Tanzia: Mama Hawa Ngulume afariki dunia!

Mkeshaji

JF-Expert Member
Jan 7, 2011
4,262
1,416
Salaam wakuu,
Taarifa nilizozipata hivi punde ni kuwa aliyewahi kuwa mkuu wa wilaya ya Kinondoni mama Hawa Ngulume amefariki dunia muda mfupi uliopita.

Mama Hawa Ngulume alikuwa akisumbuliwa na kansa kwa muda mrefu.

Mwenyezi Mungu aipumzishe roho ya marehemu mahali pema peponi, Amina.

Innalilah wa innalilah Rajuun.
 
Pumzika kwa Amani Mama.

images
 
Dah! Mkuu kumbe nawe ni mmoja wa kipindi kile cha "Introduction to third phase cost sharing". Nakumbuka ilikuwa kivumbi pale magomeni.

Tuko wengi mkuu
Kindondoni ilikuwa balaa akiwepo huyu mama
Unaambiwa kamlete mwenyekiti wako wa serikali za mitaa pale kwake ili ahakikishe kweli unakaa mtaani kwake
hata baada ya Mkuu wake Makamba kuweka msisitizo aliitupa barua ya Makamba kule akasema yeye ana utaratibu wake na hauingiliwi na yeyote
R.I.P mama Ngulume
 
RIP Mama Hawa Ngulume.

Sasa sijui leo Serikali wataenda katika msiba wake. Kwani walimtelekeza pasipo msaada wowote huyu mama, Yaani mafisadi wanafikiria pesa tu na siyo kuwahudumia Watanzania. Alishatoka katika Gazeti analalamika Serikali imemtelekeza akiwa anaumwa lakini kipindi kile walimtumia sana na tena alikuwa mbabe sana huyu mama, na kwa kutetea sheria walizoweka waliomtelekeza.

Namkumbuka akiwa mkuu wa Wilaya Bagamoyo alivyowachapa mangumi ya kiuhakika madereva na makonda wa mabasi ya Bagamoyo - Mwenge

Rest In Peace mama yetu.

MIZAMBWA
INANIUMA SANA!!!
 
Konisaga wa Nyamagana ajifunze. RIP Hawa.
 
Back
Top Bottom