Uchaguzi 2020 TEF yamaliza Mgogoro wa TBC na CHADEMA, wapeana Mkono

Wakiongea ujinga tunakata tena! No way!
I thought so. TBC na CCM ni kama Chanda & Pete. Huwezi attack CCM na TBC wakakuacha hewani.

Haya “maelewano” hayana tija in a big picture na yamelenga kuondoa tu ile sintofahamu ya kufukuzana kwa aibu kutoka mkutanoni
 
Faida gani kwa Chadema imepatikana kwa kuweza kufanya maridhiano na TBC ?

Kwa mujibu wa ilani ya CDM,moja kati ya mambo ya muhimu ambayo Chadema wameahidi kuyafanya ndani ya siku mia moja ni pamoja na maridhiano,kama inavyosema ilani haya yafuatayo :

"Serikali itapeleka Bungeni Muswada wa Sheria ya Maridhiano, ambayo pamoja na mambo mengine itaanzisha Tume ya Maridhiano kwa lengo la kuondoa hofu ya uwezekano wa vitendo vya kulipiza visasi na kuunganisha nguvu za wananchi wote bila ubaguzi wa vyama katika kuongoza Taifa letu''.

Hivyo kama Chadema wangeweza kumaliza siku thelathini bila ya kupata maridhiano na TBC wangeonekana kweli hawana uwezo wa kuleta maridhiano mengine,kama maridhiano haya madogo yamewashinda.

Mtego huu wameuvuka salama.
 
Chadema, unafahamu msemo wa ukipewa milimita chukua kilomita! Hii ni nafasi nzuri sana. Itumieni ipasavyo. Hizo dakika 30 fanyeni yafuatayo:
  1. Ziendelezeni cheche za kwenye kampeni - yale mabomu ya Lissu anayowapiga CCM yarudieni kwenye TV na radio kila mtanzania asikie. Udini, ukabila, ukatili, ahadi za uongo, ushamba na kadhalika.
  2. Sisitizeni tofauti yenu na CCM
  3. Waambieni nyinyi mtafanya nini na kwa njia gani. Mkisema Elimu bure hela inatoka wapi, Afya bure jibu lenu la bima kwa kila mtu ni rahisi kueleweka. Jinsi gani miundo mbinu yenu italeta maendeleo. na kadhalika.
  4. Tangazeni msamaha kwa vyombo vya kiusalama na kusisitiza Tanzania ya neema kwa wote siyo tu kwa wapambe wa chama fulani.
  5. Wahakikishieni wanaCCM watakuwa na nafasi kwenye Tanzania mpya (mnaweza sema mko tayari kubadili katiba kuunda serikali ya mseto) Siyo wote CCM ni makapi.
  6. Mseme nini mtakachofanikisha kwenye mwaka mmoja, miaka mitatu na miaka mitano. Nashangaa watu wanatoa ahadi lakini hawasemi plan yao ni nini. Kwa sasa tunajua kwenye siku 100 mtashughulikia katiba.
 
Naona tbc wameomba pooh!
Baada ya kutimuliwa graph kwa upande wa watazamaji ilishuka balaa, wameona walikosea wanajaribu kuomba radhi kiaina tena kinafiki lakini kilicho ndani yao wanakijua wenyewe!
Hao nec na tbc wanatuhadaa, ningekuwa Mbowe nisingeenda!
 
Sasa hivi msimu huu hakuna chombo Cha habari kitauza habari au ketengeneza faida bila kutangaza au kuwa karibu na chadema. Hakuna! hakuna!

Tuwaonee huruma watu wa habari wanaumia Sana.

Lissu tu ndo atawakomboa
 
Faida gani kwa Chadema imepatikana kwa kuweza kufanya maridhiano na TBC ?
Kwa mujibu wa ilani ya CDM,moja kati ya mambo ya muhimu ambayo Chadema wameahidi kuyafanya ndani ya siku mia moja ni pamoja na maridhiano,kama inavyosema ilani haya yafuatayo :
"Serikali itapeleka Bungeni Muswada wa Sheria ya Maridhiano, ambayo pamoja na mambo mengine itaanzisha Tume ya Maridhiano kwa lengo la kuondoa hofu ya uwezekano wa vitendo vya kulipiza visasi na kuunganisha nguvu za wananchi wote bila ubaguzi wa vyama katika kuongoza Taifa letu''.
Hivyo kama Chadema wangeweza kumaliza siku thelathini bila ya kupata maridhiano na TBC wangeonekana kweli hawana uwezo wa kuleta maridhiano mengine,kama maridhiano haya madogo yamewashinda.
Mtego huu wameuvuka salama.
Hapa ni kuutafuta usawa was jinsi habari zinavyo tolewa na sii zaidi ya Hilo .kwani wanayo nafasi ya kupotosha pindi wakiamua kufanya hivyo,Kama kuonyesha Hali ya kukubalika kwa chama Fulani kwa maana ya wingi au uchache wa wahudhuriaji.
 
Si mlisema hamuombi samahani? Imekuaje tena? Mmeona mambo hayaendi?

Mpaka hapo cdm ilipo haina promo yoyote ya vyombo rasmi vya habari, lakini mziki wake usipime. Jana ITV wenyewe kwenye kipindi chao cha dakika 45 wamepata watazamaji wa kumwaga. Hapo ndio utajua ukikubalika wala hutumii nguvu kubwa. Cdm ni chama cha kizazi hiki, huku ccm ikiwa ni chama cha kizazi kilichopita ndio maana inatumia mabavu na hila kubaki madarakani.
 
Walie wakati wanakila kitu unafikiri na wao wanatoa mabakuli ya kuomba michango ya pesa kama wanasaccos??

Hata Nyerere alitembeza bakuli ili kwenda kudai uhuru wa Tanzania, nini cdm?
 
I thought so. TBC na CCM ni kama Chanda & Pete. Huwezi attack CCM na TBC wakakuacha hewani.

Haya “maelewano” hayana tija in a big picture na yamelenga kuondoa tu ile sintofahamu ya kufukuzana kwa aibu kutoka mkutanoni
Sheria za utangazajj haziruhusu kuonyesha au kutangaza mtu akimwaattack mwingine bila kumpa nafasi mwingine kujitetea. Lazima ubalance habari
 
Back
Top Bottom