Tatizo siyo watu wanaoishi "mabondeni" bali ni wale wanaoishi "magogoni"

Tatzo ni la hawa waishio 'magogoni',kwasababu:-

1. Wanadai watu wanakatazwa kujenga mabondeni,mbona wanawapelekea huduma muhimu kama vile umeme kama kweli watu hawatakiwi kujenga mabondeni wasingewapa huduma hizo muhimu kuonesha kuwa hawatakiwi kuishi kule..

2. Ukiona serikali imewafukuza watu mabondeni ujue wana maslahi na hicho kiwanja(kuna kigogo ana shida nacho/kuna mzungu kapewa kwa jina la uwekezaji)..

CONCLUSION:-
serikali legelege haiwezi ikafanya maamuzi sahii/yenye msimamo..
 
Tatizo liko kwa wote,tena hasa wa mabondeni maana at the end of the time wanaokufa ni wao.

Watu wa mabondeni wanaelewa kabisa kuwa mvua zikija hapo hapakaliki but still wanaendelea kuishi mabondeni, to me nawaona kama wamekubali liwalo na liwe.

MAGOGONI- hawa wana uwezo kabisa wa kuhamisha watu kutoka mambondeni ila wanashindwa kutoa order. Mafuriko yakija wao labda ni kutumia pesa ili kuwahifadhi waathirika.

CONCLUSION:
Watu wa mabondeni wana matatizo maana wao ndo wanaoathirika directly. Kwa hiyo wanatakiwa wahame haraka iwezekanavyo
 
Hadi wanamaliza kujenga na kuhamia, serikali yenye dola na vyombo/taasisi nyingine wanakuwa likizo ya miaka mingapi?
 
Tatizo ni la watu wa Magogoni kwa sababu zifuatazo:-
1. Wameshindwa kusimamia sheria za mipango miji mpaka wametufikisha hapa tulipo ambapo zaidi ya asilimia sabini ya makazi ya jiji hayajapimwa.
2. Wameshindwa kuweka miundombinu ya maji taka ambayo ingezuia mafuriko kwenye maeneo mengi ya jiji
3.Wameshindwa kuwahamisha wananchi waliojenga katika maeneo hatarishi na kuwapatia maeneo mbadala ya kuishi
Nawasilisha hoja.
 
kama hao wa mabondeni ndio waliowaweka madarakani hao wa Magogoni, hivi mwenye tatizo hapa ni nani?
 
Watu wa Magogoni hawana kosa hata kigogo, wamepiga baragumu la kutosha kuhusu hatari za kuishi mabondeni, lakini watu wa mabondeni wameweka pamba masikioni.

Isitoshe baadhi ya watu wa mabondeni wana nyumba za thamani sana na ni waeleewa ambao wangeonyesha mfano, lakini wanendelea tu kuweka pamba masikioni.
 
Ni vigumu kuwalaumu watu waliojenga mabondeni. Nyumba haijengwi kwa siku moja, serikali ilikuwa wapi wakati wanajenga?

Na huwezi kusema kuwa wamevunja sheria kwa kujenga mabondeni kwa sababu serikali ipo!

Kama serikali inaweza kutabiri vurugu, na uwepo wa Al-shaabab wanashindwaji kusimamia ujenzi wa nyumba sehemu za mabondeni? Watu hawa wanapata huduma muhimu za jamii, i.e umeme, sasa leo wanawakana kwa vipi?
 
Magogoni kwa maana ya watawala ndo tatizo kubwa! kama eneo halistahili wanakuwa wapi watu wanajenga mpaka kuingiziwa huduma kama umeme ndani ya nyumba zao? serikali legelege ya kitu kidogo!
 
ukitoka nyumbani kwako ukaenda kulala barabarani kisha ukatafuta mtu kwa kulaumu eti kwa nini lori limekukanyaga lazima una matatizo
 
Tulivyokuwa watoto tuliimba ''Mvua njoo Katarina usije''..........Katrina ikaja 2005......thirty years after I last sang the song.......a coincidence?......sorry for being out of the way
 
waende wap.?
Tanzania ina maeneo mengi sana,hawawezi kosa pa kwenda.Mimi nilishawahi wauliza baadhi yao,walinijibu kuwa wanapenda kuishi pale jangwani kwa sababu ni karibu na mjini,so wanakwenda kwa mguu tu.Hiyo siyo sababu ya kumfanya mtu ariski maisha yake.
 
Waishio mabondeni hawana tofauti na waliovamia bara bara...... Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Dar ilivamia barabara, vivyo hivyo na watu wengine na taasisi za umma na binafsi........

Waishio mabondeni hawana tofauti na wezi wa EPA etc......

Waishio mabondeni hawana tofauti wasafishao wanyama pori hai........

Kimsingi ninasema makundi yote hayo yalianza / yanaendelea kufanya wafanyayo serikali inayojidai pofu kwa sababu mbali mbali ikiona....... Ila haichukui tahadhari mapema kuepusha madhara na hasara...... Yenyewe mara zote inajiandaa kulipa ili huenda na "wao" watoke ktk huo ulipaji. We have a very curative/reactive government....... Sasa hv wanasema japo JK anajua serikali yake haina hela amesema serikali imetoa hekari 2000 Kinondoni to relocate hao wahanga / waathirika wa mafuriko! Kimsingi anasema japo Idara ya Hali ya Hewa kuanzia mwezi wa tisa walitabiri hayo mafuriko, ila serikali yake isiyo tumia "processed info" for evidence-based decision making ilikaa kimya ikijiandaa kutoa hekari 2000 sasa hv na kuzika watu.......

Tutaendelea poteza maisha ya Watanzania wenzetu na mali zao hadi lini?

VIONGOZI LEGELEGE KILA KITU KWAO NI LEGELEGE..............
 
Ni ajabu sana wakati tuna kama kilometa za mraba 945,083 za ardhi watu bado tunabana hapa Dar penye hardly kilometra 1,600 za mraba!​
 
Watu wa magogoni ndio wana makosa!!

Utajuaje kuwa eneo fulani si makazi kulingana na mpango mji? Ni lazima uende ardhi wakafanye survey na ikibidi wakupimie eneo lako.

Juzijuzi tu nina kashamba kangu huko Bunju kabla sijaanza kuweka kanyumba kangu nikajaribu kufanya utaratibu wa kukapima, niliambiwa niandae Tsh 1'500'000/=. Nikaongezea Tsh 500'000/= ikawa mil. 2 nikanyanyua chumba sebule ndo nakokaa nikimuomba Mola lisitokee la kutokea!

Gharama za upimaji viwanja ziko juu mno!
 
Back
Top Bottom