Tanzania daima na wivu wenu mpo?

Jay Milionea

JF-Expert Member
Apr 19, 2015
1,185
154
Gazeti lenu la leo jumatano mmechapisha habari ya ajabu ajabu sana, naona mwandishi kamlilia sana mwalimu nyerere akidhani atafufuka leo, lakini haya yote ya nini? Kama rais mchapakazi asiye na undugu wla urafiki tumempata, sasa mnalialia nini na gazeti lenu hilo? Mnaanza kumdai dkt. Magufuli kuhusu ahadi zake za viwanda kwa tanzania nzima, kwani huyu rais wetu ameanza kazi yake lini? Msiwe wapotoshaji kwa umma, maana lengo lenu hapo ni kuamsha hisia za watu tu, kama uchaguzi ulishapita sasa jukumu kubwa lililopo usoni ni kuijenga nchi yetu sote!!

Rais magufuli ni rais wa watu wote, na ameshaanza kuonyesha utendaji kazi wake kwa baadhi ya maeneo kama vile wizara ya fedha, muhimbili na nadhani kwengine ataenda pia.

Kama mnavyokumbuka ilani ya chama cha mapinduzi (ccm) ndiyo guide line yake katika kutenda yale aloyaahidi ikiwemo mengine ambayo hakuahidi, sasa sio vema kuanza kumpiga vijembe mapema hivi maana watu wengine wanatafsiri kuwa huko ni kukosa cha kuongea na kujawa na wivu, kama ushindi ameshapata na ndo rais wetu huyo hakuna jinsi.

Ushauri wangu kwa wanaukawa ni kushirikiana na na kuijenga nchi yetu lakini majungu na lawama sio vema kuzitoa kwa kipindi hiki ambacho ana siku 6 tuu tangu awe ofisini kwake.

Tulitegemea mngeongea mambo mazuri ya kumpa mbinu zaidi jinsi ya kuleta maendeleo nchini lakini nyie mmejawa na chuki, wivu na lawama eti kisa kachaguliwa kuwa rais, sasa huyo rais wenu angeweza kufanya mabadiliko ndani ya wiki 1 au hizi siku 6? Acheni wivu jamani mnaonekana mmeishiwa hoja mmejawa wivu tuu.

nb: jelous people never win ng'oooooooo!!
 
Tanzania Daima halina habari zenye weledi. Ni ushabiki wa wazi kwa miliki wao Mbowe tu.
 
Dj Mbowe bado ajaamini kama kala bure hela za Lowassa anaogopa atashindwa cha kulipa maana alimuaidi kwenda Ikulu
 
Umesema Rais kaanza kazi wizara ya fedha..hivi unajua maana ya kufanya kazi ww kilaza.. yaani mazingaombwe ya kuuliza walioenda kunywa chai..basi unaona kafanya kazi..wewe sio mzima..
 
Hata siku moja huwezi kuta Tanzania daima iakandika habari ya maana zaidi ya kulaumu na kukosoa vitu ambavyo havipo wale hawana tofauti na mbulula
 
Mbona tz daima linauzika Sana tofauti na Uhuru, habari na jambo Leo?
 
Hvi kuna mwanadamu mwenye akili timamu anasoma hicho kijigazeti uchwara cha kufungia mihogo?
 
Back
Top Bottom