Tbc1 sidhani kwa hili kama mko sahihi

kichenchele

JF-Expert Member
Jun 28, 2010
539
176
moja ya vituo vya television ninavyopenda kuangalia taarifa ya habari ni TBC1, lakini juzi nikiwa naangalia taarifa ya habari ya saa 2:00 usiku nikiwa ninafuatilia habari kwa umakini mkubwa, ghafla kikaingizwa kipengele kinachosemekana ni kipya kipengele hiki kinajulikana kwa jina la ENZI HIZO, tena kimechomekwa katikati ya habari, hali hii iliniondolea hamu ya kuendelea kuangalia taarifa ya habari kabisa. mimi ningewashauri TBC1 waandae kipindi maalumu cha kuweza kuonyesha kipindi hiki lakini taarifa ya habari iachwe ijitegemee kuliko kuchanganya mambo.kweli mnataka kupoteza mvuto wa habari, naomba kuwasilisha hoja.
 
ushauri wako ungekuwa na maana kama angekuwepo mtu mzima TiDo, lakini sio huyu kasuku aliyeteuliwa hivi majuzi na JK
 
Tangu wamtimue mtaalam wa mikakati Tido, tbc sasa imekuwa haina mvuto wa tija kwa karibu watz wote waliopevuka! Sasa hivi kinachowabeba ni kipindi cha Zecomedi ambacho kinafuatiliwa zaidi na watoto na akina mama tu.
 
mbona mambo ndo yamenoga, tena taarifa ya habari inavutia sana..mi nawapa dole gumba....keep it up tbc1
 
moja ya vituo vya television ninavyopenda kuangalia taarifa ya habari ni TBC1, lakini juzi nikiwa naangalia taarifa ya habari ya saa 2:00 usiku nikiwa ninafuatilia habari kwa umakini mkubwa, ghafla kikaingizwa kipengele kinachosemekana ni kipya kipengele hiki kinajulikana kwa jina la ENZI HIZO, tena kimechomekwa katikati ya habari, hali hii iliniondolea hamu ya kuendelea kuangalia taarifa ya habari kabisa. mimi ningewashauri TBC1 waandae kipindi maalumu cha kuweza kuonyesha kipindi hiki lakini taarifa ya habari iachwe ijitegemee kuliko kuchanganya mambo.kweli mnataka kupoteza mvuto wa habari, naomba kuwasilisha hoja.

wapoteze mvuto mara ngapi?
 
Back
Top Bottom