Tatizo la ufaulu duni wa masomo ya Mathematics na Physics bado halijaeleweka!

Attelan

JF-Expert Member
Oct 12, 2023
434
701
Niende moja kwa moja kwenye mada. Kutokana na takwimu za Ufaulu wa masomo ya Physics na Mathematics zilizotolewa baada ya matokeo ya Mtihani wa kidato cha Pili kutangazwa, Physics na Mathematics zinaburuza wanafunzi.

Tatizo hili lipo tangu kitambo, japo kuna wale waliobahatika kufundishwa na walimu bora miaka hiyo na walifanikiwa kuisoma Phyiscs ile yenyewe na walitoboa na wanaiweza Physics kwa undani (kwa kiasi chake).

Kiukweli kwa mwenendo huu Physics na Mathematics bado yanaonekana kama madude mazito na Si wadau, si Serikali, wanafunzi wala walimu waliotambua kwanini bado haya masomo yanawanyuka sana madogo na ndio maana bado yanaendelea (masomo) kuwanyuka watu!
 
Naunga mkono hoja
Bahati mbaya imekuwa kama sifa madogo wanafeli alafu jamii inawaambia hayo masomo ni kawaida kuwa magumu.

Kuna shule matokeo yake ya Mtihani wa Taifa wa kidato cha Pili wa mwaka 2022 kulikuwa na C moja na D moja katika somo la Physics, waliobaki wote walipata 'F'. Ikafika hatua mwalimu wa Taaluma akawaambia wanaotaka kusoma Physics wajitokeze hata kama wana 'F', walijitokeza wanafunzi 27.

Ukiwaona hao wanafunzi ambao kwa mwaka huu (2024) wapo kidato cha Nne wanatia huruma, hawana muelekeo, hawaelewi hata mada rahisi za kidato cha kwanza. Ni kama wanasogeza tu siku.

Nikiandika sana nitaishia kutukana na ku'panic' niishie hapa.

Hii Elimu imetupwa na kuachwa solemba kabisa
 
Sababu zinazochangia ufaulu duni ni pamoja na,

1. IQ ndogo za wanafunzi

2. Wanafunzi kutumia muda wao mwingi kwenye mambo ya ngono, bangi, vigodoro, tamthilia, muziki na mpira

3. Usimamizi mbovu wa wazazi/walezi kwa watoto wao.

4. Jamii kuyachukulia masomo hayo kama masomo ya "Wateule" kitu kinachoathiri kisaikolojia mitazamo ya wanafunzi.

5. Mazingira duni ya kujifunzia.

6. Upungufu wa walimu wa masomo hayo, mfano utakuta shule ina wanafunzi 800 ila ina mwalimu mmoja au wawili wa hisabati, kwa mazingira hayo hakuna muujiza wa walimu kumudu kufundisha vema idadi hiyo.

7. Ualimu imebaki ni kazi kama kazi zingine na sio wito tena, hivyo walimu wako busy na maisha kuliko kazi.

8. Siasa.

.Acha niishie hapo kwa sasa.
 
Hali ni mbaya sana, kuna uwezekano hata walimu wa masomo hayo kwa sasa ni weupe balaa.....si unajua mitaala ilishachakachuliwa ndo mavuno yake tunayoshuhudia sasa.

Na vijana siku hizi wamekuwa bize na mambo kibao mara TV, bongo fleva, tamthilia, amapiano, miso misondo na matakataka kibao yaliyoletwa na utandawazi ukilinganisha na enzi zetu ambapo mambo ya TV na simu za mkononi hayakuwepo.​
 
Ukijumlisha na hii kauli ya "Mwalimu hapa ni wapi?" Watastandardize sana matokeo.
 
Sababu zinazochangia ufaulu duni ni pamoja na,

1. IQ ndogo za wanafunzi

2. Wanafunzi kutumia muda wao mwingi kwenye mambo ya ngono, bangi, vigodoro, tamthilia, muziki na mpira

3. Usimamizi mbovu wa wazazi/walezi kwa watoto wao.

4. Jamii kuyachukulia masomo hayo kama masomo ya "Wateule" kitu kinachoathiri kisaikolojia mitazamo ya wanafunzi.

5. Mazingira duni ya kujifunzia.

6. Upungufu wa walimu wa masomo hayo, mfano utakuta shule ina wanafunzi 800 ila ina mwalimu mmoja au wawili wa hisabati, kwa mazingira hayo hakuna muujiza wa walimu kumudu kufundisha vema idadi hiyo.

7. Ualimu imebaki ni kazi kama kazi zingine na sio wito tena, hivyo walimu wako busy na maisha kuliko kazi.

8. Siasa.

.Acha niishie hapo kwa sasa.
Mkuu umemaliza kila kitu. umepita mule mule. Hata hivyo, niliwahi kuandika kwa urefu kuhusu suala la ufaulu duni wa wanafunzi wa kizazi hiki kwenye uzi huu hapa chini.

Moderator tafadhali unganisha huu uzi na uzi uliotangulia ili tuwe na maoni ya pamoja kwa mustakabali chanya wa elimu ya watoto wetu.
 
  • Thanks
Reactions: K11
Haya masomo sio magumu kama inavyosemekana ila tatizo ni walimu wa haya masomo, hapa nadhani muundo wa maslahi ya mwalimu wa masomo ya sayansi uwe tofauti na mwalimu wa sanaa mfano stashahada ya daktari na mwalimu wa fizikia au hesabu iwe sawa.
 
Hili tatizo ndilo linaweza kukuonesha uwezo wa akili za watu wetu na namna wanavyoweza kutatua changamoto mbalimbali katika jamii yetu.

Hisabati, fizikia, kemia na baiolojia ni maisha, kwani hayo masomo yanahitaji akili nzuri ambazo ndo zinahitajika katika kuinua uchumi, kuongeza ubunifu, kutatua changamoto za magonjwa, kukuza teknolojia.

Taifa lipo hapa lilipo kwa sababu akili za watu wengi hazipo kwenye ubora unaotakiwa kwa mstakabali wa maendeleo ya watu wenyewe na nchi kwa ujumla.

Sent from my TECNO LC6 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom