Waziri wa Znz yuko sahihi kusema yafuatayo:
1. Kuwa wao hawajavunja sheria yeyote kusajili meli hizo.
2. SMZ kwa kupitia ZMTA wako huru kusajili meli yeyote bila kushauriana na waziri husika wa muungano.
3. Na kwamba kwa kupitia agent wao Dubai (Philtex) ndio walisajili hizo meli.
Sawa lakini implication ya hilo ni kubwa nae kama haelewi basi kuna taabu hapa. Maana kwa kuanzia ile point yake kuwa hizo meli zinamilikiwa na raia wa uingereza kupitia virgin iland na seychelles si kweli, ama sivyo hawa jamaa(USA) wasingepoteza muda wao, hiyo ni katika namna ya Iran kukwepo vikwazo.
Pili tayari wameshajua meli hizi zimesajiliwa Znz kukwepa vikwazo na hii sasa haisaidii maana tayari wanazijua hivyo hazitapata bima kama walivyokuwa wanataka mwanzo.
Tatu kipato kikuu cha Znz ni utalii na hao watalii wengi Znz wanatoka mataifa hayo ya magharibi sio arabuni au Iran, hivyo hizo nchi zikiwashauri raia wao wasije Znz basi hilo pengo ni kubwa, na hata karafuu wakiamua kugomea kuziwekea vikwazo meli zao ndio mwisho wa Smz.
Hiyo yote ni kuwa na upeo mdogo wa kufikiri, kwa nini ujiingize kwenye mgogoro usiokuhusu, tena ilhali wewe mwenyewe uko goigoi na maskini bin taabani? Hivi US wakituwekea vikwazo au kutuvamia(sidhani kama watafanya hivyo) Iran wana ubavu au hata uwezo wa kuja kutusaidia? haya ndio mambo ya kufikiri kabla ya kuropoka tu bila kujua athari ya matendo yako.
Mwisho wa yote, nafikiri Znz watakubali kuwa walifanya kosa na si ajabu huyo Waziri au mkuu wa ZMTA wakaondolewa au kujiuzulu, hili si swala dogo kabisa.