Tanzania: Adui yetu ni nani na tuna fursa gani za kumshinda? Tunamlenga au tunamkwepa?

Adui mkuu wa Tanzania ni Ufusadi ingekua kila mtu anauchukia ufisadi basi tungefika pazuri. Hii kansa ya ufusadi sio vyama ni hulka ya watu.ingekua watu wanafuata maadali ya uongozi na kilichopangwa kinafanywa basi uadui wa mtanzania ungekua mdogo sana
 
Niliwahi kusema hapa kwamba hata mwenyezi Mungu angefanya miujiza wake a kamleta malaika akapewa uongozi kupitia kwa hao wajomba moja Kati ya mambo Mawili litaokea.

Ama wanarubuni awe fisadi na anakataa watamnyang'anya silaa
 
Unajua nimekuwa nikatafakari sana mashambulizi yetu hapa. Halafu yule mama Anne Malecela naye amenifanya nizame kwenye fikra zaidi.

Kwa kweli tumekuwa mahodari sana wa kuonesha matatizo yetu na wakati mwingine hata kupendekeza namna ya kumaliza matatizo yetu. Juzi pia wapinzani wamefungua ukurasa mpya kabisa wa siasa zetu kwa kuweza kuwakilisha sio tu bajeti mbadala kwa mara ya kwanza lakini kwa kuwakilisha bajeti yenye akili kuliko ile ya serikali ya CCM.

Hii imethibitika zaidi baada ya hata wataalamu wa kiuchumo nchini mwetu kuishauri serikali "kuiba" baadhi ya nondo zilizomo katika bajeti ya wapinzani. Of course mimi pendekezo langu lilikuwa radical zaidi; nilimshauri dada Zakia aachene na bajeti yake uchwara na badala abebe bajeti ya kaka Hamad na Zitto nzimanzima kama ilivyo. Hata hivyo najua wataendelea na bajeti yao hiyohiyo kimkandamkanda maana wanajua tutasahau na wataibua liskendo lingine la kutusaulisha hili li bajeti.

OK, where am I going? Kuzama kwangu katika fikra hizi kumenifikisha katika hitimisho hili: sote tupo katika campaign. Lakini bahati mbaya inaonekana tunafanya campaign isiyo! Campaign yeyote lazima itambue mambo manne muhimu: muathirika ni nani? adu ni nani? fursa ya kumshinda adui ni zipi? na tukishamshinda adui tunapata nini?

Kwa maoni yangu ni wazi kwamba sisi wananchi sote tu waathirika. Adui yetu mkuu ni CCM. Fursa pekee tuliyo nayo ya kumshinda huyu adui ni uchaguzi wa 2010. Wapinzani wameonesha kwamba wanaweza wakawa mbadala mzuri. Zaidi ya yote kumbe kule CCM kuna akina Anne ambao wanafikiri kama sisi. By the way tayari tunaye Mzee ES hapa; huyu kuasi sio vigumu na anaweza akatupa mikakati ya ndani ya kumtwanga adui CCM kwenye uchaguzi.

Hivyo basi kuanzia sasa tutumie muda mwingi zaidi katika namna ya kushawishi wananchi kuelewa umuhimu wa kuifukuza CCM madarakani katika uchaguzo ujao. Hili ndiyo jambo ambalo litushughulishe zaidi kuanzia sasa hadi uchaguzi ujao. Hata wenzetu wakenya waliweza kuishinda KANU baada ya kugundua kwamba KANU ndio alikuwa adui wao mkubwa kuliko kitu kingine chochote. Ndiyo hayo tunaona leo wakenya wanaanza kutembea kifua wazi na mabega juu kwa kujivunia ukenya wao.

Huu ndio wito wangu wa leo.
Naaam....
 
Kitila,

Swali zuri sana hili. Lina vipengele vitatu na navijibu kama ifuatavyo. Nikipata msonge unipe cheti nikatundike ukutani kwangu na nikipata karai au chini yake, basi umezee na usiwaambie wengine.

(a) Adui yetu namba moja kabisa kwetu ni UJINGA wa raia wetu; mengine yote ni derivatives za ujinga huo.

(b) Fursa yetu kumshinda adui ni kutoa elimu thabiti ya uraia kwa lugha rahisi sana kutumia njia zinazopenya sana ili raia wetu waelelewe haki na wajibu wao katika kuchagua viongozi, makosa waliyofanya siku za nyuma, na jinsi makosa yao yalivyowatia katika ufukara mkubwa wakati viongozi waliowachagua wakineemeka.

(c) Hatumkwepi adui huyu ndiyo maana anaendelea kutusumbua ila hatujamlenga kabisa katika kumshambulia; tunashambulia madhara yake huyu tukimwacha mwenyewe. Ni kama vile tunashambulia harufu ya kinyesi kwa kupulizia air freshener bila kuzoa kinyesi chenyewe.
Namba 2 ni CCM
 
Adui wetu mkubwa ni CCM na viongozi wake. Nasema hivi kwa sababu viongozi wa CCM na ambao pia ndio viongozi wa Tanzania wamekuwa ni waongo wakubwa katika kutetea maslahi ya chama chao. Kinachoniudhi zaidi ni kwamba wameipa CCM kipaumbele kuliko hata nchi yao!!! Wanajua mabaya mengi yanayotendeka ndani ya nchi yetu, lakini wabunge na viongozi mbali mbali wa juu ndani ya CCM wanayafumbia macho ili kuhakikisha wanaendelea kuwa madarakani milele.

Hivi kweli wabunge wa CCM ambao ndio wengi bungeni kama wana mapenzi ya kweli na Tanzania wakaamua kusimama kidete ili mikataba ya uchimbaji madini ipelekwe bungeni ili ikaangaliwe na kujadiliwa au bajeti haipiti mikataba hiyo kweli itaendelea kufichwa?

Pia vyama vya upinzani ni adui wetu wa pili. Nasema hivi kwa sababu ubinafsi wa viongozi wa vyama hivyo, kwa kuogopa kuunda chama kimoja chenye nguvu ambacho kitakuwa na nguvu kubwa na wafuasi wengi ambao wanaweza kuhakikisha kwamba kinapata viti vingi bungeni. Viongozi hawa pamoja na kufanya vibaya katika chaguzi za vyama vingi kila kukicha hawaelekei kuwa na mikakati yoyote ya kuangalia wapi wamekosea na nini kifanyike ili wajiimarishe kupambana na CCM.

Kwa maoni yangu cha kwanza ni kuungana ili kuunda chama chenye nguvu. Pili ni kujitangaza katika wilaya zote za Tanzania na pia kutangaza sera za chama na kuwasikiliza wananchi wana maoni gani, malalamiko yao ni yapi.

Lakini hizi njemba utazisikia ikiwa imebaki miezi 15 kabla ya uchaguzi mkuu na wakisha shindwa wanaingia mitini mpaka karibu na uchaguzi mwingine!!! Hawana mikakati yoyote. Wao wanataka tu kuingia Ikulu. Kumbe wangeweka kipaumbele katika kupata viti vingi bungeni ili wananchi waone sera na utendaji wao na kuwaamini hatimaye wananchi kuamua kuwaondoa CCM madarakani, lakini wapi ubinafsi wameweka mbele kuliko mapenzi ya kweli kwa nchi yao!!! Inasikitisha sana!
Umepotelea kwa majirani moja kwa moja aisee
 
Unajua nimekuwa nikatafakari sana mashambulizi yetu hapa. Halafu yule mama Anne Malecela naye amenifanya nizame kwenye fikra zaidi.

Kwa kweli tumekuwa mahodari sana wa kuonesha matatizo yetu na wakati mwingine hata kupendekeza namna ya kumaliza matatizo yetu. Juzi pia wapinzani wamefungua ukurasa mpya kabisa wa siasa zetu kwa kuweza kuwakilisha sio tu bajeti mbadala kwa mara ya kwanza lakini kwa kuwakilisha bajeti yenye akili kuliko ile ya serikali ya CCM.

Hii imethibitika zaidi baada ya hata wataalamu wa kiuchumo nchini mwetu kuishauri serikali "kuiba" baadhi ya nondo zilizomo katika bajeti ya wapinzani. Of course mimi pendekezo langu lilikuwa radical zaidi; nilimshauri dada Zakia aachene na bajeti yake uchwara na badala abebe bajeti ya kaka Hamad na Zitto nzimanzima kama ilivyo. Hata hivyo najua wataendelea na bajeti yao hiyohiyo kimkandamkanda maana wanajua tutasahau na wataibua liskendo lingine la kutusaulisha hili li bajeti.

OK, where am I going? Kuzama kwangu katika fikra hizi kumenifikisha katika hitimisho hili: sote tupo katika campaign. Lakini bahati mbaya inaonekana tunafanya campaign isiyo! Campaign yeyote lazima itambue mambo manne muhimu: muathirika ni nani? adu ni nani? fursa ya kumshinda adui ni zipi? na tukishamshinda adui tunapata nini?

Kwa maoni yangu ni wazi kwamba sisi wananchi sote tu waathirika. Adui yetu mkuu ni CCM. Fursa pekee tuliyo nayo ya kumshinda huyu adui ni uchaguzi wa 2010. Wapinzani wameonesha kwamba wanaweza wakawa mbadala mzuri. Zaidi ya yote kumbe kule CCM kuna akina Anne ambao wanafikiri kama sisi. By the way tayari tunaye Mzee ES hapa; huyu kuasi sio vigumu na anaweza akatupa mikakati ya ndani ya kumtwanga adui CCM kwenye uchaguzi.

Hivyo basi kuanzia sasa tutumie muda mwingi zaidi katika namna ya kushawishi wananchi kuelewa umuhimu wa kuifukuza CCM madarakani katika uchaguzo ujao. Hili ndiyo jambo ambalo litushughulishe zaidi kuanzia sasa hadi uchaguzi ujao. Hata wenzetu wakenya waliweza kuishinda KANU baada ya kugundua kwamba KANU ndio alikuwa adui wao mkubwa kuliko kitu kingine chochote. Ndiyo hayo tunaona leo wakenya wanaanza kutembea kifua wazi na mabega juu kwa kujivunia ukenya wao.

Huu ndio wito wangu wa leo.
Wewe ni mchumia tumbo, phd mzigo kwa taifa!
 
Huwezi kuibadili CCM, bali CCM itakubadili wewe. (Kitila mkumbo, 2017)

Sent from my TECNO KD6 using JamiiForums mobile app

1617668656090.png

Imani yangu siku zote imekuwa ni hiyo,...kwamba adui mkubwa wa taifa hili ni CCM na hakuna aliyeingia humo akapona. Pamoja na kuwa moja wa wachangiaji enzi hizo JF, kuna mengi sana ya kujifunza ukiweza kuusoma uzi huu tangu post ya kwanza ya aliyeuanzisha Kitila Mkumbo kama nilivyofanya.

Si Kitila Mkumbo peke yake, wako wengi tu waliotumbukia kwenye hilo domo la zimwi CCM. Hata hivyo tuko wachache ambao tulitambua mapema kabisa hatari ya kurandaranda karibu na hilo domo na kwa kiasi tumefanikiwa kulikwepa. Naam, adui nambari wani wa taifa letu hili tunalolipenda ni hilo zimwi CCM.

Long live Jamii Forums.
 
Kitila,

Swali zuri sana hili. Lina vipengele vitatu na navijibu kama ifuatavyo. Nikipata msonge unipe cheti nikatundike ukutani kwangu na nikipata karai au chini yake, basi umezee na usiwaambie wengine.

(a) Adui yetu namba moja kabisa kwetu ni UJINGA wa raia wetu; mengine yote ni derivatives za ujinga huo.

(b) Fursa yetu kumshinda adui ni kutoa elimu thabiti ya uraia kwa lugha rahisi sana kutumia njia zinazopenya sana ili raia wetu waelelewe haki na wajibu wao katika kuchagua viongozi, makosa waliyofanya siku za nyuma, na jinsi makosa yao yalivyowatia katika ufukara mkubwa wakati viongozi waliowachagua wakineemeka.

(c) Hatumkwepi adui huyu ndiyo maana anaendelea kutusumbua ila hatujamlenga kabisa katika kumshambulia; tunashambulia madhara yake huyu tukimwacha mwenyewe. Ni kama vile tunashambulia harufu ya kinyesi kwa kupulizia air freshener bila kuzoa kinyesi chenyewe.
Na huyu adui yupo haswa kwa wasomi wengi sana Wa kuanziaShahada ya kwanza na kuedelea hadi uzamivu
 
Back
Top Bottom