Bams
JF-Expert Member
- Oct 19, 2010
- 16,547
- 41,058
Kuna mambo huwa yanafanywa na baadhi ya viongozi wetu, mpaka unajiuliza tunaongozwa na watu wa namna gani! Maana ni kama hata kwenye kile kiwango cha akili ya kawaida, hawamo.
Nchi zetu hizi hazipati maendeleo kutokana na kukosa viongozi katika maana ya viongozi. Kuwa kiongozi maana yake ni wewe kuwaonesha njia unaowaongoza. Kama kiongozi unakuwa mwongo maana yake utatengeneza watu wengi waongo. Kiongozi ukiwa mwizi, utatengeneza wevi wengi sana. Lakini pia kiongozi ukiwa mwadilifu utatengeneza waadilifu wengi. Kiongozi ukiwa mkweli, utatengeneza watu wakweli wengi.
Jamii yetu kujawa na watu wengi wa ajabu ajabu, kuwa na watendaji wengi Serikalini wevi, wafujaji, waongo, kunaashiria ndivyo walivyo wakuu wao.
Ninachojiuliza, hivi hawa watawala wetu kwa kuyapata madaraka huwa wanaamini wameuaga ubinadamu, wao sasa siyo wanadamu? Na kwa vile wao ni juu ya wanadamu, hawawezi kuugua wala kufa? Nadhani kwa kuamini kuwa wao ni zaidi ya wanadamu, ndiyo maana wengine huwa wanaiba mpaka wanakufuru. Mtu anaiba kiasi hata akiishi miaka 2,000 hawezi kumaliza utajiri wa wizi alioutengeneza.
Mimi naamini, kwa mwanadamu kuumwa au hata kufa, ni mambo ambayo humpata mwanadamu yeyote, na hakuna mwenye uwezo wa kuyazuia. Kuumwa au kifo siyo aibu na wala siyo kosa la mgonjwa au marehemu. Kama haya ninayoyasema ndiyo ukweli, kwa nini watawala wa Tanzania, kiongozi akiugua huwa wanapenda kusema uwongo?
Hayati Magufuli wakati anaugua, katikati ya minong'ono kuwa Magufuli ni mgonjwa, watawala waliamua kusema uwongo kuwa Magufuli yu mzima. Akiwa tayari ameaga Dunia, baadhi ya viongozi waliendelea kusisitiza kuwa yumzima.
Angalao Kikwete yeye aliamua kuweka wazi alipokuwa anaumwa, tena akaenda ndani zaidi hadi kuelezea alikuwa anaumwa nini.
Kule South Afrika, Mandela alipougua mafua makali, nchi ilitangaziwa. Baadaye alipougua tena na kulazwa, wananchi walipewa taarifa, na baadaye kupewa taarifa ya maendeleo yake karibia kila siku. Mseveni alipougua, wananchi walitangaziwa. Malkia Elizabeth alipovunjika mfupa, wananchi walijulishwa.
Hawa wa kwetu kusema uwongo kiongozi akiugua wanataka kutuambia kiongozi siyo mwanadamu, na hivyo haguswi na maradhi, ajali wala kifo?
Kuna minong'ono kuwa Makamu wa Rais ni mgonjwa, na kwamba yupo nje kwa matibabu, lakini watawala wanawadanganya wananchi kuwa yupo nje kikazi.
Kama ni kweli kuwa Makamu wa Rais anaumwa na yupo nje kwa matibabu, hawa wanaosema yupo nje kwa ziara ya kikazi, kweli wana akili timamu? Na kama hawana akili timamu, nchi inayoongozwa na watu wasio timilifu, mwisho wake ni nini?