TBC1 yasitisha kuonesha baadhi ya Mikutano ya Bunge moja kwa moja (Bunge LIVE)

Chenge amehairisha bunge kuruhusu kamati kujadili TBC kurusha bunge live baada ya upinzani kuhoji uhalali na busara zilizotumika kufikia uamuzi huu.
Bora na jioni tuendelee kufatilia live. Wasitunyanyase kiasi hicho
 
Haina taabu, kujua kilichotokea bungeni muda huo huo au kujua baadaye hakubadilishi chochote.
 
Kwamba gharama ta kurusha live ni kubwa, hivyo watarekodi na kurushwa kuanzia saa nne usiku. Live itakuwa asubuhi tu kipindi cha maswali na majibu. Na Star TV nao...

Wanaweza kutwambia TBC2 inawahingizia kihasi gani cha revenue kwa mwaka?? Kwa nini hawatumii channel hiyo kurusha session ya Bunge hata kama channel hiyo inapaswa kulipiwa.
 
itv
whazap zipo tutaona tuu
Kama information zote zinapatikana kupitia TBC, basi watakuwa wametukomesha, lakini kama kuna njia nyingine ya kupata information, wamechemsha. Mbona hapa nilipo napata habari za bungeni kama kawa!
 
Upinzani wa 2015-2025 hauna capacity wala ability ya ku challenge utawala wa Mpya wa CCM 2015-2025!
hihihihihihiih ccm ni ileile haina mbinu mpya,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,, reginald mengi yupo ajili yetu sisi wazalendo tutaona mpaka huku kwetu nanjilinji
 
Cku zote viongoz wetu si watu wa kutatua matatizo ni watu wa kuyaahirisha tu, hii dunia ya sasa imebadirika huwez kuongoza kwa kuahirisha matatizo na ujanja ujanja, haya mambo athari zake huwa hazionekani hapo hapo huwa zinachukua muda, baadae mtakaa uchi tu lazima. Sasaiv ukizuia tv zisioneshe wabunge watarecord SOUND CLIPS watatuma kwenye social media tutapata ukweli tu japokuwa inaweza isiwe timely hizo recorded mtaangalia ninyi na wake zenu by the way hakuna mtu anaangalia tbc saiv
 
Nimejaribu kuangalia Tbc baada ya kusema kulusha live ni gharama vipindi wanavyoonesha ni vya hovyo hovyo.. Kwa hiyo ni bora Tbc walushe harusi live kuliko mkutano wa bunge
 
Tatizo siyo gharama amesema hivyo ili wavivu msilalamike lkn sababu hasa ni kwamba huu ni muda wa kazi na siyo wa kuangalia luninga, hivyo fanyeni kazi na Bunge mtaliona jioni baada ya kazi au wkend!
Barbosa najua unaweza kufikiri zaidi ya hapo, too sad kuwa umeamua kuchagua upande wa kitu/MTU na wala Si upande hoja/misingi.
 
Kama information zote zinapatikana kupitia TBC, basi watakuwa wametukomesha, lakini kama kuna njia nyingine ya kupata information, wamechemsha. Mbona hapa nilipo napata habari za bungeni kama kawa!
wala haitaathiri kitu tbc walikuwa wanaonyesha documentary wakati wa mambo ya msingi kitaifa yakiendelea, mi sijaona pengo lolote, wala hawajaanza leo kutokuonyesha so hakuna kilichopotea vivaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa nape;););););)


tunaomba harusi ,kitchen party na baikoko kwa wingi live on air
 
Sasa hizo pesa za kulipia vipindi vya bunge nadhani ni sehemu ya kodi zetu swali langu ni kuwa je TBC hawapati ruzuku toka serilkalini au nayo imebinafsishwa kama UDA ,na kama wanapata sasa kigugumizi cha nini wakati wananchi ndio wanaiwezesha ? Kuna baadhi ya vipindi havina manufaa kwa jamii na wanavionyesha huwa vinagharamiwa na nani ,au ndo hawataki wananchi waone mawaziri mizigo wakichambuliwa ?


Ni hivi:

Kinachoonekana hapo ni kubinya Uhuru wa Kupata habari.


Wanasema Hapa Kazi Tu lkn hawataki tuone Mijadala ya hiyo kazi...


Huu ni Ujinga wa kiwango cha Juu Sana
 
Jambo hili kweli linaingia akilini?Waananchi ambao ndio walipa kodi waachwe waamue ikibidi hata kupitia kura ya maoni.

Huu ni uthibitisho mwingine kuwa tatizo la nchi hii ni system na ili kuiindoa hii system,ni lazima kwanza CCM itoke madarakani na kamwe si vinginevyo.

Magu anaendelea kufeli katika sera zake.
 
Back
Top Bottom