Tatizo siyo watu wanaoishi "mabondeni" bali ni wale wanaoishi "magogoni"

Kwanini watu wanajenga mabondeni?

Siku volcano ya Mlima Kilimanjaro ikiamka na kuleta madhara utauliza pia kwa nini watu wanajenga milimani? Kunaweza kuwa na sababu mbalimbali. Kwa mfano, kuna watu wengine kabla ya kuhamia Dar Es Salaam walikuwa wanaishi mabondeni huko walikotoka ambako kulikuwa na uhakika wa kupata chakula na maji. So, wapokuja Dar wakaona ni deal kujenga mabondeni pia.

Lakini ukweli ni kwamba Dar Es Salaam nzima ikiwemo Magogoni imejengwa mabondeni. At the moment tunawalaumu waliojenga jangwani na Rais anashauri wandoke lakini siku ikitokea sunami naye atakubali kuhama magogoni au ataikarabati Ikulu na kuendelea kuishi pale?

"Naweza kusema binadamu kiumbe cha ajabu." Source - Candid Scope
 
Waziri wa mambo ya nchi za nje ...ni moja wa wamiliki wa nyumba...kwenye bonde la Jangwani ...,nyumba hiyo ipo kwenye bonde la jangwani sehemu iliyopo chini ya mtaa wa mchikichini....,watu winging Wenye nyumba eneo hilo ni pamoja na mbunge zungu,diwani abuu Jumaa...na mfanyabiashara fida Hussein

Anayetaka kuona nyumba ya Membe aende mtaa huo asipite ofisini anuse kupitia wananchi wa kawaida....nyumba hiyo ya Membe kuna kipindi ilivunjwa....mwaka juzi na manispaa ya ilala ...lakini Akaijenga tena...na inasadikika amejenga guest ....au pia anaweza kuitumia kupangisha wananchi wa kawaida...

Huyo ndio Kati ya vigogo aliyewafanya wananchi wa kawaida eneo lile kupata kiburi...

Pole rais mtarajiwa kwa dhahama ya nyumba yako kuharibiwa na mafuriko...
 
Siku volcano ya Mlima Kilimanjaro ikiamka na kuleta madhara utauliza pia kwa nini watu wanajenga milimani? Kunaweza kuwa na sababu mbalimbali. Kwa mfano, kuna watu wengine kabla ya kuhamia Dar Es Salaam walikuwa wanaishi mabondeni huko walikotoka ambako kulikuwa na uhakika wa kupata chakula na maji. So, wapokuja Dar wakaona ni deal kujenga mabondeni pia.

Lakini ukweli ni kwamba Dar Es Salaam nzima ikiwemo Magogoni imejengwa mabondeni. At the moment tunawalaumu waliojenga jangwani na Rais anashauri wandoke lakini siku ikitokea sunami naye atakubali kuhama magogoni au ataikarabati Ikulu na kuendelea kuishi pale?

"Naweza kusema binadamu kiumbe cha ajabu." Source - Candid Scope

Ni makosa kuwahamisha watu wanaoishi bonde la mto msimbazi na kuwaacha wanaoishi kule Mikocheni, Mwenge, Msasani nk. Hao wote wameadhirika. Waanze kuhama wale wa Mikocheni , Mwenge na Msasani, na hawa wa bonde la mto msimbazi watakuwa wa mwisho.

Kinachowasogeza watu pale jangwani si makazi ya gharama nafuu tu, ila nafuu ya maisha kama usafiri wa kwenda makazini, na shuguli nyingine. Ukiwapeleka watu hawa Mkulanga na wakati ni wa kipato cha chini na wengine ni wamachinga, fikiria usafiri wa siku kuja na kurudi huko watamudu?

Mafuriko ni ya msimu, lakini makazi ni ya kudumu, hivyo bora tatizo la muda ambalo linapita na baadaye watu wanaweza kurudia hali ya kawaida kuliko waanze tena adha ya kukaa kwenye mahema na kuumwa na mbu porini huko kusiko na matumaini, na kwa maneno mengine serikali ina mpango wa kwenda kuwatelekeza watu hawa porini, bora wabaki tu walipo.

Jambo ambalo serikali ijitahidi kufanya ni kujenga miundo mbinu itakayosaidia kupunguza tatizo la mafuriko, kwani miundo mbinu ingekuwa mizuri maji yangefuata mikondo iliyoandaliwa badala ya kusambaa kama ilivyotokea. Mafurika kama haya si Tanzania tu, sehemu nyingi tu duniani mataifa maskini na tajiri huathirika kila mwaka, lakini hawasuluhishi tatizo hilo kwa uwahamisha watu na kwenda kuwatelekeza porini, ila wanachofanya ni kujitahidi kuboresha miundo mbinu ya maji taka, na miundombinu ya kuyaongoza mafuriko yafuate mkondo ili maji yasisambae zaidi hapo ningewaona wanaona mbali. Vinginevyo ni kutafuta njia ya mkato ambayo ni kuwaongezea matatizo zaidi waathirika.
 
  • Thanks
Reactions: EMT
Mhh, sasa serikali masikini kama ya Tanzania mnaishauri ifanye nini?

Kuna mji mwingine si taki kuusema, mhhh Mungu apitishie mbali kwa kweli. Ngoja niuseme tu, lakini ni assumption tu, hivi itakuwaje tetemeko la ardhi likiikumba Mwanza? Mhhhh
 
Mhh, sasa serikali masikini kama ya Tanzania mnaishauri ifanye nini?

Kuna mji mwingine si taki kuusema, mhhh Mungu apitishie mbali kwa kweli. Ngoja niuseme tu, lakini ni assumption tu, hivi itakuwaje tetemeko la ardhi likiikumba Mwanza? Mhhhh


Mwanza haiwezi kukumbwa na tetemeko kubwa la ardhi. Arusha, Mbeya, Rukwa na Kigoma ndiyo yanaweza kupatwa na tetemeko kubwa. Hata Dar inaweza kupatwa kiasi na tetemeko la Ardhi au Tsunami.
 
Ikulu ingekuwa mwathirika wa kwanza

Nafikiri tunawalaumu tuu wa mabondeni lakini lakini liktokea janga kama sunami (Mungu epusha mbali) hata wale ambao tunadhani hawaishi mabondeni watakuwa waadhirika wakubwa. With all the talkings on climate change, hatuna hata effective emergency services in place kukabiliana na majanga kama haya. Watu watasema serikali masikini. Sidhani kama watu wengine wanajua wafanye nini linapotokea a certain natural disaster. Tupo tupo tuu.

Preventions from natural disasters are the only techniques which human being can implement to survive. Iif they are implemented on time lots of lives might be saved. Lakini you cannot prevent all natural disasters. So, we need some protection mechanisms in place just in case. Kwa mfano, tetemeko la Japani lilikuwa more than 500 times stronger than the one that hit Haiti. Halafu la Haiti was not followed by a catastrophic tsunami lakini death toll Haiti ilikuwa 10 to 20 times higher than in Japan because of the protection mechanisms that were already in place.
 
Nadhani kwa hili suala nitakuwa na tatizo kama alivyoniambia Nyani Ngabu na kupitia mijadala kama huu naweza kujikuta napunguza ukubwa wa tatizo nililo nalo.

Naomba tukubaliane kuwa chanzo cha matatizo yetu si upungufu wa sheria au watendaji, ni kutojali sheria na kuzisimamia kama inavyopaswa. Tunaona ajali za bara barani, mafuriko katika miji, kipindu pindu, wizi wa fedha za umma n.k zinavyotamalaki

Bus linaloruhusiwa kuchukua abiria 55 linajaza hadi 105, ajali ikitokea huwa ni maafa na masikitiko. Bus hilo ndilo pekee linahudumia mji fulani na vijiji fulani. Wakazi wa huko wanapaswa kulitumia kupata riziki zao na hawawezi kununua magari.
Endapo tutaitumia 'excuse' ya umasikini wao basi hatuna sababu ya kuwa na sheria za bara barani kuwalinda. Tuache waumie tu.

Kipindu pindu kinapozuka askari humwaga vyakula vya akina mama Ntilie ambao hujitafutia riziki zao.
Kwa hoja ya umasikini na riziki hatuna sababu ya kuwafungia biashara au kumwaga vyakula vyao kwasababu hawawezi kufungua 5 stars hotel na hawawezi kuuza mahali pengine kama Mkuranga kwasababu wanapata riziki zao Dar city na ni rahisi kwao kupata mahitaji ya biashara zao.

Tuache madereva wa dala dala wakojoe shule ya uhuru kwasababu wakati wanafanya hivyo huwa wapo katika harakati za kuatfuta riziki na hawawezi kwenda kuanzisha dala dala mkuranga. City haijawajengea vyoo na hivyo ni halali wao kuendelea kujisadia. Hawa ni masikini na wanatafuta riziki zao

Ninachosema hapa ni kuwa kama tunakubali kuwaacha watu hao waishi kwa 'excuse' za umasikini na riziki ,basi excuse hizo zinaweza kuwa extended kila mahali na hapo tutakuwa na vurugu tu kama ambavyo imeanza kuonekana sasa.
Hatutakuwa na moral authority ya kuiambia serikali ifanye ABC kwasababu tumeshajenga excuse ya umasikini na riziki. Sheria ipo wazi hakuna kujenga mabondeni, kwanini tuanze kupindisha kwa sababu za riziki na umasikini?

Bonde la Jangwani halikujengwa wakati wa mkoloni na umasikini ulikuwepo. Sasa kwanini tutafute sababu ili hawa watu waishi pale halafu kila mwaka rambi rambi tu!! na kisha kusema serikali haifanyi kitu. Mimi nadhani tuanze kuibana serikali itumie sheria ili kuzuia maafa kama inavyotumia sheria kumwaga vyakula vya akina mama Ntilie, kushtaki madereva wanaojaza n.k.

Ni kutokana na kutofuata seheria za mipango miji, jiji limesambaa bila utaratibu huku likiwa na vijiji ndani yake. Hivi hatuoni wenzetu wanafanya nini?

Kuna nchi niliwahi kufika, kuna mabonde yapo mjini na hayajajengwa, kuna sheria hata tawi la mti likiangukia paa lako hupaswi kuliondoa ni mamlaka husika. Miji hiyo inasimamiwa na sheria na hicho ndicho tunapaswa kuanza nacho.

Mimi napenda kuiangalia sheria inasema na si kuangalia excuse zitokanazo, na hapo ndipo nahisi tatizo langu lilipo.
 
Wanapewa umeme, maji, shule, zahanati, barabara na masoko. Wanauongozi wa vyama, dini na serikali. Kura zao ni za muhimu pia ili kupeleka watu pale "magogoni". Endelea kujadili.
 
Mkuu wa mkoa wa Dar Es Salaam,Kamanda wa polisi kata ya Ilala, mbunge wa Ilala,waziri wa mmabo ya ndani na Meya wa jiji Madiwani wote wa kata zilizoathilika wanatakiwa wajiuzulu mara moja. They have thined against us , for what they have done and for what they have not done.
 
Naomba kuuliza hivi ni nani kati yetu ambaye akijua kuwa vyombo vya sheria havitasimamia sheria hatochukua advantage ya udhaifu huo? Nguruvi ametoa pointi nzuri sana ambayo naiangalia kwa upande mwingine - watu wanajua kuwa akijaza abiria wengi kwenye gari atapata fedha nyingi lakini ujasiri wa kufanya hivyo anajua ni kwa sababu akisimamishwa na traffic anaweza kupenyeza kitu kidogo; watu wanavunja sheria hizi na taratibu hizi si kwa sababu hawazijui; bali kwa sababu wanajua hakuna kitakachotokea.

Leo hii tunashuhudia ajali za ajabu za mabasi na vyombo mbalimbali (rejea ile mada ya "Fizikia ya Ajali") vya usafiri. Ajali kama hizi haziweti kutokea nchi kama Marekani bila kusababisha outrage. Ajali hizi haziwezi kutokea kwenye nchi zilizoendelea kwa sababu suala la usalama wa vyombo vya usafiri linasimamiwa vikali sana. Lakini nchini mwetu hili siyo suala la kushtua kwani wanaoishi magogoni wanajua ajali ikitokea watatuma rambirambi kwa mkuu wa mkoa husika na kutaka "madereva kupunguza mwendo"! Lakini nani anasimamia quality assurance ya vyombo vya usafiri?

Tunachoona kwenye suala hili la watu wa mabondeni ni kuwa wametumia nafasi ile ile ambayo wengi ya wananchi wetu (hata wasioishi mabondeni) wanaitumia. Wangapi wanaoishi MBezi Beach wakipata upenyo wa kupita mahali wasiporuhusiwa kwa magari watapita? Tatizo liko kwenye law enforcement. Hatuna vitu vinavyosimamia compliance vizuri na hivyo kuweka hii hali ya "kutii au kutotii". Ndio maana nimepuuzia kabisa hii kampeni ya polisi ya kitu kinachoitwa "kutii sheria bila shurti"! Ni nani ambaye anapenda kutii sheria bila kujikuta anashurutishwa kufanya hivyo?
 
Walitembelea bondeni au mafuriko yaliwatembelea wao. Ulitaka magogoni wazuie mvua? au Tanzania ndio nchi ya kwanza duniani kukumbwa na majanga ya mafuriko?
hapo kwenye avatar yako nimemzimia sana yule ninja aliye nyuma yako. mimi nataka kuoa, niunganishie, mfuko wangu pia mzima, futari, ubwabwa vinapatikana bila shida.
 
Back
Top Bottom