Kobello
JF-Expert Member
- Feb 20, 2011
- 8,637
- 7,920
Sheria inasemaje kuhusu kutohudhuria vikao na kususia uhalali wa halmashauri?<br />
<br />
Mtanyosha tu maelezo mwisho wa siku, sheria ni msumeno mama! Soma katiba vizuri, uanachama ndo tiketi ya wao kubaki kuwa madiwani otherwise hawana namna zaidi ya kukubali yaishe. Hawnauwezo wa kukilazimisha chama kiendelee kuwadhamini kama wameshindwa kutimiza masharti ya uanachama. Na kwenda mahakamani huku wakiacha kukata rufaa kwenye ngazi za chama ndiyo wamekoroga kila kitu kabisa!
Kama wewe ni diwani,je unawakilisha wanachama wenzako tu? Kama hapana,wanakata wasio wanachama wa chama cha diwani mhusika wanashirikishwaje kwenye maamuzi au shughuli mbalimbali za halmashauri ya jiji? Huoni kuwa kususia vikao na kutowakilisha wananchi
ni kuwanyima haki zao?
Je, ni bora kuwa mwanachama ili uwe diwani hewa,au usiwe mwanachama ili uwe diwani wa kweli anayeshughulikia au wakilisha wanakata wenzake regerdless of party affiliation?
Kama uchaguzi wa rais ulikiukwa,mbona wabunge bado wanaingia mjengoni? Why are they submitting themselves to an illegitimate government?
Ukinivua uanachama,nikienda mahakamani halafu nikashinda,mtanirudishia dhamana niliyopewa na wananchi kuwaongoza? Je kama mwingine akiwa keshachaguliwa atafanywaje?
Jibu hayo kwanza.....bado ninayo mengine mengi tu.