Tatizo la GPS kwenye Tecno H5, naomba msaada

Kontelo

JF-Expert Member
Aug 16, 2013
572
160
Habari zenu wakuu,

Natumia simu tajwa hapo juu lkn tatizo nililonalo ni kuwepo kwa GPS kila mda ukipiga simu hutokea na hata ukiwasha internet hutokea pia. Nimejaribu mara kwa mara kuzima GPS kwenye location settings lakini ni bure.

Hakuna kinachobadilika tatizo hurudia pale pale. Mwenye uelewa na hizi simu anipe maelekezo maana napata kero.
 
hili tatizo linanitokea sana nikiweka line ya Airtel,inakera maana inamaliza battery kweli kweli mwenye solution atusaidie
 
Hili tatizo lipo kwenye simu za Huawei y 330 hizi za tigo, tangu nifanye unlocking na kuanza kutumia lain ya airtel, GPS imekua ikinisumbua sana hapa nimeshahangaika kutafuta solution hadi nimechoka
 
kuna mshkaji akiweka lain ya zantel no problem lakini akiweka airtel tu Gps inaanza kujiwasha na kila ukiizima inawaka. jee is it safe to say that airtel sim card has all to do with this mess???
 
hili ni tatizo hasa laini ya airtel mimi mwenyewe inanisumbua kwenye tecno m5
 
Kwangu pia imetokea. Ninatumia Huawei Y330. Tatizo limetokea baada ya ku-unlock na kuweka line ya Airtel.
 
Habari zenu wakuu,

Natumia simu tajwa hapo juu lkn tatizo nililonalo ni kuwepo kwa GPS kila mda ukipiga simu hutokea na hata ukiwasha internet hutokea pia. Nimejaribu mara kwa mara kuzima GPS kwenye location settings lakini ni bure.

Hakuna kinachobadilika tatizo hurudia pale pale. Mwenye uelewa na hizi simu anipe maelekezo maana napata kero.

Tatizo hili lipo sana kama unatumia line ya airtel, na pia kama unatumia line ya mitandao mingine na unapata tatizo hili angalia kama kuna application unayoitumia yenye access na location yako, application kama vile facebook, antivirus, easy finder na program yoyote ya anti-theft kama vile avast au LOOK Out.
 
Mimi nadhani kwa simu kama tecno P5 (hata mie nimeshawahi kuwa nayo) ni tatizo sugu sana, kwa maana nilishawahi kuja hapa jamvini last year kwa similar case CHIEF MKWAWA akanipa ujuzi wake kuwa nifunge launcher nyingine. Hapo tatizo liliisha kwa muda ila then baada ya muda likarudi upya.
Nilichokifanya niliuza simu, nikanunua nyingine Samsung S2, hata nayo ilipokufa kwa kudondoka from gorofani nilinunua Huawei W1, iko poa sana (hii ni windows phone) as niliapa hata kama ni low budget phone kamwe sirudi tecno hata iweje.
ushauri, tafuta any other reliable low budget phone far from tecno, kwa upande wa Android zipo nyingi sana kuliko windows maana mbali na hapa hakuna tena smart phone ya low budget kama hizo mbili (OS).
 
Last edited by a moderator:
GPS kuwa ON muda wote ni kama security measure kama unatumia mobile locator Application yoyote.. see the image below, as avast is one of the security app. Screenshot_2014-11-25-13-06-25.png
 
Nifuatilie kwa makini:
Usisumbuke kutafuta suluhisho la hiyo Gps kwenye simu yako. Mimi natumia Tecno M7. Mwaka jana nilipata tatizo kama hilo nikahangaika sana kulirekebisha kwa setting kwenye simu yangu, ikashindikana. Nilibadili hata Launcher haikusaidia. Nikamshirikisha fundi mmoja mtaalamu sana wa simu naye akashindwa. Fundi wa pili ndio akanipa ukweli kuwa ni issue ya mtandao wa Airtel. Na kweli ukiweka line ya mtandao mwingine Gps haijiwashi kabisa ila ukiweka Airtel tu inawaka na kila ukiiweka off inajiwasha yenyewe baada ya muda mfupi tu.

Niliwapigia Airtel Huduma kwa Wateja nikaeleza shida yangu na mtoa huduma akaniahidi kulishughulikia. Jioni ya siku hiyo akanipigia simu akinieleza kuwa ameshalishughulikia, nizime simu na nisiiwashe tena mpaka kesho yake asubuhi. Kesho yake nilipowasha, kweli halikuwepo tena.

Mwaka huu limejitokeza tena mwezi Juni nikawapigia tena Airtel Huduma kwa Wateja lakini niliambulia kupewa ahadi za tatizo kushughulikiwa mpaka nikakata tamaa. Niliamua kuhama mtandao jumla kwa maana ya ununuzi wa vifurushi maana shida hiyo inatokea kwenye Slot 1 ambayo ina access ya 3G na hutokea uwapo katika eneo lenye network ya 3G tu. Slot1 nimeweka Vodacom na Slot 2 Airtel na Gps haijiwashi kabisa. That's the only solution. Atakaekuelekeza tofauti na hapo mwongo!
 
Halafu hilo tatizo lina faida kwa sababu ukitumia app ya mobile spy inakuonyesha mtu yuko wapi. Kwa hiyo mke au mume wako ak-install kwenye phone yako, atakuwa anafuatilia mwennendo wako hata ukiwa sehemu inaonyesha jina la eneo hilo, hata kama ni hoteli au Guest House.
 
Back
Top Bottom