Tendwa, Mkuchika watofautiana kuhusu waliotimuliwa udiwani AR

Sijajua uwezo wa akili yako Mkuu eric cartman kuna wakati inatupasa kusoma tu na kubonyeza like pasi kuchangia
Labda nikuulize wewe taratibu za uchaguzi na viongozi wa kuchaguliwa zinalindwa na chama au katiba?

Halafu ndio tuendelee. Unajua usishabikie kitu bila ya kukielewa vizuri.

Tatizo lipo kwa anayewateua,ktk hali ya kawaida unaweza mteua mtu kama Mkuchika kuwa waziri tena wizara nyeti ya Tamisemi? Pili ni uwezo mdogo wa Pinda. Tamisemi ipo ktk ofisi yake. Ameshindwa kusimamia sheria na taratibu za serikali ya mitaa mpaka tumepoteza maisha ya watu na wengine kuachiwa vilema. Amebakia kuhangaika na Jairo.

Kutofautiana katika misimamo ni jambo la kawaida tu hasa unapoendesha au unapowajibika kwa maamuzi makubwa.
Ni kweli katiba imeruhusu kuwa na uhuru wa kutoa maoni lakini ikaweka kigezo cha kutokuvunja sheria
Kwahiyo kutofautiana kwenye maamuzi ya au la kuvunja sheria yanataka ujazo muafaka sitahiki na muafaka, maake kwenda kinyume kwa kutoa maamuzi yasiyo sitahiki adhabu lazima itolewe.sasa, huyo mdau ana paswa kuisoma katiba, aielewe, na pia aelewe adhabu zinazoambatana na kuvunja katiba, ndo aropoke kufagilia maamuzi yasiyositahiki kisheria kwa kisingizio cha kukuza demokrasi.Kama mtu hana uhakika kuna idara ya mwanasheria mkuu, kwanini asiende kupat ushauri ?msajiri wa vyama vya siasa nimwanasheria na ana idara sheria kwanini mkuchika asiende kupata ushauri badala ya kuivunja katiba kwa kisingizio cha demokrasia.Pia kwa nini mkuchika awe mbabe kushindana na mihimili mingine?
Tuwe wachambuzi wa masuala ya kisheria, demokrasia, siasa na utawala bora na si kukurupuka, je ikatoke mahakama ikawona wanasitahiki kufukuzwa unanachama, nani atalipa mafao na posho wanazolipwa hivi sasa?mkuchika alitakiwa kuwa na subira aone mahakama inasema nini ndo atoe msimamo wake.

Mtaalam wa utawala anisaidie hili swali:
Je, Mayor anawajibika kwa Madiwani au kwa Waziri mkuu TAMISEMI? na kwamba kwa nini atumie waraka wa TAMISEMI kuwatambua madiwani badala ya ule wa chama kilichomsimamisha kwenye uchaguzi?
Pia nani anayetambulisha jina la Diwani? na kwamba nani anatoa taarifa kwa msimamizi wa uchaguzi kuhusu mabadiliko ya chama [mfano kubadili bendera]?
KAMA MAJIBU YA HAYO MASWALI HAPO JUU HAYARIDHISHI THEN:-
1. Mayor wa Arusha kafanya uhaini
2. Muchika Kafanya Uhaini
3. Mkurugenzi kafanya uhaini
4. Madiwani wamefanya jinai kwenda kikaoni

Mtaalam wa utawala anisaidie hili swali:
Je, Mayor anawajibika kwa Madiwani au kwa Waziri mkuu TAMISEMI?;
Pia nani anayetambulisha jina la Diwani? na kwamba nani anatoa taarifa kwa msimamizi wa uchaguzi kuhusu mabadiliko ya chama [mfano kubadili bendera]?

Barua ya Mkuchika haipo kwani yeye sio waziri wa TAMISEMI kwa m,ujibu wa sheria ni kuwa waziri ni Mizengo Pinda na ndio barua zake zinatambulika kisheria na hivyo ni kama haipo ni kihereher tuu cha Mkuchika .

Kuhusu Meya , anawajibika kwa madiwani waliomchagua ila sio kwa waziri .

Nami namunea huruma...huyu baba ambae amepoteza dira na hata mwelekeo umebakia ushabiki na masaburi yake kama wametumia pesa zao magamba kuwanunua wale madiwani walie tu maana wakumbuke hata magamba walitaka kumpoka kadi SS ili aukose uspika ina maana cdm wangeweza kuwarudisha hata kama cdm wangekuwa ndio chama tawala?mbona wanajidhalilisha namna hiyo??aibu sana hata kwake mwenyewe ss ametlshatoa hukumu ......hakimu amuite na kumpa onyo kali na karipio kuwa asichezee mahakama....

Mtaalam wa utawala anisaidie hili swali:

Je, Mayor anawajibika kwa Madiwani au kwa Waziri mkuu TAMISEMI? na kwamba kwa nini atumie waraka wa TAMISEMI kuwatambua madiwani badala ya ule wa chama kilichomsimamisha kwenye uchaguzi?

Pia nani anayetambulisha jina la Diwani? na kwamba nani anatoa taarifa kwa msimamizi wa uchaguzi kuhusu mabadiliko ya chama [mfano kubadili bendera]?

KAMA MAJIBU YA HAYO MASWALI HAPO JUU HAYARIDHISHI THEN:-

1. Mayor wa Arusha kafanya uhaini

2. Muchika Kafanya Uhaini

3. Mkurugenzi kafanya uhaini

4. Madiwani wamefanya jinai kwenda kikaoni
Duh!!
Tendwa hahusiki na uchaguzi wa madiwani.Tendwa anahusika na vyama vya siasa na wanachama wao.
Meya anawajibika kwa halmashauri,huwezi kumfukuza kazi kiongozi aliyechaguliwa na wananchi,unless akivuliwa uanachama kihalali.Either akubali yaishe au mahakama ithibitishe uhalali wa kufukuzwa uanachama.
Msilazimishe mambo,acheni demokrasia ifuate mkondo wa sheria.Kuandamana kuelekea kambi ya jeshi ni uhaini na ni tendo la vita.

....................Mengi yanakuja tusubiri,hili jambo liko wazi na nadhani ni muda wa wananchi kudai hela zetu wanazolipwa watu wasiotambulika wanatoka wapi(watu walifukuzwa uanachama) naomba CDM tufungue kesi kupinga maamuzi yote yatakayofikiwa wakati hawa wanafiki wakiwa vikaoni maana haijulikani wanafanya hayo kwa manufaa ya nani? maana hawaudhurii vikao vya chama kujua msimamo wa chama chao,na wanakwenda kutoa maamuzi gani sasa...............huu ni uhuni na kuendesha nchi namna hii sidhani kama ni uungwana wanaousema hao viongozi,ni uchokozi wa CDM na tukichukua hatua tutasemwa kuwa sisi ni washari,hapa ukiandamana nani atabisha? hapa ukipandwa na hasira nani hatabisha? tuwe wazi na tuache uchokozi wa wazi kwa vyama vingine jamani.....

Hakuna haja ya kutukanana, matusi hayo kila mmoja anayafahamu na ana uwezo wa kutukana. Mkuchika hajatengua maamuzi ya CDM bali ameweka "pending" kutambua maamuzi hayo ili kupisha maamuzi "Mama" ya mahakama. yeye "mkuchika" ndio kiongozi mkuu katika Tamisemi, mwenye dhamana ktk wizara hiyo.ndio maana walimpelekea maamuzi ili ayatambue.sasa kama kuna "hitilafu" hapo unategemea atafanya nini kama sio kusubiri ili hitilafu hiyo iondolewe? Hatutajenga kwa kutukanana japo unaona kuwa tu mbalimbali na hatuwezi kuonana, ila si desturi nzuri.

Mbona hujazungumzia tofauti za mtazamo kati ya Mkuchika na Tendwa wote wateuliwa wa Rais mmoja?

Mkuchika alipelekewa maamuzi na Meya wake maana hatambuliki na asili mia kubwa ya wana Arusha. Mbaya zaidi hao madiwani wamefungua kesi kurudishiwa uanachama wa CDM. Mahakama haijawarejeshea kwa hiyo wanakosa sifa ya udiwani, kwa sababu kwa mujibu wa katiba udiwani lazima utokane na dhamana ya chama cha siasa.

Ila kimasaburi ya ccm zidumu fikira za mwenyekiti hata kama ni kiwete kichwani haya yanawezekana.

Ndiyo maana nikauliza kuna Kesi Mahakamani ya wale waliokuwa Madiwani wa Arusha kuomba/kutaka warudishiwe uanachama? Tuanzie hapo!

Kwa mtazamo tuuu hapo mkuu ni kuwa mahakama nayo imetumiwa kwa mgongo kama ule wa akina Luhanjo na akina Jairo order from juu kuko this ridiculous mahaka ndio muhimili mwingine kabisa unashindwa kuwashauri hao madiwani kisheria na kikatiba kuwa hilo swala haliwezekani bali wao ni kuunga na hao madiwani kuweka pinga mizi kusudi ili tu kuwepo na hali chafu basi wakose wote ndio taswira inavyo jengwa hapo ndio hayo sasa Tendwa, Mkuchika, mwanasheria, na serikali na waziri mkuu wanapo pisha still wanatuona sie ma zuzu vile na ndio me nika sema kuwa kama kweli CCM wanajiamini kuwa Mayor anatoka kwa kundi lao kwanini wasirudie kura worry yao hapo ni nini?? au matokeo ya ubunge walijua walichakachuana na ndio maaana they dont even thrust among themselves na ndio wakakimbilia kukwapua cheo cha Mayor harakaharaka ili waingie kwenye vuta nikuvute ili hali kama hii ije, CCM wakikosa jimbo walilokuwa nalo obvious watafanya juu chini kuwa chafua tuuu na kuwagonganisha wao wana kaa kimya na kutumi dolla na kuvunja Katiba na sheria za nchi.

My Take:
Hawatorudishiwa uwanachama wao kwani CDM ilisha toa Tamuko period.

NB: Hilo sakata lote "Mayor/Madiwani-Arusha"CCM wana husika kwa 100% take my words wana JF period

.....Either akubali yaishe au mahakama ithibitishe uhalali wa kufukuzwa uanachama..

Nani akubali yaishe ?????

Mahaka itathibitisha je itapitia Katiba ya Chama hicho, hebu nipe kidogo tafsiri yako mahakama ithibitishe uhalali wa kufukuzwa? refer kwa Kesi ya hao madiwani kuanzia muafaka ulipo anzia kinyemela alafu mahaka ituthibitishie kuwa hata ule mkataba ulikuwa halali au batili?

Nani akubali yaishe ?????

Mahaka itathibitisha je itapitia Katiba ya Chama hicho, hebu nipe kidogo tafsiri yako mahakama ithibitishe uhalali wa kufukuzwa? refer kwa Kesi ya hao madiwani kuanzia muafaka ulipo anzia kinyemela alafu mahaka ituthibitishie kuwa hata ule mkataba ulikuwa halali au batili?
Diwani akubali yaishe.....akikata rufaa,mahakama ndio itathibitisha uhalali wa kufukuzwa.

Suala hili lina utata, lipo mahakamani. Mkuchika yupo sahihi, hawezi kutambua kuvuliwa kwao wakati suala lipo katika vyombo vya sheria. hata kwa mfano suala la kujivua kwa Rostam kama lingekuwepo mahakamani.bunge lisingeweza kutambua kutokuwepo kwa mbunge katika jimbo la igunga. hivyo kauli ya mkuchika ipo sahihi hadi pale mahakama itakopotoa maamuzi yake. "Mnyonge mnyongeni haki yake mpeni" wale bado ni madiwani kama sheria inavyomtambua "mhalifu" kuwa hana hatia hadi pale sheria itakapomtia hatiani. Tenda ndiye aliyekurupuka.

Mtanyosha tu maelezo mwisho wa siku, sheria ni msumeno mama! Soma katiba vizuri, uanachama ndo tiketi ya wao kubaki kuwa madiwani otherwise hawana namna zaidi ya kukubali yaishe. Hawnauwezo wa kukilazimisha chama kiendelee kuwadhamini kama wameshindwa kutimiza masharti ya uanachama. Na kwenda mahakamani huku wakiacha kukata rufaa kwenye ngazi za chama ndiyo wamekoroga kila kitu kabisa!

Hapo Nnape Mnauye ndio ajue kuwa CCM ni sehemu ya "mgogoro" wa CDM na waliokuwa madiwani wake, maana waziri anatoa maagizo kwa mkurugenzi kukiuka katiba, Waliokuwa madiwani wanatambua kuwa wao si wanachama wa CDM ndiyo maana wanaiomba mahakama iwarudishie uanachama wao. Mkuchika nae anasema ni wanachama hadi hapo mahakama itakapo amua vinginevyo. Kweli mwaka huu vioja ni vingi na bado vinakuja toka kwa aina ya viongozi wa serikali hii

Kwa hili nimejifunza kitu kimoja kwamba katiba na sheria za tz zimetungwa kwa ajili ya walala hoi na kukandamiza vyama vya upinzani na kwa maslahi binafsi ya ccm

Namshukuru Mungu kuzidi kutuonye jinsi serikali yetu wanavyotetea ujinga na upumbavu kwa maslai ya chama yasiyotusaidia chochote sisi raia zaidi yakutugandamiza

Back
Top Bottom