NostradamusEstrademe
JF-Expert Member
- Jul 1, 2017
- 3,032
- 4,028
Tarehe kama ya leo na mwezi kama wa leo miaka 47 iliyopita ndio tulihitimisha halaiki tulizocheza kwa miezi sita ajili ya kuzaliwa CCM na Azimio la Arusha kutimiza miaka 10.
Nilikuwa nasoma UHURU Shule ya msingi Arusha nikiwa darasa la tano.Kwamaana hiyo darasa la nne sehemu kubwa hatukuwa darasani ndio tukahitimisha tarehe 5 feb 1977.
Nilikuwa kile kikosi cha kufungua vitabu majukwaani.Nyerere alikuja alivyopigiwa mizinga na baada ya halaiki akaondoka kwenda Zanzibar kushiriki kuzaliwa kwa CCM siku hiyo hiyo si mnajua speed ya ndege
Wahenga wenzangu wanaokumbuka mkuje huku mtoe comment zenu.Kwa sasa tuna wajukuu kwa vile waliozaliwa kipindi kile wana wajukuu.
Ushabiki wa kisiasa tuweke pembeni maana wengine tumeshakuwa wapinzani sasa hivi ila wakati ule wa chama kushika hatamu siasa ilikuwa kwenye damu zetu hata watoto wa primary tulikuwa tunafundishwa kutumia bunduki angalau kujua sehemu zake na kusafisha kijaruba na mtumbo.
Pia wakati wa vita vya Kagera tulichimba mahandaki mashuleni kwetu.
Mwalimu wangu Shedrack primary huko uliko mungu aendelee kukutunza huyu mwalimu alikuwa Mkurya.
Namkumbuka mwalimu Firm mwalimu wa kiswahili,hesabu alikuwa Mpare pia namkumbuka mwalimu Malai alikuwa mchaga yeye alitufundisha hesabu.
Mwalimu mama Urasa,