Tatizo la kutapika safarini (Motion Sickness)- fahamu chanzo, tiba na kinga ya tatizo hili

Hata mimi ninasumbuliwa na tatizo hilo kwa muda mrefu tangu nikiwa mtoto hadi hivi sasa nina umri wa miaka 28.Kutapika, Kichefuchefu na Kizunguzungu Kichwa kugonga na hupelekea ninapotapika natapika nyongo.
 
Nionacho tumbo huchafuka zaidi kwenye rough roads, mfano Nzega-Tabora, Mwanza/Shinyanga-Bariadi, Mwanza-Kigoma/Mbeya, Mbeya-Sumbawanga/Mpanda etc. Katika barabara za lami michafuko ya tumbo hutokea nadra kulinganisha na rough roads.

Nimekuwa nikisafiri mara nyingi kwa bus na hata nikiwa self driving...akina dada ndio huongoza kwa kulakula hovyo njiani, na hii huwa ni hali mithili ya kujionyesha mbele za wengine. Nimeshuhudia dada 1 nikiwa safarini Nzega akila mishikaki na chipsi na juice, chini ya kilometa 10 akaanza kusimamisha bus akajisitiri.

NIFANYACHO: Binafsi hujiepusha kula vyakula vyenye vimiminika njiani, badala yake hupendelea kunywa maji, soda na aidha slices za breads. Vyakula hivi hunisaidia sana kwani huwa nasumbuliwa sana na tumbo nje ya safari, na husitirika na matumizi ya aina hii ya vyakula.
 
unaposafiri kaa mbele kabisa kwenye gari, hakikisha unaangalia kupitia wind screen na sio vioo vya dirishani. Hii itakuepusha kuona kama miti au majengo yakikimbia na hivyo kusababisha mvurugo wa tumbo. Hakikisha kabla hujaanza safari umekula chakula na epuka kutumia vyakula vyenye sukari nyingi.
 
Helow Jf doctorz..
Shukran kwa michango yenu mizuri ktk jamii.
Me ningependa kujua,kuhusu tatizo la kichefuchefu na kutapika wakati wa safari either mtu awe amekula kabla ya kupanda gari au hajala,au pia akala katikati ya safari,iwe gari binafsi ama ya umma,eithr safari ndefu au fupi,je kunasababishwa na nini na nini tiba yake..
Nimejaribu Nosic everytime lakini bado.

we unasafiri usiku unakesha kuagana na baba jr wako unategemea usipate kichefuchefu?...
 
Mimi nilikuwa na huo ugonjwa tangu utotoni nilipofika ukubwani nikaacha. Sikuenda kwa Dr wala nini, ninanvyofahamu ni kuwa saa nyingine inasababishwa na position uliyokaa kwenye gari, kama mdau alivyosema kuona miti inakimbia, jengine tafuta siti inaweza kuingia hewa ili kupunguzia hiyo hali.

Cha zaidi mimi binafsi ni kutokuwa na uzoefu wa kusafiri safiri longroute pia inachangia. Maana mimi niliacha baada ya kuanza kufanya kazi, ambapo pana umbali si chini ya 50 km on daily basis. Chengine avoid safari za mchana zinakuwa mbaya zaidi.
 
Wadau kuna hili tatizo la kutapika katika gari watu wengi wanatapika tatizo hua nini?
 
Wadau kuna hili tatizo la kutapika katika gari watu wengi wanatapika tatizo hua nini?

Hata mimi hali hii hunisumbua sana..mwaka jana nilipanda basi kutokea Ubungo,kabla halijafika getini mimi nimeshatapika. Lakini nikipanda gari ndogo hali hii hainipati kabisa.
 
Hili jambo hutegemea mtu na mtu maana kuna wengine hata kama hajala kitu anapopanda basi lazima mwanzo,mwisho anatapika kama vile anaumwa sana japo watu wengine huwa yaani hili kwao si tatizo la kutapika.

Madokta wanatakiwa waje wasaidie kujibu kwa kitaalam, japo nilisafiri kwenda Znz (Nchi jirani kwasasa) wakati natoka Dar asbh sikula kitu saa tatu nikafika Znz nilipanda KILIMANJARO sasa kule mwenyeji wangu akaniandalia madikodiko yaani asbh chai nzito,supu ya pweza na chapati, kwakuwa nilikuwa silali basi mchana nilipikiwa wali na ngisi walioungwa nazi.

Saa tisa nikapanda Kilimanjaro kurudi Dar oooh! Aibu boti karibu asilimia kubwa ya watu wanatapika kama watoto mmh nikaona nami kichefuchefu mate tehe mdomoni nikawaza hii mbona kali ikanibidi niende sehemu ya mbele ya boti iliyo wazi ili upepo unipige nilifanikiwa kufika dar bila kutapika.
 
Kichefuchefu hicho husababishwa na nini,maana mtu mwengine anaingia ktk gari akiwa fresh kabisa lakini muda mfupi tu anadai kuumwa kichwa,na anaanza kutapika.

Nenda Pharmacy yoyote pindi upatapo safari nunua vidonge vya Motion sickness....

Muhimu hivi unavitumia pindi unaposafiri...Motion Sickneee siyo ugonjwa..
 
wana jukwaaa habarini za leo
nina tatizo la kutgapika safarini toka nikiwa mdogo na hadi leo as matured bado linan linanisumbua sana naombeni msaada nitumie dawa gani maana unlikely yo others si enjoy kabisa safari inakua mateso tu
 
  • Thanks
Reactions: ffn
Back
Top Bottom