Kama kuvamia Tanzania, adui haitaji kutumia nguvu ya Jeshi bali dini, rushwa na ujinga

MALCOM LUMUMBA

JF-Expert Member
Jul 26, 2012
20,897
63,784
Tanzania ina madhaifu makuu matatu ambayo yameshaonekana mpaka sasa DINI, RUSHWA na UJINGA (NAIVETY).

SOMO LA KWANZA: UFALME WA UJERUMANI (UJINGA or NAIVETY)

Usidanganyike, huhitaji kutumia nguvu kubwa kuvamia taifa la watu ambao wamehalilisha rushwa kama sehemu ya utamaduni wa maisha yao. Adui hahitaji kutumia kujiingiza kwenye vita kubwa ambayo itamgharimu hata yeye, bali anachohitaji ni kumwaga mapesa mengi kwa watawala halafu kazi inakuwa imekwisha. Tokea mwaka 1871, Ufalme wa Ujerumani ndiyo taifa lililokuwa na nguvu iliyomithirika barani Ulaya. Kiufupi hakukuwa na taifa duniani ambalo lingeweza kupambana kijeshi na Ujerumani.

Mwaka 1917, miaka mitatu baada ya vita ya kwanza ya dunia, Uingereza, Urusi na Ufaransa walikuwa wamecharazwa vibaya mno na jeshi la Ujerumani na walikuwa wanapanga kusalimu amri. Kifupi ni kwamba, miaka miwili ya mwanzo ya vita ya kwanza ya dunia, Uingereza na Ufaransa zilivurugwa bila hata risasi yao moja kufika kwenye ardhi ya Ujerumani. Bahati mbaya sana Ujerumani alikuwa na tatizo kubwa la UJINGA. Serikali ya Ujerumani ilikuwa imajaa WAYAHUDI kwenye nafasi nyeti za kimaamuzi, huku wengi wakiwa hawajichukulii kama WAJERUMANI.

Mwaka 1917, Wazayuni waliwaambia Waingereza kwamba wasisalimu amri wao watawasaidia kushinda kwa kuhakikisha Marekani anaingia kwenye vita, ila tu baada ya vita kuisha waahidi kwamba watawapa eneo liitwalo Palestina liwe nchi ya Wayahudi. Uingereza kupitia waziri wake wa mambo ya nje, Arthur Balfour akatoa tamko liitwalo The Balfour Declaration ambapo akasema endapo Wayahudi duniani kote wataungana kuisadia Uingereza basi watapewa ardhi Palestina.

Maelfu ya Wayahudi waliokuwepo Ujerumani kwenye nafasi kubwa kisiasa na kibiashara wakaanza kufanya hujuma dhidi ya Ujerumani, na baadaye nchi ikashindwa vibaya vita mno. Wajerumani wameenda kusaini mkataba wa Versailles mwaka 1919, wanawakuja Wayahudi ambao Wajerumani wako kwenye mkutano wakidai Palestine, wakabaki kushangaa na kufahamu kwamba kumbe tulisalitiwa na watu ambao tulidhani ni raia wenzetu. Watu hawapendi kusema ukweli, ila hii ndiyo ilikuwa ni moja ya sababu chama cha KINAZI kupata nguvu kubwa Ujerumani na kuanza kuua maelfu ya Wayahudi.

SOMO LA PILI: DOLA LA RUMI (UJINGA or NAIVETY)

Moja ya sababu ya dola la Rumi kuanguka ni kuruhusu wageni kuingia bila mpangilio, wakidhani kwamba watawadhibiti endapo watasumbua. Karne ya nne, Rumi ilivamiwa na maelfu ya wakimbizi wa Kijerumani (Germanic Tribes) ambao walikimbia vita nchini kwao kwasababu The Huns kutoka Asia waliwaua na kuwachinja vibaya. Baada ya kupokelewa Rumi walianza kukaa kama raia wa kawaida. Rumi ilivyoingia kwenye matatizo makubwa ya vita za wao kwa wao, makabila haya yaliamua kutumia mwaka huu kuamua kutengeneza nchi zao ndani ya dola la Rumi.

Mara zote walipojaribu, vikosi vya kirumi viliwadhibiti, ila baada ya kipindi kupita wajerumani wakapata nguvu sana na kuamua kuvamia Roma, kuuchoma moto na kumteka mfale. Mwaka 410, chifu wa Kijerumani aitwaye Odoacer alivamia Ujerumani na kumpindua Kaisari Romulus na kuanzisha ufalme wake mpya wa Italia. Huu ndiyo ukawa mwisho wa dola la Rumi la Magharibi (The Western Roman Empire). Baada ya hapo warumi na kutawala kote dunia, wakajikuta wamegeuka watumwa wa vikabila vya watu ambao walikuwa hawafahamu hata kuandika, havina ustaarabu wowote ule, ambao hapo mwanzo waliwaajiri kama wachunga ng'ombe wao na wafanyakazi wa ndani.
 
SOMO LA TATU: DOLA LA KIKOMUNISTI LA YUGOSLAVIA (UJINGA, UDINI NA RUSHWA)

Baada ya vita ya pili ya dunia kuisha 1945, dola la kikomunisti la Yugoslavia liliibuka shirikisho la kikomunisti lenye uwezo mkubwa sana kujiendesha na kupata mafanikio makubwa mno ndani ya muda mfupi. Yugoslavia chini ya dikteta Josip Broz Tito, lilikuwa shirikisho la mataifa yafuatayo, Slovenia, Croatia, Bosnia & Herzegovina, Serbia, Montenegro na Macedonia. Taifa hili mwanzoni lilioneka lina umoja mkubwa, jambo ambalo lilipelekea uvamizi wa nje kutoka mataifa makubwa kutofanikiwa.

Shirika la kijasusi la Yugoslavia, liitwalo UDBA lilikuwa na uwezo usio wa kawaida. Dikteta wa Urusi Joseph Stalin kwa mara kadhaa alijaribu kupenyeza majasusi wa NKVD kumuua Raisi Josip Broz Tito, lakini hawakufanikiwa. Tito aliwahi kumtishia Joseph Stalin kupitia barua kwamba, amatumia majasusi wengi kumuua lakini yeye atatuma mmoja tu na hatarudia kutuma tena. Joseph Stalin na Lavrentiy Beria waliogopa mno na wakaacha kucheza na Yugoslavia.


Mbali na kuwa na idara bora za Ujasusi, na kuonekana kuwa na mshikamano uliojengwa kupitia Ujamaa, Yugoslavia leo halipo. Nchi wanachama zilizounda Yugoslavia zimekuwa maadui wa kutupwa hadi kupelekea mauaji ya kimbari (Srebrenica Massacre) kufanyika miaka ya 90's wakati wa vita vya wao kwa wao. Nini kiliisibu YUGOSLAVIA kuanguka vile? UJINGA, UDINI na RUSHWA.

Yugoslavia kabla ya uhuru iliwahi kutawaliwa kwa miaka mingi na Waturuki (The Ottoman Empire), jambo ambalo lilipelekea raia wengi wa nchi hiyo kuwa WAISLAMU hata baada ya uhuru. Kiasili, watu wa Yugoslavia ni SLAVIC, hivyo dini kuu ya ukanda ule ni UKRISTO WA KIORTHODOKSI. Wakati nchi iko chini ya ukomunisti, dini haikuwa na nguvu sana, ila baada ya Tito kufariki na Ukomunisti kuondoka, watu wakaanza kuzungumzia dini zao, huku wakijihusisha na mataifa makubwa yenye dini hizo.

WAISLAMU, wa nchi ile walikuwa wanawapenda sana Waturuki kwasababu waliamini kwamba Uturuki ndiyo taifa kubwa la kiislamu kipindi hicho na ndiyo ndugu zao kuliko wakristo wa nchi ile. Hivyo Uturuki alitumia mwanya huu kuendelea kuwaunga mkono waislamu wa nchi hiyo huku akiwa anaangalia fursa kubwa za kiuchumi. Upande wa pili, WAKRISTO wa nchi ile waliamini kabisa kwamba URUSI, ambalo ndiyo kitovu cha dini ya Kiorthodoksi ndiyo ndugu zao kuliko waislamu.

Kibaya zaidi ni kwamba, Waislamu wengi kutoka nchi jirani ya Albania walianza kuhamia Yugoslavia na kukaa eneo la Serbia liitwalo Kosovo. Watu walimuonye dikteta Tito kwamba awafukuze kwasababu ni wahamiaji haramu na wengi wao ni wakimbizi, lakini hakutilia mkazo. Aliamini kwamba angeweza kuwageuza wale Waislamu kutoka Albania na kuwafanya raia wa Yugoslavia. Akawajengea chuo kabisa kule Kosovo na kuwapa elimu bora kabisa, lakini ilipofika miaka ya 90's wale vijana wa Kiislamu wakaanzisha kundi la uasi kutaka kuitoa Kosovo nje ya Yugoslavia huku wakiwa wanaungwa mkono na mataifa ya nje ya kiislamu kama Uturuki.

Upande mwingine Wakristo wakiongozwa na Serbia, wakiungwa mkono na Urusi, wakakianzisha na kuanza kuua maelfu ya Waislamu ambao walichukuliwa kama watu ambao wanataka kuvunja muungano. Mwishowe vita vilikuwa vikubwa, na nchi ikaanza kumeguka na mataifa ya Magharibi yakiongozwa na NATO yakatumia mwanya huu kuivamia nchi ya Yugoslavia na kuigawanya vipande-vipande mpaka leo hii. Serbia akapoteza eneo la Kosovo ambalo lilikuwa sehemu ya nchi yao, lakini leo hii linakaliwa na wageni wa kiislamu kutokea Albania, ambao Tito aliwaruhusu kukaa.

Mataifa kama Slovenia na Croatia, yalitamani maisha ya nchi za Magharibi hivyo watu wake kama Raisi Franji Tudman wakapewa milingula na msaada kutoka nchi za Magharibi ili kupambana na ndugu zao Serbia. Walichinjana vibaya mno kisa kutamani maisha ya kifahali ya Magharibi ambayo wanayaona kwenye vyombo vya habari. Mpaka leo hali imekuwa mbaya kwenye hizi nchi na mahusiano hakuna.

DINI, UJINGA na RUSHWA viliiua YUGOSLAVIA.
 
Mwaka 2023, taifa lilionesha mianya mibaya ya UDINI hasahasa kwenye suala la bandari. Hoja kuu za waliopinga mkataba ilikuwa ni kwamba ule uwekezaji ulifanywa kwa minajili ya UDINI, RUSHWA na UJINGA. Upande wanaotetea walisema kwamba UDINI ndiyo sababu za mkataba kupingwa, mbona na ninyi mliruhusu mataifa ya wazungu kuja kuwekeza kwasababu za DINI.

Kiufupi, mpaka kufika sasa, taifa la Tanzania linaweza kujitia moyo kwamba liko salama ila ukweli ni kwamba haliko salama eneo lolote lile. Tunasema hivi kwasababu ukweli ni kwamba, hata miaka ya 70's kuelekea vita ya Kagera, majasusi wengi waliotumiwa na Idd Amin walikutwa ni watu wa Kagera, wengine wasomi wakubwa kabisa, na wengine walifanya hivyo kwasababu za kidini. Baada ya JWTZ kufika Kampala na kuwafahamu watu hao, walibaki midomo wazi tu.

Nchi ni taasisi ngumu sana kuongozwa, binafsi huwa naamini kabisa WAFIA DINI, WALA RUSHWA na WAJINGA hawatakiwi kabisa kuongoza taifa. Wakomunisti mbali na kupingana nao kwenye mambo mengi, lakini hili la kupinga DINI na RUSHWA huwa nawaelewa mno. Nchi ikiwa na dini moja, kama UISLAMU au UKRISTO basi ipo salama, bali ikuwa na DINI MCHANGANYIKO, haiko salama kabisa na lazima serikali ihakikishe WAFIA DINI hawasogei kabisa kwenye kiti cha URAISI.

Hebu fikiria, Askofu anajisifu hadharani, kwamba kuna siku waliwahi kumuita Raisi fulani na kumkalisha kitako kwasababu tu ni mshirika wao na walimsomesha seminari. Wanamkalisha kitako na kuanza kumpa amri kuhusu mambo ya kitaifa. Wao wanaamini kwamba kwasababu mshirika wao alikubali kukalishwa kitako, basi lazima kila Raisi akalishwe kitako. HILI HALIKUBALIKI HATA KIDOGO KWASABABU LINAJENGA NYUFA KWENYE TAIFA.

Upande mwingine, unakutana na SHEIKH ambaye hata shule hajafika, na hana uelewa wa mambo mtambuka amekusanya rundo la waumini, wengine wasomi kabisa anaanza kuwahubiria kwamba Waarabu wa nje ni ndugu zao hivyo wakubaliwe kufanya lolote lile hapa nchini hata kama ni baya kiasi gani. Wengine wako hata radhi kujiunga na mitandao ya kigaidi yenye itikadi kali kueneza Jihadi. HILI NALO HALIKUBALIKI HATA KIDOGO NA ANAYELIFANYA HILI INABIDI AACHISHWE KUONA MWANGAZA WA JUA.

Nafahamu kwamba ntawakwaza wengi kwasababu watanzania hupende mno dini kiasi cha kujitoa ufahamu, lakini popote pale penye UDINI huwezi kukosa kuona UJINGA ukiwepo. Binafsi sikatai dini, ila sipendi kuona DINI inatumika kama SERA YA KIUTAWALA. (HAIWEZEKANI)

Wengine mpaka leo kwenye makanisa ya kiroho, wanalipwa fedha na mashirika ya kizayuni kuhakikisha kwamba Propaganda za kibaguzi za Kizayuni zinahubiriwa madhabahuni, zikisema kwamba kuna taifa teule ambalo hata lifanyeje hamtakiwi kulikemea na inabidi mliunge mkono kwasababu ndiyo MPANGO WA MUNGU. Ubaya ni kwamba taifa hilo ambalo mnaliita TAIFA TEULE ndiyo linahusika kuwafundisha kijeshi majasusi wa nchi inayoruga CONGO. Kiufupi siku Tanzania inafanyiwa hujuma, fahamuni kabisa kwamba TIAFA TEULE LA BWANA litakuja kuwaunga mkono wavamizi kwasababu rasilimali za nchi hii zinahitajika mno kuendeshea teknolojia mpya za karne ya 21.

EITHER WAY, YOU FOOLS ARE DOOMED!
 
Hamna unachokijua ungekuwa na akili hiyo elimu unayojifanya kwamba unajitambua imeletwa na wazungu ndio maana unasoma kwa kingereza ,lugha sio yako ile imekutawala ili uwe msomi ..

Unatawaliwa milele na wazungu yaani nyenzo muhimu kama elimu ambayo ndio imebeba utamaduni wa jamii yote ...Tunafuata ya mzungu ...Kaa kwa kutulia .!
 
Walianza taratibu wakifahamu kwamba watanzania kwenye UKABILA siyo sanaaa, lakini likija suala la UKRISTO na UISLAMU basi hapatakalika. Watanzania bila kufikiri tukajaa mkenge.
Watanganyika wenyewe ndiyo waliopanda na kueneza MBEGU ya udini,Tena wakidhani Wana akili Sana!!
 
Hamna unachokijua ungekuwa na akili hiyo elimu unayojifanya kwamba unajitambua imeletwa na wazungu ndio maana unasoma kwa kingereza ,lugha sio yako ile imekutawala ili uwe msomi ..

Unatawaliwa milele na wazungu yaani nyenzo muhimu kama elimu ambayo ndio imebeba utamaduni wa jamii yote ...Tunafuata ya mzungu ...Kaa kwa kutulia .!
Ujinga+ujinga=mtanganyika
 
Back
Top Bottom