Tanzia: Mama Hawa Ngulume afariki dunia!

Apumzike kwa amani mama yetu na iwe fundisho kwa wengine wanotumiwa!

ina maanisha nini? wasiotumiwa (kama kweli wapo) hawafi? nadhani kila mtu anatumiwa ila swali linakuwa unatumiwa na na nani? mkeo? mumeo? watoto? bosi kazini? rafiki? etc

liwalo na liwe & mix with yours
 
Inanikumbusha siku Ditopile amededi, kituo kimoja cha tv kilipata wakati wa kuwahoji madereva wa daladala pale Mwenge. Dereva mmoja alipoulizwa unasemaje kuhusu kifo cha Dito na blabla zingine, yule dereva, alisema huku akitabasamu kuwa 'tunamwombea mungu amrehemu, lakini alimtia shaba mshikaji wetu, dereva mwenzetu'. MEMA YAWEZA KUSAHAULIWA, MABAYA HUDUMU.
Kwa ukweli huyu mama alikuwa Baunsa; anazijua ngumi na alikuwa anatumia ubabe kila kona haogopi Mwanamume au Mwanamuke wote kwake anaona kama watoto wake. Ukiongea naye yakubidi kuchukua hatua usiwe karibu naye unaweza kushitukia ngumi imerushwa.


RIP Mama


MIZAMBWA
INANIUMA SANA!!!
 
Duhh!...mama alikua jembe sana

Lol! Mkuu watu8, Wasukuma wa bonde la Usangu wakikusikia ukisema huyo mama RIP watatamani wakuloge na wewe,kama tunavyoweza kuamini kuwa walimloga mmbabe huyo aliye kuwa akiwacharaza viboko wasukuma wa bonde la usangu na kuwatia hasara kubwa sana kwa kutaifisha mifugo yao. Kama unaamini uchawi basi huyu mama kalogwa na wasukuma waliodhurumika dhuruma kuu chini ya uongozi wake alipokuwa mkuu wa wilaya ya Mbarali.
 
Alikuwa mtata na mbabe sana, alijua ataishi maisha yake yote akiwa kiongozi hivyo akaacha kujipanga kimaisha, magamba walimtupa mara baada ya kuanza kuugua, ilibidi aje hadharani kuomba msaada.

Bwana ametoa na Bwana ametwaa jina la Bwana litukuzwe.
 
Nilishachanganya madawa hapa, nilidhani ni Hawa Ngu'mbi! anyway..Lala salama Mama! mungu atakufufua siku ya mwisho!

Mkuu Mchaka Mchaka, Kama Mungu atasikia Dua za Wasukuma wa Bonde la Usangu, huyu mama atafufukia Jehanamu kwenye mateso ya milele kulipa uovu aliowatendea.
 
RIP Mama Hawa,
Poleni wafiwa wote, Mungu awape faraja.
Nilipata kumjulia hali pale Lugalo alipokuwa amelazwa,
Serikali ilimsaidia alipokwenda India kwa matibabu, aliporudi imekuwa dana dana hadi watoto wake wakakata tamaa wakaamua kuachilia mbali.
 
RIP mama Hawa Ngulume.

Niliishi vizuri sana na huyu mama kule Temeke kama mpangaji kwenye nyumba yake miaka ya 88 mpaka 90. Wakati huo alikuwa mtumishi wa kawaida kwenye chama na nilikuwa mwanafunzi UDSM.

Pole sana kwa familia nzima.
 
Mwenyezi Mungu ailaze roho yake mahali pema peponi na awape nguvu na faraja wanae, ndugu, jamaa na marafiki katika kipindi hiki kigumu kwao~AMEN.
 
Dah! Mkuu kumbe nawe ni mmoja wa kipindi kile cha "Introduction to third phase cost sharing". Nakumbuka ilikuwa kivumbi pale magomeni.

Nakumbuka sana kipindi kile pale magomeni, tulimfungia hadi mlango baada ya kuleta urasimu uliotuudhi sana by then. Lakini yatupasa kusameana kama binadamu kwan mapungufu ni kwa kila mtu. R. I. P MAMA NGURUME
 
Nakumbuka sana kipindi kile pale magomeni, tulimfungia hadi mlango baada ya kuleta urasimu uliotuudhi sana by then. Lakini yatupasa kusameana kama binadamu kwan mapungufu ni kwa kila mtu. R. I. P MAMA NGURUME

Mungu ampumzishe vema mama Ngulume.
Tuliopita UDSM miaka ya 2000 kuja 2004 tumkumbuka kwa kutugomea kujaza fomu za mikopo. Wasukuma wa Mbarali nadhani wakisikia watachinja ng'ombe wengi sana. Alichowafanya hakisahauliki maishani mwao.
 
Amewahi pia kuwa mkuu wa wilaya ya Kondoa enzi zake,hivi mpaka mauti yanamfika alikuwa wapi?
 
Lol! Mkuu watu8, Wasukuma wa bonde la Usangu wakikusikia ukisema huyo mama RIP watatamani wakuloge na wewe,kama tunavyoweza kuamini kuwa walimloga mmbabe huyo aliye kuwa akiwacharaza viboko wasukuma wa bonde la usangu na kuwatia hasara kubwa sana kwa kutaifisha mifugo yao. Kama unaamini uchawi basi huyu mama kalogwa na wasukuma waliodhurumika dhuruma kuu chini ya uongozi wake alipokuwa mkuu wa wilaya ya Mbarali.

aisee...hao ni Wasukuma wa kule Madibira, Rujewa, Ilembula au sehemu gani?...huyu mama nilimjua akiwa Kinondoni, then akahamishiwa Pwani(nadhani Kibaha), baada ya hapo sijui alipelekwa wapi
 
Namkumbuka sana huyu mama baada ya uchaguzi wa mwaka 2000 tulitimuliwa chuoni wote, then ndio tukarudishwa kwa masharti ya kujaza loan form, huyu mama alitutesa sana, wewe mtu ametokea kigoma mama anamwambia alete barua ya balozi wa nyumba 10. Let her RIP
 
Mungu Amsamehe Makosa yake na Amlaze Mahali Pema Peponi.
Tusimhukumu kwani nasi tunasubiri kuhukumiwa.
Nitashangazwa sana leo wakitokea viongozi wa CCM kudai wanasikitika, wamepoteza mtu, pengo halitazibika blah blah blah. Tujikumbushe Makala hii.
Nilipeleka taarifa kwenye chama changu kwamba ninaumwa nahitaji msaada, sikujibiwa - Hawa Ngulume

Aliyewahi kuwa mkuu wa Wilaya ya Mbarali, bi Hawa Ngulume yuko katika hali mbaya nyumbani kwake, Goba Kinzudi jijini Dar es Salaam akisumbuliwa na ugonjwa wa vichomi na mapafu.

"Nimeona nitumie chombo cha habari kufikisha ujumbe (wa ugonjwa) kabla sijafa,” alisema mkuu huyo wa zamani wa alipoongea na Mwananchi.


6003571.jpg
[/COLOR]
Bi. Hawa Ngulume
Akizungumza nagazeti la Mwananchi (credit) nyumbani kwake jana, Ngulume alisema kwa miezi mitatu sasa yuko hoi na hawezi kutembea bila kusaidiwa na hivyo anaiomba serikali imsaidie aweze kwenda kutibiwa nje ya nchi. Alisema ameamua kutumia gazeti la Mwananchi kufikisha ujumbe kwa serikali na CCM kuhusu maradhi yanayomsumbua baada ya njia nyingine kushindikana.

“Nilipeleka taarifa kwenye chama changu kwamba ninaumwa nahitaji msaada, lakini sikujibiwa; pia nimefanya juhudi za kutaka kumwona Waziri Mkuu ili anisaidie, lakini juhudi hazikuzaa matunda. Nimeona nitumie chombo cha habari kufikisha ujumbe kabla sijafa,” alisema.

Ngulume, ambaye ni kada maarufu wa CCM aliyetumikia nafasi ya ukuu wa wilaya kwa miaka 18, alisema maradhi hayo yalianza kumsumbua baada ya kumalizika kwa mchakato wa kura za maoni za chama hicho. Alisema aliomba ridhaa ya chama hicho kimsimamishe kuwa mgombea ubunge katika Jimbo la Singida Mjini.

“Katika mchakato ule Mohammed Dewji alishinda, na mimi nikawa mshindi wa pili. Niliporudi Dar es Salaam nikaanza kujiandaa kwenda kumpigia debe mshindi kama ulivyo utaratibu wa chama chetu, ndipo nikaanza kuumwa ghafla,” alisema.

Mkuu huyo wa zamani wa wilaya ambaye amewahi kushika wadhifa huo kwenye wilaya mbalimbali zikiwemo za Bagamoyo, Ilala na Kibaha, alisema amekuwa akitibiwa katika hospitali za Lugalo, IMTU na Ocean Road.

“Kuna kipimo ambacho nilitakiwa kuwekewa kwenye kinywa katika Hospitali ya Ocean Road ili kiweze kubaini kama kwenye mapafu kuna maji au la, lakini ilishindikana kwa sababu ya kukosa pumzi, na hawana kipimo cha aina nyingine,” alisema.

Alishauriwa kwamba aende India ambako kuna vipimo vya aina nyingi ambavyo havihitaji kuwekwa katika kinywa na kwamba vipimo hivyo vingemfaa kutokana na matatizo yake ya pumzi. Alisema katika kuhangaika alifika katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, lakini cha kushangaza alikaa kuanzia saa 8.00 mchana hadi saa 11.00 jioni bila kuhudumiwa.

“Ndipo mtu mmoja anayenifahamu aliyekuwa akipita nilipoketi, akanisalimia kwa kuniita mheshimiwa. Muuguzi mmoja jina ninalihifadhi akaja kutaka kunihudumia, nikamwambia ina maana siwezi kupata huduma hadi niwe mheshimiwa, nikaondoka kwa hasira," alisema.

Alisema baada ya kutelekezwa na kunyanyapaliwa Muhimbili, amekuwa akipata matibabu kwenye hospitali za binafsi kwa ajili ya kutuliza maumivu.

“Maumivu ninayoyapata ni makali sana, nina vichomi utadhani kuna msumemo unaokata viungo vyangu ndani ya tumbo. Ninalia usiku kuchwa kwa maumivu, wanaonisaidia ni majirani tu ambao hufika kila mara kunijulia hali,” alisema.






Source: Nilipeleka taarifa kwenye chama changu kwamba ninaumwa nahitaji msaada, sikujibiwa - Hawa Ngulume - wavuti
 
Mungu Amsamehe Makosa yake na Amlaze Mahali Pema Peponi.
Tusimhukumu kwani nasi tunasubiri kuhukumiwa.
Nitashangazwa sana leo wakitokea viongozi wa CCM kudai wanasikitika, wamepoteza mtu, pengo halitazibika blah blah blah. Tujikumbushe Makala hii.

Kama Yaliyoandikwa Kwenye Hiyo Habari ni Matamko yake, Basi Ujue Katika hii dunia malipo ni Hapa hapa!! Shime ndugu Zanguni Tutende Mema Kwani Hatujui ya Kesho!! Kifo cha Huyu Mama Kiwe fundisho kwa wengine wenye roho Katili kama yeye!! Kama Yamungu alivyochoma Nyumba Kule Meatu!! Yu wapi sasa?
 
Back
Top Bottom