Tanzia: Mama Hawa Ngulume afariki dunia!

Nakumbuka mwishoni hapa serikali ya chama mapinduzi ilishindwa kusikia kilio chake cha muda mrefu.
R.I.P mama yetu Hawa Ngulume
 
Dah! Mkuu kumbe nawe ni mmoja wa kipindi kile cha "Introduction to third phase cost sharing". Nakumbuka ilikuwa kivumbi pale magomeni.

Wengine tulienda wilaya ya Ilala baada ya mama Ngulume(RIP) kuwa mkali kupitiliza,yule wa Ilala alitusaidia
 
Pumkiza mahali pema peponi Komredi Hawa Ngulume! Kamwambie Mwenyezi Mungu yote waliyokutendea wana-CCM wenzako.Inauma sana
 
Nitamkumbuka kwa mengi. kwanza zoezi la kuwaamisha wafugaji kule Mbarali alilolisimamia hadi kumzaba kibao mwenyekiti wa Kijiji kama si mtendaji wa kata kwa ku side na wafugaji. The mama wa "TOUGH" DURING HER LIFE TIME. R.I.P Mama
 
RIP Hawa Ngulume, Pamoja na tofauti tulizowahi kuwa nazo lakini bado nlikukubali kama Mama na Kiongozi wa ukweli.
Pumzika kwa Amani.
 
Your time has come. Rest now. Alishawahi kumzaba mtu kibao enzi zake.
 
Alikuwa mtata na mbabe sana, alijua ataishi maisha yake yote akiwa kiongozi hivyo akaacha kujipanga kimaisha, magamba walimtupa mara baada ya kuanza kuugua, ilibidi aje hadharani kuomba msaada.

Bwana ametoa na Bwana ametwaa jina la Bwana litukuzwe.

Kwani wakuu wa wilaya hawakatiwi bima ya afya na mwajiri wao ??
 
dah aalikuwa kiboko alippkuwa dc kndoni, hasa baada ya mgomo wa udsm na kutakiwa kusaini fomu pale kwake alikuwa hasikilizi mtu hata maelekezo toka kwa rc

Nakumbuka tuligombana naye baada ya kukataa kuniwekea sahihi katika fomu ili nirudi chuoni; akaniambia niende wilayani kwangu (kanda ya ziwa).Hata hivyo DAS aliniita ofisini kwake akanitilia mkwaju.

R.I P mama.
 
Mungu amrehemu

Hivi ndio huyu kuna kipindi walimgombea Malecela yeye na mama Kilango?
 
Namkumbuka enzi zake,

Tulitakiwa atusainishie loan form .... Du RIP mama.


Duh!! Aiseeeeee, anyway huyu mama basi tu Mungu a R.I.P, nakumbuka alinifokea na kukataa ku saini fomu zangu za mgomo akaniambia niende Shinyanga kusainiwa, nikaenda Ilala ndo nikasainiwa bila shida! duh kati ya mwaka 2000/2001 UDSM tulipofukuzwa, R.I.P mama!!
 
Back
Top Bottom