Tanzania Presidents: Nyerere, Mwinyi, Mkapa and Kikwete

MotoYaMbongo

JF-Expert Member
Jan 7, 2008
2,146
884
Hawa ni marais kuanzia wa kwanza hadi wa sasa.

Nyerere alikuwa hana mchezo na wahujumu uchumi wa nchi híi, he was serious na alikuwa mkali sana, Mwinyi yeye ni ruksa tu, Mkapa dharau na kejeli kwa wenye mawazo mbadala, ndo chanzo cha ufisadi, Kikwete sasa ndo ameamua kuwakumbatia na amedhibitisha bungeni juzi kwa kuwabembeleza kama uncle zake.

Nalaani kitendo hicho.

Nawasilisha hoja
 
acheni kumsifu mtu kijinga, yeye ndio wa kwanza kututiya kwenye njaa, alikuwa akiwabadilisha watu toka kampuni hii kwenda kampuni hii baada ya kuuwa moja mtu alipelekwa kwenda kuuwa nyingine. na hii inajulikana kwanini mnaendelea kumsifu, alitufanya watanzania tuishie darasa la saba tujuwe kusoma na kuandika halafu tusome magazeti yake tufuate mawazo yake tuamke
 
Hawa ni marais kuanzia wa kwanza hadi wa sasa.

Nyerere alikuwa hana mchezo na wahujumu uchumi wa nchi híi, he was serious na alikuwa mkali sana, Mwinyi yeye ni ruksa tu, Mkapa dharau na kejeli kwa wenye mawazo mbadala, ndo chanzo cha ufisadi, Kikwete sasa ndo ameamua kuwakumbatia na amedhibitisha bungeni juzi kwa kuwabembeleza kama uncle zake.

Nalaani kitendo hicho.

Nawasilisha hoja

Tatizo kubwa tulilonalo wa Tz ni plae tunapotaka kuzungumzia historia na bila kuangalia facts, kila ulichosema hapo ni sahihi au sio sahihi inategemea una uthibitisho gani na mimi nina uthibitisho gani.Liwalo na liwe hao marais na assume walifanya makosa.mwingine amekufa na wengine wako hao lakini hawataweza kuwa tena marais.Amebaki mmoja amabye anatakiwa kufukia mabonde yote ya yaliyoachwa na watu wa nyuma naye ni Kikwete.

Kwa kukusaidia hata usema nini Mkapa pamoja na utakavyomsema vyovyote vile Kikwete hajafika na hatamfikia Mkapa mpaka anakufa!Mkapa hawezi kupiga domo kama unavyotaka wewe!Kiburi hana na kejeli hana, sisi ujinga umetujaa, twende mahakamani afunguliwe mashtaka, kutofanya hivi sisi ndi tunakuwa wajinga na wenye viburi tena vikubwa!.Ufisadi mwingi umeanzia kwa Mwinyi , so mkapa ana makosa ya kuukumbatia, Kikwete naye ana makosa hayohayo....... si ajabu Mbowe na ikawa hivyohivyo who knows.Nyerere hakuwa Mungu na hali hii mbaya Nyerere ndio chanzo.

Wengi huwa mnaona viongozi ni Mungu watu!, na ndiyo hii CCM wenye kaptula zao na wanaandamana kuunga mkono hotuba ya Kikwete!
 
kutuambia kwamba mkapa hajatutia umasikini wa kiama ni kutuambia kwamba sie wote ambao tumeona usfisadi wake tuwaongo wakumbwa,Hapa unatutia nguvu hatutachoka mpaka tukuonyeshe ukweli. Kuna mungu huyu mtu ametuibia sana sizani kama analala usingizi kwa madhambi aliyofanya. Tanzania kuna umaskini mkumbwa sana yeye kakomba kila kiti na marafiki zake. Huu ni ukweli.
 
Kikwete apewe muda awashughulikie mafisadi.

Hivi unategemea apewe report asubuhi jioni akurupuke na kutaja majina?

Mnachotaka ni kutajwa majina au watu kupelekwa mahakamani na sheria ikachukuwa mkondo wake na huko ndio majina yatajulikana.

mmesema waliohusika ni vigogo, mnafikiri kumchomoa kigogo ni rahisi.

WATANZANIA HATUNA SUBIRA.

Taifa Starz inafunga mechi moja mnawaita bungeni na kuwamwagia pesa, mechi inayofuata wanafungwa mnasema maximo mafukuzwe, HATUBEBEKI mpaka tupate Rais kama Idd Amin DADA.

NA HIYO IFUTEEEEE
 
Kaka Mweusi.

Nianze kwa kukuomba usome vizuri historia ya nchi hii. Tumetoka wapi,tupo wapi na tunaelekea wapi.
Mwaka 1961 sekta ya viwanda ilikuwa na ukubwa gani?,vilevile sekta ya kilimo , sekta ya elimu n.k.
Soma Azimio la Musoma na utekelezaji wake.Soma Azimio la Iringa la siasa ni Kilimo.

Soma Azimio la Arusha nini yalikuwa manufaa yake baada ya kutangazwa kwake na utekelezaji wake hasa katika kujenga industrial base na kukuza sekta ya elimu. Kabla ya 1967 elimu ilitolewa kwa ubaguzi,ni watoto wa machifu na wale wanaofanana na hao, ndio walipata fursa ya kupata elimu.

Serikali ya Mwalimu ilitoa ruzuku kwenye elimu na hivyo kila mwananchi alipata elimu bure.Vivyo hivyo huduma ya Afya ilitolewa bure. Kama binadamu Mwalimu alikuwa na mapungufu yake,lakini aliyofanya kwa nchi hii ni mengi , mazuri na ya msingi.

Tulifika mahala tuna tengeneza gari zetu sisi wenyewe aina ya NYUMBU,hakuna gari ya aina hiyo dunia nzima. Tulikuwa na TAMCO kibaha ambapo tuliassemble SCANIA na viwanda vingine vingi mfano TANITA,MWATEX,SPM Mgololo n.k

Kwa wale waliokuwa watu wazima wakati huo waliandaliwa mpango wao wa ELIMU YA WATU WAZIMA kwa lengo la kuwajengea uwezo hasa wakulima ,kuwa wakulima bora na kujifunza mbinu na maarifa mapya kwa njia ya kujisomea.

Mwaka 1982 , Literacy Rate kwa TZ ilikuwa 92% the highest after Egypt. NCHI ILIKUWA INASONGA MBELE,YOU COULD SEE KWAMBA KUNA MTU PALE MAGOGONI AMBAYE YUPO CONCERNED na maisha ya mtanzania wa kawaida.

Mwalimu alikuwa ni scholar ambaye hakuogopa mijadala,those days chuo cha Mlimani kilikuwa ni kisima cha maarifa na mijadala mikubwa ya kisomi yenye kutafakari njia sahihi yakuchukua sisi kama taifa na kama waafrika,watu walitoka mbali kuja kwetu kujifunza.Wanamapinduzi wakubwa wa kiafrika waliangalia Tanzania kama nchi ya mfano , waliangalia Chuo kikuu chetu cha Mlimani kama kiwanda cha kujenga fikra sahihi.Haya yote yalifanyika chini ya uongozi wa Mwalimukama raisi na Mkuu wa Chuo.

Kumbuka Mwalimu alikuwa na uhaba mkubwa wa wasomi,mahitaji ya mameneja wa mashirika na viwanda yalikuwa makubwa kuliko idadi ya wasomi ambao wangeweza kuchukua nafasi hizo.Ndio maana alihangaika mzee wa watu kujaribu kuhamisha huyu kumpeleka pale na wa hapa kumpeleka kule.Lakini hilo peke yake halitoshi,kusema alikosea kwa kubadilisha viongozi walioharibu na kuwapeleka pengine,kuna mambo mengi yalitokea internally na yale ambayo ni external yaliyo sababisha matatizo yale yaliyokuwepo.Hivyo kufa kwa mashirika au kuzorota kwa mashirika ni jambo linalohiotaji mjadala.

Naomba jiulize pamoja na kusifu sera ya ubinafsishaji.

JE ,WAWEKEZAJI WANGAPI WAMEWEKEZA KWA KUJENGA VIWANDA NA MASHIRIKA MAPYA KAMA SI YALE ALIYOACHA MWALIMU?

Ndugu Kaka Mweusi.
Nina imani wewe ni msomi. Basi naomba kwa unyenyekevu mkubwa,tumia elimu uliyonayo kufahamu wapi tulipo,tumetoka wapi na wapi tunaelekea.

TUEPUKA KUTUMIA MANENO YA KEJELI.
Rejea quote yangu hapo chini.
" Pride............. tread"
 
Kikwete apewe muda awashughulikie mafisadi.

Hivi unategemea apewe report asubuhi jioni akurupuke na kutaja majina?

Mnachotaka ni kutajwa majina au watu kupelekwa mahakamani na sheria ikachukuwa mkondo wake na huko ndio majina yatajulikana.

mmesema waliohusika ni vigogo, mnafikiri kumchomoa kigogo ni rahisi.

WATANZANIA HATUNA SUBIRA.

Taifa Starz inafunga mechi moja mnawaita bungeni na kuwamwagia pesa, mechi inayofuata wanafungwa mnasema maximo mafukuzwe, HATUBEBEKI mpaka tupate Rais kama Idd Amin DADA.

NA HIYO IFUTEEEEE

Nakuunga Mkono Mkuu!
Ila JK kama rais ana uwezo wote wa kuzika ufisadi mkubwa uliyoikumba nchi hii na kuididmiza kwenye umaskini wa kupindukia!Tukumbuke yale ya Babangida wa Nigeria kama sijakosea ambaye kuna Waziri mmoja mwanamke ambaye aliangaika five years mpaka zile fedha ziliporudishwa.
JK ana uwezo wa kuadhibu mafisadi mana kama Olmert amekuwa implicated in corruption na saa hivi amejiuzulu na anashughulikiwa na kama JK yuko implicated afanye hivyo maana uoga wake sasa unatutia shaka hata kama hao ndio waliomweka hapo alipo sasa ila kapitiliza na cowardship yake!
 
CCM yaonya wanaotaka kumchafua Mwinyi

Brandy Nelson, Mbeya
Mwananchi
Date::12/31/2008

CHAMA Cha Mapinduzi (CCM), mkoani Mbeya,kimevionya vyama vya upinzani vyenye lengo la kumchafua rais mstaafu wa awamu ya pili, Ali Hassan Mwinyi kwenye kampeni za uchaguzi mdogo wa jimbo la Mbeya Vijijini.

CCM inatarajia kuzindua kampeni zake za ubunge Januari 4 kwenye kijiji cha Ilembo kilicho tarafa ya Isangati, ikiongozwa na rais huyo wa serikali ya awamu ya pili.

Mwenyekiti wa CCM mkoani Mbeya, Nawabu Mulla alitoa onyo hilo wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu taarifa iliyotolewa kwenye vyombo vya habari kuwa wabunge wa CCM wagawanyika na kuwa Rais mstaafu Ali Hassan Mwinyi atakashifiwa endapo atahudhuria uzinduzi huo.

Mulla alisema kuwa, endapo kuna vyama vya upinzani vitatimiza lengo lao la kumkashifu kiongozi huyo, CCM haitakubali kwani kufanya hivyo ni kosa la jinai na hivyo hatua za kisheria zitachukuliwa.

"Navionya vyama vya upinzani vinavyosema kuwa vitamkashifu rais wetu mstaafu wa awamu ya pili wakati wa uzinduzi wa kampeni ya uchaguzi katika jimbo la Mbeya Vijijini, kuwa hatutakubaliana na vitendo hivyo... tutawachukulia hatua za kisheria kwa kuwafikisha mahakamani kwani kufanya hivyo ni kosa la jinai," alisema.

Alisema kuwa kuna watu ambao wamekuwa wakitangaza kuwa Mwinyi asije kufanya uzinduzi wa kampeni na asipofanya hivyo atachafuliwa.

Mwenyekiti huyo pia alisema kuwa Halmashauri ya Kuu ya CCM mkoani Mbeya inakanusha chama hicho kimegawanyika, akisema kuwa, hakuna wabunge waliogawanyika ndani ya chama hicho.

Alisema kuwa katika kikao hicho cha halmashauri kilichofanyika jana, wamejipanga kuhakikisha kila mbunge anapangiwa majukumu yake katika kuhakikisha CCM inatetea vizuri kiti hicho kilichoachwa wazi na mbunge wake, Richard Nyaulawa.

"Hakuna mgawanyiko ndani ya chama chetu cha CCM na hakuna wabunge waliogawanyika wote ni kitu kimoja na tumejipanga vizuri na tunamwomba Mwenyezi Mungu atusaidie ili tuweze kupata ushindi kwa asilimia kubwa na tuna imani kuwa tutashinda," alisema.

Alipohojiwa kuhusu CCM kuwaweka vijana wake wilayani Mbarali kwa ajili maandalizi ya kampeni, mwenyekiti huyo, alisema kuwa, kambi hiyo ni moja ya mikakati ya umoja wa vijana ambayo ipo muda wote na siyo maalum kwa ajili ya uchaguzi.

Alisema kuwa, mara nyingi kumekuwepo kambi za vijana wa CCM kwa ajili ya kujifunza itikadi za chama hicho na kwamba kambi hiyo ni kwa ajili ya shughuli za vijana.
 
CCM yaonya wanaotaka kumchafua Mwinyi

CHAMA Cha Mapinduzi (CCM), mkoani Mbeya,kimevionya vyama vya upinzani vyenye lengo la kumchafua rais mstaafu wa awamu ya pili, Ali Hassan Mwinyi kwenye kampeni za uchaguzi mdogo wa jimbo la Mbeya Vijijini.

Maana yake ni kuwa MWINYI ni mchafu.
 
kila siku humu jf watu wamekuwa wakimtupia lawama za kila aina mwalimu julius kambarage nyerere (rip). Kuanzia elimu, uchumi, udini, muungano, rushwa, rostam, mashirika yetu ya uma ambayo yamekufa 15yrs baada ya yeye kuondoka.

Nadhani wakati umefika wa kuanza kuangalia na kuyajadili yaliyofanywa na mwinyi na mkapa kwa ajili hata wao walikua marais wa tz, sijui wana jf mtawajadili wote kwa pamoja au mwinyi kwanza alafu mkapa. Au mnaweza mkangonjea atakyekufa kwanza alafu ndio mtamjadili yeye kwanza.
 
Nyerere ndiye aliyekuwa na nguvu za kiutawala tangu 1961 hadi alipofariki.Hawa wengine ni wafuasi tu na alikuwa akiwakemea kama watoto wadogo.Mamlaka ya mwalimu yalikuwa hayana kizuizi na kila alichokitaka kilikuwa.Mwinyi na Mkapa walikuwa kama viongozi walioteuliwa na Nyerere ili watanzania wawapigie kura.
 
Binadamu anapopatwa na marazi Daktari humuangalia chanzo cha maradhi hayo na hapo tena ndio kutafutiwa matibabu ya kutibu maradhi yake,ukija kwenye magari na mambo yote kwa ujumla utafutwa nini chanzo chake leo hii kila kona utasikia sifa za Rais mstafu Ali hassan mwinyi na kumpa jina mzee ruksa lakini ruksa lakini basi Mzee huyo huyo wa ruksa ameleta Balaa ndani ya nchi kuliko hata hizo ruksa alizotowa kwa nini kikasema hivyo.

Mzee huyu huyu ndie aliyelipinga azimio la Arusha alilolileta Mwalimu na kugeuza liwe Azimio la ZANZIBAR leo nchi nzima imo katika hadhabu na mateso kila kona viongozi wananuka wizi nchi hatujuwi wapi tunakwenda ni mwinyi wakubebeshwa mzigo huu wa maovu unaoendelea kwa viongozi
 
nyerere ndiye aliyekuwa na nguvu za kiutawala tangu 1961 hadi alipofariki.hawa wengine ni wafuasi tu na alikuwa akiwakemea kama watoto wadogo.mamlaka ya mwalimu yalikuwa hayana kizuizi na kila alichokitaka kilikuwa.mwinyi na mkapa walikuwa kama viongozi walioteuliwa na nyerere ili watanzania wawapigie kura.

kwa hiyo unamaanisha makosa ya mwinyi na mkapa sio yao bali ni ya nyerere?
Kwa hiyo wizi wa mwinyi na mkapa sio wao ni wa nyerere?
 
Binadamu anapopatwa na marazi Daktari humuangalia chanzo cha maradhi hayo na hapo tena ndio kutafutiwa matibabu ya kutibu maradhi yake,ukija kwenye magari na mambo yote kwa ujumla utafutwa nini chanzo chake leo hii kila kona utasikia sifa za Rais mstafu Ali hassan mwinyi na kumpa jina mzee ruksa lakini ruksa lakini basi Mzee huyo huyo wa ruksa ameleta Balaa ndani ya nchi kuliko hata hizo ruksa alizotowa kwa nini kikasema hivyo.

Mzee huyu huyu ndie aliyelipinga azimio la Arusha alilolileta Mwalimu na kugeuza liwe Azimio la ZANZIBAR leo nchi nzima imo katika hadhabu na mateso kila kona viongozi wananuka wizi nchi hatujuwi wapi tunakwenda ni mwinyi wakubebeshwa mzigo huu wa maovu unaoendelea kwa viongozi

ruksa ndio chanzo cha rushwa.

Rushwa ni legacy ya mwinyi......
 
Mwinyi alijitahidi kwa kuruhusu mitumba bongo watu wakapata nguo za kuvaa,but ndiye aliyetoa mianya mikubwa ya rushwa. Ndiye aliyeanzisha biashara ikulu ambapo mkapa naye akaiga na mengine mengi. Tusimtupia kila lawama nyerere (rip) kilakitu!!
 
Na Nyerere alikuwa akiwaita ikulu kuwachapa viboko pindi wakikaidi.....Mwinyi alikuwa akiwaita ikulu kuwaomba watu wakae kwa amani bila kugombana...Mkapa alikuwa akiwaita ikulu kufanya madili....
 
Lakini mwinyi si ndio aliofungua dirisha ili hewa safi iingie katika chumba baada ya kuwa na joto kali kwa muda mrefu, lakini kwa bahati mbaya vijidudu kama mbu na nzi ndo wakajiingiza (rushwa) au mshasahau Tanzania ilivyokuwa (kiuchumi) kipindi cha nyerere, kwamba hata kama ulikuwa unapesa, chakula utauziwa kijamaa jamaa, eg. 2kg kwa kila mtu regardless una hela kiasi gani, nguo wote wanavaa sare, kumiliki TV ni mhujumu uchumi. Hata hivyo kama utafanya cost benefit analysis basi benefit ni kubwa zaidi kuliko maafa, hivyo ni kiongozi bora.
 
Nyerere ndiye aliyekuwa na nguvu za kiutawala tangu 1961 hadi alipofariki.Hawa wengine ni wafuasi tu na alikuwa akiwakemea kama watoto wadogo.Mamlaka ya mwalimu yalikuwa hayana kizuizi na kila alichokitaka kilikuwa.Mwinyi na Mkapa walikuwa kama viongozi walioteuliwa na Nyerere ili watanzania wawapigie kura.

He wa simply a dictator!
 
Binadamu anapopatwa na marazi Daktari humuangalia chanzo cha maradhi hayo na hapo tena ndio kutafutiwa matibabu ya kutibu maradhi yake,ukija kwenye magari na mambo yote kwa ujumla utafutwa nini chanzo chake leo hii kila kona utasikia sifa za Rais mstafu Ali hassan mwinyi na kumpa jina mzee ruksa lakini ruksa lakini basi Mzee huyo huyo wa ruksa ameleta Balaa ndani ya nchi kuliko hata hizo ruksa alizotowa kwa nini kikasema hivyo.

Mzee huyu huyu ndie aliyelipinga azimio la Arusha alilolileta Mwalimu na kugeuza liwe Azimio la ZANZIBAR leo nchi nzima imo katika hadhabu na mateso kila kona viongozi wananuka wizi nchi hatujuwi wapi tunakwenda ni mwinyi wakubebeshwa mzigo huu wa maovu unaoendelea kwa viongozi

AZIMIO LA ARUSHA LILISHAKUWA MUFLIS; Hiyo ndiyo sera ya CCM kuwa mbele kwa kila kitu. Wakati wa Nyerere makada ndio waliokuwa wakitanua, alipokuja Mwinyi CCM iliwaita matajiri wale pamoja (Azimio likawa Muflis), Wakati wa Mkapa CCM walikimbilia Commission na hisa na sasa siasa za matusi na kugombania madaraka kama walivokuwa wapinzani huko nyuma.
CCM ni chama cha kukimbilia maslahi basi, tangu wakati wa Nyerere.
 
Back
Top Bottom