Hot bird
Member
- Jan 18, 2021
- 56
- 100
Ninaandika mambo haya kwa masikitiko kutokana na mustakabali wa elimu ya nchi inavyoharibiwa na baadhi ya viongozi kutojali.
Leo nitatoa habari za hali ya rushwa na kutojali ubora wa elimu iliyotawala SUA, hiki ni chuo kikuu kilichopo hapa Morogoro, chenye kampasi kuu Magadu na kitivo kingine kipo Mazimbu.
Katika mtalaa wao wa masomo wa mwaka 2020 na kuendelea, mwanafunzi akifeli mitihani ya supplementary ataruhusiwa kufanya upya mtihani wa kozi husika hii inaitwa “third attempts” ila akifeli hapo ndio anakuwa amedisco.
Sasa cha kusikitisha kuna wanafunzi kadhaa wa kozi za Ualimu Chemistry na Biology (ECB) wamefanya hiyo mitihani ya “third attempts” na wamefail ila bado wameendelea na chuo huku wenzao waliofail wakidisco. Hii imeulizwa sana kwa watawala hapa college ila hakuna majibu ni kama wameziba masikio.
Mitihani hiyo ni CHE100 na ZOO (hizi ZOO ni nyingi)
Nimeamua kuileta hapa maana tunasikia kuna watu wamekula pesa kucheza na elimu hapa chuo, hata ukitoa taarifa hakuna anayefanyia kazi. Haya mambo yametawala sana hapa Mazimbu kuliko kule Magadu ilipo kampasi kuu, japo kule yapo pia ila hawachezi na mitihani wale jamaa.
TCU na TAKUKURU fatilieni haya mambo, inaumiza kuona kuna watu wanapeta bila kupingwa kisa ukabila, udini na rushwa, yaani mwanafunzi kufahamiana na lecture tu hapo uhakika wa kupata A upo, sio fair aisee.
Mimi ninafanya kazi hapahapa chuoni japo sijaajiriwa na serikali wala SUA, ila ni staff kwenye kazi yangu hapahapa, hivyo nimeandika nilichokiona kwa macho yangu lakini mkiona taarifa yangu haina ukweli njooni muhakikishe.
NB: Mkitaka majina ya wahusika yaani hao wanafunzi nitawapa hapahapa, situmii PM, ila nimeshawatajia kozi husika angalieni mtapata ukweli.
Leo nimetoa taarifa hii, kuna ushahidi nakusanya jinsi elimu inavyochezewa hapa chuoni huku TCU na Wizara ya Elimu zikidanganywa, hii nitaileta baada ya wiki toka leo.