Chakaza
JF-Expert Member
- Mar 10, 2007
- 39,838
- 71,302
Ni maafa, tena makubwa sana. Waziri Nape kaleta kauli ya serikali Bungeni kuwa maonyesho ya moja kwa moja Bungeni hayatakuwepo tena eti ni gharama na TBC1 hawana uwezo wa kugharamia shilingi Bil 4 kwa mwaka.
Dalili za kutoruhusu mijadala hiyo hasa kwa sasa wanapoijadili hotuba ya Rais ni kuwa hawataki wananchi waone wabunge wanavyo ichambua na kuiagiza serikali ifanye nini. Jee zuio hili lina baraka za Rais Magufuli?
Mbona yeye anapotumbua majipu anapenda kupata coverage ya TV na Radio na awe hataki serikali yake kuwa kikaangoni watu waone? Hii ni dalili mbaya sana ya utawala wake na ni dhahiri anayoyafanya yana ashiria kuwa ni maigizo tuu na hana nia ya dhati ya uwajibikaji kwa mawaziri ambao tayari kaonyesha kutokuwa na imani nao kuweza kuwakabili wabunge.
Namsifu sana Mhe Zitto Kabwe kwa kuonyesha ujasiri wa kulipigania hilo ingawa amekumbana na vikwazo toka kwa Mwenyekiti wa Bunge Chenge. Chenge pamoja na kutajwa kuwa ni mweledi katika mambo ya sheria lakini leo kaonyesha ni mtupu kabisa na kawekwa pale kwa malengo maalum.Sisi wananchi kama wamiliki wa TBC1 tupinge kwa nguvu chombo hicho kuzuiwa kutuonyesha Bunge live.