Tendwa, Mkuchika watofautiana kuhusu waliotimuliwa udiwani AR

Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
219,422
911,172
Tendwa,Mkuchika nao watofautiana vikali

*Ni kuhusu madiwani waliofukuzwa CHADEMA
*Tendwa: Diwani akiishafukuzwa ndio kikomo
*Mwanasheria: Mkuchika sasa amekiuka katiba

Na Gladness Mboma

WATENDAJI wa juu ndani ya serikali ya Rais Jakaya Kikwete wamezidi kutofautiana vikali na
kutoa misimamo inayokinzana, safari hii ikiwa ni zamu ya Msajili wa Vyama vya Siasa, Bw. John Tendwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, (TAMISEMI), Bw. George Mkuchika kuhusu sakata la madiwani wa CHADEMA waliofukuzwa uanachama mkoani Arusha.

Wakati Bw. Mkuchika akiruhusu madiwani watano waliofukuzwa na CHADEMA kuruhusiwa kuendelea kuhudhuria vikao vya baraza na kutakiwa kulipwa stahili zao zote, Bw. Tendwa ameshangazwa na uamuzi huo na kusema kuwa serikali haiwezi kutengua uamuzi wa chama.

Akizungumza na gazeti hili jana, Bw.Tendwa alisema kuwa alishangazwa na uamuzi huo wa Bw. Mkuchika na kusema kuwa Bunge au diwani akiishafukuzwa uanachama ndio kikomo cha uongozi na ili kurudishia uongozi ni lazima hoja itenguliwe na mahakama.

"Serikali haiwezi kutengua uamuzi wa chama, haiwezekani hata kidogo, na kama mtu siyo mwanachama hawezi kuwa na wadhifa wa kubunge au diwani ni nafasi za siasa," alisisitiza.

Bw. Tendwa alitofautiana na Bw. Mkuchika kwa uamuzi wake wa kuandika barua kwa Meya wa Manispaa ya Arusha Bw. Gaudence Lyimo kuhusu hatima ya madiwani ya kutaka waendelee kuhudhuria vikao vyote vya baraza na kulipwa stahili zote hadi mahakama itakapotoa uamuzi.

Alisema kuwa yeye mpaka sasa haamini kama kweli Bw. Mkuchika ameamuru madiwani hao waendelee na kuhudhuria vikao vyote vya baraza huku wakiwa wamevuliwa uanachama na kwamba ameingilia uhuru wa mahakama.

"Huwezi kutengua lolote la mahakama, kwa kuwa kufanya hivyo utakuwa umeingilia uhuru wa mahakama," alisema.

Alisema kuwa hata Meya wa Arusha alitakiwa kuangalia sheria zinasemaje badala ya kukubali kupelekwapelekwa, kwa kuwa kesi hiyo iko mahakamani walichotakiwa kusubiri ni uamuzi wa mahakama pekee, ambao ndio yenye mamlaka ya kuwarejeshea uanachama au la.

Hivi karibuni, Bw. Mkuchika alidaiwa kukiuka Katiba ya nchi kutokana na kuandika barua ya kuruhusu madiwani watano waliofukuzwa na CHADEMA kuruhusiwa kuendelea kuhudhuria vikao vya baraza na kutakiwa kulipwa stahili zao zote.

Akizungumza na waandishi wa habari mwishoni mwa wiki baada ya kuahirishwa kwa kesi ya viongozi wa chama hicho katika Mahakama Kuu Mwanasheria, Bw. Method Kimomogolo alitoa kauli hiyo baada ya Katibu Mkuu wa CHADEMA Dkt. Willibrod Slaa kuonyesha nakala ya barua iliyotoka kwa Bw. MKuchika yenye kumb Na. HA 23/235/01/16 ya Agosti 23 mwaka huu iliyotumwa kwa Meya wa Manispaa ya Arusha, Bw. Lyimo kuhusu hatima ya madiwani hao.

Nakala ya barua hiyo ambayo ilibeba kichwa cha habari kisemacho: "Kuvuliwa uanachama hivyo kukosa sifa ya kuwa diwani huku mwisho wa barua hiyo ikisema kuwa 'kutokana na na madiwani hao watano kufungua kesi na kuiomba mahakama kuwarejesha uanachama wataendelea kuhudhuria vikao vyote vya baraza na kulipwa stahili yote hadi mahakama itakapotoa uamuzi'.

Bw. Kimomogolo alisema maamuzi yaliyofikiwa na Bw. MKuchika yalikiuka Katiba ya Muungano kwa vile mtu anayehitaji kugombea uongozi katika nafasi yoyote ni lazima awe na dhamana ya chama.

Alisema kuwa vipengele vingine vinaweka bayana kuwa katika suala la urais, ubunge na udiwani utakoma pindi chama kilichomwekea dhamana kitaondoa dhamana yake na kusema kwa kuwa tayari CHADEMA ilikwishaindoa dhamana kwa madiwani hao sasa hawana sifa.

Bw. Kimomogolo alisema kuwa inashangaza kuona serikali iliyopinga mgombea binafsi mahakamani na kushinda kesi, inakuja kuwatambua madiwani ambao mdhamini wao wamekwishawafukuza ambaye ni CHADEMA.

"Kwenye kesi aliyofungua Mchungaji Christopher Mtikila, ambapo mahakama imeamua hakuna mgombea binafsi, hivyo maamuzi yanayofanywa na madiwani hao kwenye kwenye vikao vya baraza nayo ni batili na posho wanazopokea ni wizi na anayewapa atawajibika kuzilipa,"alisema.

Naye Dkt. Slaa alisema kuwa alishangazwa na maamuzi hayo kwa kuwa madiwani hao walikwishavuliwa uanachama na kupelekea kukimbilia mahakamani ili kurejeshewa uanachama wao hivyo iwapo waziri ataendelea kuwatambua wakati chama hicho kiliondoa dhamana ni kukiuka taratibu za sheria.

Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa hiyo,Bw. Estomii Chang'a alikiri kuipata barua hiyo na kwamba anachokitekeleza ni maamuzi hayo yaliyotoka ngazi za juu.

Madiwani waliofukuzwa CHADEMA baada ya kukaidi maamuzi ya Kamati Kuu yaliyowataka kujivua nyadhifa walizopata kupitia muafaka walioingia bila baraka za chama hicho na kata zao kwenye mabano ni Naibu Meya Bw. Estomii Mallah (Kimandoli),Bw. Charles Mpanda (Kaloleni),Bw. Ruben Ngowi (Themi) na Bibi. Rehema Mohamed (Viti Maalum).

Huyo Meya wa Arusha anastahili kupima mambo na kutenda kwa mujibu wa sheria kwani si kila maagizo yanayotolewa na mamlaka ya juu ni legal & legitimate.

Maamuzi ya kuweka mbele maslah ya chama chao kwa mazingira hayo ya madiwan si sahih.

Na sijui hao madiwan mshauri wao ni nani? (Au Mh. Pinda!) kwan wamepotoka kbs. Kwa kuacha kukata rufaa kwenye BARAZA KUU kama KATIBA ya chama chao (kwa wakati huo) inavyotaka ni kosa kisheria ambalo wanaweza wakapigwa PO

Tofauti hizo kila kona na hakuna wa kuwasaidia wala kuwashika mkono kwani wao nao hawawezi kufikili

Tendwa,Mkuchika nao watofautiana vikali

*Ni kuhusu madiwani waliofukuzwa CHADEMA

*Tendwa: Diwani akiishafukuzwa ndio kikomo

*Mwanasheria: Mkuchika sasa amekiuka katiba

Na Gladness Mboma

WATENDAJI wa juu ndani ya serikali ya Rais Jakaya Kikwete wamezidi kutofautiana vikali na

kutoa misimamo inayokinzana, safari hii ikiwa ni zamu ya Msajili wa Vyama vya Siasa, Bw. John Tendwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, (TAMISEMI), Bw. George Mkuchika kuhusu sakata la madiwani wa CHADEMA waliofukuzwa uanachama mkoani Arusha.

Wakati Bw. Mkuchika akiruhusu madiwani watano waliofukuzwa na CHADEMA kuruhusiwa kuendelea kuhudhuria vikao vya baraza na kutakiwa kulipwa stahili zao zote, Bw. Tendwa ameshangazwa na uamuzi huo na kusema kuwa serikali haiwezi kutengua uamuzi wa chama.

Akizungumza na gazeti hili jana, Bw.Tendwa alisema kuwa alishangazwa na uamuzi huo wa Bw. Mkuchika na kusema kuwa Bunge au diwani akiishafukuzwa uanachama ndio kikomo cha uongozi na ili kurudishia uongozi ni lazima hoja itenguliwe na mahakama.

"Serikali haiwezi kutengua uamuzi wa chama, haiwezekani hata kidogo, na kama mtu siyo mwanachama hawezi kuwa na wadhifa wa kubunge au diwani ni nafasi za siasa," alisisitiza.

Bw. Tendwa alitofautiana na Bw. Mkuchika kwa uamuzi wake wa kuandika barua kwa Meya wa Manispaa ya Arusha Bw. Gaudence Lyimo kuhusu hatima ya madiwani ya kutaka waendelee kuhudhuria vikao vyote vya baraza na kulipwa stahili zote hadi mahakama itakapotoa uamuzi.

Alisema kuwa yeye mpaka sasa haamini kama kweli Bw. Mkuchika ameamuru madiwani hao waendelee na kuhudhuria vikao vyote vya baraza huku wakiwa wamevuliwa uanachama na kwamba ameingilia uhuru wa mahakama.

"Huwezi kutengua lolote la mahakama, kwa kuwa kufanya hivyo utakuwa umeingilia uhuru wa mahakama," alisema.

Alisema kuwa hata Meya wa Arusha alitakiwa kuangalia sheria zinasemaje badala ya kukubali kupelekwapelekwa, kwa kuwa kesi hiyo iko mahakamani walichotakiwa kusubiri ni uamuzi wa mahakama pekee, ambao ndio yenye mamlaka ya kuwarejeshea uanachama au la.

Hivi karibuni, Bw. Mkuchika alidaiwa kukiuka Katiba ya nchi kutokana na kuandika barua ya kuruhusu madiwani watano waliofukuzwa na CHADEMA kuruhusiwa kuendelea kuhudhuria vikao vya baraza na kutakiwa kulipwa stahili zao zote.

Akizungumza na waandishi wa habari mwishoni mwa wiki baada ya kuahirishwa kwa kesi ya viongozi wa chama hicho katika Mahakama Kuu Mwanasheria, Bw. Method Kimomogolo alitoa kauli hiyo baada ya Katibu Mkuu wa CHADEMA Dkt. Willibrod Slaa kuonyesha nakala ya barua iliyotoka kwa Bw. MKuchika yenye kumb Na. HA 23/235/01/16 ya Agosti 23 mwaka huu iliyotumwa kwa Meya wa Manispaa ya Arusha, Bw. Lyimo kuhusu hatima ya madiwani hao.

Nakala ya barua hiyo ambayo ilibeba kichwa cha habari kisemacho: "Kuvuliwa uanachama hivyo kukosa sifa ya kuwa diwani huku mwisho wa barua hiyo ikisema kuwa 'kutokana na na madiwani hao watano kufungua kesi na kuiomba mahakama kuwarejesha uanachama wataendelea kuhudhuria vikao vyote vya baraza na kulipwa stahili yote hadi mahakama itakapotoa uamuzi'.

Bw. Kimomogolo alisema maamuzi yaliyofikiwa na Bw. MKuchika yalikiuka Katiba ya Muungano kwa vile mtu anayehitaji kugombea uongozi katika nafasi yoyote ni lazima awe na dhamana ya chama.

Alisema kuwa vipengele vingine vinaweka bayana kuwa katika suala la urais, ubunge na udiwani utakoma pindi chama kilichomwekea dhamana kitaondoa dhamana yake na kusema kwa kuwa tayari CHADEMA ilikwishaindoa dhamana kwa madiwani hao sasa hawana sifa.

Bw. Kimomogolo alisema kuwa inashangaza kuona serikali iliyopinga mgombea binafsi mahakamani na kushinda kesi, inakuja kuwatambua madiwani ambao mdhamini wao wamekwishawafukuza ambaye ni CHADEMA.

"Kwenye kesi aliyofungua Mchungaji Christopher Mtikila, ambapo mahakama imeamua hakuna mgombea binafsi, hivyo maamuzi yanayofanywa na madiwani hao kwenye kwenye vikao vya baraza nayo ni batili na posho wanazopokea ni wizi na anayewapa atawajibika kuzilipa,"alisema.

Naye Dkt. Slaa alisema kuwa alishangazwa na maamuzi hayo kwa kuwa madiwani hao walikwishavuliwa uanachama na kupelekea kukimbilia mahakamani ili kurejeshewa uanachama wao hivyo iwapo waziri ataendelea kuwatambua wakati chama hicho kiliondoa dhamana ni kukiuka taratibu za sheria.

Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa hiyo,Bw. Estomii Chang'a alikiri kuipata barua hiyo na kwamba anachokitekeleza ni maamuzi hayo yaliyotoka ngazi za juu.

Madiwani waliofukuzwa CHADEMA baada ya kukaidi maamuzi ya Kamati Kuu yaliyowataka kujivua nyadhifa walizopata kupitia muafaka walioingia bila baraka za chama hicho na kata zao kwenye mabano ni Naibu Meya Bw. Estomii Mallah (Kimandoli),Bw. Charles Mpanda (Kaloleni),Bw. Ruben Ngowi (Themi) na Bibi. Rehema Mohamed (Viti Maalum).

Sarakasi za serikali ya Jakaya Kikwete hazitakaa ziishe, kila mtu anatafuta kuonyesha ufundi wake ni kwa kiasi gani anaweza kubinuka ama kupiga msamba!!

Hii ni dalili tosha kwamba serikali na ccm hupandikiza watu wao ndani ya vyama vya upinzani, sasa hapa wameona kwa chadema mamluki na wasaliti hawavumiliwi mkuchika kaamua kujitosa kuwaokoa huku akikiuka katiba na sheria bila hata aibu.

Mkuchika fani yake ni mwanajeshi, kwa hiyo maamuzi yake siku zote ni kukurupuka tu hatumii akili. Alifanya hivyo ili kumfurahisha Chatanda kwa kuwa wote wanatoka Tanga, sasa ngoja tuone.

Sarakasi za serikali ya Jakaya Kikwete hazitakaa ziishe, kila mtu anatafuta kuonyesha ufundi wake ni kwa kiasi gani anaweza kubinuka ama kupiga msamba!!

Hii ni dalili tosha kwamba serikali na ccm hupandikiza watu wao ndani ya vyama vya upinzani, sasa hapa wameona kwa chadema mamluki na wasaliti hawavumiliwi mkuchika kaamua kujitosa kuwaokoa huku akikiuka katiba na sheria bila hata aibu.

Kutofautiana katika misimamo ni jambo la kawaida tu hasa unapoendesha au unapowajibika kwa maamuzi makubwa.

Ndugu Mwita kutofautiana ni sahihi kabisa na ndio demokrasia. Najua kabisa kwamba Msajili anatenda bila kushurutishwa na serikali yeye ni mlezi wa vyama vyote vya siasa nchini. Yuko sahihi kuwa tofauti na serikali lakini sasa katika macho ya wananchi inaleta picha mbaya wakati huyu anasema hivi na yule ansema vile tena hadharani.

Kuna mtu aliwahi kusema kuwa serikali imekuwa kama mavi ya mbuzi sikumuelewa! Kumbe alikuwa anamaanisha jinsi kinyesi cha mbuzi kinavyogawanyika hakiwezi kushikana kila kipingili kiko kivyake!!

///// Mungu atubakishe salama hihi miaka minne ya ccm iliyobaki tutaona kila vi2ko na sarakasizake

Sarakasi za serikali ya Jakaya Kikwete hazitakaa ziishe, kila mtu anatafuta kuonyesha ufundi wake ni kwa kiasi gani anaweza kubinuka ama kupiga msamba!!

Hii ni dalili tosha kwamba serikali na ccm hupandikiza watu wao ndani ya vyama vya upinzani, sasa hapa wameona kwa chadema mamluki na wasaliti hawavumiliwi mkuchika kaamua kujitosa kuwaokoa huku akikiuka katiba na sheria bila hata aibu.

Suala hili lina utata, lipo mahakamani. Mkuchika yupo sahihi, hawezi kutambua kuvuliwa kwao wakati suala lipo katika vyombo vya sheria. hata kwa mfano suala la kujivua kwa Rostam kama lingekuwepo mahakamani.bunge lisingeweza kutambua kutokuwepo kwa mbunge katika jimbo la igunga. hivyo kauli ya mkuchika ipo sahihi hadi pale mahakama itakopotoa maamuzi yake. "Mnyonge mnyongeni haki yake mpeni" wale bado ni madiwani kama sheria inavyomtambua "mhalifu" kuwa hana hatia hadi pale sheria itakapomtia hatiani. Tenda ndiye aliyekurupuka.

Kutofautiana katika misimamo ni jambo la kawaida tu hasa unapoendesha au unapowajibika kwa maamuzi makubwa.

Kutofautiana katika misimamo kweli ni jambo la kawaida, lakini when it comes to uamuzi ni lazima kuwa na uamuzi wa pamoja, ndo hapo tunaposema "collective responsibility".

Kinachoonekana hapa ni kila mmoja kujaribu kumfurahisha bwana wake ili aonekane anafanya kazi ya chama vizuri.

Kama imefikia hatua hata vikao vya cabinet vinaahirishwa kwa kukosa "koram", si ajabu kwa maamuzi kama haya kwakuwa ni dhahiri kwamba hawapati muda wa kukaa pamoja kujadiliana na kukubaliana. Hii ndo staili ya mavi ya mbuzi kama wanavyosema wadau!!

Suala hili lina utata, lipo mahakamani. Mkuchika yupo sahihi, hawezi kutambua kuvuliwa kwao wakati suala lipo katika vyombo vya sheria. hata kwa mfano suala la kujivua kwa Rostam kama lingekuwepo mahakamani.bunge lisingeweza kutambua kutokuwepo kwa mbunge katika jimbo la igunga. hivyo kauli ya mkuchika ipo sahihi hadi pale mahakama itakopotoa maamuzi yake. "Mnyonge mnyongeni haki yake mpeni" wale bado ni madiwani kama sheria inavyomtambua "mhalifu" kuwa hana hatia hadi pale sheria itakapomtia hatiani. Tenda ndiye aliyekurupuka.
wewe ndugu unatumia akili za mirembe sasa chadema kwa kutumia katiba wamehukumu mkuchika akishatengua hukumu mahakama ni ya nini?huna akili na naweza kukuita punguani kwani umeshindwa hata kusoma maelezo ya msajili wa vyama ambaye anawajibika ikulu.
hebu tumia akili hiyo kidogo uliyobaki nayo ya kuvukia barabara.
wewe mkuchika,mery chatanda na magamba wote hamna akili na katika siku uliyoniudhi ni leo.

Suala hili lina utata, lipo mahakamani. Mkuchika yupo sahihi, hawezi kutambua kuvuliwa kwao wakati suala lipo katika vyombo vya sheria. hata kwa mfano suala la kujivua kwa Rostam kama lingekuwepo mahakamani.bunge lisingeweza kutambua kutokuwepo kwa mbunge katika jimbo la igunga. hivyo kauli ya mkuchika ipo sahihi hadi pale mahakama itakopotoa maamuzi yake. "Mnyonge mnyongeni haki yake mpeni" wale bado ni madiwani kama sheria inavyomtambua "mhalifu" kuwa hana hatia hadi pale sheria itakapomtia hatiani. Tenda ndiye aliyekurupuka.

Waliokuwa madiwani wamekwenda mahakamani kuomba mahakama iwarudishie uanachama wao wa chadema, mahakama haijatoa uamuzi kama wanarudishiwa uanachama ama vinginevyo kwa kuwa kesi hiyo haijaanza kusikilizwa. Sasa hapa mkuchika anatokea wapi? anatumia sheria ya nchi gani? bila shaka anatumia sheria ya ccm!!

Hata hivyo kama tukijenga hoja kwamba jamaa wamefungua kesi mahakamani kupinga kuvuliwa uanachama, basi ni mahakama ndiyo ilipaswa kutoa ruling ya ku reinstate uanachama wao as well kuendelea kutambulika kama madiwani halali. Sasa kama mahakama haijatoa uamuzi huo mkuchika hapa amekurupuka na kuandika barua ya ku reinstate udiwani wao kwa sheria ipi? kwa mamlaka gani? ameelekezwa na mahakama kufanya hivyo?

Hapa mkuchika amechemka vibaya na hakuna namna anaweza kukwepa huu upuuzi alioufanya na hakuna maneno yoyote unayoweza kuyatumia kumtetea ukaeleweka, hili liko wazi hata kwa mtu asiye mwanasheria, alimradi anatumia akili yake vizuri anamuona mkuchika alivyochemka.

Kutofautiana katika misimamo kweli ni jambo la kawaida, lakini when it comes to uamuzi ni lazima kuwa na uamuzi wa pamoja, ndo hapo tunaposema "collective responsibility".

Kinachoonekana hapa ni kila mmoja kujaribu kumfurahisha bwana wake ili aonekane anafanya kazi ya chama vizuri.

Kama imefikia hatua hata vikao vya cabinet vinaahirishwa kwa kukosa "koram", si ajabu kwa maamuzi kama haya kwakuwa ni dhahiri kwamba hawapati muda wa kukaa pamoja kujadiliana na kukubaliana. Hii ndo staili ya mavi ya mbuzi kama wanavyosema wadau!!

Sidhani kama kuna tatizo kwasababu wawili hao hawawajibiki kwa boss mmoja.

3 Reactions
Reply
Back
Top Bottom