The Palm Beach
JF-Expert Member
- Dec 30, 2015
- 808
- 1,647
Kama kuna eneo ambalo serikali ya JMT inayoongozwa na TANU/ASP kisha CCM tangu uhuru 1961 imefeli spectacularly kisera na kimipango ni la upatikanaji wa huduma bora na ya kuaminika ya nishati ya umeme.
Ni aibu sana kuwa na umeme usioeleweka na unaokatikakatika hata mara 50 kwa siku. Sababu ambazo hutolewa na serikali za marais wote Nyerere, Mwinyi, Mkapa, Kikwete na Samia ni zilezile. (lakini JPM alikuja akabidili mambo, akazikataa sababu hizo na mambo yakawa nafuu saaana).
Inashangaza sana kiasi cha mtu kujiuliza hivi hawa viongozi tuliowapa dhamana ya kimaamuzi na ki - raslimali fedha na watu wana akili nzuri za kufikiri kweli au kuna shida fulani vichwani mwao.
Haiwezekani TANESCO watangaze mgawo au kukosekana kwa huduma ya umeme kwa mikoa kadhaa kwa siku nzima kwa madai ya matengenezo ya miundombinu halafu wakirejesha huduma hiyo still tatizo linabaki kuwa palepale.!
Unajiuliza hawa watu walikuwa wanatengeneza nini iwapo tatizo la kukatika na kuwaka la umeme liko palepale.?
Na tatizo hili limekuwepo na kudumu tangu miaka ya u - Rais wa Mkapa, likaja likawa baya zaidi wakati u - Rais wa Jakaya Kikwete na sababu ambazo hutolewa ni zilezile miaka yote.
Lakini, mimi nikiri wazi kabisa kuwa, wakati wa u - Rais wa John P. Magufuli tatizo hili lilikuwepo lakini lilikuwa nafuu sana kwa kiwango cha kuvumilia na kueleweka kwa zaidi ya 90%.
Cha kushangaza ni kuwa tatizo hili limekuwa baya zaidi mara tu baada ya Rais Magufuli kufa na kuingia huyu mama. Watu tunajiuliza kulikoni? Je, ni serikali inafanyia hujuma wananchi wake.?
Na hata hawa wawekezaji hususani wa kutoka mataifa ya kigeni tunapowaalika kuja kuwekeza hapa nchini kwetu wanatuelewa vipi wanapokumbana na shida hizi?
Hivi CCM humuoni aibu ingalau kwenye ishu hii tu? Mimi nadhani sasa ni wakati mwafaka mkubali kuwa kwenye eneo hili sera na mipango yenu imeshindwa then GIVE UP na kama taifa tukae pamoja, tujadili na kutafuta namna kuifanya nchi isonge mbele...
Rais Samia hii hali haivumiliki. Hawa wananchi mnaodhani mnaweza kuwatendea vyovyote mtakavyo eti tu kwa sbb nyie ni "watawala" au "serikali", wana kikomo cha uvumilivu...
Itafika wakati tutasema, ENOUGH is ENOUGH na matokeo ya kauli hii yanaweza kuja kusababisha nyie viongozi mkakiimbia nchi hii bure.!
Shauri lenu. Jirekebisheni. Toeni huduma sahihi kwa wananchi ili mdai TOZO na KODI zingine kwa uhalali na siyo kwa namna hii...!