TARURA mnatuchosha madereva

Fuqin

JF-Expert Member
Dec 2, 2018
293
596
Mambo vipi wadau... Alhamis iliyopita nilienda mjini na gari wakaja watu wa tarura wakanipa risiti ya kulipia ilikuwa na control namba lakini cha ajabu mpaka leo imegoma kulipia kila nikiweka control namba naambiwa (control error) nikaenda kwa wakala kulipia kasema imegoma kuingia.

kwahyo mimi ni wakitembea na kikaratasi tuu au wanataka hii gari yenyewe wapige mnada kisa buku tu??? msaada wenu muhimu wadau...
 
Hiyo pesa inajidabo, sina uhakika kama ni kila wiki au mwezi. buku inakuwa buku 2, - buku 4, - buku 8.......

Hawa jamaa wangese sana yani anakuandikia alafu hakwambii leo kuna dada kacheki nakuta nadaiwa 16,500 hata sijui deni limeandikwa lin, huu utaratibu ni wa hovyo, mtu akiwa na kimashine tu akiona target haisom anakubambikizia deni
 
Nahisi hawa ndg zetu wa TARURA wamehamia huku kabla ya kuandaa vizuri mfumo wao, na sasa umegeuka kuwa mzigo kwa mlaji.
Ni sehemu ya Serikali, lakini unashangaa ukiingia kwenye mifumo ya kulipa malipo kwa njia ya Mtandao, ukachagua malipo kwa Serikali ukiweka Control No yao inaleta error msg kwamba haipo au imepitwa na muda.

Kwa nini wasihakikishe kwanza mfumo wao upo sawa na unasoma na mifumo ya E-Gov pamoja na mifumo mingine yoote ya malipo kwa njia ya kidigitali, yaani z-pesa, tigo pesa, m-pesa, airtel money, bank zoote zenye mifumo hiyo n.k nk.
Hii ya kutaka watu waende kwa wakala, ni kupotezea watu muda wa kujihusisha na uzalishaji au utoaji wa huduma.

TARURA amkeniiiiiii, tupo kwenye zama za full digital
 
Ikifika 30,000 inakomelea hapo
Saivi ni kuangalia gari yako mara kwa mara maana wenye zile POS kama hajakusanya anaweza kukaa barabarani ananakili namba na kuziandikia. kunatakiwa kuwe na control mechanism iwe kama polisi kwamba unaandikia kwa leseni ya dereva ili muonane na ujue kama unadaiwa

Angalieni kama mnadaiwa parking fees:
Termis Web System
View attachment 1967172
 
Mambo vipi wadau... Alhamis iliyopita nilienda mjini na gari wakaja watu wa tarura wakanipa risiti ya kulipia ilikuwa na control namba lakini cha ajabu mpaka leo imegoma kulipia kila nikiweka control namba naambiwa (control error) nikaenda kwa wakala kulipia kasema imegoma kuingia.

kwahyo mimi ni wakitembea na kikaratasi tuu au wanataka hii gari yenyewe wapige mnada kisa buku tu??? msaada wenu muhimu wadau...
Nimeangalia nimekuta ninaadeni la elf 20, na nyingine elfu 2 gar moja. Hata sijui zimetoke wapi. Yaani mti anakulima parking fee kimya kimya. Inabidi mfumo wao wanyeshe ni lini na wapi. Mi ili deni hata sijui limetoka wapi?
 
Mambo vipi wadau... Alhamis iliyopita nilienda mjini na gari wakaja watu wa tarura wakanipa risiti ya kulipia ilikuwa na control namba lakini cha ajabu mpaka leo imegoma kulipia kila nikiweka control namba naambiwa (control error) nikaenda kwa wakala kulipia kasema imegoma kuingia.

kwahyo mimi ni wakitembea na kikaratasi tuu au wanataka hii gari yenyewe wapige mnada kisa buku tu??? msaada wenu muhimu wadau...
Hifadhi maulizo yote tarehe muda na location..vitakusaidia baadae
 
Kiufupi serikali inapenda kufanya mambo kidigital wakati uwezo huo hawana,tarura limekuwa janga jipya kwa wenye magari,iliwahi nisumbua siku 4 nzima kila ukiweka mtandao unagoma,huu ni unyanyasaji kwa wamiliki wa vyombo vya moto
 
Saivi ni kuangalia gari yako mara kwa mara maana wenye zile POS kama hajakusanya anaweza kukaa barabarani ananakili namba na kuziandikia. kunatakiwa kuwe na control mechanism iwe kama polisi kwamba unaandikia kwa leseni ya dereva ili muonane na ujue kama unadaiwa

Angalieni kama mnadaiwa parking fees:
Termis Web System
View attachment 1967172
Wabongo mlivyo wabishi na mnavyowadharau hao wakatisha tiket mtawapa hizo leseni ili aandike deni?
 
Wabongo mlivyo wabishi na mnavyowadharau hao wakatisha tiket mtawapa hizo leseni ili aandike deni?
Mbona mwanzo wakati tunalipa cash tulilipa? Utashindwaje kulipa parking ya 1000 au 2000 na unajua umekaa masaa2 kwenye maegesho. Kuna wastaarabu anakuandikia anaweka kwenye kioo risit ina control no.

Wengine wapuuzi anakuandikia na haweki risiti. Hawa ndio tunaowalalamikia
 
Hiyo pesa inajidabo, sina uhakika kama ni kila wiki au mwezi. buku inakuwa buku 2, - buku 4, - buku 8.......

Mimi sina hili wala lile, nikasema nicheki kama nadaiwa nakuta 5,000/= sikumbuki ni wapi nilipaki, na haionyeshi.
Je hakuna wizi unaweza fanywa hapo kwa kuongezewa madeni bila kujua?
Huu mfumo wao hauko sawa, wa kijinga, kiwizi, kijanja janja.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom