Msisafishe masikio kwa kutumia pamba, sikio lina utaratibu wa kujisafisha lenyewe

John Haramba

JF-Expert Member
Feb 4, 2022
365
1,373
Dkt. Jane Bazilio ambaye ni Daktari Bingwa wa Pua, Koo na Masikio kutoka Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Pwani-Tumbi anaelezea kuhusu afya ya sikio.

Anasema "Watu wengi wamekuwa na matatizo ya kupata fangasi kwenye masikio, natoa wito kwa Wananchi kuwa wakati wa kuoga wasiingize maji kwenye masikio na pia wasitumie pamba stick kusafisha masikio.

“Sikio huwa linajisafisha lenyewe, halitakiwi kuingiza kitu chochote kule ndani.

“Unapotumia pamba unaondoa nta kwenye sikio, na watu wengi wanajua ile nta wanayoitoa ni uchafu kutokana na rangi yake ya brown, ule si uchafu una kazi yake ya kulinda sikio na ina njia zake za kutoka, wasiiitoe kwa kuwa inalinda sikio.”

“Kuna wazazi ambao wanatumia pamba kusafisha watoto wanaamini wanawasafisha lakini kumbe wanapunguza ile nta na wakati mwingine inawezana kumbe nyingine inaingia ndani kidogokidogo, mwisho wake inaweza kujaa kwenye sikio na kuziba.
 
Haya mambo mengine mimi kwakweli bado nashindwa kuyaelewa.Unasema sikio linajisafisha lenyewe,sasa yale ma nta kuna wakati yanakuja mpk mlangoni mwa sikio unawezaje kuyaacha,au hata kama si mlangoni lakini ukiangalia sikio la mtu ndani kidogo unayaona,hii kwangu no,ntasafisha labda tu sitaingiza pamba ndani.Hii dhana pia ni sawa na ile ya wanawake kusema kunajisafisha kwenyewe usitie kidole,hii dhana sijui hata imetokea wapi...
 
Back
Top Bottom