Tanzia: Mkuu wa Mkoa wa Mara aanguka ghafla na kufariki dunia!

Duh! kweli si lazima uugue ili kufa. Wapendwa tujiweke tarayi kwa sababu katika saa tusiyodhani mwana wa adamu yuaja. Hata hivyo liko tumaini kwamba Yesu atakapokuja tutaonana tena na mpendwa wetu.

Hebu na tufarijiane kwa maneno hayo!
 
Huyu jamaa ni kada wa Chama Cha Mama baba na watoto?
Wanatakiwa waelewe kwamba kiburi walicho nwcho viongozi wa hii ccm ni cha muda tu, na kwamba Mungu ndie pekee atakae wahukumu muda autakai. Mwenye macho na asikie na kuona.
 
01.madini%20ABG.16.jpg


Habari za uhakika zilizopatikana hivi punde ni kwamba mkuu wa mkoa wa mara John Tupa ameanguka ghafla na kutokwa na povu Wakati akitoka nje ya ofisi ya Mkuu wa Wilaya (DC) Tarime na kuelekea kupanda gari yake tayari kuanza ziara ya Tarime...

Amekimbizwa hospitali ya Wilaya; lakini taarifa za uhakika ni kuwa AMEFARIKI DUNIA.

Taarifa zaidi zitafuata!
pole zao wote wanaomtegemea..
 
RIP huyu mzee nimemjua siku nyingi miaka ya 90 tangu akiwa mjeshi bukoba kabla ya kuwa mkuu wa wilaya na baadae mkuu wa mkoa.

Tusipende kuhusisha vifo vya watu na imani za kishirikina japo ktk jamii zetu hizi za kiafrika haya mambo yapo lakini kwa status yake huyu marehemu na cheo alichokuwa amefikia lazima alishajilinda vya kutosha kama desturi zetu zilivyo so yanaweza kuwa magonjwa mengine au hata sumu
 
Pole tupa

Angalizo tupa usichezee tarime tenda tu haki na mche mungu sana hapo TM kuna mafundi balaah!!

Tarime hakuna mafundi wa kupuliza, kule kuna mafundi wa mapanga.

Mwenyezi Mungu akupumzishe pahala pema mzee Tupa. Mara walikupenda lakini Mungu amekupenda zaidi.
 
Back
Top Bottom