Tanzania Presidents: Nyerere, Mwinyi, Mkapa and Kikwete

Alikuwa anapunguza big government.nyumba Za serikali kazi kutunza

Kazi kuzitunza? Mbona walijenga MPYA za MAWAZIRI na Manaibu Mawaziri? Alisign contracts na Makampuni ya DHAHABU sasa ina Maana bado kuziendesha hizo NYUMBA ilikuwa VIGUMU? Mbona wakati wa UTAWALA wa NYERERE pesa zilipatikana? Sababu Walikuwa Wanazi-Assign kwa Makampuni ya UMMA na Hayo Makampuni yaliwajibishwa kuzitunza hizo NYUMBA... Sasa kwanini walipeana??? Mama Mkapa anazo KIBAO...
 
Huyu ndie alieuza nchi, mikataba yote mibovu ni ya kwake matundo ya kazi ya mkapa ndio haya tunayo umianao sasa, Alioyanya Mwinyi tuliyaona kipindi cha Mkapa na anayofanya Kikwete tutayaona atakapo ondoka. Sijui umenielewa?


Mkapa alikuwa na cabinet ya wasomi sana na sio wanasiasa.uchumi ulikuwa
 
sikuzote unapokua mloo au FISADI lazima utatoa sababu za KIFISADI ili uhalalishe Ufisadi wako kwani ulikua unatoa pesa mfukiono mwako ku Tunza hizo nyumbaa??? alikua anaona ahibu baadae ambiwe ahame pale SEEVIYOU..ni bahati tungesikia pia IKULU imeuzwa sababu iko BAHARINI KUNANUKA wageni hawawezi fikia pale hizo ndio Lugha za MAFISADI hatushangai kusikia hayo
je nyerere alifanya vyema ???zaidi ya kutulisha YANGA na kuweka watu VIZUIZINI???ndio maana watu wakawa huwezi kuongea wala kulalamika wala kutoa maoni kama ww lei umetoamida hii ungekua ndani UNANYEA DEBE nahakuna hata ndugu yako atakae luhusiwa kukuona mpaka atake yeye jehuyo ndio BORA?????

Hey kid.....What a stupid ****in language!

Yawezekana Nyerere aliwaweka ndani sababu ya lugha chafu kama yako. Acha kuniharibia kiswahili changu adhimu, katolee povu hukoo feri ulikokulia, swain!
 
From spiritual dimension, "Tanganyika"

Tanzania haijawahi kuwa na kiongozi bora tokea mwanzo wake. Hii ni matokeo ya laana ya kumuacha Mungu, Period.

Tanzania ilikabidhiwa kwa shetani baada ya uhuru kwenye lile tendo la kupandisha bendera juu ya mlima Kilimanjaro. Apandacho mtu ndicho huvuna, Ndio maana tupo hapa tulipo leo ni mavuno ya yaliyopandwa na Baba zetu waliotangulia. Tangu tupate uhuru 1961, kiwango cha ubora wa maisha ya mtanganyika kimeshuka sana, umasikini umekithiri, mkandamizo umeongezeka. We were better 50 years back than we are today,niliangalia picha za uhuru through TBC (during 50 yrs celebrations) nikaona jinsi watu walivyo kuwa, walikuwa vizuri na imara kuliko kuliko tulivyo leo. Hatukupata kiongozi mwenye maono ya mbele (visions of the future), si kwa bahati mbaya bali ni Mungu aliwanyima kuona mbele. Karibu wote waliwaza pale walipo ku prove haya angalia Serikali na Muundo wake, angalia Miundo mbinu yetu yaani ni problem, problem problems. Angalia wananchi, asilimia kubwa wana amini uchwawi (shetani kuliko Mungu). Hapakuwepo wa kusimamia ndoto za kuiondoa Tanzania katika umasikini badala yake tumeingia kwenye mtego wa misaada ambao hatutatoka mpaka atokee mtu makini wa kusema basi. Kuna mambo yanayo endelea ambayo hata viongozi wenyewe hawaelewi ni kwa sababu they are all designed and ochestrated behind the scenes and governed by evil principalities and powers (in the spiritual realms). Yapo maswali ambayo viongozi wetu hawana majibu, mfano kuna wakati Rais wetu alijibu kwenye interview kwamba hajui kwa nini Tanzania ni masikini; ni kweli, hakukosea hata kidogo, alisema ukweli ingawa wengi tumlimshangaa. kwani haiingii akilini kwamba pamoja na rasilimali zote zisizoisha tulizonazo ambazo kila mweupe anajichukulia kupeleka kwao, Hajui kwa nini Tanzania ni maskini, ukweli ni kwamba kuna uovu unao fanyika nyuma ya pazia ambao unasababisha tuyaone haya (bacause the truth is evil that is behind the scenes). Ukitazama vizuri katika awamu zote Kiongozi wa awamu moja wapo anapofanya vizuri, basi awamu inayo fuata lazima aharibu fuatilia sequence ya viongozi wetu (we labor in vain). Kumbe badala ya kuwachukia viongozi wetu tungeanza kimchukia aliye nyuma yao kwanza (ambaye ni shetani) na ku deal naye mpk atoke, ndipo tutapata ushindi katika Mungu. Kwa mfano tunapo wasema vibaya, tunalaaniwa licha ya mapungufu yao, kwa sababu imeandika you shall not speak evil of the ruler of thy people, any time you speak evil you invite a curse. Je ni mara ngapi tumewasema vibaya? Tuombee nchi yetu ili pawepo na Mwanga (Nuru).

Ni tanzania hii hii ndio inayolalamikiwa na nchi nyingine kupandikiza viongozi wa ki-shetani kwa mataifa mengine ya afrika wakati ilipokuwa na ajenda iliyoitwa kuzisaidia nchi nyingine za afrika kupata uhuru wake. Kumbe ilikuwa ni agenda ya kishetani, wakati sisi tunajisifu tuliwasaidia wengine kupata uhuru, una yaliyofichika nyuma yake.

leo hii kila mtanzania analalamika, kuanzia viongozi wa ngazi ya juu zaidi (Rais) mpaka wananchi wa kawaida ni malalamiko tu kila kona. Tunaweza kufikiri labda kikija chama kingine ndio kita badilisha maisha haya ya watanzania, hamna kitu.

Hili ndilo tatizo kuu limesababisha haya yote tuyaonayo leo, na halitaondoka hata aje Rais wa Marekani kuongoza hapa Tanzania, bali ni pale watanzania tutakapo amua kumrudia Mungu kwa rehema ya kweli. Maana ndiye pekee anayeweza.

Najua post yako ya pili itatutaka tutoe sadaka, nakuahidi kuwa nitakupinga vikali.
 
Nyerere, Mkapa, Mwinyi, Kikwete. Nyerere kajenga umoja wa nchi yetu unaochezewa sasa. Alikuwa kiongozi siyo mtawala, aliipatia elimu kipaumbele hata wakati fulani wajua kusoma na kusoma Tz ikaongoza Afrika,aling'atuka mwenyewe tofauti na wengine ambao hung'ang'ania kubaki madarakani hata kwa kuchakachua, hakuwa fisadi, alikuwa na moral authority, muadilifu, aliwapenda watu wote nk.
 
Nimesoma posts nyingi hapa na ninachokiona (kwa mtazamo wangu) ni poor logic of comparison. Na hii imewaathiri zaidi Nyerere na Mwinyi.
1. NYERERE: Huyu jamani tukumbuke hakuichukua hii nchi toka kwa rais mwingine. Tunapaswa kuzingatia kuwa walioondoka walikuwa Wakoloni na sisi tukabaki wenyewe. Kuna jamaa mwenye kuitwa zomba alifikia sehemu ya kusema kuwa Nyerere aliua kilimo kwa sababu aliichukua nchi ikiwa ya kwanza kwa kusafirisha mazao Africa lkn in few years trend ikabadilika. Hapa utagundua kuwa zomba hajui tofauti ya uchumi wa Tanganyika chini ya mkoloni na Tanganyika tukiwa wenyewe.

Nyerere alianza uongozi wa nchi akiwa na rasilimali watu haba. Hapa mtakimbilia kusema 'mbona aliwaweka kando wasomi' lkn nataka kwanza mjue kuwa wengi wa hao wasomi hawakuwa Wazalendo na nia zao zilitisha kuliko mnavyofikiri kwa hiyo YES, walikuwa tishio na si kwa utawala wa Mwalimu, bali Tanganyika yenyewe. Tukumbuke kuwa hata Siasa ya Ujamaa ilikwamishwa na hao hao wasomi kwa kuwa ilibana maslahi yao. Wakati wa Nyerere, hakukuwa na teknolojia tuliyonayo leo, je twapaswa kumlaumu kwa hilo?

2. MWINYI: Huyu naye aliipokea nchi ikiwa kwenye transition period kutoka kwenye UJAMAA kwenda kwenye UBEPARI (Wa kilofa). Katika hali ile ya kukabiliana na mabadiliko na pressure ya kukua kwa uchumi wa dunia, tutamlaumu bure Mwinyi. Nyerere alishakubali matokeo kuwa UJAMAA umefeli, na ikawa kazi ya Mwinyi kubadili misingi kwa namna isiyotishia mshikamano wa Taifa. Hiki ndio chanzo cha kuyumba hapa na pale ukizingatia na kiongozi mwenyewe hakuwa na makucha

3. MKAPA: Hili lilikuwa jembe. Kutoka pale alipoachia Mwinyi, yeye ndio hasa aliupa nafasi UBEPARI na leo unaona tumechangamka japo tunaumia. Utakuwa mwehu wa mawazo kutokumbuka kuwa mfumuko wa bei tk kipindi cha huyu jamaa ulidhibitiwa na madeni ya nje yalilipwa kwa kasi ambayo iliwafurahisha wakopeshaji hata leo wanampa misaada huyu muombaji. Dhambi kubwa ya huyu jamaa wa kusini ni WIZI. Nitamkumbuka kwa kuwa alikuwa Rais mtendaji na si mnung'unikaji (Hakuna aliyethubutu kumpa ultimatum)

4. KIKWETE: Hapa kuna tatizo. Kuna aliyoweza kufanya, tena mengi zaidi ya yeyote kabla yake. Swala linakuja, kwa kiasi gani cha mtaji? Watanzania si watu wa hesabu na hili linampa credit Kikwete. Aliyetumia 100 kununua 40 anasifiwa zaidi ya aliyetumia 50 kununua 30. Watanzania wanaangalia kiasi gani kimeletwa bila kujali kiasi gani kimetumika. Rasilimali za nchi yetu sasa zimechimbika kweli kweli na wenyewe tunasherehekea. Kupata 100 kwa kumuuza twiga ndio kunakoshangiliwa na Watanzania wasiofahamu kuwa tungeweza kumkodisha kwa 20 kwa mwezi. Ni kwa Rais huyu ndio tumeshuhudia Mwekezaji anapewa shirika halafu serikali hiyo hiyo iliyompa dhamana inalipa mishahara na hatujiulizi dhana ya uwekezaji inalalia wapi

1. Nyerere
2. Mkapa
3. Mwinyi
4.
 
Last edited by a moderator:
Kila mmoja alikuwa na uzuri na ubaya wake pia. Wewe mwenye nyuzi hii ungekuwa wazi kwenye nyanja maalum
ili wanajamvi waweze kuchangia katika tathmini zao kuhusu nyuzi yako bana
 
Nimesoma posts nyingi hapa na ninachokiona (kwa mtazamo wangu) ni poor logic of comparison. Na hii imewaathiri zaidi Nyerere na Mwinyi.
1. NYERERE: Huyu jamani tukumbuke hakuichukua hii nchi toka kwa rais mwingine. Tunapaswa kuzingatia kuwa walioondoka walikuwa Wakoloni na sisi tukabaki wenyewe. Kuna jamaa mwenye kuitwa zomba alifikia sehemu ya kusema kuwa Nyerere aliua kilimo kwa sababu aliichukua nchi ikiwa ya kwanza kwa kusafirisha


kweli no 4 haipo kabisa
 
Last edited by a moderator:
Namfagilia waa waa aa Nyerere, sababu alikuwa anaichukia rushwa kwa moyo wake wote, kwa akili zake zote, nguvu zake zote, ....
 
Namfagilia waa waa aa Nyerere, sababu alikuwa anaichukia rushwa kwa moyo wake wote, kwa akili zake zote, nguvu zake zote, ....

Wakati wa Nyerere ndio rushwa ilianza kuota mizizi na mashina kushamiri na akashindwa kabisa kuizuia hiyo mizizi na mashina kusambaa. Tuulize tuliokuwepo usisikie ya kujazwa Ubaguzi wa Ujinga.
 
Siwachukii dada yangu, ila nataka walipe kodi kwa kadri ya kipato chao. Remember, to whom much is given, much is expected. siyo kukwepa kulipa kodi kwa kuficha hela zao Cayman Islands kama alivyofanya nanihii.
Jasusi,richer will be richer and poor will be poor.poverty is a curse bible says that
 
je nyerere alifanya vyema ???zaidi ya kutulisha YANGA na kuweka watu VIZUIZINI???ndio maana watu wakawa huwezi kuongea wala kulalamika wala kutoa maoni kama ww lei umetoamida hii ungekua ndani UNANYEA DEBE nahakuna hata ndugu yako atakae luhusiwa kukuona mpaka atake yeye jehuyo ndio BORA?????
Nyerere was a champion of equal justice.ndio title yake hapa duniani.Halafu unga wa yangu Huku USA very expensive halufu mkate wa siha ni mkate mzuri
 
Wakati wa Nyerere ndio rushwa ilianza kuota mizizi na mashina kushamiri na akashindwa kabisa kuizuia hiyo mizizi na mashina kusambaa. Tuulize tuliokuwepo usisikie ya kujazwa Ubaguzi wa Ujinga.
Watu walienda jela mzee ngaiza
 
Kazi kuzitunza? Mbona walijenga MPYA za MAWAZIRI na Manaibu Mawaziri? Alisign contracts na Makampuni ya DHAHABU sasa ina Maana bado kuziendesha hizo NYUMBA ilikuwa VIGUMU? Mbona wakati wa UTAWALA wa NYERERE pesa zilipatikana? Sababu Walikuwa Wanazi-Assign kwa Makampuni ya UMMA na Hayo Makampuni yaliwajibishwa kuzitunza hizo NYUMBA... Sasa kwanini walipeana??? Mama Mkapa anazo KIBAO...
Wengi wanakaa Kwenye nyumba zao.Rais ambaye alichaguliwa Kuwa rais na hakuwa na nyumba ni kikwete.Nyerere alikuwa anakaa msasani
 
Wengi wanakaa Kwenye nyumba zao.Rais ambaye alichaguliwa Kuwa rais na hakuwa na nyumba ni kikwete.Nyerere alikuwa anakaa msasani

Mwinyi alikuwa anakaa IKULU wakati wa URAIS wake; Kwahiyo MKAPA hakukaa IKULU???
Nyerere alikaa IKULU Mpaka JESHI ilipomjengea NYUMBA MSASANI na kuumpa kama zawadi wakati ULE Wa Zamani... Na ENEO lote wakati huo NYUMBA zilikuwa CHACHE MSASANi isipokuwa Wavuvi na Walima MPUNGA Wengi walikuwa wanapata MSAADA wa NYERERE na hata ARDHI yao alikuwa anawasaidia KUTOCHUKULIWA na WALAFI...
Sasa HIVI OH LAH...

Lau Masha alikuwa anakaa NYUMBA ya SERIKALI ya WIZARA ilimchukua MDA kuhama; NYUMBA hizo ni nzuri za KISASA; Akamsababisha Shamsi VUAI kukaa Sana HOTELINI na kuiingizia GHARAMA SERIKALI...
 
Back
Top Bottom