TANZANIA: Turekebishe la Ustaafu wa Siasa!

- Heshima watu wote, I mean one page tupo ukurasa mmoja ninachosema ni kwamba tukiwawezesha Wazee tutakuwa tunafungua nafasi kwa Vijana wetu kuingia kwenye nafasi, kama Kiongozi wa zamani alikwua Mundishi si auri tu kwenye fani yake mbona nchi za wenzetu wanarudi walikotoka wakimaliza siasa?

- Kwa nini sisi inakuwa vigumu?

Es!
 
Wazee ukiwaambia hivyo mtagombana! Ni wazo zuri wakae pembeni vijana washike hatamu
 
Mkuu ES (Mzee wa Data) karibu tena Jamvini,
Tanzania ya Leo ukistaafu siasa na ukarudi katika Taaluma yako au ukawa Mkulima/Mfugaji, Watanzania wanakuona umeishiwa au UMEFULIA, nadhani (labda ni Ulimbukeni). hii ni kwasababu ya ile dhana (Potofu) kwamba ukiingia katika Siasa basi wewe Umeuchinja, mambo yako Super. Leo hii Mtanzania akiteuliwa kuwa Waziri au Mbunge anashangilia na kufanya Party, kwamba mambo yake sasa Poa. Uongozi sio dhamana tena.
Nadhani si sahihi kujilinganisha na wanasiasa wa Marekani, labda wanasiasa wa Marekani wana Vision na Mission, kwamba anafanya siasa muda fulani na akistaafu anarudia taaluma yake. Huku kwetu Mwanasiasa unaweza muuliza swali leo akistaafu atafanya nini, akakujibu nitarudi kijijini kulima, lakini baada ya kustaafu ikitokea Rais kamteua kuwa Balozi, atakubali kwenda kuwa Balozi, Why, B'se No Vision, No Mission. Anataka aendelee kuula na kubaki na status
 
Sauti ya Umeme karibu tena jukwaani.

Hili swala uliloliteta hapa ni gumu sana hapa kwetu na Afrika kwa ujumla. Imagine Mzee Mkapa jana katoka maneno kama haya kwenye kapeni Arumeru.......

Aidha, Mkapa alikanusha ...........“Mimi ninamheshimu sana Mwenyekiti wangu wa CCM na uamuzi wa Kamati Kuu ya chama maana nimezaliwa CCM na kukulia ndani ya CCM.

Sasa wewe unategemea Mzee aliyezaliwa miaka ya 30s au 40s ambaye naye anadai amezaliwa na kukulia CCM kama sisi unategemea kweli ataweza kuishi bila CCM?? Check hapa chini..............aneendelea kwa kusema............

Kwa maana hiyo siwezi hata siku moja kuhoji au kutoa masharti pale ninapoombwa na chama kutekeleza jukumu lolote
 
- Heshima mbele wakuu wote JF, baada ya muda mrefu sana tupo wote tena unajua mishe mishe ya maisha.

Leo ya ustaafu kutoka kwenye siasa zetu Tanzania, I mean tufike pahali tujikite as a nation kulitengeneza hili la Ustaafu kutoka kwenye politics, hatuna mazingara yanayofaa as the results Wazee wetu wengi hawataki kustaafu ni kwa sababu wanaogopa wataenda wapi? Leo kule US kina Condoleeeza Rice, Cohen, Kissinger, wamestaafu siasa na wamerudi kwenye professional zao za Ualimu pamoja na kulipwa posho nzito wanapotoa hotuba kwenye midhahara. Hivi karibuni Rais Kaunda, alikuwa anafundisha Boston College, wamemlipa vizuri tu as of their standards na sasa naamini yupo sawa sana kuliko alivyokuwa kabla ya kwenda kufundisha tena kazi yake ya zamani.

- My point ni kwamba panahitajika a serious National agenda au Kipengele kipya kwenye katiba cha kusimamia Ustaafu wa Wazee wetu kutoka kwenye siasa na kuwahakikishia comfortability na kuwezeshwa pamoja na heshima, ili wakitoka kwenye politics zetu warudi walikokuwa kabla, kama Udakitari, kama ni ualimu, Sheria hili linahitaji nguvu ya Taifa kulisimamia, ama sivyo hii vita kali iliyopo sasa ya kuingia kwenye uongozi wetu wa Siasa za taifa haitapungua karibuni na ndio chanzo cha siasa za majitaka na makundi, ambazo zinalitafuna sana hili taifa tunaishia kukosa viongozi bora wengi kwa sababu ya Vita kali ya kuingia na wasiotaka kutoka, uchaguzi ukiisha kunabaki makovu na majeraha makubwa sana mpaka hatuwezi kusameheana kisa simply hatuna pengine pa kwenda na tulishaamini kwamba nafasi tulizonazo ni zetu milele kumbe ni za wananchi na infact ni za Taifa na ni haki kwa kila mwananchi kugombea!

MUNGU AIBARIKI TANZANIA!

Field Marshall Es: WAZEE WA SAUTI YA UMEME!

tuanze na malechela kwanza
 
Sio kila kitu tuige huko US na Zambia jamani, mbona nyie vijana mlioko huko hamtuletei vitu vinavyoendana na nchi yetu? Acheni ulimbukeni fikirini kutokana na mazingira ya hapa yalivyo biashara ya kufananisha ndo inatupoteza hatuna jipya. Mwishoni utatuambia tuanze kujenga nyumba za kuwalea vikongwe kama Ulaya
 
- Heshima watu wote, I mean one page tupo ukurasa mmoja ninachosema ni kwamba tukiwawezesha Wazee tutakuwa tunafungua nafasi kwa Vijana wetu kuingia kwenye nafasi, kama Kiongozi wa zamani alikwua Mundishi si auri tu kwenye fani yake mbona nchi za wenzetu wanarudi walikotoka wakimaliza siasa?

- Kwa nini sisi inakuwa vigumu?

Es!
Mkuu siasa zetu hizi za Africa ni ngumu. Hata Banda wa Zambia baada ya kutunga sheria kwamba koongozi mstaafu asijihusishe na siasa. Sheria hiyo imeanza kumbana mwenyewe na haipendi ila tu kwa kuwa imeambatanishwa na mafao basi anaitii kwa shurut!

Viongozi wetu wana kazi nyingi tu za kufanya nje ya siasa lakini wanapenda wawepo siasani wasije wakashughulikiwa. Najua Ben Mkapa ana shughuli nyingi huko duniani lakini hukimbia na kuja kufanya siasa za hapa na pale. Tulimuona mwaka 2010 akituambia kuwa hakufanya kampeni kwa kuwa alikuwa na shughuli za kimataifa. Ilibidi arudi kuja kukipa tafu chama chake kwenye kampeni. Siasa hizo wala si njaa bali tuwe pamoja tulindane.
 
- Heshima mbele wakuu wote JF, baada ya muda mrefu sana tupo wote tena unajua mishe mishe ya maisha.

Leo ya ustaafu kutoka kwenye siasa zetu Tanzania, I mean tufike pahali tujikite as a nation kulitengeneza hili la Ustaafu kutoka kwenye politics, hatuna mazingara yanayofaa as the results Wazee wetu wengi hawataki kustaafu ni kwa sababu wanaogopa wataenda wapi? Leo kule US kina Condoleeeza Rice, Cohen, Kissinger, wamestaafu siasa na wamerudi kwenye professional zao za Ualimu pamoja na kulipwa posho nzito wanapotoa hotuba kwenye midhahara. Hivi karibuni Rais Kaunda, alikuwa anafundisha Boston College, wamemlipa vizuri tu as of their standards na sasa naamini yupo sawa sana kuliko alivyokuwa kabla ya kwenda kufundisha tena kazi yake ya zamani.

- My point ni kwamba panahitajika a serious National agenda au Kipengele kipya kwenye katiba cha kusimamia Ustaafu wa Wazee wetu kutoka kwenye siasa na kuwahakikishia comfortability na kuwezeshwa pamoja na heshima, ili wakitoka kwenye politics zetu warudi walikokuwa kabla, kama Udakitari, kama ni ualimu, Sheria hili linahitaji nguvu ya Taifa kulisimamia, ama sivyo hii vita kali iliyopo sasa ya kuingia kwenye uongozi wetu wa Siasa za taifa haitapungua karibuni na ndio chanzo cha siasa za majitaka na makundi, ambazo zinalitafuna sana hili taifa tunaishia kukosa viongozi bora wengi kwa sababu ya Vita kali ya kuingia na wasiotaka kutoka, uchaguzi ukiisha kunabaki makovu na majeraha makubwa sana mpaka hatuwezi kusameheana kisa simply hatuna pengine pa kwenda na tulishaamini kwamba nafasi tulizonazo ni zetu milele kumbe ni za wananchi na infact ni za Taifa na ni haki kwa kila mwananchi kugombea!

MUNGU AIBARIKI TANZANIA!

Field Marshall Es: WAZEE WA SAUTI YA UMEME!

FMES,

..lakini mafao ya viongozi wakuu[raisi,vp,pm] wastaafu ni mazuri, hilo halina ubishi.

..pia hatuwezi kujilinganisha na USA kwasababu wenzetu private sector inalipa kuliko public sector kama siasa. yaani wanapoingia kwenye public sector, siasa, etc wanakuwa pale kujitolea na kutumikia. Bill Clinton is making money baada ya kustaafu. David Axelrod is making more money as Obama campaign stategist kuliko wakati alipokuwa White House kama Senior Advisor to the president of US.

..kwa msingi huo utaona kwamba hapa Tanzania mambo ni kinyume-nyume. Ukiwa ktk public sector mfano bungeni, then it is an opportunity to make tons of money, ukirudi kwenye private sector ndiyo sasa "unajitolea" au "unatumikia." Hicho ndicho kinachopelekea watu wengi kujaribu kila njia kuingia ktk siasa na wakifanikiwa hawataki kutoka.

..kwa mtizamo wangu hoja yako ingekuwa nzuri zaidi kama ungetuasa, kama taifa, tutafute njia ya ku-reverse hii trend ambapo private sector haivutii kulinganisha na public sector, haswa siasa. Siasa ibakie kwa wale ambao wana moyo na usongo wa masuala ya public policy, na kutumikia wananchi. wakati huo huo Private sector tuwe na watu wanaosukumwa na utashi wa kutengeneza mapesa na faida.

..pia masuala ya pensheni na public services[huduma za afya,..] yarekebishwe across the board, I mean kwa kila Mtanzania. nafahamu viongozi wakuu wastaafu almost wana-maintain maisha waliyokuwa wakiishi wakati wa utumishi wao. I dont think we can say the same kwa civil servants waliokuwa wakifanya nao kazi.
 
Bwana FM ES, au ndugu William Malecela, Tatizo la unganganizi wa madaraka ni moja ya tatizo sugu ama gonjwa sugu linalokabili wengi wa viongozi wanaotawala ktk nchi zetu za kiafrika Tanzania ikiwamo
Hali ya kiongozi kuamini kwamba yeye ndio bora, ama akizidi kuwapo ndipo atakapokusanya zaidi ni moja ya visababishi vya tatizo hili.
Tufike mahali tuwe na sheria yenye kuhimiza kwamba ukiwa mtawala wa kisiasa baada ya miaka ama nane au kumi ungatuke ili kupisha mawazo mapya na nguvu mpya.
Mfano unaona kama hizi nafasi za upendeleo kwa kina mama watu flani kama Anna Abdala na wengine wengi wamefanya kama ndo zao peke yao.
 
FMEs idea yako ni nzuri lakini inatekelezeka kwa baadhi ya vyama. Kuna wazee wamekwishastaafu siasa lkn bado ni wanasiasa kwa kutumia remote control. Tukifanikiwa kwanza kuondoa tatizo la "fulani anawaandaa/aliwaandaa/aliwabeba akina nani kabla hajang'atuka" tutaweza hii kitu vinginevyo tutaendelea kutwanga unga wa ngano
 
Bwana FM ES, au ndugu William Malecela, Tatizo la unganganizi wa madaraka ni moja ya tatizo sugu ama gonjwa sugu linalokabili wengi wa viongozi wanaotawala ktk nchi zetu za kiafrika Tanzania ikiwamo
Hali ya kiongozi kuamini kwamba yeye ndio bora, ama akizidi kuwapo ndipo atakapokusanya zaidi ni moja ya visababishi vya tatizo hili.
Tufike mahali tuwe na sheria yenye kuhimiza kwamba ukiwa mtawala wa kisiasa baada ya miaka ama nane au kumi ungatuke ili kupisha mawazo mapya na nguvu mpya.
Mfano unaona kama hizi nafasi za upendeleo kwa kina mama watu flani kama Anna Abdala na wengine wengi wamefanya kama ndo zao peke yao.

- Mkuu hujanitendea haki jina langu ni FMES, mods vipi? ha! ha! ha! ha!

es!
 
Sio kila kitu tuige huko US na Zambia jamani, mbona nyie vijana mlioko huko hamtuletei vitu vinavyoendana na nchi yetu? Acheni ulimbukeni fikirini kutokana na mazingira ya hapa yalivyo biashara ya kufananisha ndo inatupoteza hatuna jipya. Mwishoni utatuambia tuanze kujenga nyumba za kuwalea vikongwe kama Ulaya

- Mkuu ni lazima tuseme mifano kwenye politics na sheria hata kama ni US,

es
 
..Mkuu Taasisi unazopendekeza ziundwe, tayari zipo, mojawapo ni Mwalimu Nyerere Foundation, wanaoiongoza hio Taasisi ni wazee wetu wastaafu, wengine wana CV nzuri tu, tatizo ni hizo siasa za Visasi, uchwara, majitaka. Kwamba ni mwiko kuikosoa Serikali iliyopo madarakani, ukifanya hivyo utakiona. Leo hii Mwalimu Nyerere Foundation ipo wapi??!!!
..Badala yake Wastaafu hao wanabaki kama ulivyooandika @Red hapo juu.
Mkuu Kivumah,
Natambua sana uwepo wa Taasisi ya Mwalimu Nyerere(MNF)!
Lakini napenda nikutahadharishe kuwa Taasisi ile , kama ulidhani ipo kwaajili hiyo, basi unatakiwa kufanya kazi ya ziada kuifuatilia.
Mkuu, Taasisi ninayoiota mimi ndotoni ni taasisi Neutral kabisa isiyohusika na chama chochote...Uliona vizuri sana MWAKA 1995 ambapo Mwalimu Nyerere aliachana na Madhumuni ya Taasisi yake mwenyewe, na akajikita kumpigia debe Mkapa, huku akiunanga vibaya sana upinzani, ambao wakati huo ulikuwa ukipeperusha bendera ya nccr-mageuzi na mgombea Mrema. Bado unaiamini Taasisi hii ya MNF?
BINAFSI SIIMINI KABISA.
 
FMES,

..lakini mafao ya viongozi wakuu[raisi,vp,pm] wastaafu ni mazuri, hilo halina ubishi.

..pia hatuwezi kujilinganisha na USA kwasababu wenzetu private sector inalipa kuliko public sector kama siasa. yaani wanapoingia kwenye public sector, siasa, etc wanakuwa pale kujitolea na kutumikia. Bill Clinton is making money baada ya kustaafu. David Axelrod is making more money as Obama campaign stategist kuliko wakati alipokuwa White House kama Senior Advisor to the president of US.

..kwa msingi huo utaona kwamba hapa Tanzania mambo ni kinyume-nyume. Ukiwa ktk public sector mfano bungeni, then it is an opportunity to make tons of money, ukirudi kwenye private sector ndiyo sasa "unajitolea" au "unatumikia." Hicho ndicho kinachopelekea watu wengi kujaribu kila njia kuingia ktk siasa na wakifanikiwa hawataki kutoka.

..kwa mtizamo wangu hoja yako ingekuwa nzuri zaidi kama ungetuasa, kama taifa, tutafute njia ya ku-reverse hii trend ambapo private sector haivutii kulinganisha na public sector, haswa siasa. Siasa ibakie kwa wale ambao wana moyo na usongo wa masuala ya public policy, na kutumikia wananchi. wakati huo huo Private sector tuwe na watu wanaosukumwa na utashi wa kutengeneza mapesa na faida.

..pia masuala ya pensheni na public services[huduma za afya,..] yarekebishwe across the board, I mean kwa kila Mtanzania. nafahamu viongozi wakuu wastaafu almost wana-maintain maisha waliyokuwa wakiishi wakati wa utumishi wao. I dont think we can say the same kwa civil servants waliokuwa wakifanya nao kazi.

Na hili la kufikiria kuwa hela nyingi iko kwenye public sector kuliko private nalo linafanywa kwa makusudi kwa sababu ya rushwa na kutofuata ethics za biashara. Leo hela inatengenezwa sana kwa makampuni yaliyoanzishwa na watu waliomo serikalini ambao wanatumia fursa hiyo kujigawia kazi wao au maswahiba wao.
 
Back
Top Bottom