Stephano Mgendanyi
JF-Expert Member
- May 16, 2020
- 1,902
- 945
KONGAMANO LA UVCCM KUELEKEA MIAKA 3 YA UONGOZI WA RAIS DOKTA SAMIA NA MIAKA 47 YA KUZALIWA KWA CCM
Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi wamefanya Kongamano kubwa kuelekea Miaka Mitatu ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan madarakani na Miaka 47 ya kuzaliwa kwa Chama Cha Mapinduzi lililofanyika Uwanja wa Kawawa mkoani Kigoma. Tarehe 28 Januari 2023.
Katika Kongamano hilo Makamu wa Rais ambaye ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi Mhe. Dkt. Philip Mpango ndiye alikua mgeni rasmi.
Aidha Mwenyekiti wa UVCCM Mohammed Ali Kawaida alimkabidhi Mhe. Dkt. Philip Mpango Fedha iliyotolewa na UVCCM kwaajili ya kumwezesha Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kuchukua fomu ya kugombea Urais mwaka 2025.