Tatizo siyo watu wanaoishi "mabondeni" bali ni wale wanaoishi "magogoni"

Nakubaliana na wewe Mwanakijiji, tatizo lipo kwa wapangaji wetu wa Magogoni. Ukitembelea nchi zilizoendelea utakuta viwanja kama vya watu wanaishi mabondeni ni bei ghali mno. Kwanza kipo karibu na mto, pili kuna kama mlima. Nchi zilizoendelea hizo sehemu ni bei ghali kama viwanja vilivyo karibu na Bahari.

Tatizo liliopo hapa kwetu ni kwamba serikali haijali wananchi, haitengenezi miundombinu ya kupitishia maji machafu na safi na mazingira mazuri ya kuwafanya watu wanoishi (mabondeni kama wanavyosema) kupata hizo huduma, ingawa kupata hizo huduma hapa Tanzania ni ndoto kama tukiendelea na wajinga hawa waliotufikisha hapa tulipo kwa upuuzi wa watu wachache, uvivu wao wa kufikiria umefika kikomo zaidi ya kukwapua kodi za Watanzania na kuzitumia kwa matumizi yao binafsi bila ya kuwajali walipa kodi wenyewe.

Hebu angalieni Nyumba zilizo sehemu kama hizo za Mabondeni na hakuna mafuriko, tusiwalaumu wakazi wa sehemu hizo wakati tatizo lipo kwa wapangaji wetu wa magogoni wliofikia kikomo cha kufikiria na Wavivu ndani ya vichwa vyao

View attachment 43929


View attachment 43930

Nafikiri, lazima tukubaliane na hali halisi ya mazingira husika na si kujaribu kulinganisha kila kitu. Mfano ulaya, mito yao ni mitulivu sana utafikiri madibwi na ndio maana wanaweza kuitumia kwa usafiri.

Pili mvua ya ulaya ni manyunyu ya afrika sijawahi kuona mvua ulaya zaidi ya manyunyu na ili kutokee mafuriko lazima haya manyunyu ya ulaya yaneyeshe kwa zaidi ya miezi hivyo kwao inakuwa rahisi kupredict maana wanakuwa wanapima mito maji yalnavyongezeka na kuona ya kwamba baada ya siku fulani maji haya yatakuwa yamefika mita kadhaa na kumwagika.

Hii ni tofauti na hali ya afrika, mito inafujo uko km 20 kutoka mto ulipo unasikia mto unaunguruma, wakati ulaya upo sentimenta 1 kutoka kwa mto wala huusikii kama una unaunguruma.

Mvua za afrika hasa Tanzania zinanyesha kwa fujo, inaweza nyesha dakika 10 na ikasababisha mafuriko, tofauti na ulaya ambapo inanyesha miezi kadhaa.

Kwa hiyo kukabiliana na majanga hasa ya afrika, kitu namba moja ni kuhama mabondeni, tukihama mabondeni itawapa fursa jwtz kuwasili na boat yao moja kabla maji hayajafika nyanda za juu.
 
Tatizo ni watanzania wote.Wakiwemo wa Magogoni na wale wa Mabondeni.

Wa magogoni ni tatizo kwa sababu yule waziri aliyekuwa anabomoa majengo yaliyovamia eneo la barabara alichapa usingizi na magogoni wameshindwa kuwajibika na kumwajibisha.

Kama bonde la Msimbazi ni eneo la wazi basi "wanaoishi mabondeni" ni tatizo, tena wanatutia hasara kama taifa yanapotokea majanga haya ya mafuriko.Magogoni inawapasa watumie pesa za walipa kodi kutalii eneo la maafa kwa helkopta na kupeleka vikosi vya "uokozi" aka kukusanya maiti. Pia wanaoishi mabondeni wanalazimisha jamii iwaonee huruma kwa uzembe wao.

Tatizo pia lipo kwa vyama vya siasa na sisi wa mitandaoni, tunafanya kazi, ubishi au debate kama fire brigades/fighters. Ni mpaka linapotokea janga ndio tunatoka usingizini na kutafuta wa kumnyooshea vidole , kutafuta mchawi wakati Elimu ya uraia ikiwa ni pamoja na haki na wajibu wa raia inatolewa wakati wa kutafuta kura tu za kuelekea magogogni au kuwarubuni raia kujiunga na chama fulani.

Kwa kifupi tunavuna tulichopanda na sote ni tatizo. Wananchi wanalaumu Magogoni halafu wanawachagua hao hao waendelee kukaa Magogoni ili na wao wapate kujenga mabondeni. Kipofu hawezi kumuongoza kipofu mwenzake!
 
Hii Serikali ni Mabwege sana. Nchi za wenzentu suala la kupima ardhi si suala la mwananchi. Sasa kazi yao ni nini?
Wanatakiwa wapime maeneo kabla ya kufuatwa ofisini. Hata nguzo za umeme inabidi unue wewe.
Kweli hii Serikali inamfurahisha Faiza Foxy na Na Vichwa maji wengine.

Ndugu yangu MkimbiziwaMbio, serikali yetu inafanya biashara badala ya kutoa huduma. Basi angalau wananchi tungefahamishwa hiyo faida inalika wapi hamna!
Haya mabilioni yalotumika miaka 50 ya uhuru siwangefidiwa hawa jamaa angalau wakapata pa kuanzia, watasema tatizo halikuwepo!!! Kaazz kweleikweli!!!!
 
Kwamba wanaoishi huko mabondeni ni kosa la serikali au kujitakia kwangu mimi naona si jibu rahisi hivyo kama maisha, uzoefu na ulinganifu katika mazingira mbalimbali duniani yanavyokwenda, si kwa kujitakia ila mazingira na uwezo wao haukukwepeka, ndio maana walichagua kuwa tayari kutaabika kwa yahayojilia kuliko kubaki kuwa homeless kutokana na nafasi, uwezo kutowawezesha, na vyombo vya dola kwa busara vimeachia hali hiyo si kwa uzembe, ila kwa mwono wa kibinadamu.

Zamani nilifikiri Watanzania tu ndio tuko wajinga hivyo, lakini nilishika tama siku moja nilipokuwa nchini Marekani mafuriko yalivyotokea katika mmojawapo ya mji ambao ni makao Makuu ya serikali ya state. Kando ya mto majengo makubwa na mahoteli yamejengwa kando yake umbali usiozidi meter 500, hali kadhalika stadium, ofisi za serikali, makampuni, makazi ya watu nk.

Cha kushangaza madaraja yamejengwa juu sana na hayakumbwi na adha ya mafuriko, lakini majengo, ofisi na mahoteli hayakuchukuliwa maanani kujengwa mbali na mto ili kuepusha kama mafuriko yakitokea. Na mbaya zaidi sehemu kubwa ilipojengwa ninayoongelea ni tambalare hali ambayo ni kiashirio cha mafuriko yakitokea hapakwepeki.

Mafuriko yaliyotokea hapo na kushuhudiwa na mimi mwenyewe ni historia ambayo haitasahaulika, kwani number one shopping center ambayo ilikuwa inaiingizia serikali mapato makubwa na resort zake ilifungwa kwa miaka 2-3 hadi kuirejesha katika hali yake ya kawaida baada ya kutumia mabilioni kuikarabati. Stadium ilikuwa ni lake-pond, vituo vya mafuta ndani ya maji, ofisi za serikali kufungwa, makazi ya watu kujaa maji, miundo mbinu kuharika nk. Sikutegemea kama watarudia huko tena bali kuhamisha.

Nilichoshangaa wamerudi tena huko na kuendelea na shughuli kama kawaida ingawa mazingira yale kwa mtazamo wangu hayaruhusu. Nilikuwa naongea na mzungu mmoja kwamba hali kama hii ingetokea Africa ninyi wazungu mngetudharau na kuona licha ya umaskini tunashindwa kufikiri vizuri na kuona mbali, lakini nini kinatokea na bado mnarudia kosa juu yakosa? Aliniangalia tena kwa mara nyingine kwa nusu dakika, kisha akainamisha kichwa na kunivuta mkono, kisha akaniambia; "binadamu kiumbe cha ajabu na hivyo ubinadamu na mazingira ya kiuchumi yanapewa kipaumbele zaidi kuliko mafuriko yanayopita kwa siku moja ukilinganisha watu ambao maisha yao ndio majengo, viwanda, ofisi na mengineyo katika maeneo haya."

Naweza kusema binadamu kiumbe cha ajabu, ni rahisi kuweka utaratibu na sheria ambayo kwa akili ya kawaida unaona itatekelezeka na huyo huyo kesho atafanya kinyume cha alichoamini kuwa sivyo. Pengine fikra za kibinadamu na utu huchukua nafasi zaidi, na pengine kutanguliza busara kuliko kutoa tamko la jumla bila kufikiria mazingira ya mwadhirika. Mambo haya rahisi kwangu kumnyooshea kidole fulani wakati mazingira ya ninayemnyooshea kidole sijakumbwa nayo. Nadharia bila vitendo ni hekaya za kufikirika.
 
  • Thanks
Reactions: EMT
Hadi wanamaliza kujenga na kuhamia, serikali yanye dola na vyombo/taasis nyingine wanakuwa likizo ya miaka mingapi?

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Yusuf Makamaba alishaenda kuendesha bomoa bomoa pale yeye mwenyewe akiwa na chuma la kuvunjia nyumba watu wa haki za binadamu uchwara walisimama kidete upande wa wabomolewaji kuilamu serikali na kuipinga hadi ikazira.Nchi zingine mambo kama haya wote wanakuwa pamoja vyama vya upinzani,NGO,Serikali n.k wakisema bomoa ni bomoa.Tanzania sivyo.
 
Hatuwezi kukimbia personal responsibility na accountability, kuanzia mabondeni mpaka Magogoni.

The buck stops at Magogoni, but it starts mabondeni.
 
Hatuwezi kukimbia personal responsibility na accountability, kuanzia mabondeni mpaka Magogoni.

The buck stops at Magogoni, but it starts mabondeni.

Huwa nafikiria kuwa yawezekana watu wa mabondeni ni watu wale wale ambao utakutana nao sehemu zote duniani. Ndio walio maskini, wasio na nafasi za kufanikiwa, na ambao hujikuta wanategemea serikali katika mambo mengi tu. NI watu hawa ambao utawaona wana squatter kwenye majiji yetu makubwa huku na ndio hawa ambao utawaona wako kwenye soup kitchens. Hawa watu wa mabondeni ndugu yangu hawana Godfather, hawana mtetezi lakini wakati wa uchaguzi ndio ambao hupewa matumaini kweli kuwa sthings will get better only if they vote for the incumbent!

Watu wa magogoni hata siku moja hawawajali watu wa mabondeni isipokuwa wakati wa kampeni!
 
wote wanamakosa

wabondeni wamejenga bondeni kwasababu hawana uwezo wa kujenga kwingineko

wa magogoni wamesababisha wabondeni wakose uwezo kutokana na sera zao
 
Kwa sababu hawana kwingine pa kujenga!

Walipelekwa kibaha wakakimbia. Ukitaka kuona hicho kilojo baada ya hapo nafikiri watapelekwa rufiji, sasa uje uone songombigo lake.teh teh teh teh rufiji haendi mtu na mabondeni watarudi.
 
wote wanamakosa

wabondeni wamejenga bondeni kwasababu hawana uwezo wa kujenga kwingineko

Ni rahisi kusema hili lakini hawa wana "uwezo" wa kujenga mabondeni, kujiletea umeme, kununua samani na hata yawezekana vyombo vya usafiri kutoka mabondeni kwenda kwenye kazi mbalimbali. Kwa sababu utagundua kuwa slums za Tanzania siyo kama za nchi nyingine ambapo utakuta ni uchumi unaojitegemea. Sasa najiuliza kwanini hawa "wenye uwezo " wa kujenga mabondeni wasiwe na uwezo wa kujenga nje ya mabonde hayo? Unless there is something we are missing!


wa magogoni wamesababisha wabondeni wakose uwezo kutokana na sera zao

Lakini watu wa magogoni wanazo sera zao ambazo wamezitekeleza na wanawalaumu watu wa magogoni kwa kutofuatilia sera za magogoni. Kweli kabisa ukisoma viatbuni sera zipo nyingi tu! Na yawezekana ni nzuri maana zingekuwa mbaya hawa watu wa mabondeni wasingekuwa na matawi ya "kile chama"
 
Wakuu zangu nimejaribu sana kulifikira hili na nimekuja na yangu...

Tatizo haswa ni MAGOGONI na pengine siwezi pia kusema magogoni isipokuwa ni dira tulochukua ktk kutafuta maendeleo. Na kilichofuata ni kukosekana kwa ajira vijijini na wananchi wengi maskini ambao hawana uwezo hivyo wamekimbilia mijini (urbanisation) na wamekuta hakuna nyumba za kutosha na kama zipo ni ghali hawawezi kuzimudu hivyo kilichobaki ni kuanzisha makazi mapya..Huko vijijini hakuna kitu kabisa vijana wote wamekimbia waliobakia ni wazee na watoto wachanga wanaolelewa na babu, bibie na mashangazi.

Serikali kwa upande wake hawa sii walengwa. Dhana ya kwamba nchi ikitajirika tutaweza kuuondoa umaskini ndiyo imetawala fikra za viongozi wengi na ndio maana kila siku wanatazama GDP inashuka ama inapanda ili kuweka record zao safi kwa wafadhili wetu..Na nawahakikishia ya kwamba leo hii uongozi uliopo na wengine wote wapo hapa kuwaridhisha wafadhili iwe IMF, WorldBank ama Taasisi zinazotazama na kupima sisi tunafaisha vipi uchumi wa dunia ktk wawekezaji na hasa Wallstreet. That's it. Dhahabu yetu ni mali ya wawekezaji walionunua hisa bank wala hawana haja ya kujua Tanzania iko wapi wala kuna matatizo gani..

Na maadam sisi wote tupo ktk maafa ya mafuriko kiuchumi ingawa hatujioni, hili ni tatizo la Unyapala na ndio maana kila kiongozi wa Kiafrika lazima ajipendekeze Uzunguni kupata support ili kesho akiingia madarakani isiwe rahisi kumwondoa. Na wazungu wamesha tupata wanapotaka. Siku hizi wanatuchagua rais kwa jina la demokrasia na hatuna ujanja wala kuhoji nia na madhumuni yao kwa sababu hakuna rais hata mmoja dunia ya leo ambaye hana mapungufu..

Makosa ni yetu sote kuamini kwamba Ujinga, maradhi na Umaskini unaweza kuondolewa na misaada kwa kutegemea maelekezo kutoka kwa wataalam wazungu ambao interest zao come first.. Na Nyapala kwa kutojua anajikuta hata yeye anajiona mzungu hivyo matatizo ya wabondeni hayamhusu, tena anawaita wajinga sana hawa watu kwenda jenga ktk mabonde na mito..mzizi wa fitna ni kwamba - Tumepoteza DIRA!
 
Tatizo kubwa ni magogoni, sababu wameshindwa majukumu yao ya kuyaendeleza maeneo ya mabondeni, kama hayafai kwa makazi ya binadamu basi yaendelezwe kwa shughuli yanayostahili mfano bustani nzuri yenye mto nk. Eneo likikaa wazi bila plan lazima watu watalivamia kwa makazi au shughuli za kibiashara. Pia magogoni wana wajibu wa kupima viwanja kuweka mitaa inayoeleweka, drainage system, mabarabara na madaraja yenye viwango. Miundombinu duni inachangia ukali wa maafa hata kama tatizo lenyewe ni dogo. Zaidi ya hapo magogoni wanatakiwa kubainisha mipaka ya mabonde mfano uwanja wa yanga uko bondeni au nje ya bonde? bondeni ni wapi na panaishia wapi? Magogoni ni wanafiki, mafisadi na mashwaiba wao wanajulikana kwa kujenga ovyo ovyo mabondeni, kwenye vyanzo vya maji, maeneo ya ufukoni, viwanja vya shule, parks nk na hawasemi kitu sana sana wanapindisha sheria ili kupisha ujenzi, magogoni hao hao wanapigia kelele maskini wanaojenga mabondeni. Ikumbukwe kuwa ujenzi ovyoovyo wa mafisadi unachangia kuziba mikondo ya maji na kusababisha mafuriko. Magogoni hawatoi sababu za kitalaam kwa nini watu waame maeneo yao ya mabondeni, tuwe wakweli kila eneo dunia hii lina mabonde na milima, ndivyo dunia ilivyoumbwa, wako wakazi wa milimani na wa mabondeni na wa tambarare. Kama magogoni wako serious na kazi waliokabidhiwa na wadanganyika wangekuja na maelezo ya kitaaluma ya namna ya kudhibiti mafuriko mabondeni na kutoa ushauri kwa wananchi wa mabondeni juu ya uimara wa nyumba zao na kuweka mipaka maeneo ambayo hayafai kabisa kujengwa hata baada ya kuwepo miundombini stahiki. Serkali ilimeshindwa kutekeleza wajibu wake na sasa inapeleka lawama kwa raia wake.
 
Jibu lako ni zuri sana lakini tulipeleke mbele kidogo - kwanini hawana "kwingine kwa kujenga"?

Sababu kubwa ni uwezo. Dar viwanja ni bei mbaya Mwanakijiji. Viko overpriced kupita maelezo. Kwa ujumla real estate business kwa Tanzania iko shaghalabaghala. Kuna viwanja na properties ukiambiwa bei zake unaweza ukapiga mtu ngumi kwa kuona kama umetusiwa vile. It's ridiculous.

Sasa zile sehemu ambazo si flood zones watu wenye uwezo ndiyo wanazipenda. Na hizo sehemu bei zake kusema ukweli hazikamatiki kwa walio wengi. Na mjini ndipo panaonekana penye fursa nyingi. Hii imesababisha msongamano wa watu. Watu hawa lazima wawe na makazi ya kuishi.

Wakaishi wapi sasa zaidi ya huko mabondeni ambako ndiko wanaweza kumudu gharama za kuweza kujipatia makazi? Kwani wao hawapendi kuishi Masaki na Mbezi beach?

Unajua ku rent chumba bondeni kule kwa Ali Maua au Kwa Mtogole ni kiasi gani kulinganisha na tuseme Upanga au Victoria?

It's a hard knock life out there for a lot of people.
 
Tatizo lipo katika sehemu nyingi na kati ya hizo ni hizi
1. Ubishi- nakumbuka huko nyuma watu wa mabondeni walikumbwa na tatizo hili, serikali ikatoa viwanja vya buree kabisa nje ya jiji, wakazi wa mabondeni wakagoma kuhama. Makamba likuwa RC wakati huo. Suala la viwanja kuwa overpriced sidhani kama lina ukweli

2. Siasa- Kuna wakati mkuu wa mkoa na waziri waliingilia kati suala hili. Watu wa mabondeni wakashusha bendera za CCM na kuweka za CUF na CHADEMA. Viongozi wa chama wakasema zoezi lisitishwe kwasababu ni kero na lishughulikiwe taratibu. Wakati huo uchaguzi ulikuwa karibu na neno taratibu lilitumika kama 'acheni'.

3. Magogoni- Ninashangaa Rais Kikwete ambaye yupo serikalini miaka 20 na ambaye amemsikia Mwinyi akisema hayo, Mkapa akisema hayo naye anayarudia. Huu ni ukasuku. Kama Rais analalamika sisi tufanyeje. Unapokuwa Rais unakubali kusimamia sheria za nchi hata kama zinamfunga mkeo jela. Sheria zipo, viongozi wapo lakini hakuna utashi wa kiungozi. Alichotakiwa Rais ni kutoa suluhu si kulalamika. Hili ndilo tatizo kubwa kuliko yote.

4. Wingi wa veyo- Kwahika nchi yetu ina watu wengi wenye vyeo na madaraka, kwa bahati mbaya hakuna anayejua nini anapaswa kusimamia. Sijui hili ni suala ni la wizara ya makazi na maendelo, sijui ni la mkuu wa mkoa kama serikali kuu, sijui ni la meya wa jiji, au la mkurgenzi wa jiji. Hata wao ukiwauliza hakuna mwenye jibu la nani ashugulikie au ashughulikiwe. Hapa hakuna uwajibikaji ni kurushiani mpira kama ule wa Jairo.

Hayo ni kwa uchache tu.

Yupo mwenzetu amesema haya ni majanga ya asili. Ni kweli lakini hatuna akili ya kupambana nayo. Nchi zote duniani zina mabonde katika miji. Kuna njia mbili, ima kuyaacha maeneo hayo kama yalivyo au kuayaendeleza kwa njia za kitaalamu.

Kufurika maji ni tatizo la drainage mbaya. Ukiangalia bonde la msimbazi hakuna namna maji yanaweza kwenda kwa kasi bila kusambaa. Kwanini river Thame pale kwa mama haileti madhara ya kijinga kama haya.

Hatuwezi kusema janga la Japan ni sawa na janga la Pamba house!!! Pamba house inafurika kila siku lakini hakuna solution huu ni mwaka wa 25, mungu anaingiaje hapo kama si uzembe.

Sidhani pia ni suala la umasikini, umasikini utauona kule kwa mfuga au uwanja wa fisi ambako watu wanaishi katika nyumba za wanazoita mbavu.
Hivi mtu ajenge nyumba ya matofali, aweke fenicha halafu apaki Toyota corrolla pale Young African au Magomeni Takadiri, halafu mtu huyu tuseme kuishi kwake mabondeni ni umasikini!!
 
Back
Top Bottom