Mwigulu uko wapi? Unatakiwa kuonekana kwenye media kila mara, usijifiche

Yoda

JF-Expert Member
Jul 22, 2018
37,621
46,266
Tofauti na mawaziri wengine waziri wa fedha Mwigulu nchemba amekuwa nadra sana kusikika na kuonekana kwenye media akizungumzia mambo muhimu ya wizara yake na nchi kwa ujumla.

Pia tofauti na wizara nyingine wizara ya fedha ndio wizara muhimu na nyeti zaidi kuliko zote katika nchi hii. Hali inafanya uhitaji wa yeyote aliye waziri katika wizara hii kuzungumzia mambo ya wizara hii kuwa muhimu sana.

Mambo muhimu ambayo Waziri wa wizara hii anatakiwa ayazaungumzie katika vyombo vya habari angalau kila robo mwaka/kila baada ya miezi mitatu ni MFUMUKO WA BEI, HALI YA AJIRA na UKUAJI WA UCHUMI. Kwa bahati mbaya sana hili limekuwa halifanyiki. Ni muhimu waziri wa wizara hii atimize wajibu wake hasa katika nyakati hizi amabazo bei za bidhaa na huduma nyingine zinaonekana kupanda kwa kiwango cha juu sana na kuzua malalamiko ya kila aina.
 
Back
Top Bottom