Tanzania Now Faces Sanctions & Diplomatic Crisis Over Iran

Status
Not open for further replies.
Nimejaribu kusoma tena hiyo barua, hebu angalieni kwenye red. Inaelekea huyu Seneta alikuwa na high hopes kwa rais wetu lakini mambo yamekuwa ndivyo sivyo.

Lakini sehemu iliyonistua ni hapo kwenye blue, anametumia maneno own accord. Hii ni aibu kweli kweli kwetu sisi Tanzania. Basically, anatuambia either we do it or else. Membe aling'aka sana na kauli ya Cameroon, sijui kama atakuwa na msuli wa kujibu hii order kwa mtindo ule ule? Tukiondoa flag ni aibu maana tunapata order toka nje (uhuru?), tusipoondoa ni mtihani (njaa?). ah, tumepatikana!

Umeipata vema Mkuu 'Omba omba hana Haki/Hawezi kuchagua!
 
nimechoka! leo nimepata fursa ya kuongea na senior intelligence officers wa serikali ya uingereza wanasema wanafuatilia hili sakata kwa ukaribu zaidi na wakijiridisha bila shaka Tanzania itawekewa vikwazo vya kiuchumi pamoja na kufuta misaada yote. Pia jamaa wamenitonya hapa Washington DC kuwa wanafuatilia kwa ukaribu suala la Dr . Ulimboka na kusema endapo akifa tu na chanzo kuwa ni mateso aliyoyapata kuna kitu kikubwa chaja (kwa sasa ibaki siri).Nilipojitambulisha natoka tanzania mmoja wao amenijibu . nanukuu

"WE HATE CHAMA CHA MAPINDUZI"

mwisho wa kunukuu
Mkuu hiyo hapo kwenye red Umeongeza Chumvi... huwezi kupitisha Siku bila Uongo!
 
Mkuu wewe huijui USA unaleta porojo za bongo! mataifa kama Japan, China, India, Europe n.k yanasalim amri ndo iwe TZ.
Kataeni mengine rakini siyo hilo.
Iran na wauza mafuta wote wameshindwa kubadilisha mafuta yasiuzwe kwa USD pamoja na kwamba ni yao.
Chezea kwingine

Wewe kweli MJIPYA naona unaleta stori za zamani Mkuu Marekani ilikuwa zamani siku hizi dunia imebadilika kwa taarifa yako Iran inauwazia mafuta Urusi na China, na Marekani wako kafyata mkia...Marekani kaomba mkopo China kapewa mkopo wa masharti kwa sababu hana shida kakubali kukopa China, sasa mtu anakudai utamwambia nini, chezea China wewe.
 
Nadhani umesoma kwa haraka haraka. Rudia tena na kwa makini zaidi, utakutana na sentence inayosomeka hivi:

"It would be preferable that Tanzania take this action of its own accord."

Swali la kujiuliza, kama hatufanya sisi wenyewe kama walivyotushauri nini kitafuata?

Mkuu wangu FJM,
Binafsi sijaona cha kushabikia katika barua hii....na hili wala sio ONYO kama tunavyotaka kuaminishwa!! Ni barua ya kawaida kabisa iliyobeba ushabiki wa kisiasa usio na tija yoyote!! Yaani humu ndani watu wana mawazo ya ajabu sana....furaha yao ni kuona nchi inaenda msobesobe ili wapate cha kuongea.....sisi tunaoweka nchi kwanza na siasa baadae tunaona ni mawazo mufilisi!! Leo hii wanatamani wakisikia wafanyakazi wote nchini wanagoma.....leo hii wanatamani wasikie nchi inawawekewa vikwazo vya kila aina....leo hii wanatamani wasikie viongozi wameiba mabilioni ya fedha BOT......leo hii wanatamani wasikie Rais wa nchi anakashifiwa na mataifa ya kigeni......leo hii wanatamani wasikie majanga ya kila aina yasiyo na athari kwao yanaikumba nchi, leo hii.....leo hii....leo hii...ORODHA NI NDEFU! Huu ni upuuzi!!

By the way, nimeshauliza kabla, hivi kuna gharama gani kwa meli ya nchi moja kupeperusha bendera ya nchi nyingine?! Mbona hata meli za maharamia nazo huwa zinapeperusha bendera?! Na mbona SMZ imeshatolea ufafanuzi suala hilo?!Yaani tunataka kuamini ya wazungu kwa kuwa tu wao ni Wamarekani?! Sio siri, najisikia aibu sana ninapoona watu wenye busara wakitegemea foreign attacks ili wao wajijenge!! Ninachoona kwa barua hii ni kwamba, tumekuza mno yaliyomo humo.....yaani imekaa kipropagandapropaganda zaidi!!
 
Thank GOD, dhambi za kisirisiri zimeiumbua serikali dhaifu ya TZ.
We know that EU will begin implementing sanctions against Iranian Oil imports from tomorrow 1st July 2012 as a matter of forcing Iranian regime from enriching uranium for nuclear weapons. Now if Tanzania is siding with this regime, then it must be punished as well in the same level and degree as Iran.
We in Tanzania should avoid double standards decision making, if we realy are against terrorism acts, then we should hold fast on it, otherwise let us admit that our gov. is literally weak:israel:
 
Maalim Abbas anauliza...je Tanzania imevunja sheria ipi ya Kimataifa?

DSC_0268.JPG
 
Kimsingi hiyo barua inaonyesha tunaunga mkono ugaidi kwa kuisadia iran,haya mambo sikuwahi sikia enzi ya mkapa
 
Chifu NasDaz, hapa suala ni zaidi ya hizo 'gharama' unazozifikiri. Naamini unaelewa juu ya embargo ya Iran kutoka USA na EU; sasa katika mtazamo huo, Iran kutumia bendera ya Tanzania ililenga katika 'kukwepa' embargo hiyo na kutaka kuiaminisha dunia kwamba mzigo ule ni wa Tanzania. Pia naamini unaelewa political tensions behind Iran-EU-USA relations; sasa inapokuja kutokea kwamba Tanzania, nchi inayotegemea misaada kwa kiwango kikubwa toka USA na EU, 'inajidhiirisha' kwa uwazi kwamba ipo 'pamoja' na Iran, unafikiri gharama zake zitakuwaje?!?

Hapo kwenye nyekundu, ndiyo moja ya gharama zinazotokea sasa, kwani Tanzania nayo yaweza kuwekwa kundi moja na maharamia na magaidi kwa vile tu imeisadia Iran kutimiza matakwa yake ya kibiashara.

By the way, nimeshauliza kabla, hivi kuna gharama gani kwa meli ya nchi moja kupeperusha bendera ya nchi nyingine?! Mbona hata meli za maharamia nazo huwa zinapeperusha bendera?!
 
Hapana haijamkalia isipokuwa mh. Raisi anaonesha jinsi gani alivyo jasiri haswa na si kama vile wachache wanavo fikiri.
 
Mkuu wangu FJM,
Binafsi sijaona cha kushabikia katika barua hii....na hili wala sio ONYO kama tunavyotaka kuaminishwa!! Ni barua ya kawaida kabisa iliyobeba ushabiki wa kisiasa usio na tija yoyote!! Yaani humu ndani watu wana mawazo ya ajabu sana....furaha yao ni kuona nchi inaenda msobesobe ili wapate cha kuongea.....sisi tunaoweka nchi kwanza na siasa baadae tunaona ni mawazo mufilisi!! Leo hii wanatamani wakisikia wafanyakazi wote nchini wanagoma.....leo hii wanatamani wasikie nchi inawawekewa vikwazo vya kila aina....leo hii wanatamani wasikie viongozi wameiba mabilioni ya fedha BOT......leo hii wanatamani wasikie Rais wa nchi anakashifiwa na mataifa ya kigeni......leo hii wanatamani wasikie majanga ya kila aina yasiyo na athari kwao yanaikumba nchi, leo hii.....leo hii....leo hii...ORODHA NI NDEFU! Huu ni upuuzi!!

By the way, nimeshauliza kabla, hivi kuna gharama gani kwa meli ya nchi moja kupeperusha bendera ya nchi nyingine?! Mbona hata meli za maharamia nazo huwa zinapeperusha bendera?! Na mbona SMZ imeshatolea ufafanuzi suala hilo?!Yaani tunataka kuamini ya wazungu kwa kuwa tu wao ni Wamarekani?! Sio siri, najisikia aibu sana ninapoona watu wenye busara wakitegemea foreign attacks ili wao wajijenge!! Ninachoona kwa barua hii ni kwamba, tumekuza mno yaliyomo humo.....yaani imekaa kipropagandapropaganda zaidi!!

NasDaz, nimekuelewa maana sisi wote ni watanzania, tuna sifa moja kubwa ya kuongea sana lakini action zero. Kwa bahti mbaya hii barua haijatoka kwa mtanzania mwenzetu, imetoka kwa mmarekani, tena kiongozi. Iwe siasa au la, lakini marekani wana sifa moja, hawana rafiki wa kudumu, na wakisema nyeusi ni nyeusi, na sio cheusi chekundu.

Tulifanya makosa makubwa sana miaka kama 5-6 hivi iliyopita. Sasa hivi hawa watu wametapakaa mpaka kwenye vitanda vyetu (net za mbu). Hata leo hii baadhi yao walikuwa wanakunywa juice magogoni. Kujiondoa kwenye hili tope la sasa itakuwa kazi kubwa sana, itabidi tujiloweke kwenye JIKI kali na kwa muda mrefu na upo uwezekano tusitakate, thanks to uranium.

Kuhusu Zanzibar, yale matatizo yetu ya muungano yanajitokeza tena. Zanzibar ni nchi, wana rais wao, katiba yao na hata bendera yao. Mbele ya dunia kuna Tanzania, lakini humu ndani tuna Zanzibar na Tanganyika. Na swala la maritime kila upande unafanya kivyake, lakini tukumbuke ulinzi na usalama na swala muungano. Sasa upande mmoja umetoa kibali cha Meli kupeperusha bendera ya muungano, je upande wa pili unajua? Na huu upande uliotoa kibali wana uhakika ni meli za mafuta tu au kuna mengine? Ulinzi vipi?

Lakini kubwa kwenye hii hoja ya muungano, rais wa Jamhuri ana mamlaka gani kwenye hii saga? Anaweza au ana nguvu (kwa sasa) kufuta hichi kibali? Muungano? Nchi moja? rais mmoja? Nahisi kuna episode nyingine ya fedheha inatunyemelea.
 
JFM,
Serikali ya Zanzibar haikuuma uma meno katika hili. Wametamka wazi kwamba, kisheria Zanzibar wana mamlaka ya kusajili meli za nje bila ya idhini yaJMT. Aidha, wametamka wazi kwamba, wana haki ya kutumia bendera ya JMT kwakuwa ZNZ nayo ni sehemu ya muungano. Lakini pamoja na kuwa na mamlaka hayo, wao wametamka wazi kwamba hakuna meli yoyote ya Iran ambayo ama wameisajili wao moja kwa moja au kupitia kwa wakala wake aliyepo Dubai. Na hata ukiisoma vizuri hiyo barua ya Berman, wala hawajasema kwamba hiyo meli imesajiliwa Tanzania bali inapeperusha bendera ya Tanzania.....na ndio maana nikauliza kwani ni ajabu kwa meli ya nchi moja kupeperesha bendera ya nchi nyingine kinyume na sheria?! Hapo kinachoonekana ni speculation tu toka USA kwamba provided meli hizo zinapeperusha bendera za TZ basi kuna uwezekano kwamba zimepata baraka kutoka TZ ama kusajiliwa TZ!!
 
Chifu NasDaz, hapa suala ni zaidi ya hizo 'gharama' unazozifikiri. Naamini unaelewa juu ya embargo ya Iran kutoka USA na EU; sasa katika mtazamo huo, Iran kutumia bendera ya Tanzania ililenga katika 'kukwepa' embargo hiyo na kutaka kuiaminisha dunia kwamba mzigo ule ni wa Tanzania. Pia naamini unaelewa political tensions behind Iran-EU-USA relations; sasa inapokuja kutokea kwamba Tanzania, nchi inayotegemea misaada kwa kiwango kikubwa toka USA na EU, 'inajidhiirisha' kwa uwazi kwamba ipo 'pamoja' na Iran, unafikiri gharama zake zitakuwaje?!?

Hapo kwenye nyekundu, ndiyo moja ya gharama zinazotokea sasa, kwani Tanzania nayo yaweza kuwekwa kundi moja na maharamia na magaidi kwa vile tu imeisadia Iran kutimiza matakwa yake ya kibiashara.

Mkuu wangu Nzi,
Nakubaliana na maelezo yako kwa ++100%....sina tatizo katika hilo!! Hoja ya kwangu ni kwamba, hao USA hawana uhakika kwamba kupeperushwa huko kwa bendera kuna baraka toka JMT....!! Kuwa na baraka kutoka JMT maana yake ni kwamba ama meli hizo ziwe zimesajiliwa na sehemu moja wapo ya JMT au kulikuwapo na makubaliano ya siri/wazi kati ya JMT/SMZ na Iran katika kutumia bendera hizo. Kinyume chake, haigharimu chochote kwa meli yoyote kupeperusha bendera ya nchi yoyote!!! Zile bendera ni vitambaa tu na sizani kama zina security mark yoyote ambayo mtu anaweza kuhoji ilikuwaje hadi wahusika wakapata bendera yenye security mark.
 
You R Right... Completely Right ... From Senior Bush to Junior Bush...

George Herbert Walker Bush, whose father was a part*
ner in the powerful London-controlled private banking firm
Brown Brothers Harriman. Relevant to the Barrick story,
Bush was U.S. vice president and chief of covert operations
in the Reagan-Bush (1981-89) administration, and U.S. Presi*
dent (1989-93). As a former President and power broker, Bush
is Barrick Gold Corp.' s chief lobbyist, a stockholder in Bar*
rick, and honorary senior adviser to Barrick's international
advisory board.
Umeona, eeh? Sasa unaelewa ni kwa nini Bush alikuja na ataendelea kuja Tanzania. Siyo kwamba anatutakia mema.
Amewekeza mirija yake huko.
 
Barrick ilikuja wakati wa Mkapa na sio wakati wa Kikwete Mikataba yote Mibovu ilisainiwa wakati wa Utawala wa

Mkapa na si Kikwete
Ni kweli Barrick ilianza kuchimba wakati wa Mkapa. Lakini mikataba ilisainiwa wakati wa Mwinyi. And guess what? Nani alikuwa waziri wa madini na nishati wakati wa Mwinyi?
 
JFM,
Serikali ya Zanzibar haikuuma uma meno katika hili. Wametamka wazi kwamba, kisheria Zanzibar wana mamlaka ya kusajili meli za nje bila ya idhini yaJMT. Aidha, wametamka wazi kwamba, wana haki ya kutumia bendera ya JMT kwakuwa ZNZ nayo ni sehemu ya muungano. Lakini pamoja na kuwa na mamlaka hayo, wao wametamka wazi kwamba hakuna meli yoyote ya Iran ambayo ama wameisajili wao moja kwa moja au kupitia kwa wakala wake aliyepo Dubai. Na hata ukiisoma vizuri hiyo barua ya Berman, wala hawajasema kwamba hiyo meli imesajiliwa Tanzania bali inapeperusha bendera ya Tanzania.....na ndio maana nikauliza kwani ni ajabu kwa meli ya nchi moja kupeperesha bendera ya nchi nyingine kinyume na sheria?! Hapo kinachoonekana ni speculation tu toka USA kwamba provided meli hizo zinapeperusha bendera za TZ basi kuna uwezekano kwamba zimepata baraka kutoka TZ ama kusajiliwa TZ!!

Unajua kiongozi hapa hatujadili hasa sheria zetu zinasemaje, whether zimekiukwa au la. Na wala barua ya bwana Berman haiulizi aina ya usajili. Message ya huyo mmarekani is very clear - stop-reflagging the NITC vessels. Na wameandika kabisa "It would be preferable that Tanzania take this action of its own accord"

Mimi na wewe tunaweza kujadili sana sheria zetu, na kauli za wanasiasa wetu toka pande mbili za muungano, lakini haibadilishi the fact that Tanzania tumepewa order. Na hata huyo mwanasiasa wa Zanzibar anayeleta za kuleta anaonekana kubishana na Tanzania bara badala ya Marekani. Kwa ujumla tuko kwenye tope.
 
JFM,
Serikali ya Zanzibar haikuuma uma meno katika hili. Wametamka wazi kwamba, kisheria Zanzibar wana mamlaka ya kusajili meli za nje bila ya idhini yaJMT. Aidha, wametamka wazi kwamba, wana haki ya kutumia bendera ya JMT kwakuwa ZNZ nayo ni sehemu ya muungano. Lakini pamoja na kuwa na mamlaka hayo, wao wametamka wazi kwamba hakuna meli yoyote ya Iran ambayo ama wameisajili wao moja kwa moja au kupitia kwa wakala wake aliyepo Dubai. Na hata ukiisoma vizuri hiyo barua ya Berman, wala hawajasema kwamba hiyo meli imesajiliwa Tanzania bali inapeperusha bendera ya Tanzania.....na ndio maana nikauliza kwani ni ajabu kwa meli ya nchi moja kupeperesha bendera ya nchi nyingine kinyume na sheria?! Hapo kinachoonekana ni speculation tu toka USA kwamba provided meli hizo zinapeperusha bendera za TZ basi kuna uwezekano kwamba zimepata baraka kutoka TZ ama kusajiliwa TZ!!

NasDaz,

..Zanzibar hawana haki ya kupeperusha bendera ya Tanzania kwenye masuala yasiyo ya muungano.

..kama suala hili la usajili wa meli halina mahusiano na muungano basi Zanzibar walipaswa kupeperusha bendera yao.

..Siku zote Zanzibar wanalilia kuwa huru na kujiamulia mambo yao wenyewe. Sasa ktk hili la kusajili meli za wa-Iran wameshindwa nini kuji-assert na kupeperusha bendera yao??
 
  • Thanks
Reactions: FJM
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom