Tatizo la Maji na Ukame: Lawama zangu zote ni kwa Waziri Lukuvi na Waziri wa Mazingira

Hapana usimuonee Lukuvi hata kidogo !
Kama population ya waTanzania inaongezeka kwa kasi ya ajabu, Juzi kati tuu tulikuwa mil20, gafla ndani ya miaka10 tumekuwa mil60! Option rahisi aliyo kuwa nayo lukuvi kama waziri ilikuwa kubadilisha matumizi ya ardhi ili ku accommodate hili ongezeko na hiki ndicho kinacho fanyika duniani kote.

kubadilisha matumizi ya ardhi kutoka mapori ya akiba au mashamba na kuwa makazi ya watu si jambo la ajabu
 
Idea yako ni ngumu sana kuielewa.

Mara mnatuambia maji yamefunguliwa mara sijui kimetokea nini.

Nyie watu bana mtamaliza sababu zote ila mwisho we mtasema tu ukweli . Nchi ishawashinda hii. Watu hawaendi kazini wanafanyia kazi nyumbani na offisini tu.

Hakuna hata siku moja rais ameenda ziara kuko mapolini, yeye anapiga ziara za kupangiwa tu. Mtanzania bila kusimamiwa hafanyi kazi.
Kwani inahitaji Rais kwenda ziara sehemu ili ajue Kuna Tatizo?
 
Sisi tuchakachuwe ya Ziwa Victoria, Tanganyika, Nyasa, Rukwa, Natron, Eyasi watu wapata maji, wala hatuhitaji kwenda baharini.
Kwa Wakazi wa Morogoro, Pwani na Dar wakachukue maji wapi?
 
Kuna diwani mmoja kule kwetu Iringa juzi katuma mapicha kwenye account yake ya facebook eti anajisifu wanachimba kisima cha milioni 50 kwenye zahanati.!

Nikishangaa sana,

Hivi sehemu kama Iringa tena kule dabaga mito kila sehemu ni kwa kupoteza milioni 50 kuchimba kisima?

Sehemu kama kigoma unaweza kukuta nako kuna uhaba wa maji wakati ziwa lipo pale pale!

Na alafu tulivyo wapumbavu, huwa tunatafuta watu wakuwatupia zigo kama hivi.
Itaje iyo mito ya Iringa inayotiririsha maji mwaka mzima
 
Hapana usimuonee Lukuvi hata kidogo
Kama population ya waTanzania inaongezeka kwa kasi ya ajabu, lukuvi kama waziri ya ardhi ulitaka afanyeje ili ku accommodate hili ongezeko? Juzi kati tuu tulikuwa mil20, gafla ndani ya miaka10 tumekuwa mil60! Option rahisi aliyo kuwa nayo lukuvi ni kubadilisha matumizi ya ardhi kutoka mapori ya akiba au mashamba na kuwa makazi ya watu,
Tatizo la ungezeko la watu kupita kiasi nalo siwezi kulikataa Ila kuhusu wavamizi wa ardhi mikoa ya Morogoro, Pwani, Rukwa, Katavi, Kigoma na Tabora hapa Lukuvi anastahili lawama kwa kuliendeleza hili kwa kuwarasimisha.

Kwa nini wanaondoka kwao? Kama Tatizo ni Malisho kwa nini wasiwekeze kwenye kuwapa teknolojia ya ufugaji wa kisasa wa kibiashara?

Mtu mmoja ana ng’ombe 1000 tena anawafuga kizamani malisho atapata wapi?
 
Kwa ujumla nchi hii haina sera wala sheria. Viongozi na watendaji wa Serikali wanafanya mambo kwa unafiki na hulka za kutaka waonekane wazuri kwa kila mtu.

Itawezekana vipi wewe kiongozi au Serikali uonekane mzuri kwa mhalifu na mtu mwema.

Angalia hata suala tu machinga kuzagaa kila sehemu. Mara sijui waondoke, mara sijui wapangwe vizuri, mara sijui watafutiwe maeneo. Kauli zote hizi ni kwa sababu ya unafiki. Badala ya kuangalia sheria, kunakuwa na kauli ambazo hazieleweki ambazo zinawapa shida hata watendaji wa chini.

Sheria kama inasema hairuhusiwi kujenga au kufanya shughuli zozote kwenye vyanzo vya maji na hifadhi ya misitu, inatakiwa iwe hivyo. Kinachofuatia inatakiwa ni usimamizi tu wa sheria, siyo hadithi nyingine.

Sheria kama inasema mifuko ya plastic hairuhusiwi, hairuhusiwi kufanyia biashara au kuweka kitu chochote kwenye barabara au hifadhi ya barabara, inatakiwa iwe hivyo. Kinachofuatia ni taratibu za usimamizi. Hayo mambo sijui watafutiwe maeneo, kuna mtu aliwahi kutafutiwa hata nyumba tu ya kupanga? Si anatafuta mwenyewe?

Unafiki, katiba mbaya inayompa madaraka makubwa kupindukia Rais kiasi cha kila mtendaji kushindwa kufanya kazi mpaka asikie kauli ya Rais ni chanzo cha matatizo mengi. Mkiwa na Rais ambaye maamuzi yake ni ya hovyo, upeo duni au ana hulka ya kujipendekeza, nchi inabakia inayumbayumba tu.
Kweli kabisa, unafiki umezidi.
 
Kwenye maji wanatumia teknolojia inaitwa desalination. Ni teknolojia ya kusafisha maji chumvi hasa ya Bahari Kwa matumizi ya kunywa. Hii inatumika Israël, Saudia, Qatar, Kuwait na Dubai.

Ni teknolojia aghali sana inayohitaji fedha nyingi sana. Swali ni Je sisi tutaiweza na hali yetu ya kiuchumi?

Kwani Ruvu, Rufiji, Ruvuma, Pangani, nk inamwaga cubic million ngapi za maji yasiyo na chumvi baharini?

Kwani maji ya maziwa Victoria, Tanganyika, Nyasa, Rukwa nk yana chumvi?

IMG_20211119_091739_123.jpg

Si mseme tu vipaumbele vyenu ni maslahi yenu yakiwamo Madege mnayotanua nayo nyie?
 
Kwanza Unajua uhusiano kati ya mvua na mazingira hasa Miti? Au hata iyo elimu hauna?
Tupe huo uhusiano maana mimi elimu sina, mwaka jana na mwaka juzi mvua zilisababisha mafuriko kuna nini kilichobadilika ili ionekane mwaka huu lukuvi ndo kazuia mvua......twende kazi.
 
  • Thanks
Reactions: PNC
Kwenye maji wanatumia teknolojia inaitwa desalination. Ni teknolojia ya kusafisha maji chumvi hasa ya Bahari Kwa matumizi ya kunywa. Hii inatumika Israël, Saudia, Qatar, Kuwait na Dubai.

Ni teknolojia aghali sana inayohitaji fedha nyingi sana. Swali ni Je sisi tutaiweza na hali yetu ya kiuchumi?
Water desalination, very expensive
 
Unafikiri kwa nini watu wanaenda kujenga au kufanya shughuli zao kwenye vyanzo vya maji?
Sababu kibwa ni ulegevu uongozi katika ngazi mbalimbali. Kuna watu watasema ni kwa sababu ya umaskini, lakini siyo kweli. Maskini wapo Duniani kote. Uharibifu wa mazingira umamwathiri zaidi maskini kuliko tajiri. Hivyo kumwacha maskini aharibu mazingira ni sawa kumjengea kaburi mgonjwa badala ya kumpa matibabu.
 
Kuna muda ni lazima ukweli usemwe maana usiposemwa lazima kumbukumbu zitakuwa za upotoshaji Mkubwa

Kwenye Tatizo linaloikumba Tanzania la ukame na ukosefu wa Maji kwa sasa lawama zangu zote nazipeleka kwa watu wafuatao

1. William Lukuvi
Akiwa Waziri wa Ardhi kuanzia Awamu ya Tano, nchi yetu imeshuhudia urasimishaji mkubwa sana wa Mapori ya akiba pamoja na hifadhi kuwa makazi ya watu!

Jambo hili limepelekea kuongezeka kwa kiasi kikubwa sana uharibifu wa Mazingira hasa ukataji Miti wa kutisha kwenye mapori mengi yaliyokuwa yanategemewa kuleta mvua uliofanywa na Jamii za wafugaji na wakulima hasa kwenye mikoa ya Katavi, Rukwa, Tabora, Morogoro, Pwani na kusini mwa Tanzania.

Mfano wa hili nimejionea kwenye Mikoa ya Katavi, Kigoma na Tabora inayoongoza kwa kuwa na Misitu mingi.

Kwenye mikoa hii kumekuwa na uvamizi sana wa maeneo yenye mapori na misitu ya asili unaofanywa na Jamii za watu wa mikoa ya kanda ya ziwa na nchi jirani za Rwanda na Burundi. Watu hawa wamekuwa wakikata miti kwenye mapori kwa Kiwango cha kutisha na hata sasa takwimu zimeanza kuonesha hivi karibuni mito iliyokuwa ikititirisha maji mwaka mzima kwenye mikoa ya Kigoma na Katavi bila kusahau Rukwa imeanza kukauka kutokana na shughuli hizi za binadamu.

Waziri Lukuvi akiwa waziri wa Ardhi badala ya kushauri Serikali watu hawa waondolewe kwenye maeneo haya na kurudishwa kwenye maeneo yao ya asili yeye amezidi kushauri serikali watu hawa kurasinishwa kwenye maeneo hayo. Hivyo tusilaumu mtu. Tatizo ni Lukuvi

2. Mawaziri wa Mazingira kuanzia Awamu ya 3,4,5 na huyu wa Awamu ya 6

Hii ni Kwa sababu Nchi yetu imekuwa na Mawaziri wa Mazingira kwenye Awamu zote. Ila kamwe nchi hii haijawai kuwa na kampeni kubwa ya upandaji Miti.

Kila siku watu wamekuwa wakisema juu ya ukame na ukataji mkubwa wa Miti Ila kusema kweli Mawaziri wa Mazingira hawajawai kuanzisha kampeni ya Kitaifa kubwa inayohusu upandaji miti yenye lengo la kuhakikisha nchi inakuwa na misitu mingi, mapori mengi ivyo kuwa salama dhidi ya majanga ya ukame.

Kwa Waziri wa Sasa wa Mazingira Suleiman Jaffo huyu ndo naona ameshindwa kabisa kazi yake maana hata suala la mifuko ya plastiki naona linaanza kurejea kwa kasi sana. Ukitembea kwa basi kutoka Dar kuelekea mikoani hali unayoikuta barabarani inasikitisha. Kuna mifuko mingi ya plastic na materials nyingine za plastiki zimetupwa kando ya Barabara hadi unafikia kujiuliza Kama kucontrol plastiki au usafi tu inatushinda kwa nini tuwe wa Waziri wa Mazingira au Wakuu wa Mikoa na Wilaya?

Nilikuwa Mkoani Dodoma siku si nyingi nikaona hadi Kuna vibanda vya chips vimeanza kuwafungia wateja wake chips kwenye mifuko ya plastiki. Waziri Jafo lawama zangu haziwezi kukuacha kwenye hili maana unamuangusha Mama Samia. Kama huwezi kazi sema.

Hatari ninayoiona mbeleni

1. Sasa tumeanza ona baadhi ya sehemu zinapata mgao wa maji na umeme kutokana na ukame unaosababishwa na maamuzi mabovu pamoja na usimamizi mbovu ubaofanywa na watu walioaminiwa na kupewa madaraka. Hali ikienda hivi ninaona nchi ya Tanzania ikishindwa kuzalisha umeme wa kutosha na baadae chakula cha kutosha.

Tukishindwa kuzalisha umeme wa kutosha kutokana na ukame Mradi wa Bwawa la Nyerere utaonekana rasmi kuwa mradi ulioliingizia Taifa hasara kutokana na kushindwa kuzalisha umeme uliotarajiwa pamoja na kujengwa kwa gharama kubwa.

2. Naona baadae Taifa litakuwa tegemezi na gharama za maisha kuongezeka maradufu jambo linaloweza kuleta hatari kwa kuongezeka kwa matukio ya uhalifu kutokana na nchi kuanza kuwa tegemezi kwenye nishati na chakula!

Tuchukue hatua sasa
Nakubaliana na wewe 100%. misitu na mapori mengi yameharibiwa kisiasa katika awamu ya tano chini ya Jiwe. Maeneo ya hifadhi yamegawiwa kwa watu, eti binadamu ni muhimu kuliko tembo lakini tukasahau kuwa mapori na misitu ndio uhai wetu wenyewe. Pia kuna kauli ya hatari sana inaendeshwa na viongozi wa kisiasa ambao pia ni viongozi wa serikali, eti wale ambao hawajayaendeleza maeneo yao wananyangánywa. Hii siyo haki, eneo la mtu hata kama ni pori na msitu liendelee kuwa mali yake na siyo lazima kufyeka misitu na mapori eti ndio kuendelezwa kama kigezo cha umiliki. Hii siyo sawa hata kidogo.
 
Unadhani vyanzo vya maji vitaendelea kuwepo Kama Mazingira yanaharibiwa?
Tanzania atuna tatizo la maji,tunatatizo la uongozi mbovu, Uwezi kuwa na ziwa kubwa la pili duniani, alafu ukakosa maji, kwani sh ngapi kuvuta maji toka Victoria mpaka dar?kuna ziwa nyasa ziwa Tanganyika manyara,mito ndio usiseme,waka Nchi kama Misri na Hisiopia zinategemea mto nile hatujawai kusikia habari hii ya upungufu wa maji,tuna viongozi wazembe tu,wanawaza misaada ya Wazungu baada ya kutumia raslimali tulizopewa mwenyezi Mungu.
 
Kwa ujumla nchi hii haina sera wala sheria. Viongozi na watendaji wa Serikali wanafanya mambo kwa unafiki na hulka za kutaka waonekane wazuri kwa kila mtu.

Itawezekana vipi wewe kiongozi au Serikali uonekane mzuri kwa mhalifu na mtu mwema.

Angalia hata suala tu machinga kuzagaa kila sehemu. Mara sijui waondoke, mara sijui wapangwe vizuri, mara sijui watafutiwe maeneo. Kauli zote hizi ni kwa sababu ya unafiki. Badala ya kuangalia sheria, kunakuwa na kauli ambazo hazieleweki ambazo zinawapa shida hata watendaji wa chini.

Sheria kama inasema hairuhusiwi kujenga au kufanya shughuli zozote kwenye vyanzo vya maji na hifadhi ya misitu, inatakiwa iwe hivyo. Kinachofuatia inatakiwa ni usimamizi tu wa sheria, siyo hadithi nyingine.

Sheria kama inasema mifuko ya plastic hairuhusiwi, hairuhusiwi kufanyia biashara au kuweka kitu chochote kwenye barabara au hifadhi ya barabara, inatakiwa iwe hivyo. Kinachofuatia ni taratibu za usimamizi. Hayo mambo sijui watafutiwe maeneo, kuna mtu aliwahi kutafutiwa hata nyumba tu ya kupanga? Si anatafuta mwenyewe?

Unafiki, katiba mbaya inayompa madaraka makubwa kupindukia Rais kiasi cha kila mtendaji kushindwa kufanya kazi mpaka asikie kauli ya Rais ni chanzo cha matatizo mengi. Mkiwa na Rais ambaye maamuzi yake ni ya hovyo, upeo duni au ana hulka ya kujipendekeza, nchi inabakia inayumbayumba tu.
Asante!
 
Nakubaliana na wewe 100%. misitu na mapori mengi yameharibiwa kisiasa katika awamu ya tano chini ya Jiwe. Maeneo ya hifadhi yamegawiwa kwa watu, eti binadamu ni muhimu kuliko tembo lakini tukasahau kuwa mapori na misitu ndio uhai wetu wenyewe. Pia kuna kauli ya hatari sana inaendeshwa na viongozi wa kisiasa ambao pia ni viongozi wa serikali, eti wale ambao hawajayaendeleza maeneo yao wananyangánywa. Hii siyo haki, eneo la mtu hata kama ni pori na msitu liendelee kuwa mali yake na siyo lazima kufyeka misitu na mapori eti ndio kuendelezwa kama kigezo cha umiliki. Hii siyo sawa hata kidogo.
Kwaiyo Wewe unaona watu wakose mahali pa kuishi kisa mazingira, mbona Marekani, China,na Nchi za Ulaya hatuoni mapoli?na hatuoni shida ya maji na umeme! Wazungu wanawadanganya tu eti mtunze mapoli wakati wao wanafanya maendeleo, Sisi huku tunaambiwa kufuga mapoli uku wakiwapa viela kidogo ambavo vinaishia katika midomo ya viongozi.
 
Hapana usimuonee Lukuvi hata kidogo !
Kama population ya waTanzania inaongezeka kwa kasi ya ajabu, Juzi kati tuu tulikuwa mil20, gafla ndani ya miaka10 tumekuwa mil60! Option rahisi aliyo kuwa nayo lukuvi kama waziri ilikuwa kubadilisha matumizi ya ardhi ili ku accommodate hili ongezeko na hiki ndicho kinacho fanyika duniani kote.

kubadilisha matumizi ya ardhi kutoka mapori ya akiba au mashamba na kuwa makazi ya watu si jambo la ajabu
Hujitambui wewe dogo.
Juzi kati maana yake nini?
 
Back
Top Bottom