SoC03 Mapinduzi ya Teknolojia ya Digitali yanavyoweza kuleta Maendeleo ya kiuchumi, kisiasa na kijamii

Stories of Change - 2023 Competition

Robert Heriel Mtibeli

JF-Expert Member
Mar 24, 2018
21,340
51,900
Salama waungwana,

Hakuna anayeupenda, kila mtu anauchukia, Kwa kweli sijawahi kuona hata mtu mmoja anayetaka kuwa Maskini. Kila mtu, jamii na taifa hupigana vita ya umaskini Kwa kila namna wawezavyo. Hii ni kusema vita ya umaskini ni vita inayostahili kuitwa vita kuu ya Dunia. Umaskini unaukaribu zaidi na Njaa, magonjwa, huduma duni za kijamii, miundombinu mibovu, kiwango duni cha elimu, vifo Kwa vitoto vichanga na kiwango kikubwa cha wanaokufa Kwa kukosa mahitaji ya msingi. Kwa ujumla ni hali ngumu ya Maisha ndio umaskini unaoogopwa.

Jitihada mbalimbali za Makusudi zimefanyika Kwa kuunda Programu mbalimbali katika kudhibiti umaskini, ikiwemo Programu ya MKUKUTA(mkakati wa kukuza uchumi na kupunguza umasikini Tanzania), ambayo malengo yake makuu yalikuwa kukuza uchumi ,kupunguza umasikini wa kipato ,ubora wa maisha ya watu na ustawi wa jamii pamoja na kuimarisha utawala bora na uwajibikaji katika awamu ya Kwanza ya Mwaka 2005/2006 mpaka 2009/2010.
Jitihada zingine ni kuunda mifuko ya Maendeleo ya jamii itakayohusika na kukabiliana na umaskini ndani ya jamii kama vile uundwaji wa Tanzania Social Action Fund (TASAF), ambao ulilenga kuzisaidia Kaya Maskini Tanzania. Hizo ni miongoni mwa jitihada chache Kati ya nyingi ambazo zimefanyika katika kupambana na umaskini ndani ya nchi yetu.

Pamoja na jitihada mbalimbali zilizochukuliwa kukabiliana na umaskini ndani ya nchi yetu, makala hii itaangazia mapinduzi ya Teknolojia ya Digitali yakavyoweza kuchochea na kusaidia Maendeleo ya kiuchumi, kijamii na kisiasa katika kuushinda umaskini hapa nchini. Lengo ni kufanya nchi yetu iwe sehemu ya furaha na watu waishi Maisha mazuri ambayo kila mmoja ataridhika nayo;

Katika kupambana na umaskini kiuchumi, kisiasa na kijamii tunahitaji kuyafanya mambo yaliyomagumu yawe rahisi, mahali kusikofikika kirahisi kufikike Kwa urahisi, tunahitaji urahisi lakini urahisi usio na madhara. Ugunduzi wa Mashine mbalimbali umerahisisha mambo mengi, lakini tunahitaji kuwa pamoja, kuwa wamoja kwani umoja wenye ushirikiano mzuri ni nguzo muhimu katika kupambana na umaskini. Na kitu pekee kitakachotuweka pamoja licha ya kuwa sehemu tofauti zenye umbali tofauti ni Teknolojia ya Digitali.

Teknolojia ya Digitali itarahisisha mawasiliano yetu, upatikanaji wa habari na taarifa muhimu za kiuchumi, kijamii na kisiasa Kwa yeyote ambaye atazihitaji, muda wowote atakaotaka Kwa Kutumia zana zana za kielektroniki, mifumo, vifaa na rasilimali zinazozalisha, kuhifadhi au kuchakata data kama Computer au Laptops. Mifano inayojulikana ni pamoja na mitandao ya kijamii, kucheza Gemu za mtandaoni au zilizokwisha kupakuliwa na simu za rununu.

Urahisi huo wa kuhifadhi, kutunza na Kupata maarifa, habari na taarifa ndio utakaoondoa ugumu katika kupambana na Umaskini katika jamii yetu. Nimezungumza habari ya maarifa Kwa sababu kupitia maarifa ndipo tutaweza kukabiliana na changamoto zinazotuzunguka katika Nchi yetu.
Mahali Fulani katika Biblia imeandikwa; Watu wangu wanaangamia Kwa kukosa maarifa" ukweli huo upo dhahiri katika jamii yetu ya Kitanzania, na Afrika Kwa ujumla.

Kwenye Ulimwengu wa Digitali hakutakuwa na haja ya mtu kusumbuka kusafiri umbali mrefu labda Kutoka Vijijini kwenda Mjini, au Kutoka Tanzania kwenda Ulaya Kwa lengo la Kupata maarifa, isipokuwa Mtu atapata maarifa, habari na taarifa akiwa popote Kwa Kutumia teknolojia ya Digital. Hii itachochea na kusaidia Watu Kupata Maendeleo.

Sir Francis Bacon katika kazi yake iitwayo, Meditationes Sacrae (1597), alisema: "knowledge itself is power" akimaanisha "Maarifa yenyewe ni Nguvu" ambapo wengine wakasema Informations is power.
Tunahitaji hiyo power ndani ya jamii yetu. Na mahali pekee tunapoweza kuipata power hiyo ni kupitia kwenye Teknolojia ya Digitali.

Maarifa, ujuzi, Elimu na habari za kilimo, ufugaji, uraia, sheria, Stadi za Maisha, afya, tabia ya nchi, na Aina zote za elimu huweza kuwekwa katika mifumo ya kimtandao, au mitandao ya kijamii na kila mtu anaweza kuipata Kwa gharama nafuu kabisa.

MAMBO AMBAYO YANATAKIWA KUFANYIWA KAZI ILI TEKNOLOJIA YA KIDIGITALI ILETE MATOKEO CHANYA KIUCHUMI, KIJAMII NA KISIASA;

1. Ijengwe miundombinu bora itakayowezesha Teknolojia ya Digitali.
Ingawaje jitihada zimefanyika kujenga miundombinu katika Teknolojia ya Digitali lakini bado yapo maeneo mengi nchini yanachangamoto ya mtandao.
Serikali ijenge Minara, mitambo na mifumo Bora nchi nzima itakayosaidia Watu Kupata mtandao bila tatizo lolote.
Mtu hata akiwa porini au kijijini au akisafiri ndani ya gari awe na uwezo wa kuwasiliana na MTU mwingine Duniani pasipo kikwazo chochote.

2. Gharama za Kodi na ushuru katika zana za Teknolojia za Digitali ziwe nafuu ikiwemo Simu za rununu au simujanja, Computer, laptop na zana zingine ili kufanya kila mtu awe na uwezo wa kumiliki Simu.
Hii sio tuu itasaidia Watu Kupata habari, taarifa na maarifa bali pia itaongeza mapato ya nchi kwani watumiaji wa Teknolojia wakiwa wengi ndivyo Ukusanyaji wa mapato katika serikali unavyoongezeka.

3. Serikali iweke gharama nafuu za vifurushi vya Bando la internet;
Mitandao ya kijamii Kwa sasa ndio soko pekee ambalo litasaidia Vijana wengi kujipatia ajira. Kama serikali itaweka gharama nafuu basi Vijana wengi watapata fursa ya kutumia mitandao ya kijamii kujiajiri, Kwa kutangaza biashara zao, vipaji vyao, ujuzi na taaluma zao, Hii itawaingizia kipato na kupunguza ugumu wa Maisha.

4. Sheria za udhibiti WA habari na taarifa zinazolenga kuleta matokeo chanya katika Nchi.
Serikali itoe Uhuru WA kupeana na kupashana habari pasipo kuingilia Uhuru wa habari, lakini katika kudhibiti idhibiti uhalifu wenye kuleta madhara ndani ya jamii.

5. Teknolojia ya Digitali iwe Kwa jinsia zote.
Umuhimu wa kuwahusisha Wanawake katika Digitali hauwezi kupuuzwa, Kwa sababu anuwai;
i) idadi ya Wanawake ni kubwa kuliko wanaume. Wingi wao usipotumiwa itakuwa NI hasara kama Kwa jamii.
ii) Wanawake ndio Walezi wa watoto., Teknolojia ya Digitali itasaidia kuwalea watoto Kwa urahisi zaidi, Kwa Kupata taarifa na habari nzuri za malezi Kwa Watoto. Zingatia, malezi ya Watoto ndio maandalizi ya taifa la kesho.
iii) Siku hizi Wanawake wengi wamekuwa wazalishaji wakubwa. Hivyo kuwahusisha kwenye Digitali kutazidisha uzalishaji katika maeneo Yao ya Kazi kama vile Umamantilie, umachinga, ufugaji, Vikoba miongoni mwa shughuli zingine.

Hivyo lazima uhamasishaji Kwa Wanawake katika matumizi ya Teknolojia ya Digitali upewe mkazo ili kuleta tija ndani ya jamii.

6. Baadhi ya Huduma za kiserikali Kwa kila wizara zitolewe Kidigitali.
Serikali kupitia kila Wizara ihudumie Watu kidigitali ili kurahisisha upatikanaji WA huduma, Hii itaondoa usumbufu na kupoteza muda Jambo ambalo litachochea uzalishaji.
Kwa mfano, upatikanaji wa Leseni, Usajili wa biashara, upatikanaji wa namba za nida au vitambulisho muhimu ni mambo ambayo yanaweza kufanyika online. Ingawaje inahitaji umakini ili kudhibiti matapeli ambao wanaweza kujitokeza katika kujisajili online.
Huduma za mitandaoni zitapunguza mazingira ya rushwa, foleni, usumbufu wa kurudishwa rudishwa, kwani mfumo utakuwa unaeleza ikiwa kuna taarifa haijakusanywa. Pia itapunguza gharama za nauli na muda unaotumiwa na watu kufuatilia kitu.

7. Elimu ya Teknolojia ya Digitali itolewe.
Kwenye mtaala, iingizwe mada ya tehama, ambapo Elimu ya Teknolojia ya Digitali itatolewe shuleni Kwa Watoto. Lakini piah ni vizuri Kila kata pawepo na mtaalamu wa mambo ya Tehama, au kama itakuwa NI gharama basi watendaji WA kila kata wawe na mafunzo ya Tehama kusudi wasaidie kuelimisha wananchi kuhusu mambo ya Tehama ikiwemo Teknolojia ya Digitali na matumizi yake.

8. Gharama ya makato ya Vifurushi vya Pesa za kimtandao ziwe nafuu.
Kutuma na kupokea Pesa kupitia mitandao ya simu kama M-PESA, Tigopesa, Airtelmoney, miongoni mwa mitandao ya simu mingine inapaswa iwe nafuu ili kuruhusu watu wengi kutumia Pesa.
Serikali pia irahisishe Watu Kutuma au kupokea Pesa Kutoka/kwenda mataifa ya nje. Hii itachochea kupunguza umaskini.

9. Gharama na vigezo vya kusajili Online TV channel ziwe nafuu.
Wapo Vijana wengi ambao watapata shughuli ya kufanya kupitia mitandao ya kijamii Kwa kuwa na online TV zao.
Serikali kupitia TCRA inaweza kuandaa mfumo maalumu wa kujaza fomu mtandaoni Wakati mtu anapofungua akaunti ya online Tv, kisha atalipia kiwango kidogo cha Pesa inaweza kuwa Kwa Mwezi au Mwaka kisha mtumiaji anaweza kuendelea na shughuli zingine katika online TV yake.

10. Serikali iweke Mfumo wa kidigitali Kwa kila mbunge awe na Akaunti yake ambayo kila mwananchi wa jimbo atakuwa na uwezo wa kuandika kero, malalamiko, wazo au ushauri Kwa mbunge wake.
Hii itasaidia Kwa mbunge Kupata Maoni ya watu wake wengi Kwa urahisi hata asipokuwa jimboni kwake. Akaunti hiyo wabunge watakuwa na wajibu wa kuwajulisha wananchi wake kinachoendelea. Pia Hii itasaidia Kwa wananchi wa majimbo mengine kujua changamoto ya majimbo mengine kupitia mfumo wa kidigitali.

11. Serikali iingize Mitaa na majina yake, Kata na miji katika mfumo wa Geographic position system (GPS) iwe Kwa Kutumia Google au namna nyingine.
Hii itarahisisha wafanyabiashara na Wateja kufanya biashara au shughuli zao Kwa urahisi.

12. Kila taasisi ya serikali iwekwe Kamera ya Ulinzi katika kila Kona, pia kila taasisi iwe na namba ya Mkuu wa kituo na website yake ili kuongeza uwajibikaji wa taasisi za umma.
Endapo Mtumishi wa umma atafanya kinyume na uadilifu, mtu ataripoti Jambo hilo mtandaoni na kupiga simu Kwa Mkuu wa kituo muda huohuo,

13. Upigaji wa Kura katika kuchagua viongozi Kwa ngazi za kitaifa mpaka ngazi ya Chini uwe Kidigitali na uwe mubashara.
Teknolojia ya Digitali itachochea demokrasia ya kweli kwamba atakayeshinda ashinde kihalali. Na tutaondoa Ile dhana ya malalamiko ya baadhi ya viongozi wanaosema wameibiwa Kura.
Lakini pia itachochea uchaguzi huru na Haki na kupunguza mazingira ya Rushwa.

14. Sheria za kulinda Haki za faragha za watumiaji wa mitandao ya kijamii na wanaoripoti Kero au Uhalifu iongezwe Makali.
Watu wapewe Uhuru WA Kutumia majina bandia ikiwa watakuwa katika Hali ya kuripoti matukio ya kihalifu au biashara haramu. Na sheria iwalinde. Hii itasaidia polisi na vyombo vya ulinzi kukabiliana na uhalifu nchini.

15. Sheria za maudhui ziseme wazi ni marufuku Kutumia picha ya MTU mwingine, kazi ya MTU mwingine, au Mali ya MTU mwingine mtandaoni bila ya ridhaa yake isipokuwa kama MTU huyo ni mashuhuri au kiongozi wa umma.
Hata hivyo hata kama ni Kiongozi au MTU mashuhuri haitapaswa kumtumia Kwa namna ya kufanya uhalifu. Ili kulinda Haki za Watu. Adhabu Kali zitolewe Kwa watakaoenda kinyume na sheria hizo.

16. Matamasha, propaganda na kila Aina ya mikakati ya kutunza Mazingira iwekwe kidigitali.
Teknolojia ya Digitali itasaidia kutunza Mazingira na kudhibiti uharibifu wa mazingira.
Teknolojia ya Digitali ndio sehemu pekee ambayo itarahisisha utekelezaji wa utunzaji wa mazingira Kwa kutoa Elimu Kwa jamii, kuvumisha habari za upandaji wa miti, utunzaji wa vyanzo vya maji, miongoni mwa mbinu nyingine za kutunza Mazingira.

17. Maudhui yasiyofaa na yanayoharibu maadili yadhibitiwe na serikali ihakikishe hayafikiki kirahisi.
Maudhui ya ngono, matusi, na yenye lengo la kuhamasisha jamii kufanya uhalifu au uharibifu wa maadili yadhibitiwe ili kulinda uadilifu WA jamii yetu.

18. Iwekwe Data Base ya kila fani na taaluma nchi nzima.
Iwe ni madaktari, waalimu, Bodaboda, wauguzi, wanasheria, mafundi nguo, Fundi washi. Kila fani iwe na data base yake. Hii itasaidia kujua idadi halisi ya nguvu kazi ya nchi na pia kuratibu mipango na Sera.

19. Serikali kuwapa Sapoti wamiliki wa Mitandao ya kijamii lakini pia kuangalia namna ya kusapoti Waandishi wenye tija waliopo kwenye mitandao ya kijamii. Ili kuhamasisha na kuwapa Moyo.

Ama Kwa hakika kama tutumia vizuri Fursa ya Teknolojia ya Digitali tupo katika nafasi nzuri ya kumuondoa adui Maskini katika mipaka ya nchi yetu.
Hata hivyo ili haya yatimie inahitaji Watu wenye sifa zifuatazo;
1. Wazalendo na waadilifu.
2. Wenye Maono
3. Wenye Nia ya kuleta Maendeleo ya Kweli.
4. Wenye Akili na ustahimilivu katika kutekeleza haya.
5. Wanaoheshimu Haki za binadamu.

Karibuni kwenye Mjadala;
 
Serikali iwekeze kwanza kwenye Elimu bora.
Watu wakishapata Elimu bora wataweza itumia mitandao kwa usahihi

Huko mashuleni wafundishwe athari, faida, ubinafsi wa mtu mitandaoni, taarifa za mtu mitandaoni nk

Bila ya hayo kufundishwa tutatengeneza jamii ya hovyo sana.

Sheria kali zitungwe kuhusu ubinafsi wa taarifa, kutumia taarifa za mtu bila ridhaa yake.

Sheria kuhusu surveillance** hii lazima itungwe na hii ndio itasababisha taasisi kufuata wazo lako la kuweka kamera za ulinzi.

Ili kamera zitumike katika kesi itabidi sheria itungwe pia na serikali iweze kuchukua na kufatilia kamera zote
 
Serikali iwekeze kwanza kwenye Elimu bora.
Watu wakishapata Elimu bora wataweza itumia mitandao kwa usahihi

Huko mashuleni wafundishwe athari, faida, ubinafsi wa mtu mitandaoni, taarifa za mtu mitandaoni nk

Bila ya hayo kufundishwa tutatengeneza jamii ya hovyo sana.

Sheria kali zitungwe kuhusu ubinafsi wa taarifa, kutumia taarifa za mtu bila ridhaa yake.

Sheria kuhusu surveillance** hii lazima itungwe na hii ndio itasababisha taasisi kufuata wazo lako la kuweka kamera za ulinzi.

Ili kamera zitumike katika kesi itabidi sheria itungwe pia na serikali iweze kuchukua na kufatilia kamera zote

Ni kweli Kabisa, serikali inayowajibu wa kutoa Elimu Bora, na Teknolojia ya Digitali itasaidia Kwa namna kubwa katika ujifunzaji na ufundishaji.

Kwenye upande wa Kamera Kwa kila taasisi itachochea uwajibikaji Kwa watumishi wanaopenda kuwa under- supervision.
 
Back
Top Bottom