Tatizo la masikio: Fahamu kuhusu sehemu za sikio, magonjwa, ushauri na tiba

Kwanza natanguliza shukrani kwa JF wote na hasa madokta wa JF kwa moyo wao wa kujituma.

Mimi nina tatizo la sikio langu la kulia kutoa usaha, na hili tatizo limeshakuwa la muda mrefu,nimeshajaribu kutumia dawa za kienyeji mpaka za hospitalini lakini ninachoambulia ni kustop kwa mda and then tatizo unirudia tena.

Naombeni msaada tafadhali.
 
Pole sana ndugu.

Nakushauri utafute daktari bingwa wa masikio (ENT), umuone. Na akikupa dawa uzitumie na akikuambia urudi tena uzingatie kwa wakati.

Kurudia kwa tatizo baada ya muda ni dalili kuwa matibabu uliyopata japo ni sahihi yanakuwa hayatoshelezi. Inawezekana ukahitaji kufanyiwa culture ili kupata tiba sahihi.

Pole na kila la kheri.
 
Hii kama ni ya muda mrefu inaitwa chronic otitis media, kwa kuwa umeshatumia dawa nyingi then hapa siwezi kukushauri utumie dawa gani, ila nenda hospital kitengo cha ENT kama alivyosema King'asti. Pale muhimbili wapo wengi mfano Dr Edwin, Dr Kimario au Prof. Mushi kama hajastaafu. Wacheki hawa watakusaidia.
 
Jaribu Dawa yangu kisha unipe feedback chukua punje tatu za kitunguu thaumu uziponde kisha utie maji kijiko kimoja achanganye vizuri.Halafu uchukue mchanganyiko huo vitone vitatu utie kwenye sikio linalouma mara mbili kwa siku muda wa wiki. Inshaallah sikio litapona.
 
Wadau naomba mnisaidie,

Nina mwanamke wangu, yeye si mwanaJF ila ana matatizo ya masikio. Anadai kwamba yanamuuma sana kwa ndani na hayatoi usaha. Tatizo lilimuanza mwaka jana na analo kwa mwaka mzima sasa. Kwa anayejua dawa hasa ya mitishamba au ya kienyeji naomba anisaidie ili my wife to be apate nafuu.

Anateseka sana.
 
Usitumie dawa yeyote kabla hujamuona ENT specialist doctor. Dawa nying za masikio ni drops na km ngoma ya cko imetoboka inaenda kuharibu v2 vngne huko ndan. Ukiziw c lazima uzaliwe nao ila uzembe km wenu unasababisha kuongezeka kwa viziwi. Toka mwaka jana anaumwa af yupo 2, hospital hazijui?
 
Usitumie dawa yeyote kabla hujamuona ENT specialist doctor. Dawa nying za masikio ni drops na km ngoma ya cko imetoboka inaenda kuharibu v2 vngne huko ndan. Ukiziw c lazima uzaliwe nao ila uzembe km wenu unasababisha kuongezeka kwa viziwi.

Toka mwaka jana anaumwa af yupo 2, hospital hazijui? Na wewe bla aibu unataka hasa mitishamba! Funguka ndugu yangu nenda nae hospital akafanyie chek up kabla hajapewa dawa. Na c kila dr. Anaweza kutbu mackio dats y nimekwambia mtafute ENT Specialist dr.
 
Back
Top Bottom