Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,329
33,138
82284265_10163515090830198_2126185959749465533_n.jpg

Tinnitus, ni Tatizo la masikio kupiga kelele, mtu husikia sauti za makelele au kitu kinaita(ringing) ndani ya sikio moja au yote mawili na sauti hizo hazitoki nje na wala hakuna mtu mwingine anazisikia zaidi ya mhusika mwenyewe.

Je unasumbuliwa sana na tatizo la Masikio kupiga kelele? haupo peke yako

Tatizo la masikio kupiga kelele hutokea kwa watu wengi takribani asilimia 15% mpaka 20%, na hasa kwa watu wenye umri mkubwa au wazee, Mtu mwenye tatizo hili la masikio kupiga kelele huweza kusikia sauti mbali mbali kati ya hizi hapa chini;

  • Muito au ringing ndani ya sikio
  • Kubweka
  • Kunguruma
  • Kitu kinagonga ndani ya sikio
  • sauti za Kusisimua au kutekenya N.k

CHANZO CHA TATIZO LA MASIKIO KUPIGA KELELE(TINNITUS)

Hakuna sababu moja ambayo inasababisha tatizo La masikio kupiga kelele,ila kuna mjumuisho wa sababu mbali mbali ambazo huongeza uwezekano wa mtu kupatwa na tatizo hili,na sababu hizo ni kama vile;

1. Tatizo la kupoteza usikivu,ambapo seli za vinyeleo ndani ya sikio kwenye sehemu ya ndani(Cochlea) ambazo zinasaidia sikio kupokea mawimbi ya Sauti kwa kupitia Auditory nerves kwenda kwenye ubongo,
Lakini baada ya ubongo kupokea hizo Electrical signals hutafsiri kama kelele badala ya sauti ya kawaida,na ndipo tatizo la masikio kupiga kelele hutokea.

2. Nywele ndani ya sikio kupinda au kutoka zenyewe kutokana na sababu mbali mbali kama vile umri mkubwa au kuwa katika mazingira ambayo kunakuwa na sauti kubwa sana mara kwa mara kama vile ya muziki n.k,

hali hii ya kuwa katika mazingira haya ya SAUTI KUBWA SANA inayopenya masikioni huweza kusababisha mtu kuwa na tatizo la masikio kupiga kelele

3. Maambukizi ya vimelea vya magonjwa mbali mbali kwenye sikio kama vile bacteria,Fangasi,Virusi n.k

4. Tatizo la sikio kuziba kutokana na sababu mbali mbali kama vile kuwa na maji mengi sikioni, nta kuzidi(EarWax), uchafu au kitu chochote ambacho kinaweza kuziba sikio lako

5. Kuumia kichwani au shingoni, hali hii huweza kuathiri sikio la ndani, nerves zinazosaidia sikio kusikia pamoja na utendaji kazi wa ubongo

6. Matumizi ya baadhi ya dawa, Mtu kuoverdose dawa au kutumia dawa kwa muda mrefu huweza kusababisha tatizo la masikio kupiga kelele,

na hapa tunazungumzia matumizi ya dawa mbali mbali kama vile;

  • dawa jamii ya Nonsteroidal anti-inflammatory drugs(NSAIDs),
  • Baadhi ya antibiotics,
  • Dawa za kutibu kansa au saratani,
  • Dawa jamii ya Diuretics, Antidepressants,
  • Kuoverdose Dawa za Malaria kama quinine N.k
7. Matatizo ya muda mrefu yanayohusisha Nerves au mfumo wa Fahamu, pia huweza kuwa chanzo cha tatizo la Masikio kupiga kelele

8. Magonjwa kama vile Menieres ambayo huweza kusababisha abnormal Inner Ear fluid pressure n.k

9. Kutokufanya kazi vizuri kwa Eustachian tube ndani ya sikio

10. Tatizo kwenye mifupa ya sikio kama vile kukakamaa ndani ya sikio ambapo kwa kitaalam hujulikana kama Otosclerosis

11. Tatizo la misuli yaani Muscle spasms ndani ya sikio, Pia huweza kuongeza hatari ya mtu kupata tatizo la masikio kupiga kelele

12. Matatizo kwenye mishipa ya damu ndani ya sikio ambayo huweza kuathiri mzuguko wa damu kwenye sikio, na matatizo hayo ni pamoja na; Atherosclerosis, Shinikizo la Damu(High blood pressure), Kinked, n.k

13. SABABU ZINGINE Za Tatizo la Masikio kupiga Kelele NI KAMA VILE;

– Ugonjwa wa kisukari

– Matatizo kwenye tezi la Thyroid

– Tatizo la maumivu makali sana ya kichwa cha mara kwa mara au Migraines

– Tatizo la Anemia au upungufu wa damu mwilini

– Magonjwa ya mfumo wa kinga ya mwili yaani Autoimmune disorders kama vile; Rheumatoid arthritis, Lupus n.k

Vyote hivi huweza kuongeza hatari ya mtu kupata tatizo la Masikio kupiga kelele

MADHARA YA TATIZO LA MASIKIO KUPIGA KELELE NI PAMOJA NA;

1. Mwili kuchoka kupita kiasi

2. Kupatwa na tatizo la mfadhaiko,msongo wa mawazo n.k

3. Kupata tatizo la kukosa usingizi

4. Kupata tatizo la kupoteza kumbukumbu

5. Kushindwa kufanya kitu kimoja vizuri na kwa utulivu au kuloose concetration

6. Kuanza kupatwa na tatizo la wasiwasi kila mara

7. Kupata maumivu ya kichwa mara kwa mara n.k

MATIBABU YA TATIZO LA MASIKIO KUPIGA KELELE

Matibabu ya tatizo la masikio kupiga kelele hutegemea na chanzo chake,hivo kwa ujumla zipo njia mbali mbali za kutibu tatizo hili la masikio kupiga kelele kama vile;

✓ Kuondoa nta au uchafu wowote ambao umeziba sikio

✓ Kutibu tatizo la mishipa ya damu,tatizo la presha,kisukari n.k

✓ Kuacha baadhi ya dawa au kubadilisha baadhi ya dawa

✓ Kupewa vifaa vya kukusaidia kusikia yaani Hearing aids n.k

✓Dawa za Asili zipo zakuwezakutibu na kuponyeshakabisa haya maradhi ya masikio kupiga makelel na kuunguruma

Hitimisho

Tatizo la Masikio kupiga kelele huweza kusababishwa na sababu mbali mbali ikiwemo; Kuoverdose baadhi ya dawa kama vile dawa za Malaria mfano Quinine Asprin n.k
Kwa Mtu Mwenye Haya Maradhi ya Asikio KupigaMakelele na Kuunguruma anitafute mimi Kwa wakati wake ili niweze kumtibia na atapona kabisa na kurudi hali yake ya kawaida kama zamani.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom