo ya kazi ya jana usiku kisha akaniambia tunakazi nyingine usiku huo. Hivyo kama nitahitaji kupumzika baada ya kula nipumzike tu kwani usiku huo tutakua na safari. Baada ya kuingalia simu upande ule wa call log nilikuta missed calls nyingi za namba mpya niliamini hizo zote zilikua ni juhudi za merry akitaka kujua nipo wapi.

Zilishushwa buckets za Heineken pamoja na kilo kadhaa za mdudu (pork) kiukweli niliya furahia sana yale maisha huku nikijaribu kuwaza ni kwa namna gani naweza tengeneza pesa mingi ka hizo.
Nilishtushwa na mlio wa simu na baada ya kupokea alikua na merry.
MERRY: massawe upo wapi mpenzi wangu?

"Samahan kaka Ras apa ni wapi" nilianza kuulizia jina la mahali nilipo kabla ya kujibu.

MIMI: nipo kijichi Merry.

Kwa maelezo ya merry alidai yupo temeke na jioni ataenda kuanza kazi sehemu moja ipo kurasini inaitwa PUB ONE hivyo kama nitahitaji kuonana naye niende hapo. Nililudi tena sabasaba kuendelea na usingizi wangu na ilipofika mida ya saa 3 usiku niliamshwa na Ras. Tulipakia mzigo na safari ilianzia, kwakua nilikua mgeni sikujua kabisa tunaelekea wapi na hata hivyo sikutaka kuuliza kila kitu niliamua kua mpole.

Baada ya masaa kama matatu hivi tulikua pembezoni mwa fukwe eneo ambalo baadae nilikuja kulijua kwa jina la mbweni.( Niliona mengi maeneo yale lakini kubwa zaidi ilikua ni bandari bubu inayoingiza na kutoa mizigo bara na visiwani).

Baada ya kumaliza kilichotupeleka eneo lile tulianza safari ya kuludi, na safari hii tulikua wawili tu na hatukua na mzigo wowote ata hivyo Ras alionekana kua mchangamfu kwani alianza kunipigisha stories pia.

Wakati tunapiga stories niligundua Ras amependa kunitumia kwenye safari yake kwa sababu kuu kama mbili hivi.
Kwanza; nilikua Smart kimuonekano ukilinganisha na washirika wake wengine ambao ungewaona tu ungejua ni wala ganja walio kubuu.

Pili; confidence na umakini kwenye kuongea, kwani sikua naonyesha dalili ya kumuogopa kwenye maongezi yetu.

Tukiwa njiani tunaludi simu iliita mfululizo na nilipoishika ilikua ni namba aliyoitumia merry kunipigia mchana.
MERRY: massawe upo wapi?

MIMI: nipo njiani naelekea mbagala

MERRY: naomba upitie nilipo kwambia nipo.

Kwakua nilishamueleza Ras black & white mpaka siku ile ameniona, ilikua rahisi kumwambia tupitie PUB ONE usiku huo kwani sikujua merry amepatwa na changamoto gani. Tulifika maeneo ya chuo cha T.I.A ambapo kulikua na bar kama mbili hivi japo sikumbuki vizuri lakin zilikua zimechangamka sana. Nilipiga ile namba na ikapokelewa na merry ambae alikuja upande wa pili wa barabara baada ya maelekezo yangu.

Merry alikuja akiwa analia huku akiniomba nisimuache eneo hilo peke ake, nilimuangalia Ras ambae nae alijua kabisa kama nahitaji msaada wake na Aliishia kusema tuingie kwenye gari. Sikumuuliza chochote merry zaidi ya kumuomba aache kulia kwani bado tunasafari ndefu.

Wakati huu sasa Ras aliamua kutupeleka mpaka nyumbani kwake maeneo ya kijichi. Tulipofika alinionyesha chumba cha kupumzika lakini akimtaka merry apumzike kisha mimi na yeye tutakua na maongezi mafupi.
Lilikua ni jumba kubwa lililopo ndani ya fensi lakini pia kilichonishangaza ni ukimya wa jumba hilo kwani hukukua na mtu yoyote tuliyemkuta ndani apo.

RASTA: dogo nimeamua kuwapa msaada wa siku moja kwa sababu yule binti umri wake na kile alichokua anakifanya pale haviendani. Msaada wangu wa mwisho, kesho tunaenda Moro kuchukua mzigo yeye tutamuacha msamvu asubuhi apande gari za mwanza aludi shule. Wewe kwakua umechagua upande huu tutaendelea kua pamoja. Nenda kupumzike.!!!
Kwa maelezo ya Ras inaonekana hakutaka dialogue ni kama alikua ana nipa taarifa.

Nilipoingia ndani merry alikua amelala usingizi mzito na sikuona haja ya kumuasha na mimi pia niliamua kupumzika.

Majira ya saa 9 kasoro usiku ndio tulianza safari na gari nyingine aina ya Rav 4. Mda ote huo sikua nimepata nafasi ya kuongea na Merry kuhusu jambo lolote kwani tuliamshwa usingizini na kujiandaa na safari kwa muda mchache.

Tulitumia almost 2:50 hours kuzimaliza 195.97 km kwani speed ya gari ilikua ikipungua sana basi ni 70km/hr.

Saa 12 asubuhi tunaingia moro huku Merry akipewa laki moja ambayo tuliamini itamfikisha bila changamoto za aina yoyote.
Niliagana na merry katika namna ambayo iliniumiza sana kwani hatukupata nafasi ya kuongea jambo lolote. Na kwa mara ya kwanza machozi yalinitoka baada ya kuona Merry akiwa akinipungia mkono maeneo ya stand ya msamvu. Alipanda gari ya kampuni ya Ally's Na huo ndio ulikua mwisho wa kuonana na Merry kwenye maisha yangu.

Nikiwa ndani ya hostels za wanafunzi wa SUA ambapo niliachwa na Ras huku yeye akitokomea porini. Majira ya saa 3 asubuhi ilitufikia taarifa ya ajali mbaya iliyohusisha magari matatu eneo la mkundi kwa makunganya. magari hayo ni ya kampuni ya sumry, shabiby na Ally's.
Kwa wenye kumbukumbu mnaweza kuikumbuka ajali hii na hapo ndipo nilipompoteza Merry ( alifia hospital akipelekwa kama majeruhi).
 
THE WEALTH OF RAPTA RUINS
(Get Rich or Die Tryin)

Msimuliaji: LUDOVIC MASSAWE

NB: SIMULIZI HII IMEAMBATANISHWA NA BAADHI YA PICHA ZINAZOTUMIKA KUELEZEA MATUKIO, HURUSIWI KUTUMIA PICHA HIZO MAHALI POPOTE.

PROLOGUE/DIBAJI

Mji wa rapta ni mji uliozama baharini kisiwani mafia kwa zaidi ya miaka 2000. Unaweza kua mji mgeni Kwa baadhi ya watu, lakini wengi mnaweza kua mmepata kuusikia uwepo wa mji huu wa kale pembezoni mwa pwani ya Africa mashariki. Wapo wanaodai mji huu unapatikana maeneo ya rufiji kwa sasa na wapo wanaodai mji huu unapatikana pembezoni mwa kisiwa cha mafia. Je! ni nani yupo sahihi?

Mji huu ulipata kuwepo mwanzoni mwa karne ya 1 na imepita zaidi ya miaka 1600 mpaka 2000 tangu kuwepo kwa mji huu. Unaaminika kuwa mji wa kwanza tajiri barani Africa na pia ni miongoni mwa miji kumi na tano inayopatikana chini ya maji. ukiacha miji kama vile Thonis-Heracleion na Alexandria iliyopo Egypt, Yonaguni Jima (Japan), Port Royal (Jamaica) Dwarka (India), Pavlopetri iliyopo south-western Greece, Villa Epecuen (Argentina) nk.

Tofauti na ilivyo kwa watanzania na wakazi wa Africa mashariki wakiwemo wana archeologia. Wengi wamechelewa kuzipata habari za mji huu, mimi nilizipata habari hizi nje kabisa ya ukanda huu. Nilizipata habari hizi nikiwa jiji la Tehran uko inchini Iran (uajemi ya kale) ndani ya maktaba ya taifa (National Library of the Islamic Republic of Iran) iliyoanzishwa mwaka 1937 ikiwa na zaidi ya items milion 15 ndani yake.

Wakati nafika Iran nilikua nikitokea nchini Colombia na Peru kwenye mashamba ya koka (coca plantations). kwa wasiojua koka leaf ndio mmea unaotumika kutengeneza madawa ya kulevya aina ya Cocaine kupitia mchakato mrefu. Na ugumu wa ku control uzalishaji wa cocaine unasababishwa au unatokana na kushindwa kuthibiti chemicals zinazotumitumika kwenye mchakato huo kwani ni chemicals za kawaida zinazotumiwa kila siku kwenye matumizi ya binadamu.

Mfano; ku process coca leaf kuwa coca paste mpaka kupata cocaine base na HCI zinatumika chemicals kama, Sulfuric Acid, Sodium Bicarbonate, Sodium Hydroxide, benzene, Potassium Permanganate, Dichromate, Ammonia Hydroxide, Sodium Hydroxide, Methyl Ethyl Ketone na kerosene. Tutajuzana mengi kuhusu cocaine hapo mbele tukiendelea na simulizi.

Sasa basi Niliwezaje kufika Colombia, Peru kisha Iran na miji mingine mikubwa duniani? Niliwezaje kuzisikia habari za mji wa rapta? nani alinipa habari hizi? na mji huu wa rapta una utajiri kiasi gan ndani yake? Nilifikaje rapta na kwa msaada wa technologia gan nilifanikisha zoezi langu? Kipi kilisababisha mji huu kuzama baharini?

Swali lingine la msingi, wageni wa kwanza wa pwani ya Africa mashariki walikua ni warumi na wachina kabla ya waarabu na waajemi, sasa imekuaje details za rapta zilizoandaliwa na warumi zikafika Iran (Persian gulf) zilifikaje huko?

Najua baada ya kutaja wachina wengi mtajiuliza maswali lakini msijali tutaona ushahidi wa uwepo wa wachina ndani ya mji wa rapta. 90% ya wachunguzi wa mji huu wanatumia taarifa za warumi zilizoandaliwa na Claudius Ptolemaeus (Claudio Ptolemy). Je wana fahamu kua details hizo kabla ya kuwafikia zilishatumiwa na waajemi wa kale Na kuna uwezekano taarifa hizo zilichakachuliwa!?

Je! Mzungu bwana Alan Sutton (mzamiaji) aliyegundua kuta za rapta akiwa kwenye helicopter hivi karibuni, ilikua ni bahati mbaya tu au na yeye ni moja ya wale treasure hunters ila hajaliweka hili wazi?
Ungana nami kwenye simulizi hii ya kuvutia ili kupata majibu ya maswali yote na kwa hakika utajifunza mambo mengi ndani yake.

SEHEMU YA 01

Mgomo sengerema secondary

Wakati unajiuliza Niliwezaje kufika Colombia, Peru na kisha Iran unatakiwa kujua safari yangu ya jasho na damu pamoja na misukosuko mingi ilianzia shule ya sekondari ya sengerema nikiwa kidato cha sita. Kwa waliopata kupita shule hii wanaweza kua mashihidi kwa namna shule hii ilivyokua ya kikomando yaan wenyewe tulikua tunaita late-summer boot camp.

Kwa haraka haraka tu ni shule aliyowahi kufundisha hayati magufuli kabla hajawa waziri na kisha raisi. Nadhani umeanza kupata picha ilikua shule ya aina gani, Ni shule ambayo kila mtu alikua jeuri kuanzia headmaster mpaka mpishi wa jikoni. Wakati nikiwa hapo tuliwahi kushuhudia kesi nyingi ngumu na za ajabu kama wanafunzi kukutwa na kombati za jeshi full set. Kuna mengi kuhusu sengerema ambayo hatuyajui nitawaeleza machache tu na ni kwa namna gani safari yangu ilianzia hapo.

Nilifika hapo kwa mbinde huku o'level nikitokea Ngerengere kizuka sekondari baada ya kufukuzwa MAKOKO SEMINARY, kiukweli nilikua mtoto mtukutu na jeuri ilifika hatua mzee wangu mzee MASSAWE alisema hizi tabia nimeridhi kutoka kwa babu yangu. Ambae alikimbia nchi baada ya kuhusika kwenye matukio mawili, lile la utekaji wa ndege ya ATC mwaka 1982 February kwa makusudi ya kushinikiza mwalimu ajiuzulu na lile jaribio la kuangusha serikali ya mwalimu Nyerere la mwaka 1980's. Babu Yangu alikua ni miongoni mwa wale maafisa wakuu waliosuka ule mpango, Tuachane na babu na tuludi zetu sengerema.

Tukio la mgomo ndio lililoanzisha safari yangu Na lilipangwa usiku baada ya mlo wa jioni, vidume baada ya kushiba dona maharage pamoja na nchima boyo akili zikatutuma tufanye mgomo usiku wa siku hiyo. Sababu za mgomo zilikuwepo japokua hazikua na mashiko sana naweza sema ni ujana tu ndio ulikua unatusumbua ukiongeza na zile bangi zakuvutia maporini (chaka).
Kama kawaida mzee baba siku hiyo ya mgomo niliwekwa kitengo cha TANESCO, yani niliambiwa ikifika saa 2 kamili usiku ni hakikishe shule nzima umeme umezima. Hii ilitokana na ujuzi wangu wa mambo ya electronics na wiring za ujanja ujanja za mabwenini especially bweni la kimweri na sokoine.

Basi ilipotimu saa 2 kamili nilihakikisha Giza limetanda shule nzima kasoro nyumba za walimu tu, na kazi yangu iliishia hapo na Majukumu mengine yaliyobaki yalikua kwa wenzangu wahamisishaji kuhakikisha kila mmoja anashiriki. Lakini pia kuna jamaa mmoja wa mwananyamala yeye alikua na dumu la petrol lita 5 sijui alilitolea wapi usiku ule huyu bwana kazi yake ilikua kuhakikisha moto unawaka maeneo yote yaliyopangwa kuchomwa.

Mpaka kufika saa nne usiku stationary ya mwalimu wetu siwezi kumtaja jina ilikua haitamaniki na baadhi ya walimu walikimbiza familia zao mjini. 90% ya wanafunzi tulikua michepuo ya sayansi yani PCM, PCB na combination nyingine hivyo tulikubaliana kutokugusa maabara wala library wala darasa, wachache sana walikua arts na cha ajabu kwenye hii shule watu wa arts walikua wamestaarabika ukilinganisha na sayansi.

Shule imejengwa mlimani kabisa kiasi kwamba ilipofika saa 4 na nusu usiku defender ilionekana ikipandisha na wote tukapotelea maporini. Jambo la kufurahisha ni kwamba askari hawakufanikiwa kukamata ata mwanafunzi mmoja kati ya wanafunzi 800. Wengi waliishia kulala kwenye miembe na majaruba ya mpunga kwa usiku huo kwani shule ilizungukwa na makachero wakutosha. Lakini massawe nikasema siwezi lala juu ya mti Kama tumbili, usiku ule ule nikaanza safari ya kuelekea mjini mitaa ya soko mjinga.

Pale mjini kuna binti alikua anasoma shule ya jilani inaitwa NTUNDURU alikua amepanga ghetto. Can you imagine!!! Shule ya boarding na bado amepanga mtaani! asee!!... Merry alikua ni hatari sana mnyaturu yule wa singida.

Mishale ya saa tano usiku nilikua mlangoni kwa merry nabisha hodi, baada ya dikaka 3 alifungua mlango nikaingia. Walikua wawili yeye na mwenzie anaitwa jane. Ndani kulikua na chupa za safari na mzinga mkubwa wa konyagi, nilipoingia nilihisi uwepo wa mwanaume mule ndani na baadae niliona funguo za sun LG na vipisi vya sigara. Ila sikujali sana nilijitupa kitandani nikapitiwa na usingizi mzito uliotokana na uchovu wa mgomo na mbio za kuwakimbia field Force.

Nilikuja kustuka saa kumi alfajiri na mlio wa pikipiki uliokua unamrudisha merry ambae alikuja yupo hoi na kwa haraka niligundua jane amebaki na yule kidume wa jana.

Merry akilewa bia hua zinashuka chini, waliosoma cuba wamenielewa hapa. Hivyo baada ya kuingia ndani hakutaka story zaidi ya kutupa nguo kwenye kila kona ya chumba hicho kama mwehu. Na mimi kutokana na nilikua namjua vizuri haikusumbua kujua anataka nini zaidi ya kuanza mtanange wa kukata na shoka uliochukua zaidi dakika 90 kama finally ya Argentina vs France kule Qatar.

Tulikuja kuamshwa na mwanga mkali wa jua la saa 4 asubuh uliokua unapita dirishani Huku merry akiwaza supu. Ilituchukua muda mfupi kujiandaa kwenda maeneo ya stendi kupata supu, nilishangaa baada ya kufika stendi nilikutana na wanafunzi wenzangu wakiwa na mabegi wengine ma tranka. Nilipowauliza walijibu shule imefungwa kwa muda wa week 3 na tutapewa utaratibu wa jinsi ya kurud tukiwa nyumbani. Hapo nilianza kuwaza namna ya kurud nyumbani huku mizigo yangu yote imebaki shule na hakuna mwanafunzi anaeruhusiwa kwenda tena shule kwa muda huo.

Basi bwana tulipata supu na mrembo merry kisha tukarud zetu ghetto kupumzika, nakumbuka ilikua siku ya alhamisi hivyo merry hakuenda shule kutokana na hangover na tulishinda ndani siku nzima mpaka kesho yake asubuhi.

Siku ya pili akili ilivurugika zaidi baada ya kupata habari kwenye vituo vya habari viwili tofauti kuhusu mgomo wa sengerema, kituo cha kwanza ni redio sengerema ilitangaza wanafunzi kumi na tisa (19) wamefukuzwa na wengine kusimamishwa masomo kwa muda usiojulikana. Hivyo hivyo kwa redio free Africa na gazeti la mwananchi, gazeti hili lilitoa majina ya waliofukuzwa na mimi nilikua jina la kwanza kwenye ile list.

Niliwaza namwambia nini mzee massawe ambae alichoshwa na tabia zangu.

Akili ikanituma kuangalia upande wa pili wa maisha na sio kukomaa na shule, niliamini siku Moja nikiludi home na pesa nyingi mzee massawe atanikubali sana jembe lake.

Baada ya kupata wazo la kutoendelea na shule nikaanza kuwaza natakiwa nianzie wapi kutafuta pesa. Apo apo akili ikaniambia dar ndio sehemu pekee naweza tengeneza pesa nyingi, lakin kwa bahati mbaya sikua mzoefu wa mji huo na wala sikutakiwa kufikia kwa ndugu yoyote na bado sina nauli ya kufika huko. Niliamini nikifika Mwanza kwenda dar itakua rahisi hivyo nikaanza mchakato wa kufika mwanza (nyegezi).

Nilimshirikisha merry kwa makusudi ili anisaidie nauli ya kufika nyegezi kwani kutoka sengerema hadi nyegezi ni kiasi cha shilingi 4000 tu. Na kwa maelezo ya merry aliniomba tufike stendi kuna mtu atampatia tukifika hapo.tukiwa stendi Merry alimfuata jamaa mmoja bonge hivi anadeal na tickets pale stendi, Kwa haraka niligundua huyo ndio sponsor waliekua nae jana. Sikujua waliongea nini na merry ila merry aliniambia tusubiri kuna coaster inatokea katolo ndio tutaenda nayo mwanza.

Haikuchukua muda mrefu ile coaster ilifika na walipanda abiria kadhaa kisha bonge akamwambia konda hawa ndio wadogo zangu wanaoenda nyegezi. na sisi tulipanda tukaanza safari, nilishangazwa na uwepo wa Merry kwenye safari sikujua na yeye anaelekea wapi kwani hakua na sababu ya kutoka sengerema siku hiyo kwani masomo kwa upande wake yalikua yanaendelea. Merry alikua mwanafunzi wa kidato cha nne NTUNDURU sekondari na ile siku tumeshinda ote ndani nilitumia fursa kumfundisha almost topics tatu za msingi.

Sasa tukiwa ndani ya coaster kuelekea nyegezi nilimuuliza kwanini na yeye ameamua kusafiri, majibu yake yalikua ni kwamba ana muda mrefu hajafika mjini mwanza hivyo alitaka kwenda kuosha macho kwa muda kisha baadae ataludi sengerema.

Nilipata nafasi ya kupiga stories na konda ndipo niligundua wametokea geita walipeleka msiba na hapo wanarudi dar es salaam. Niliamini safari yangu kufika Dar es Salaam imerahisishwa nachotakiwa ni kuwaza namna gani naweza kushawishi jamaa ili aniruhusu nisafiri nae.

Majadiliano na konda yalikua hivi.

Konda:"dogo! we ni mwanafunzi Nini? Jana tukiwa na msiba tulibeba madogo kama watatu hivi wakiwa na suruali nyeusi na tishet za bluu kama ulivyovaa wewe"

Merry alijibu fasta kama ameulizwa yeye,

Merry: ndio sisi ni wanafunzi, ila tumerudishwa nyumbani ghafla sababu ya mgomo wa juzi usiku.
(konda hakujua kama sengerema ni shule ya wavulana pekee)

Konda: kama wanafunzi wenyewe ndio nyinyi hiyo shule kazi ipo. Kwaiyo nyumbani ni wapi??
Nilitumia swali hilo kama fursa ya kufanikisha misheni yangu.

Mimi: home dar na hatujatumiwa nauli sijui tunafikaje?

Konda: we mtoto wa kiume jitahidi upambane.

Jibu lile lilinikatisha tamaa ya kuendelea na maongezi yale.
Haikuchukua muda tulikua tumefika kivukoni busisi. Abiria wote tulishuka na kupanda kivuko, lakini nilifurahi baada ya kumuona konda anajisogeza kwa merry na kujiongeresha. nilijua kwa ujanja wa merry anaweza kufanikisha safari yangu kirahisi sana.

Baada ya kufika upande wa pili tulirudi ndani ya coaster na kuendelea na safari na wakati huu merry aliniambia ameshampanga konda hivyo tutafika wote dar es salaam.

Merry alikua binti mjanja sana na anamacho Fulani akikuangalia tu unajua atakua fundi, hahahahahaha kwa wale tuliopita sengerema miaka ile najua mtakua mnamkumbuka kwani alikua maarufu sana. Especially tukienda shuleni kwao kwa ajili ya michezo wengi walimtolea macho, nitakuja kueleza nilimpataje hapo baadae.

Baada ya kufika nyegezi tukijiandaa na safari ya kuanza kuitafuta dar es salaam nilishangaa konda aliniita na kunipa buku tano nikatafute msosi. Na kisha konda na merry walipotelea kusiko Julikana, Nilijua merry ameshafanya yake tayar niliishia kuitunza ile buku tano nikiamini itanisaidia mbele ya safari kwani sikua na chochote mfukoni.

Baada ya nusu saa merry na konda walirudi huku nikimuona merry na vifurushi vya kutosha bila shaka ilikua ni misosi na kimoyomoyo nikasema merry hajawahi kuniangusha ata siku moja. Tulikaa kwenye siti na kuendelea na safari Huku tukipiga msosi mzito nakumbuka ilikua ni Sato na chipsi kavu za kutosha.

Mimi: merry ulisema unaishia nyegezi vipi mbona unaendelea na safari???

Merry: sijawahi kufika Dar es Salaam, nadhani hii ni fursa ambayo sitakiwi kuichezea. Najua nipo na wewe hakuna kitachoharibika nitakaa week moja kisha nitarudi shule.

Daaaaah!!!!! Nilihisi mwili unakufa ganzi nilitaman kumwambia Mimi mwenyewe sina pa kufikia ila nikapiga moyo konde. tukaendelea na safari yetu huku stories zikiwa nyingi. Merry pekee ndio alikua na simu Mimi kilichokua mfukoni ni ile buku tano, kibiriti cha gesi na scientific calculator tu.

Baada ya safari ya muda mrefu wote tulipitiwa na usingizi, safari ile ni ya kutwa nzima kwani nakumbuka tuliingia morogoro usiku wa saa tano tena hiyo ilikua ni baada ya abiria kulalamikia speed ya gari ilikua kali mno. Tulipotoka moro baada ya kufika maeneo ya chalinze nilipitiwa tena na usingizi mzito. Nilikuja kushtuliwa na konda akidai alitusahau tumeshaingia mjini mda mrefu.

Konda: nyie mnashukia wapi tumeingia Dar es Salaam tayari.
Lile swali lilikua gumu kwangu kwani sikua ata najua tunapoelekea baada ya kufika dar. Kwa Dar es Salaam nachojua ni ubungo tu hivyo nilimjibu tunashuka ubungo.

Konda: ubungo tumepita tayari sisi tunaelekea mbagara, shukeni hapa mrudi vertinary mkapande gari za ubungo.

Kiukweli sikumuelewa konda ata kidogo kila alichonambia kilikua kipya ila sikutaka kuonyesha kutokujua mbele ya Merry hivyo tulishuka. Tulishushwa eneo moja lina mataa na ilikua saa saba na nusu usiku, nikiwa sijui cha kufanya Merry alianza kulalamika maumivu makali ya tumbo.
Nilijua tu itakua njaa kwani ni muda mrefu hatujapata chakula, baada ya kupepesa macho huku na kule niliona sehemu kwa mbaali kuna watu na mataa mengi yanawakawaka nikajua fika hapo patakua na bar hivyo hatuwez kosa msosi.

"Massawe hapa na kwenu kuna umbali gani?" Lilikua ni swali la Merry na mimi sikuona haja ya kuendelea kumficha ukweli, nilimueleza kila kitu kama nimeenda huko kutafuta maisha na nimeachana rasmi na masomo baada ya kufukuzwa shule na nilimueleza siwezi kurudi moshi kwa mzee massawe hatonielewa kabisa.

Kwa maumivu ya tumbo aliyokua anapitia Merry hakutaka kuendelea na mjadala nilimuona akiongoza kwenye lile eneo tuliloliona likiwa na watu wengi usiku ule.
Baada ya kufika eneo Hilo niliona maandishi makubwa yakiwakawaka yameandikwa SUGAR REY. Ni dhahiri ilikua ni bar, nilishangazwa na mavazi ya wadada wa eneo hilo na sio mimi tu ata merry pia.
"Hhhmmm kweli hii ndio dar es salaam ninayoisikia kila siku" yalikua ni maneno ya Merry. Tukiwa bado tumeduwaa alikuja bodaboda

Bodaboda: vipi mnaenda?

Mimi: hapana tumefika bro.

Bodaboda: punguzeni kushangaa basi.

Tulisogea mpaka eneo lile nikiamini hatuwezi kukosa chakula ukizingatia nilikua bado na lile buku tano la konda.

Tulipofika tu merry alimfuata Binti mmoja aliekua amekaa pembeni akiwa kwenye pozi Kama anamsubiri mtu na waliongea baadae wakafatana sikujua wameenda wapi. Nilijisogeza kwa jamaa wa bodaboda wakiwa na makoti makubwa nikajiunga kupiga nao story huku nikimsubiri Merry.

Mimi: bro samahan hawa wadada mbona wapo wengi na wana mishe gani apa mbona wamevaa kiasala asala?

Bodaboda: hao wanajiuza mjomba. We mgeni nini?

Mimi: ndio mi mgeni.

Bodaboda aliniangalia tu na hakuendelea kuongea chochote Zaidi ya kuwafata abiria wawili waliokua mbele yake.
Baada ya muda kidogo hivi nilimuona merry akiludi eneo nililokuwepo.

Mimi: merry punguza kujifanya unamjua kila mtu apa sio singida hii dar rafiki angu.

Merry: lile tumbo lilikua ni la siku zangu na sio njaa kama ulivyohisi hivyo nilienda kwa yule mdada kuona kama ata nipa msaada wowote si unajua sijatembea na chochote. Lakini pia nimemueleza changamoto niliyonayo kwamba hatuna pa kulala na ndio tumefika mjini.

Mimi: akasemaje?

Merry: kasema atanisaidia kwa leo sehemu ya kulala ila kuanzia kesho nitajua pa kwenda, lakini pia amenieleza kama sina ndugu kabisa atanionyesha kazi ya kufanya na tutakua tunachangia wote kulipa pango la nyumba hivyo mi nimeona niende nae tu.

Kiukweli sikutamani merry aondoke na yule dada lakini sikua na jinsi kwani hata hivyo sikua na sehemu yoyote ya kumpeleka. Merry alinikabidhi simu yake ili iwe rahisi kunipata siku inayofuata kwani alikua anajua sikua na simu. Tuliagana na merry na mimi nikabaki eneo hilo nikiwaza naelekea wapi kwa usiku huo wala sikutaka kujutia maamuzi yangu ata kidogo niliamini nipo sahihi kabisa.

Tunaendelea baadae usikae mbali.View attachment 2583318
Mkuu
Naomba unitag kila unapoweka chapisho jipya la hii hadithi yenye ukweli mwingi..

I am interested sana na Raphta. Nitaandika baadaye nikijuacho baada ya kusoma story nzima
 
Back
Top Bottom