Teknolojia ya digitali itabadilisha nini

Masulupwete usiogope. Hii ni karne ya Sayansi na Teknologia. Kuhusu mfumo wa Digital ambao ni wa Dunia nzima sio Tz. peke yake ni kuwa, mfumo huu unatumia nafasi (space/Bandwidth) kidogo kwa kurusha vitu vingi kwa mpigo, ambapo mfumo wa "Analogue" ni kinyume chake, yaaani inatumia nafasi kuubwa kwa kurusha vitu kidogo.

Kuhusu antena za glopu, zitaendelea kupeta, ila TV zetu zenye kioo cha "tumbo" hazitaweza kutafsiri na kudisplay picha zitakazorushwa kwa mfumo wa Digital. Sasa hapo ndipo Ving'amuzi vinapohitajika, ili kutafsiri "Signal" itakayopokelewa na antena na kisha kuipa Tv yako signal ya AV (Audio/Video. yaani Picha na Sauti) iweze kudisplay kilichorushwa toka Studio.

Suala la kulipishwa channels ni jambo jingine. Tv. zetu za bure zitaendelea kuwepo tu, yaani ITV, CH 10 TBC1 na zinginezo. Watakachobadilisha wao ni Transmitter zao tu, wataweka za Digital.
Nadhani kwa kifupi utakuwa umeelewa.


Zaidi ya asilimia 90 ya tv zetu ni za dizaini hii (Penye nyekundu)
 
Back
Top Bottom