Tengeneza pesa kwa ujuzi wa kurekebisha simu

eddie255

Senior Member
Oct 30, 2017
104
53
Je, umekuwa upo katika hali ya kujiuliza unaweza kujifunza ujuzi gani ambao utakuingizia pesa ya kujikimu kila siku. Nakumbuka mwaka 2015 nilikuwa kama wewe nimekaa nyumbani bila ujuzi wowote na kushindwa hata kuingiza pesa ya kula. Ndipo kwenye pita pita zangu YouTube nikakutana na huu ujuzi wa kurekebisha simu na hapa ndipo ulikua mwanzo wa kujifunza kwa kusoma online, pamoja na kwenda kusomea rasmi.

Kupitia hili sasa naweza jitengenezea zaidi ya Laki tano kwa mwezi. Hivyo naomba niweze kusambaza nilichokipata ili nisaidie vijana wenzangu kupata ujuzi huu ili na wao uwasaidie kujikwamua kwa namna moja au nyingine.

AINA ZA UFUNDI SIMU
Software,
hapa utarekebisha simu bila kuifungua. Mfano flashing, unlocking and Repair.

Hardware, hapa utarekebisha simu kwa kuifungua.

Software, hapa kwenye software ndio nitakapo gusia sana, ambapo kumegawanyika sehem tatu ambazo ni flashing,  unlock and  repair.

Flashing
; Maana yake ni kusasisha msimbo (program) kwenye chipset. Kuna aina mbalimbali za chipset kulingana na simu husika. Mfano MTK SPD, RDA, MSTAR, haijalishi kwa simu ndogo mfano Tecno t340 au Itel it5300.

Vitu ni vingi kwaiyo siwezi viweka vyote kwa sababu ya muda, ila tuendelee uweze kujipatia madini, uweze kupiga pesa.
Uko tayari kupata maujuzi? Twende kazi!

PROGRAM ZA KUFLASH SIMU

MIRACLE -
hii ni moja ya program ya kuflash na unlock simu za kichina kulingana na chipset zake. Kwa simu za kisasa, smartphone, zinazutumia chipset za MTK au SPD. Ina uwezo wa kuzisoma parttern au password na kutoa lock bila ku-format/ku-hard reset, pia inatoa network lock kwa baadhi ya simu, ili simu iweze kutumia laini ya mtandao wowote[kwa qualcomm].

Pia inaflash mafile yaliyopo katika format ya scatter kama wengine wanaoyatumia katika sp flash tool na bin na nyinginezo. Inatoa Factory reset protection {FRP} kwa simu za MTK, SPD, na QUALCOMM, ambazo zimewekewa hiyo option. Kwa simu za kisasa za smartphone zinazutumia chipset za MTK au SPD ina uwezo wa kuzisoma parttern au password na kutoa lock bila ku-format/ku-hard reset.

Pia inatoa networck lock kwa bahadhi ya simu ili simu iweze kutumia laini ya mtandao wowote [kwa qualcomm]. Pia inaflash mafile yaliyopo katika format ya scatter kama wengine wanaoyatumia katika sp flash tool na bin na nyinginezo.
Inatoa Factory reset protection {FRP} kwa simu za MTK, SPD, na QUALCOMM ambazo zimewekewa hiyo option.

Kwa leo naomba niishie hapa, nitakuja kuendelea na kujua jinsi simu yako ina chipset gani na drivers za kuweka kwenye computer yako ili uweze kuanza kazi na uanze kujipatia pesa.

Ndio maana leo nataka niwape hii ofa watu 10 tu, ambao wataweza kuingiza kile wanachojifunza kwenye vitendo na siyo kujifunza na kuishia Kujua pekee.

Darasa la Flashing Skills ambapo utafundishwa ujuzi wote na kuwa chini ya uwangalizi kwa miezi mitatu.

Utajiunga kwenye darasa kwa OFA ya Tsh. 20,000/- tu (badala ya Tsh. 50k).

Tutumie Ujumbe mfupi WhatsApp 0658190978. OFA hii ni ndani ya masaa 24 tu.
Kwanza jizoeshe kuzitambua simu kwa picha na kwa maandishi pia (kutambua model number)

SEHEM YA PILI
Utendaji kazi ktk kazi ya kuservice simu ktk upande wa software unahitaji akili kutulia na kuelewa formula mbili 2

Kwanza jizoeshe kuzitambua simu kwa picha na kwa maandishi pia (kutambua model number)
Pili pata experience ya matumizi ya computer
Maana sio kila kazi utaifanya mkononi tu bila computer.

Tuwe makini sasa hapa

Kila program inafanya kazi kulingana na uwezo wake kulingana ilivyoandaliwa. Huwezi flash LG ktk tool ya samsung au uflash Mtk ktk tool ya Qualcomm

Hapo nimetaja brand za simu na brand za chipset (cpu za mobile devices)

Je tutaitambuaje kuwa simu ya mteja inatumia cpu gan na ni tool gan inaweza ifanyia kazi!?

Hapa tunahitaji kufungua device manager ktk pc na kuconnect simu na kucheck ktk upande wa ports au kila kona kucheck wap device mpya imeongezeka. Simu ikiwa ktk flash mode lazima itadetect kwa utambulisho wa chipset yake. Mfano ukiconnect Tecno F1 ktk pc utaona ktk device manager upande wa ports inaandika (Mediatek preloader…..

Ukiconnect simu ambayo ina chipset ya qualcomm utaona ktk ports inaandika (qhsusb bulk) au (edl qualcomm 9008 au namba tofauti)

Tukishajua simu yetu ni mtk au qualcomm hatuishii hapo. Lazima tujue pia ni version gan ya hyo chipset. Mfano Tecno F1 inatumia MT6580 kwahyo hapo lazima tudeal na toola ambayo inadeal na Mtk na pia ina uwezo wa kuservice Mt6580…

Siku hizi simu mpya zina bootloader zake zinakuwa secured (secure boot based devices)

Ili kuweza kuziservice hizo lazima utumie custom DA (custom loaders/Download Agent)

DA always ni specifically kwa model flan. Mfano sasa hv ukiingia mtandaon unatafuta TECNO F1 DA file. Utaipata na utadownload.

Tools za sasa zina option ya kuload Custom DA/Other loaders kama AUTH (Authentication file) & Preloader. Tofauti na tools za zaman zilikuwa na default DA files kwa simu nying tu. Unakuta tool ina DA mbili au tatu inaservice simu nying sana sababu hazikuwa secured.

Kwa maana huwezi service secure boot based model bila custom DA ktk tool ambayo haina specifically built in DA kwa device husika.
Kama utapenda kujiunga na group ya bure ya kupewa Ujuzi tutumie ujumbe UJUZI whatsapp 0658190978
Itaendelea
 
Darasa ni la online na kama yupo Dar anaweza kuja ofisini kupata ujuzi zaidi ila ataanzia online inabd awe na computer ya kufanyia kazi kwa kila anachofundishwa
 
Kwa mtu ambae hana pc unamsaidiaje,
Unaweza ukajifunza ili kupata ujuzi baada ya kujua unaweza kwenda kuomba kazi kwenye ofisi ya mtu ambapo utakua tayari na ujuzi na itakusaidia kukubalika haraka maana utaongeza thamani hapo unapoenda kuliko kutokua na ujuzi inakua ngumu kukubaliwa
 
Back
Top Bottom