Tanzania & Rushwa: What Is The Alternative?

Siasa za majina ndio zinakufanya hata hapa JF ujulikane kwani baba yako asingekuwa mtu mzito hapa nani angekujua wewe kwanza usingiweza kufurukuta wala hata huko USA usingeenda tena unatakiwa uishukuru rushwa sana ndio iliyokufikisha hapo ulipo

- Hapana mengine muwe mnafikiri japo kidogo sana, unasema Rsuhwa ndiyo iliyonipeleka baharini? Halafu ikanipeleka US kwenda kazini kila siku Saa nane za usiku na kazi za masaa 15 kila siku? rushwa ndiyo niliyonipeleka kwenda US kufanya kazi tatu, masaa 18 kwa siku?

- I mean great thinker, nilifikiri huwa wanafikiri japo kidogo kabla ya kuandika sasa vipi hapa?

Willie!
 
Heshima mbele sana Great Thinkers:-

- Sio siri kwamba Tanzania, tunasumbuliwa sana na tatizo moja sugu kuliko yote nalo ni tatizo la Rushwa. Miaka nenda miaka rudi tunahangaika pale pale na infact ndio kwanza hili tatizo linazidi kushamiri, I mean how did we get here na hili tatizo?

- Nimesikia viongozi wengi tena kwa miaka mingi sana wakilia sana kuhusu rushwa, lakini sijawahi kusikia wakisema alternative ya rushwa ni nini hasa?

- Wa-Tanzania tufike mahali tujulize tulifikaje hapa na Rushwa, wapi tunakwenda nayo? na What is the alternative?

William @DSM City!

Mkuu naomba ututendee haki kwa jambo moja:

Wewe ni miongoni mwa wanasiasa walioshiriki katika kugombea ubunge wa bunge la Afrika Mashariki kupitia tiketi ya CCM. Kati huo uchaguzi kulikuwa na tetesi nyingi kwamba katika mchakato huo wagombea wengi kama siyo wote, hasa wale wa CCM, walitoa rushwa katika kila ngazi. Hapa nina maana ya wakati wa kura za wabunge wa CCM na wakati wa kura za wabunge wote kama mgombea alipita ile hatua ya kwanza. Je mkuu katika huo mchakato kuanzia kura za maoni (yaani ndani ya CCM) hadi kwenye uchaguzi wenyewe unaweza kulisemeaje suala la rushwa?
 
Hapo kwenye nyekundu kamuulize Mzee Malecela ni vipi waliianzisha rushwa na kuiacha mpaka imeota miziz, wakati anagombea Urais wa mwaka 2005 na kina Kikwete ni kiasi gani cha Rushwa alipokea na kukitoa ili ashinde uchaguzi wa Urais na akashindwa baada ya vijana kuchachamaa kumtaka Kikwete!

NA hapo kwenye red ya pili

Umesikia WAKILIA au WAKILA Rushwa including mdingi wako! acha KUTUYEYUSHA baada ya kushindwa kule ubunge Africa Mashariki ndio unaiona Rushwa sasa hivi.

hebu toa upp uuzi wako hapa! unatutia hasira na KODI ZETU

- Mkuu wapi solution ya Rushwa kwa taifa lako na la baadaye? Hizi swaga zako kila mwananchi anaweza kuziongea, isipokuwa inapokuja solution ndio inakwua kivumbi, sema solution mkuu!

Willie!
 
- hapana mengine muwe mnafikiri japo kidogo sana, unasema rsuhwa ndiyo iliyonipeleka baharini? Halafu ikanipeleka us kwenda kazini kila siku saa nane za usiku na kazi za masaa 15 kila siku? Rushwa ndiyo niliyonipeleka kwenda us kufanya kazi tatu, masaa 18 kwa siku?

- i mean great thinker, nilifikiri huwa wanafikiri japo kidogo kabla ya kuandika sasa vipi hapa?

Willie!
ndio sio kila mtanzania anaweza kwenda nje?
 
- Kulikuwa na results pale, Waziri Mkuu na mawaziri wanne walijiuzulu, ingawa haikuwa the best solution ya Rushwa!

Willie!
Ziko best solutions mbili Willie:
-Turudishe Azimio la Arusha na miiko/maadili yake ya UONGOZI;
-Ile sheria ya rushwa ya enzi za Mwalimu irudi kama ilivyokuwa. Yaani mtu kama Mzee Chenge angesimamishwa tu mahakamani akatueleza na kututhubitishia jinsi alivyoipata ile dola milioni kule Jersey, sio PCCB kutafuta ushahidi!
Kijana kama wewe kuendelea kuiunga mkono CCM hivi ilivyo sasa imenisikitisha sana.
 
Mkuu naomba ututendee haki kwa jambo moja:

Wewe ni miongoni mwa wanasiasa walioshiriki katika kugombea ubunge wa bunge la Afrika Mashariki kupitia tiketi ya CCM. Kati huo uchaguzi kulikuwa na tetesi nyingi kwamba katika mchakato huo wagombea wengi kama siyo wote, hasa wale wa CCM, walitoa rushwa katika kila ngazi. Hapa nina maana ya wakati wa kura za wabunge wa CCM na wakati wa kura za wabunge wote kama mgombea alipita ile hatua ya kwanza. Je mkuu katika huo mchakato kuanzia kura za maoni (yaani ndani ya CCM) hadi kwenye uchaguzi wenyewe unaweza kulisemeaje suala la rushwa?

- Well, mkuu hoja zako nzito sana, ila muhimu sana kama ungelifungulia thread yake yaani Rushwa na uchaguzi wa EALA, kuingia hiyo ishu hapa ni kuchanganya ishus mbili tofauti, wananchi wenye akili nyingi hawatatuelewa Great Thinkers tunaanza kuchanganya mambo as if hatukuenda shule!

- Hii topic inahusu nini alternative ya rushwa?

Willie!
 
- mkuu unajua niliendaje nje? Si ungeuliza basi maana kama nilienda kwa rushwa basi hii nchi haina rushwa, uliza basi kabla ya kukimbilia huku kwenye uwanja wa dunia!

Willie!
kwangu mimi mtoto wa nyoka ni nyoka bwana,hata ule ubunge umeugombea tu kirushwa rushwa,kama sio rushwa hukustahili hata kuchukua fomu.....
 
Ziko best solutions mbili Willie:
-Turudishe Azimio la Arusha na miiko/maadili yake ya UONGOZI;
-Ile sheria ya rushwa ya enzi za Mwalimu irudi kama ilivyokuwa. Yaani mtu kama Mzee Chenge angesimamishwa tu mahakamani akatueleza na kututhubitishia jinsi alivyoipata ile dola milioni kule Jersey, sio PCCB kutafuta ushahidi!
Kijana kama wewe kuendelea kuiunga mkono CCM hivi ilivyo sasa imenisikitisha sana.

- Siuingi mkono kila kila kitu ndani ya CCM kama ambavyo siungi mkono kila kitu ndani ya Wapinzani, idea za kurudi kwenye Azimio la Arusha hayafai kwa sababu ni hayo hayo ndio yametufikisha hapa tulipo, sasa vipi tena great thinker kulilia turudi tena kule kule, jamani ongeeeni progressive solutions sio mambo ya kurudi kwenye maazimio ya Arusha, yale yalishapitwa, tulishindwa nayo mwanzoni hatuwezi kuyaweza sasa,

- Unasema zamani tulikuwa na sheria ya rushwa, niambie iliwahi kumfunga waziri gani? au kiongozi gani wa juu Tanzania aliwahi kufungwa au kuachishwa kazi kwa sababu ya rushwa? please unaona sasa ndio maana hata taifa linakwisha na rushwa cause hata great thinkers hatuna solutions1

- I mean great thinker unasema solution ni kurudi kwenye maazimio ya Arusha, really? tulifkaje hapa sio ni hayo hayo maazimio nonsense, I mean twende kwa mbele sio kurudi kinyume nyume! azimio la Arusha halikuweza then, haliwezi hata sasa!

Willie!
 
dawa ni kutaifisha mali za hao mafisadi na kuwafunga jela. tukisema wanyongwe watanyongwa wengi mno.
 
- Siuingi mkono kila kila kitu ndani ya CCM kama ambavyo siungi mkono kila kitu ndani ya Wapinzani, idea za kurudi kwenye Azimio la Arusha hayafai kwa sababu ni hayo hayo ndio yametufikisha hapa tulipo, sasa vipi tena great thinker kulilia turudi tena kule kule, jamani ongeeeni progressive solutions sio mambo ya kurudi kwenye maazimio ya Arusha, yale yalishapitwa, tulishindwa nayo mwanzoni hatuwezi kuyaweza sasa,

- Unasema zamani tulikuwa na sheria ya rushwa, niambie iliwahi kumfunga waziri gani? au kiongozi gani wa juu Tanzania aliwahi kufungwa au kuachishwa kazi kwa sababu ya rushwa? please unaona sasa ndio maana hata taifa linakwisha na rushwa cause hata great thinkers hatuna solutions1

- I mean great thinker unasema solution ni kurudi kwenye maazimio ya Arusha, really? tulifkaje hapa sio ni hayo hayo maazimio nonsense, I mean twende kwa mbele sio kurudi kinyume nyume! azimio la Arusha halikuweza then, haliwezi hata sasa!

Willie!
Sio kosa lako Willie. Haukuishi "practically" ndani ya Azimio la Arusha. Umezaliwa ukakuta tayari maisha yameandaliwa. Enzi zile ungemfunga nani? Mawaziri wote walikuwa masikini kabisa na walifuatiliwa nyendo zao kwa karibu kabisa. Hakukuwa na uwekezaji kwenye SIASA. Tafuta ule mkanda wa Mwalimu pale Kilimanjaro Hoteli na waandishi wa habari mwaka 1995. Utajua Mwalimu alivyoidhibiti rushwa hasa kwa VIONGOZI.
Amiin nakwambia bila Azimio la Arusha kurudi rushwa is here to stay permanently!
 
hahahaaaah William baana,
unalizwa ******/makalio ya nyani wakati mkia unauona, hahaaah !

ccm ndio mama wa uoavu, ccm imelea waovu , inakumbatia waovu inacheza kiduku na wezi wa mali za umma.

ccm ni kila kitu katika maovu, baba na mama wa uhalifu, viongozi wanalea watoto wao kuja kurithi mfumo wa wizi na uhalifu, ccm ni chama cha ufalme na kichifu, na yanafanyika hayo kwa lengo moja la kulinda na kujihami dhidi ya madhila yanayoendelea.
Hatutawaomba mtoke kwenye madaraka, kwa nguvu ya umma tutawang'oa , tutawashitaki na kuwafunga jela.
Mafisadi hawana muda mrefu wa kuendelea kula rushwa na kutafuna raslimali za taifa hili....hapa ni lazima ccm mpishe umma kwenye mamlaka na madaraka ya taifa.
 
Wewe umezaliwa ,umelelewa na umekuwa kwa rushwa
bado unaendeleza rushwa... Kumbuka juzi ulitoa rushwa source wewe mwenyewe
naona hii topic ni ngumu wewe kuizungumzia
ni sawa na kutoa kijiti kwenye jicho la mwenzako na wewe una borit
shikamoo kaka

No more to add !
 
Sio kosa lako Willie. Haukuishi "practically" ndani ya Azimio la Arusha. Umezaliwa ukakuta tayari maisha yameandaliwa. Enzi zile ungemfunga nani? Mawaziri wote walikuwa masikini kabisa na walifuatiliwa nyendo zao kwa karibu kabisa. Hakukuwa na uwekezaji kwenye SIASA. Tafuta ule mkanda wa Mwalimu pale Kilimanjaro Hoteli na waandishi wa habari mwaka 1995. Utajua Mwalimu alivyoidhibiti rushwa hasa kwa VIONGOZI.
Amiin nakwambia bila Azimio la Arusha kurudi rushwa is here to stay permanently!

Mkuu tatizo ni kuwa hawa watu wanaobeza azimio la Arusha hawakuishi katika kipindi hicho sasa ni vigumu kuelewa faida zake ndio hawa watu toka 80's
 
- Siasa za majina ndio zimelifikisha hili taifa hapa tulipo, sasa ungetegemea Great Thinker aonyeshee mfano wa kufikiria nje ya box la majina wapi, yale yale tu kelele as usual hakuna solution na kwenda kulala, mkuu ongea solution kwa ajili ya the future ya taifa!

Willie!
Wanyongwe au wewe unasemaje....
 
Back
Top Bottom