TBC: Huduma hospital Dar zaendelea kuimarika

Msidhani watu bado wanaishi zama za kale! Hata kama ukifungia jamiiforum, facebook, etc...watu hawarudi, leo madaktari bingwa ndio wamemalizia kabisa!
Kama hadi leo hii unategemea taarifa toka kwa TBC yenye ushabiki na si mantiki, ambayo hata wafanyakazi wake wenyewe hawaingalii...pole!
Toka lini huyo daktari awe na njaa huku ana njia mbadala nyingi(kwenda hospitali binafsi, kujiajiri mwenyewe, kwenda nje)
Hebu tuone mwisho aibu hii ni kwa nani, ila sijawahi kuona mwajiri kushindwa kumlipa mwajiriwa na kutotoa mazingira bora ya kazi na MPEWA huduma akishangilia KUTOPEWA HUDUMA KABISA KWA MWAJIRIWA KUACHA KAZI.
 
utafiti umeufanyia mabwe pande

Hiyo ni Muhimbili ya wapi?

Endeleni kujidanganya na huu uzushi wenu hakuna mtakaowapata, propaganda zenu hazijengi ila zinabomoa zaidi hata ule moyo wa kibinadamu uliopo kwa baadhi ya madaktari wanaofikiria kuwaunga mkono wenzao waliopo kwenye mgomo.

Sasa wakati huo huotunaambiwa leo wametangaza mgomo, na wakati huo huo tunaambiwa wamerudi........acheni siasa za kijinga, HAKUNA DR. ALIYERUDI KAZINI!!

na hao bigwa pia wamegoma sasa. ww kalia kughushi tu

Hakuna daktari aliyeko kazini we endelea kutengeneza tamthilia za kukufurahisha badala ya ku propose solution.

uongo wa mchana kweupeee!!!nilikuwa mhimbili mchana leo hii pale Muhas taarifa za uhakika ni kwamba hata madaktari bingwa wameanza mgomo.

Mbona mchana Madaktari Bingwa wametangaza kugoma?

Mh, siamini hadi kesho nitakapojionea mwenyewe, maana nchi hii
hamchelewi kuchakachua hata nyaraka nyeti...

Ni uongo wa tbc huu na magamba kupotosha wananchi na kuwapa matumaini hewa. Mgomo rasmi umeanza na lugalo yazidiwa na wagonjwa. Acheni umanyanya huo.

hii taarifa inaonekna imepikwa...kawadanganyeni vichaa


Tafakari chukua hatua, Kuna nini mbona pro-CDM hawataku kuona mgomo unaisha?
 
hongereni kwa kuchagua fungu jema....... I can join you to fight the good fight
 
Hii itakuwa namna ya kufunika kikombe ili mwanaharamu apite!
Mchana madr bingwa nao wametangaza mgomo bse hawana watu wa kufanya nao kazi alafu mnasema hali shwari.
Mnaleta propaganda kwenye life and death issues?
 
Mi nlishaachaga kuangalia TBC..Tangu wam-frustrate mzee Tido,bhaaas, kwisha kazi yao..
 
Unajua nadhani shida ni neno "Upinzani", watu wanatafsiri kana kwamba kila kitu ni KUPINGA..upinzani ni sawa na kusema vyama ambavyo sera zake haziendani na chama tawala!!Watu mnaoshindwa kuleta hoja n kuongelea ushabiki wa vyama si mahala pake, Hapa tunaongelea wananchi kupata huduma..na wananchi kuwa kimya(huku wakiumia) na wachache ambao hawajafika hospitali kuendelea kuamini taarifa za habari za baadhi ya vyombo vya habari kama vile shirika la utangazaji la Taifa(TBC)
 
Sio mambo ya CHADEMA wala CCM chama, ni upofu wa watu waliopewa madaraka wanaacha kutatua matatizo badala yake wanatupia kelele za propaganda. Madaktari hawajaanza kusema leo kuhusu kudorora kwa huduma za afya. Wabunge wenyewe (angalia hansard) kila wakikaa wanalia na huduma za afya. Lakini kila mwaka wakubwa wanatoa ahadi bila ya kuzifanyia kazi. Sasa imefikia mahali kila mwenye pisa ni India!

Ni juzi tu madaktari wenyewe wameshindwa kumtibu mwenzao (Dr Ulimboka) kwa sababu hawana vifaa! Kwanini viongozi hawalioni hilo? Na kwa nini bunge linatumika kuzima watanzania mdomo?

Huwezi kurekebisha mfumo huu kwa siku moja kama ni madai serikali ilishaanza ya kuyafanyia kazi kama hotuba ilivyojieleza mbona mpaka leo hii jumuiya ya madakatari haijatoa taarifa yao kuipinga yale yaliyosemwa na mh. Raisi? Vifaa wezi wa dawa na vifaa kutoka hospitali za serikali ni waajiriwa wa sekta ya afya wakiwamo madaktari au hilo pia hulijui?

Chama
Gongo la Mboto DSM
 
niliwambia na sasa narudia kuwambia kinachofanyika sasa ni kuwagawa madaktari na kuwachonganishwa kwa wananchi.
kuna vikundi vingi vitajitokeza juu ya kulaani mgomo na kupindishwa ukweli..hawa tunawajua. mtayumbishwa sana kipindi hiki watanzania.
 
Taarifa kutoka Muhimbili. Refer TBC. Mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni, kwenye mabaya asemwe ili ajikosoe lakini kwenye mazuri yake pia asifiwe.





JULAI 2, 2012


Huduma katika Hospitali ya Taifa Muhimbili zimerejea katika hali ya kawaida baada ya Madaktari kurejea kazini Jumatatu ya leo Julai 2, 2012.


Tathimini iliyofanyika kuanzia asubuhi saa mbili hadi saa 11 jioni inaonyesha kuwa katika Idara ya Tiba, Madaktari Bingwa 19 kati ya 21 wamefika kazini ambapo watatu wako likizo. Aidha Registrars wote 12 walikuja kazini. Kliniki zote za tiba zimefanyika kama kawaida.


Katika Idara ya watoto, yenye Madakatari Bingwa 16, kati yao 14 walikuja kazini wengine wawili wako likizo na Registrar watatu kati ya sita walikuja kazini ambapo watatu wako likizo


Upande wa OPD yenye Registrars saba, sita kati yao walikuja kazini na mmoja yuko likizo. Aidha Madaktari Bingwa wote walikuja kazini.


Idara ya Magonjwa ya Afya ya Akili yenye Madakatri Bingwa 10, tisa walikuja kazini na mmoja wao yuko masomoni.


Upande wa Emergency Medicine, Registrars wote 10 walikuja kazini.


Kuhusu huduma za upasuaji, wagonjwa wote waliolazwa wodini wameonwa, na baadhi ya kliniki za huduma ya upasuaji zilifanyika. Hata hivyo, upasuaji haukufanyika kwani hakukuwa na orodha ya wagonjwa waliopangwa kufanyiwa upasuaji..


KWA UJUMLA, MADAKTARI WAMEREJEA KAZINI.


Imetolewa na;




Aminiel Buberwa Aligaesha
Afisa Uhusiano Mwandamizi
Julai 2, 2012
 
Back
Top Bottom