Teknolojia ya digitali itabadilisha nini

Masulupwete

JF-Expert Member
Feb 15, 2012
2,366
2,397
Nimekuwa nikisikia kuhusu mabadiliko ya teknolojia toka mfumo wa analoji kwenda digitali. Naomba nielweshwe mabadiliko haya yataleta ahueni gani kwa mtu wa kawaida. Mfano, Je tutaendelea kudundika na antena zetu za balbu au teknolojia itatutaka kununua dikoda?
 
Ndo maana yake!
Kila kitu digito antena zote zitatupwa chooni.....anza kusaka mawe ya dikoda na ujipange kuilpia kila mwez
 
Hakuna chanel za bure tena labda za dini nazo lazima uwe na dikoda.
 
Hakuna chanel za bure tena labda za dini nazo lazima uwe na dikoda.

Kwa ufupi unamaanisha teknoloj inakuja kuongeza ugumu wa maisha. Ni ya nn basi au ndo mambo yaleyale yakuiga kila kitu km ilivo kawaida yetu
 
Tuna tatizo la cut & paste bila kujali madhara ya hicho tunakiingiza. Kwa staili hii nina hakka watz walio weng tutafungia tv zetu stoo.
 
Kwa ufupi unamaanisha teknoloj inakuja kuongeza ugumu wa maisha. Ni ya nn basi au ndo mambo yaleyale yakuiga kila kitu km ilivo kawaida yetu

hakuna kinachoigwa mkuu...ni maazimio ya dunia nzima...kuna nchi zilishaanz kutekeleza, na nyingine bado kama kina siye ila km sijakosea ifikapo 2015 dunia nzima itakua na mfumo wa digitali ktk urushaji na upokeaji wa matangazo ya tv
 
Kwa ufupi unamaanisha teknoloj inakuja kuongeza ugumu wa maisha. Ni ya nn basi au ndo mambo yaleyale yakuiga kila kitu km ilivo kawaida yetu

huu ni ukoloni mambo leo, yaani wazungu wakaona dawa ni kutumia ujinga huo, kwa lengo la kututawala. haki iko wapi?

nawasilisha hoja
 
hakuna kinachoigwa mkuu...ni maazimio ya dunia nzima...kuna nchi zilishaanz kutekeleza, na nyingine bado kama kina siye ila km sijakosea ifikapo 2015 dunia nzima itakua na mfumo wa digitali ktk urushaji na upokeaji wa matangazo ya tv

Sasa uharaka wa desemba 2012 unatoka wapi wkt hao wenyew walioadvance wameweka lengo ni hadi 2015.Huu ni utumwa mpya!
 
  • Thanks
Reactions: FJM
Tanzania haijajipanga bado kuanzisha huu mfumo wa kidigitali...ndani ya mikoa 30 ya Tz ni mikoa isiyozidi 10 ndiyo ina hivi vitu ving'amuzi, isitoshe hazijawa configured enough kwani channels zinakatakata mno hata uweke vipi hizo antenna zao, Kinachoshangaza ving'amuzi vinalipiwa bei kubwa sana lakini channels za mpira hazionyeshi(esp EPL) Huu ni wizi.
 
Tuna tatizo la cut & paste bila kujali madhara ya hicho tunakiingiza. Kwa staili hii nina hakka watz walio weng tutafungia tv zetu stoo.
Mkuu Masulupwete, pole kwa wasiwasi huo, haya ni baadhi tuu ya mavuno ya globalaizesheni ambapo sisi nchi za kina yakhe tunapokea tuu amri kwa ajili ya utekelezaji na hakuna mjadala!.

Ila hili la digital ni ukombozi mkubwa katika TV, hii inatoa fursa kila mkoa, kila wilaya, kila sekta etc kuwa na uwezo wa kurusha matangazo yake ya TV bila kuhitaji kuwa ni kituo cha utangazaji!.

Hata sisi jf, nitamshauri Max, tutakwenda hewani. Zile Padomatic toka kule Mwanakijiji.com zitaruka live kwa wote kuona, kutakuwa na Chadema TV, CCM TV, CUF TV hata mimi kama mtu binafsi nitakuwa na TV Channel yangu Pasco wa JF Live Tv!, humo nitamwaga ma thread ya maana kutoka humu jf!.
 
Nimekuwa nikisikia kuhusu mabadiliko ya teknolojia toka mfumo wa analoji kwenda digitali. Naomba nielweshwe mabadiliko haya yataleta ahueni gani kwa mtu wa kawaida. Mfano, Je tutaendelea kudundika na antena zetu za balbu au teknolojia itatutaka kununua dikoda?

nenda jukwaa la tech na gadgets hii kitu imeelezewa vizuri tu na michango ya kila aina..
 
Masulupwete usiogope. Hii ni karne ya Sayansi na Teknologia. Kuhusu mfumo wa Digital ambao ni wa Dunia nzima sio Tz. peke yake ni kuwa, mfumo huu unatumia nafasi (space/Bandwidth) kidogo kwa kurusha vitu vingi kwa mpigo, ambapo mfumo wa "Analogue" ni kinyume chake, yaaani inatumia nafasi kuubwa kwa kurusha vitu kidogo.

Kuhusu antena za glopu, zitaendelea kupeta, ila TV zetu zenye kioo cha "tumbo" hazitaweza kutafsiri na kudisplay picha zitakazorushwa kwa mfumo wa Digital. Sasa hapo ndipo Ving'amuzi vinapohitajika, ili kutafsiri "Signal" itakayopokelewa na antena na kisha kuipa Tv yako signal ya AV (Audio/Video. yaani Picha na Sauti) iweze kudisplay kilichorushwa toka Studio.

Suala la kulipishwa channels ni jambo jingine. Tv. zetu za bure zitaendelea kuwepo tu, yaani ITV, CH 10 TBC1 na zinginezo. Watakachobadilisha wao ni Transmitter zao tu, wataweka za Digital.
Nadhani kwa kifupi utakuwa umeelewa.
 
itakuwa ngumu sana , wanatayalisha tz kuwa walevi maana wote tutakimbilia baa zenye decoda, sijui walokole wataenda makanisani kwao?
 
Pasco unavyoielezea inaonesha ni kitu rahisi saaaana na kitamfikia kila mtu mpaka wa chini ya dola moja si ndio?
 
Mimi huu mfumo bado siuelewi kabisa labda mpaka utakapoanza kufanya kazi.
 
:A S 465:Hii kitu inaelezewa kwa maelezo mepesi na kutufanya tuamini ni kitu rahisi kisicho na gharama. Baadhi tunaweza kukubaliana na maelezo hayo kwa sababu ni kitu kigeni na bado mfumo wenyewe haujaanza kufanya kazi. Walio wengi hatuelewi the whole set up.

Ila inavoonekana kwa namna yoyote iwayo hii kitu lazma itutoe pesa...hata km hutanunua dikoda badala yake ukaamua kwenda bar.
 
Back
Top Bottom