TBC: Huduma hospital Dar zaendelea kuimarika

Hizi ni propaganda chafu na ni aibu kuona raisi dhaifu anadiriki kudanganya umma kuhusu mgomo wa madarakani. Bila aibu raisi anadiriki kusema kuwa madaktari wasiotaka kazi waondoke? Je, anayepata hasara katika hili ni nani? Si ni Tanzania ambayo inapoteza maisha ya Watanzania wasio na hatia na vilevile kupata hasara kwa pesa ilizotumia kusomesha madaktari hao? Kiongozi wa nchi mwenye uzalendo angaliona hilo lakini huyu hana uzalendo na ndiyo maana yeye kila siku ni kiguu na njia. Yeye na serikali yake hawana uwezo wa kutatua matatizo bali kuongeza matatizo na kutugawa Watanzania katika misingi ya udini, ukanda, ukabila, rushwa na ufisadi. Ni lazima tuamke na kudai kuwajibika kwa serikali hii. Madaktari wana haki ya kudai masilahi bora na hakuna aina yoyote ile ya vitisho itakayoweza kubatilisha haki ya madaktari. Propaganda chafu za TBC na magazeti udaku ya Daily News, HabariLeo na Uhuru hazitafanikiwa.
 
Tunashukuru Madakatari wetu kwa kurudi kazini kuendelea na kazi kutibu Watanzania wenzetu.
 
Acheni uzushi na kupotosha watu. hakuna huduma muhimbili national hospital. Unatoa taarifa za uongo kwa faida ya nani??? Upuuzi mtupu
 
Huu ndio uzalendo endeleeni kupiga mzigo, serikali itaendelea kuyafanyia kazi yale yote yaliyo ndani ya uwezo wake; majadiliano pkee ndio njia muafaka.

Chama
Gongo la Mboto DSM
 
kwamba huduma ya afya hospitali za serikali yaendelea kuimarika na huku tamko la madkatari bigwa ni kuendelea kugoma?

Mkuu mbona tumemsikia Dr akiongea anasema wamerudi kazini na wanamuomba rais waendelee na mazungumzo.
 
Fedhehaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa kwa taifa hiliiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii
 
Endeleni kujidanganya na huu uzushi wenu hakuna mtakaowapata, propaganda zenu hazijengi ila zinabomoa zaidi hata ule moyo wa kibinadamu uliopo kwa baadhi ya madaktari wanaofikiria kuwaunga mkono wenzao waliopo kwenye mgomo.
 
TBC kwanini iendelee kupata ruzuku- kodi za watanzania wakati wanatoa habari za kupotosha?
 
Sasa wakati huo huotunaambiwa leo wametangaza mgomo, na wakati huo huo tunaambiwa wamerudi........acheni siasa za kijinga, HAKUNA DR. ALIYERUDI KAZINI!!
 
Mtatapa tapa sana!! Endeleeni kuchezea watu tu, unafikiria mtu atakayebe a mgonjwa wake halafu akafika hospital akakuta hamna kitu atafurahi?
 
Back
Top Bottom